Kutoka Ibn Abbas (r.a) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake, kumwambia Mua’dh ibn Jabal wakati alipomtuma kwenda yemen:1. “Hakika wewe utawaendea watu wa kitabu 2. Utakapo waendea, walinganie kwenye shahada wakiri kwa moyo kuwa hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye peke yake, na hakika Nabii Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. 3. Ikiwa watakukubalia hilo, basi waeleze kwamba hakika Mwenyezi Mungu amewafaradhishia sala tano mchana na usiku. 4. Ikiwa watakukubalia hilo, basi waeleze kuwa Mwenyezi Mungu amewafaradhishia juu yao, zaka ya mali zao, inachukuliwa kutoka kwa matajiri wao na inapelekwa kwa maskini wao.  5. Ikiwa watakukubalia hilo, basi jiepushe na kuchukua malizao bora zaidi. 6. Na ogopa duwa ya aliye dhulumiwa, kwani hakika hakuna kati yake na Mwenyezi Mungu pazia” . Imepokelewa na Bukhari na Muslimu. 

Kutoka kwa Mua’dh ibn Jabal (r.a) amesema:1. Nilikuwa nimepanda nyuma ya Mtume (s.a.w) katika mnyama. 2. Akasema Mtume (s.a.w): “ewe Mua’dh! Je, wajuwa ni ipi haki ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake? na ni ipi haki ya waja kwa Mwenyezi Mungu”?  3.Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi zaidi juu ya hilo. 4.Akasema Mtume (s.a.w): “hakika haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake ni kumuabudu yeye peke yake wala wasimshirikishe na chochote 5. Na haki ya waja juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kutomuadhibu yeyote asiemshirikisha na chochote” 6.Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je nisiwabashirie watu? Akasema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: “Hapana usiwape bishara hii, kwani watakuwa wavivu”

Kutoka kwa Abu Hurayrah, (Mwenyezi Mungu amuwiye radhi), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani zimshukie) amesema: 1.“Watu wangu wote wataingia Peponi isipokuwa wale wakatao kataa 2.Wakasema Maswahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani atakayekataa?  3.Akasema Mtume (Rehema na Amani zimshukie): “Mwenye kunitii mimi ataingia Peponi, na mwenye kuniasi atakuwa amekataa.” Imepokewa na Al-Bukhari

Kutoka kwa Umar bin Al-Khattab – Mwenyezi Mungu amuwiye radhi –amesimulia kuwa:siku moja tulikuwa tumekaa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani ziwe juu yake) ghafla alitokea mtu mwenye mavazi meupe mno, mwenye nywele nyeusi sana, hana athari yoyote safari ndefu, na hakuna kati yetu aliyemfahamu.Alisogea na kukaa karibu na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akiegemeza magoti yake juu ya magoti yake na akaweka mikono kwenye mapaja yake.Kisha akasema: Ewe Muhammad nieleze kuhusu Uislamu.Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie: “Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hapana Mola anaeabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja.Na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, Kusimamisha Sala.Kutoa zaka.Na kufunga mwezi wa Ramadhani.Na kuhiji kwenye Nyumba tukufu ikiwa mnaweza kuifikia.”Mtu yule akasema: umepatia. Tukamshangaa mtu yule anamuuliza kisha anamsadikisha.Kisha akasema mtu yule: Basi niambie kuhusu Imani. Mtume Akasema: Imani ni Kumuamini Mwenyezi Mungu.Na Malaika wake.Na vitabu vyake.Na Mitume wake.siku ya mwisho.Na kuamini makadirio yake, ya kheri au shari.” Mtu yule akasema: Umesema kweli.Kisha akasema: “Basi nielezee kuhusu Ihsani(wema/ufanisi)” Akasema Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake):ni Kumuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona, na ikiwa humuoni, basi Yeye anakuona.Akasema mtu yule: Basi nielezee kuhusu Kiyama).” Mtume Akasema: anaeulizwa si mjuzi zaidi kuliko muulizaji. Akasema mtu yule: Basi nielezee ishara zake, Mtume akasema: “ni mjakazi atakapomzaa bosi wake,Na kuwaona wasio na viatu, walio uchi, wachungaji wa kondoo wakishindana kujenga majumba ya kifahari.Msimulizi anasema: Kisha mtu huyo akaondoka, nikatulia muda kidogo, kisha Mtume akaniambia: Omar, umemjua ni nani muulizaji? Nikasema: “Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanajua zaidi.” Akasema: Ni Malaika Jibril amekuja kuwafundisheni dini yenu.)

