3 - KUSUHUDIA KUWA MUHAMMAD NI MTUME WA MWENYEZI MUNGU:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ  قَالَ: «كُلُّ أُمَّتِي يَدْخُلُونَ الجَنَّةَ إِلَّا مَنْ أَبَى»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَنْ يَأْبَى؟ قَالَ: «مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أَبَى» رواه البخاري. 

Kutoka kwa Abu Hurayrah, (Mwenyezi Mungu amuwiye radhi), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani zimshukie) amesema:

1.“Watu wangu wote wataingia Peponi isipokuwa wale wakatao kataa 2.Wakasema Maswahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani atakayekataa?  3.Akasema Mtume (Rehema na Amani zimshukie): “Mwenye kunitii mimi ataingia Peponi, na mwenye kuniasi atakuwa amekataa.” Imepokewa na Al-Bukhari

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

(“Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu”

[Al Imran: 31].

(“Na anaye tafuta dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwake, na Akhera atakuwa miongoni mwa walio khasirika.”

[Imran: 85].

Na akasema Mwenyezi Mungu: “Na mkimtii Yeye basi mtaongoka, na hakuna jukumu kwa Mtume ila kufikisha ujumbe ulio wazi.”

[An-Nur: 54].

 

“Basi wajihadhari wale wanaokwenda kinyume na amri yake, usije ukawapata mtihani au ukawapata adhabu chungu.”

[An-Nur: 63].

Na akasema Mwenyezi Mungu: “Na chochote anachokupeni Mtume basi kichukueni, na anachokukatazeni basi jizuieni na mcheni Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu”

[Al-Hashr: 7].

Miradi ya Hadithi