Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, amesema: “Qiyama kitakapokaribia, ndoto ya Mwislamu haitakua uongo. Mwenye ndoto za kweli zaidi katika nyinyi ni yule msema kweli katika mazungumzo Ndoto ya Muislamu ni sehemu moja kati ya sehemu arobaini na tano za utume. Kuna aina tatu za ndoto: ndoto njema ni habari njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Ndoto ya huzuni kutoka kwa Shetani. Na Ndoto kutokana na yale yanayompata mtu moyoni mwake. Akiona mmoja wenu jambo ambalo analichukia basi na asimame na aswali wala asiwaambie watu jambo hilo.”

Kutoka kwa Hudhayfah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Tulikuwa pamoja na Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, akasema: Ni nani kati yenu aliyemsikia Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam akitaja mitihani? Baadhi ya watu wakasema: Tulimsikia, akasema Hudhayfah: Labda mnakusudia fitna ya mtu kukhitalifiana na familia yake na jirani yake? Wakasema: Ndiyo. Akasema: Hayo huondoshwa na swala, saumu na sadaka. Lakini ni nani miongoni mwenu aliyemsikia Mtume Rehema na Amani zimshukie akitaja yale yanayopeperusha mawimbi ya bahari? Hudhaifa akasema: Basi akawanyamazisha watu wakanyamaza, nikasema: Mimi ndiye, Mtume Alisema: Wewe ndio!  Hudhayfah amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam akisema:“Majaribu yanawasilishwa kwenye nyoyo kama ukiri wa mkeka mmoja baada ya mwingine. Moyo wowote utakao ipokea fiitna, doa jeusi litawekwa ndani yake, na moyo wowote utakaoipinga, doa jeupe linapigwa ndani yake. Mpaka nyoyo zinakuwa katika aina mbili: Nyeupe kama Safa, na hakuna fitna itakayomdhuru kwa muda ambao mbingu na ardhi zitadumu. Na nyingine ni nyeusi tii kama chungu kilicho funikwa  ,haujui wema. Na wala haukemei uovu isipokuwa kwa kile ulichokunywa kutokana na matamanio yake. Hudhayfa akasema: Nikamueleza kuwa: Kuna mlango uliofungwa baina yako na fitna, unakaribia kuvunjika. Omar akasema: kuvunjika!, Umkose baba yako? ungekuwa umefunguliwa, bila shaka ungerejeshwa. Nikasema: Hapana, utavunjika. Na nikamwambia: Kwamba mlango huu ni mtu atauawa au atakufa, pasina kosa lolote

Kutoka kwa Ma’qil bin Yasar, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema: Mtume rehma na Amani zimshukie amesema: “Kuabudu wakati wa ghasia ni kama kuhama kuja kwangu”  .

Kutoka kwa Abu Said na Abu Hurara – Mwenyezi Mungu awe radhi nao – kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema: “Haimpati mwislamu uchovu, wala maradhi, wasiwasi, huzuni, maumivu, au dhiki. inayompata Mwislamu. Hata kuchomwa kwake na mwiba, ispokuwa Mwenyezi Mungu atamfutia baadhi ya dhambi zake kwa ajili yake.” 

Kutoka kwa Anas bin Malik, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume Swalla Allaahu alayhi wasallam amesema: 1- “Kila mwana wa Adamu ni mwenye dhambi. 2- Na wabora wa wakosefu ni wale wanaotubu”.

Kutoka kwa Abu Hurayra, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie.1- “Atakayekuwa na dhulma kwa ndugu yake, heshima yake au kitu chochote kile, basi na amrudishie hayo leo kabla ya siku ambayo haitakubaliwa dinari wala dirham. 2- Akiwa na kheri itachukuliwa kutoka kwake kwa kiasi cha dhulma yake, na ikiwa hana amali njema itachukuliwa baadhi ya maovu ya aliyeifanyiwa dhulma na kubebeshwa”.

Kutoka kwa Amr Ibn Al-Aas, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:1- Mwenyezi Mungu alipouweka Uislamu moyoni mwangu, nilimjia Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam na nikasema: “Kunjua mkono wako na nikupe kiapo cha utii. 2- Kisha akanyoosha mkono wake, na akasema: nikazuwia mkono wangu. Akasema Mtume: “Una nini ewe Amr? Akasema: Nikasema: Nataka kukupa sharti, akasema Mtume: “Unaweka sharti la nini?” Nikasema: kusamehewa, 3- Akasema Mtume: “Je, hujui kwamba Uislamu unafuta yaliyotangulia? 4- Na kuhama kunafutilia mbali yaliyokuwa kabla yake? 5- Na kwamba Hija inafuta yaliyotangulia kabla yake?”

Kutoka kwa Hakim bin Hizam, Allah amuwiye radhi, amesema:1- Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, unaonaje mambo niliyokuwa nikiyaahidi kabla ya Uislamu, kama vile kutoa sadaka au kuwaacha huru watumwa, kuunga udugu, je nitapata dhawabu? 2- Akasema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Umeyasilimisha yote yaliyotangulia katika kheri” ).

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma Na Amani Zimshukie) akisema: 1. “Mungu amejalia huruma katika mafungu mia moja, 2. kisha akabakiza kwake sehemu tisini na tisa (za huruma) na akateremsha ardhini sehemu moja tu. 3. Kutokana na sehemu hiyo viumbe uhurumiana, (kiasi kwamba) farasi hunyanyua kwato yake kwa mtoto wake kwa kuogopea asimkanyage) .” imepokelewa na Bukhari Na Muslim .

1- Kutoka kwa Anas bin malik radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie akisema: Mwenyezi Mungu aliyetukuka amesema: “Ewe mwana wa Adam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe kwa yale yaliyokuwa ndani yako, wala sijali. 2- Ewe Mwana Aadam hata kama dhambi zako zikifika kwenye mawingu ya mbingu, kisha ukaniomba msamaha, nitakusamehe na sitojali.  3- Ewe Mwana Aadam, kama utanijia na madhambi makubwa kama ardhi, kisha ukakutana Nami hukunishirikisha na chochote, nitakupatia msamaha sawa na ukubwa wa madhambi”