Kutoka kwa Tamim al-Dari (Radhi za Mwenyezi ziwe juu yakr) kwamba Mtume (Rehma na Amani zimshukie) amesema:1."Dini ni kunasihiana" 2.  Tukasema: Kwa ajili ya nani? 3.Akasema: “Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,4.Na kwa kitabu chake. 5.Na kwa Mtume wake. 6.Kwa viongozi wa Waislamu. 7. Na watu wote”.

Kutoka kwa al-Abbas ibn Abd al-Muttalib(Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) kwamba alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani zimshukie) akisema: 1.“Ameipata ladha ya imani. 2. Aliyemridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndio mola wake mlezi  3. Na Uislamu kuwa Dini aliyoichagua. 4. Na Muhammad kuwa ndio Mtume wa haki”

Kutoka kwa Tariq bin Shihab amesema:  1. Alikuja Myahudi mmoja kwa Omar, Mwenyezi Mungu awe radhi naye akasema: Ewe Amirul-Muuminina, katika kitabu chako kuna Aya unayoisoma.  2. Akasema Omar: Aya gani? Akasema: “Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndio Dini yenu” [Al-Maidah: 3]. 3.Akasema Omar, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi: Naijua siku ilipoteremshwa, na mahali ilipoteremshwa: Imeteremshwa kwa Mtume wa Swalla Allaahu alayhi wa sallam katika Arafah, siku ya Ijumaa .

Kutoka kwa Abu Hurayrah, (Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimfikie):“Imani ina daraja sabini na kitu, au sitini na kitu.Daraja bora zaidi ni kusema: Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki Isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja tu.Na daraja la chini kabisa ni kuondoa maudhi njiani.Na haya (aibu) ni daraja katika daraja za Imani.” Hadithi hii Imepokelewa na Imam Bukhari Na Muslimu.Imepokewa na Al-Bukhari (9) na Muslim (35),

Kutoka kwa Imran bin Huswein, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, amesemaNiliingia kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) nikamuacha ngamia wangu mlangoni.Wakamjia Mtume baadhi ya watu katika familia ya Tamim, akawaambia: “pokeeni bishara enyi familia ya Tamim.”Wakasema familia ya Tamim: Umetubashiria, basi tupe mara mbili.Kisha wakaingia baadhi ya watu wa Yemen, Mtume akasema: pokeeni Bishara enyi watu wa Yemen, kwani familia ya Tamim hawakuikubali”.Wakasema watu wa Yemen: Tumeikubali, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.Wakasema watu wa Yemen: Tumekuja kukuuliza kuhusu hili jambo (la Uislamu).Akasema Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake): “Mwenyezi Mungu alikuwepo, wakati hakuna chochote kilicho kuwepo ispokuwa yeye.Na Kiti chake cha enzi kilikuwa juu ya maji.Na akaandika katika kitabu kila kitu.Na akaumba mbingu na ardhi”.Akaita Muitaji akasema: Ngamia wako ametoweka, ewe Ibn al-Huswein, basi nikaondoka mbio nikimtafuta, Ghafla nikamuona akitokomea kwa umbali.Wallahi, nikatamani laiti ningemuacha”

Kutoka kwa Abuu Dharri, kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), aliyo yapokea kutoka kwa mola wake Mtukufu, hakika yeye amesema: “Enyi waja wangu, hakika mimi nimejiharamishia dhuluma, na nikaifanya kuwa haramu baina yenu, basi msidhulumiane.Enyi waja wangu, nyote mmepotea, ila niliye muongoza, basi niombeni uongofu, nami nitawaongoza.Enyi waja wangu, nyote mnanjaa ila niliye mpatia chakula, basi niombeni chakula, nami nitawapatieni.Enyi waja wangu, nyote mko uchi, ila niliye mvisha, basi niombeni mavazi nami nitawapatieni.Enyi waja wangu, hakika nyinyi mnakosea usiku na mchana, na mimi ninasamehe madhambi yote, basi niombeni msamaha nami nitawasamehe.Enyi waja wangu, hakika nyinyi hamuwezi kufanya juhudi za kunidhuru, mkanidhuru, na hamuwezi kufanya juhudi za kuninufaisha, mkaninufaisha.Enyi waja wangu, lau kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho kati yenu, majini na watu, wakiwa ni kama moyo wa mtu mmoja aliye mcha Mwenyezi Mungu kati yenu, hilo haliongezi katika ufalme wangu chochote.Enyi waja wangu, lau kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho kati yenu, majini na watu, wakiwa ni kama moyo wa mtu mmoja aliye muasi Mwenyezi Mungu kati yenu, hilo halipunguzi katika ufalme wangu chochote.Enyi waja wangu, lau kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho kati yenu, majini na watu, wakisimama katika uwanja mmoja, wakaniomba, nikampa kila mmjo alicho kiomba, hilo halipunguzi chochote kwa nilivyo navyo, ila ni kama kiasi cha sindano inapo ingizwa baharini. Enyi waja wangu, hayo ni matendo yenu ninayadhibiti, kisha nitawalipa. Atakae pata kheri, basi amshukuru Mwenyezi Mungu, na atakae pata kinyue asimlaumu yeyote zaidi yake mwenyewe”

