Kutoka kwa Said bin Abi Burdah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abi Musa Al-Ash’ariy Mwenyezi Mungu awe radhi nao, 1. Mtume rehma na Amani zimshukie alimtuma Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji vinavyotengenezwa huko, akasema: “Ni nini? Akasema: Al-bit’u na Al-mizru, basi nikamwambia baba Burdah: Al-bit’u ndio nini? Akasema: mchanganyo wa asali, na Al-mizru, ni mchanganyo wa shayiri. 2. Akasema: “Kila kilevi ni haramu”  

Kutoka kwa Al-Miqdam bin Ma’di Karib, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani ziwe juu yake akisema: 1. “Hakuna mwanadamu aliyejaza chombo kibaya kuliko tumbo. 2. Inamtosha mwanadamu vijitonge kadhaa vya kusimamisha uti wake wa mgongo.  3. Ikiwa haitaepukika, basi theluthi kwa chakula chake, na theluthi kwa kinywaji chake, na theluthi kwa ajili ya pumzi yake”

Kutoka kwa Jabir bin Abdullah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zumshukie aliwahutubia watu wakati wa Hija, na akasema: 1. Damu zenu na mali zenu ni tukufu kwenu, kama utukufu wa siku yenu hii, katika mwezi wenu huu, katika mji wenu huu, 2. Fahamuni ya kwamba, kila kitu kilichokuwepo zama za kabla ya Uislamu chini ya miguu yangu kimefutwa? 3. Damu ya visasi vya Jahiliyyah zimefutwa, na damu ya kwanza kuifutilia mbali ni katika damu yetu ilikuwa ni damu ya Ibn Rabi`ah Ibn al-Harith. Alikuwa amelala kitandani huko kwa Bani Sa'd, na Hazal akamuua. 4. Riba ya Jaahiliyyah imefutwa, na riba ya kwanza ninayoifuta ni Riba ya Abbas bin Abdul Muttalib, hakika yote imefutwa. 5. Basi mcheni Mwenyezi Mungu kwa wanawake. Mliwachukua kwa amana ya Mwenyezi Mungu, na mkahalalishiwa sehemu zao za siri kwa neno la Mwenyezi Mungu. 6. Ni wajibu kwa wao kwamba mtu yeyote asikanyage tandiko lenu. Wakifanya hivyo basi wapigeni si kwa ukali. Na ni wajibu kwenu chakula chao na kuwavisha kwa wema. 7. Nimewaachieni kitu ambacho nyinyi hamtapotea baada ya hayo, ikiwa mtashikamana nacho; nacho ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Na ninyi mtaulizwa kuhusu mimi mtasemaje? Maswahaba Wakasema: Tunashuhudia kwamba umewasilisha, umetekeleza, na umetoa ushauri. Naye akasema Kwa kidole chake cha shahada, huku akikiinua mbinguni na kukielekeza kwa watu: "Ee Mwenyezi Mungu shuhudia, Ee Mungu shuhudia" mara tatu

Kutoka kwa Abdullah bin Amr – Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili – kutoka kwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, amesema: 1. “Muislamu ni yule ambaye Waislamu wamesalimika kutokana na ulimi wake na mikono yake.  2.  Muhajir ni yule anayeyaaacha aliyoharamisha Mwenyezi Mungu.”

Kwa kutoka kwa Abu Huraira, Allah amuwiye radhi, amesema: 1. Alikuja mtu kwa Mtume rehma na amani zimshukie na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni nani katika watu anastahiki zaidi usuhuba wangu? 2. Akasema Mtume: (Mama yako) Akasema: Kisha nani? Akasema: (Mama yako), akasema: Kisha nani? Akasema: (mama yako) 3. Akasema: Kisha nani? Akasema Mtume: (Baba yako), na katika riwaya akasema: (Mama yako, kisha mama yako, kisha mama yako, kisha baba yako, 4. Kisha anafuatia aliye karibu yako”

 Kutoka kwa Ibn Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, amesema: Mtume rehma na amani ziwe juu yake amesema: “Jibril alikuwa akiniusia kuhusu jirani mpaka nikadhania kuwa atakuwa miongoni mwa warithi

Kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume rehma na amani zimshukie amesema: “Hatokuwa na imani yeyote miongoni mwenu mpaka ampendelee nduguye kile anachojipendelea” 

Kutoka kwa Nu’man ibn Bashir Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema: Amesema Mtume rehma na Amani zimfikie: “Mfano wa Waumini, katika mapenzi yao, rehema, na upole, ni kama mwili mmoja  Ikiwa kiungo kimoja kitapata kasoro juu yake, sehemu nyingine yote ya mwili inakabiliwa maumivu na kukesha na homa

Kwa kutoka kwa Jarir bin Abdullah Mwenyezi Mungu awe radhi naye kutoka kwa Mtume, rehma na Amani zimshukie, amesema: “Asiye na huruma hatahurumiwa” 

Kutoka kwa Abdullah bin Omar – Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili – kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake amesema: “Si haki ya Muislamu mwenye kitu cha kuweza kuusia. Anakaa siku mbili bila wasia wake kuandikwa pamoja naye.”

