3 - KUSUHUDIA KUWA MUHAMMAD NI MTUME WA MWENYEZI MUNGU:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ  قَالَ: «كُلُّ أُمَّتِي يَدْخُلُونَ الجَنَّةَ إِلَّا مَنْ أَبَى»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَنْ يَأْبَى؟ قَالَ: «مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أَبَى» رواه البخاري. 

Kutoka kwa Abu Hurayrah, (Mwenyezi Mungu amuwiye radhi), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani zimshukie) amesema:

1.“Watu wangu wote wataingia Peponi isipokuwa wale wakatao kataa 2.Wakasema Maswahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani atakayekataa?  3.Akasema Mtume (Rehema na Amani zimshukie): “Mwenye kunitii mimi ataingia Peponi, na mwenye kuniasi atakuwa amekataa.” Imepokewa na Al-Bukhari

Muhtasari wa Maana

Mtume (Rehma na Amani zimfikie) alibainisha wazi kuwa ummah wake wote utaingia peponi kwa Fadhila na Rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu isipokuwa wale waliokataa kuingia humo na wakagoma kuingia, nao ni waliopinga Utume wake na kukiuka Sunnah (mwenendo) wake

Miradi ya Hadithi