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake:Hakika Mwenyezi Mungu ana majina tisini na tisa.mia moja ispokuwa moja,Mwenye kuyadhibiti ataingia Peponi.”Akaongeza katika riwaya nyingine: “hakika yeye (Mwenyezi Mungu) ni witiri anapenda witiri.” imepokelewa na Bukhari Na Muslim

Kutoka kwa Abu Musa al-Ash’ariy, (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake) alisimama na kutueleza mambo matano, akasema:“Hakika Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mtukufu, halali usingizi.Wala hahitajii kulala,Anashusha mizani na kuinyanya.Matendo yote yanayo tendeka usiku hupelekwa kwake kabla ya Matendo ya mchana, na Matendo yote yanayo tendeka mchana hupelekwa kwake kabla ya Matendo ya usiku.Kizuizi (kati yake na viumbe wake) ni Nuru - na katika riwaya: Moto.Akiondoa kizuizi hicho, Utukufu wa uso wake utachoma kila kiumbe ataefikiwa na macho yake katika viumbe wake”Related by Muslim, 179.

Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie“Malaika waliumbwa kutokana na Nuru,Majini wameumbwa kwa Moto.Adam aliumbwa kwa jinsi mlivyoelezwa”

Kutoka kwa Aisha, Mama wa waumini (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema:“Ufunuo na (wahyi) wa kwanza kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ulianza kwa kuota njozi njema usingizini, akawa kila anachokiota chochote basi kinatokea kama alivyoona usingizini.Kisha akapenda kujitenga,Na alikuwa anajitenga katika Pango la Hira, akifanya ibada masiku kadhaa, kabla ya kurudi katika familia yake, anaandaa akiba ya chakula kwa ajili yao, na kisha (akitaka kurudi kule pangoni) anaenda kwa Bi Khadija na anamuandalia akiba ya chakula (kwa kadiri ya masiku atakayokuwa akianya ibada).Mpaka akafunuliwa ufunuo (wahyi wa kwanza) akiwa ndani ya pango la Hiraa. Malaika Jibril akamjia na kusema: Soma. Akasema: “Mimi sijui kusoma”.Mtume (Rehma na Amani zimfikie) anasimulia mwenyewe kwa kusema: Basi (Malaika Jibril) akanishika na kuniminya mpaka nikachoka, kisha akaniachia na kuniambia: Soma, Nikasema: “Mimi sijui kusoma”. Kisha (Malaika Jibril) akanishika kwa mara ya pili na kuniminya mpaka nikachoka, kisha akaniachia. Na kuniambia: Soma, Nikasema: “Mimi sijui kusoma”. akanishika tena na kuniminya mpaka nikachoka, (alifanya hivyo) kwa mara ya tatu mpaka nikakosa nguvu kabisa. Kisha akaniachia na kusema: “Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba (1) Amemuumba mwanadamu kutokana na tone la damu (2) Soma! Na Mola wako Mlezi ni Mkarimu kushinda wote (3) [Al-Alaq: 1-3] (Baada ya hapo) Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimfikie) akarudi (akiwa na aya hizo za mwanzo kichwani) huku amejawa na woga, akaingia (nyumbani) kwa Bi khadija (Radhi za mwenyezi mungu zimfikie) akisema: “Nifunikeni jamaani, Nifunikeni” Wakamfunika hadi hofu ilipoisha.Mtume aka msimulia Bi Khadija kilichotokea, kisha akasema “Hakika naiogopea saana nafsi yangu”Bi Khadija akamwambia: Hapana (usiogope), Wallahi Mwenyezi Mungu hawezi kukufedhehesha.Kwani wewe Unatabia ya kuunga Udugu,Na kuwasaidia wanyonge (wasiojiweza).Na unajitolea kuwasaidia waliotingwa.Na unawakirimu wageni,Na unawasaidia watu katika kutatua matatizo.(Baada ya hapo) Bi Khadija akampeleka kwa kaka yake (mtoto wa baba mdogo wake) aliekuwa anaitwa Waraqah bin Nufal bin Asad bin Abdul Uzza, bwana huyu Alikuwa ni mnaswara (kisha akatoka na kuingia katika dini ya Nabii Mussa), na alikuwa anafahamu akuandika Kiebrania, basi akawa akiandika injili kwa lugha ya Kiebrania, na alifanya kazi hiyo muda mrefu na kuandika alichoweza kuandika, mpaka akazeeka na akapofuka macho.Khadija (alipomuendea mtu huyo) akamwambia: Ewe binamu yangu, msikilize mpwa wako (anachosema). Warqah akamwambia: Ewe mtoto wa ndugu yangu, umeona nini? Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimfikie) akamsimulia (habari za Malaika aliemtokea pangoni), Waraqah akamwambia: huyo ndio malaika (Jibril) aliemteremsha Mwenyezi Mungu kwa Nabii Mussa (Rehma na Amani zimfikie).Natamani ningelikuwa kijana zama hizo (za mtume wa mwisho), na nikawa hai wakati watu wako watakapokufukuza! (Nikashirika kukuhami).Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimfikie): “Hivi ni (kweli) Watanifukuza?” Akasema Waraqah: “Ndio, hakuna mtu yeyote aliyewahi kuja (na ujumbe) kama uliokuja nao wewe isipokuwa atafanyiwa uadui”.Na ikiwa itanidiriki siku (ya kudhiriri kwako nikiwa hai) basi nitapambana kukunusuru (hadi upate) ushindi mnono.Waraqah hakuchukua muda mrefu akawa amefariki, na wahyi ukawa umekata (kwa muda).” Imepokelewa Na Bukhari na Muslim.