Kutoka kwa Abd al-Rahman bin Samra, amesema: Amesema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: 1- “Ewe Abd al-Rahman ibn Samra, usigombee kuwa kiongozi. 2- Ukipewa uongozi kwa kugombea na ukikabidhiwa utatelekezewa. 3- Na ukipewa bila ya kuomba, utasaidiwa tu. 4- Na ukiapa kiapo na ukaona bora kuliko hicho basi toa kafara ya kiapo kisha ufanye hilo lililo bora zaidi”  

Kutoka kwa Ibn Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kwamba Mtume, amani iwe juu yake, amesema:  1- “Muislamu lazima asikilize amri ya Kiongozi na atii   2- Katika yale anayoyapenda na kuyachukia;  3- Isipokuwa Uasi, basi ikiwa ataamrishwa kutenda dhambi, hapo hatakiwi kusikiliza wala kutii amri”

Kutoka kwa Ubaada bin As-Samit, Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema:1- Niliweka kiapo cha utii kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie, nikiwa katika kundi, na akasema: “Naweka kiapo cha utii kwenu kwa sharti kwamba msimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu chochote, msiibe, msizini, msiwaue watoto wenu. Wala msije na uwongo mnao uzua baina ya mikono yenu na miguu yenu, wala msiniasi kwa wema. 2- Na atakaye tekeleza hayo miongoni mwenu, basi ujira wake uko kwa Mwenyezi Mungu, na likimpata lolote katika hayo basi nitamuhukumu hapahapa duniani. Kufanya hivyo ndio kafara yake na inamtakasa. Na yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atamfichia siri, basi hukumu yake ni kwa Mwenyezi Mungu. Akitaka atamuadhibu, na akipenda atamsamehe”  

Kutoka kwa Abu Yahya Suhaib bin Sinan, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie.1- “Ni la kustaajabisha jambo la Muumini, kwani mambo yake yote ni kheri, na hayo si ya kila mtu isipokuwa kwa Muumini peke yake.  2- Ikimpata kheri hushukuru, na inakuwa ni kheri kwake. 3- Na yakimpata matatizo husubiri, na inakuwa ni kheri kwake.” .

Kutoka kwa Abdullah bin Masoud Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka kwa Mtume, rehma na Amani zimshukie, ambaye amesema:1- “kuweni wakweli, kwani ukweli humpeleka mtu kwenye wema, na wema humwongoza mtu kwenye Pepo, Na mtu huendelea kusema ukweli na kujitahidi kuwa mkweli mpaka aandikishwe kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli.  2- Na mwache kusema uongo, kwani uongo humpeleka mtu kwenye uovu, na uovu humwongoza mtu kwenye moto, na mtu huendelea kusema uongo na kujitahidi katika uongo mpaka, anaandikwa kwa Mwenyezi mungu kuwa ni mwongo.

Kutoka kwa Abu Masoud, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema Mtume rehma na Amani zimshukie: “Katika maneno ya bishara ya utume waliyoyapata watu ni: Ikiwa hauna haya, basi fanya chochote unachotaka”

Kutoka kwa Abu Shuraih al-Kaabi, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume, rehma na amani zimshukie, amesema: 1- “Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi amkirimu jirani yake. 2- Na anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi amkirimu mgeni wake stahiki zake.” Akasema swahaba wa Mtume: Na stahiki zake ni nini, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Mchana mmoja na usiku mmoja, na ugeni ni siku tatu, tofauti na hayo ni sadaka juu yake” 3- Na anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi na aseme mema au anyamaze” .

Kutoka kwa Shaddad bin Aws, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: “Mambo mawili niliyohifadhi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, swala na salamu zimshukie, amesema:1- “Hakika Mwenyezi Mungu amejaalia wema juu ya kila kitu. 2- Ukiua, basi lifanye hilo kwa uzuri zaidi. 3- Na mnapochinja basi mchinje vizuri, na mmoja wenu aunoe vizuri upanga wake, na apumzishe kichinjwa chake”

Kutoka kwa Abu Said na Abu Huraira, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimshukie): 1. “Utukufu ni vazi lake, 2. Kiburi ni shuka lake, 3. Basi mwenye kuninyang’anya vazi hilo nitamuadhibu.”

Kutoka kwa Abu Hurairah Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema:1- Mtu mmoja alimwambia Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Ninasihi. 2- Akasema Mtume: “Usikasirike” 3- Mtume alirudia mara kadhaa akisema: “Usikasirike”