Kutoka kwa Abu Musa al-Ash’ariy, (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake) alisimama na kutueleze mambo matano, akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mtukufu, halali usingizi. Wala hahitajii kulala, Anashusha mizani na kuinyanya.Matendo yote yanayo tendeka usiku hupelekwa kwake kabla ya Matendo ya mchana, na Matendo yote yanayo tendeka mchana hupelekwa kwake kabla ya Matendo ya usiku. Kizuizi (kati yake na viumbe wake) ni Nuru - na katika riwaya: Moto. Akiondoa kizuizi hicho, Utukufu wa uso wake utachoma kila kiumbe ataefikiwa na macho yake katika viumbe wake” ( Muslim (179).

kutoka kwa Ibn Abbas (r.a) amesema:“Alipewa utume Nabii Muhammad (s.a.w) Akiwa na umri wa miaka arobaini.Basi alikaa mjini makkat miaka kumi na tatu (13) akipewa ufunuo.Kisha akaamrishwa kuhama basi akahamia Madina miaka kumi.Na alikufa akiwa na umri wa miaka sitini na tatu(63)”

Kutoka kwa Al-Miqdaam bin Maadi Karb, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kwamba Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema:“Je, inawezekana kwa mtu kumpa khabari ya Hadithi kutoka kwangu akiwa ameegemea kiti chake, na akasema: Baina yetu na nyinyi kuna Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi chochote tunachokikuta humo ni halali tunaihalalisha, na tunayoyakuta ndani yake kuwa ni haramu tunayaharamisha.Aliyoharamisha Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam nayo ni haramu kwa Mwenyezi Mungu.”Kwa kauli ya Abu Daawuud: “Nimepewa Kitabu (Qur`an)  pamoja na mfano wake ”.

Kutoka kwa Abu Hurayrah (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehme na Amani zimfikie) amesema: -:Naapa kwa Yule Ambaye nafsi ya Muhammad Iko Mikononi Mwake. Hakuna hata mmoja katika Umma Huu atakae sikia ulinganizi wangu.Awe Myahudi au Mnaswara (Mkristo)Kisha akafa bila ya kuyaamini niliyotumwa nay o, isipokuwa atakuwa miongoni mwa watu wa Motoni.” Imepokewa na Muslim.

Kutoka kwa Anas bin Malik (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema:Wakati mimi na Mtume (Rehma na Amani zimshukie) tunatoka msikitini tulikutana na mtu mmoja kwenye uwanja wa msikiti, (sehemu ya mbele) akasema (yule mtu): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Qiyama ni lini?Mtume (Rehma na Amani zimshukie) akasema: “Umeandaa nini kwa ajili yake?”Mtu alikuwa huyo kana kwamba amekata tamaa.akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijajiandaa kwa funga nyingi, swala, wala sadaka.Lakini mimi nampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake.Akasema Mtume (Rehma na Amani zimshukie): «Wewe utakuwa pamoja na uwapendao (siku ya kiama)

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam."Msiwatukane Maswahaba zangu, Msiwatukane Maswahaba zangu,Naapa kwa yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, kama mmoja wenu akitoa dhahabu kama sawa na Mlima wa uhudi, basi hatafikia gao la mmoja wao, wala nusu yake.