Kutoka kwa Anas bin Malik, ambaye amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie.1. “Pepo imezungukwa na yanayo chukiza. 2. Moto umezungukwa na matamanio”.

Kutoka kwa Sufyan bin Abdullah Al Thaqafi, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema:1- Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu niambie kitu katika Uislamu ambacho sitamuuliza yeyote baada yako - na katika Hadithi ya Abu Usama: asiyekuwa wewe. 2- Akasema Mtume: “Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo”.

Kutoka kwa Abu Barzah Al-Aslamiy, ambaye amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wasallam: 1- “Mja hatatembea kusogea mbele Siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe 2- Kuhusu umri wake: Aliumaliza vipi? 3- Ujuzi wake: alifanya nini? 4- Kuhusu pesa zake alizipata wapi? Na Alizitumia katika lipi? 5- Na kuhusu mwili wake: aliuchoshaje? .

Kutoka kwa Nuuman bin Bashir – Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili – amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimshukie) akisema – na al-Nu’man aliashiria kwa  vidole vyake kwenye masikio yake: 1. “Halali iko wazi, na haramu iko wazi. 2. Na kati ya halali na haramu kuna mkanganyiko ambao si watu wengi wanao ufahamu. 3. Basi mwenye kujiepusha na mashaka atakuwa ameitakasa dhamira na heshima yake ya kidini. 4. Na anayeingia katika mashaka huanguka katika haramu kama mchungaji anayechunga wanyama wake pembezoni mwa ngome, inakuwa ni karibu zaidi kulisha katika mazao. 5. Hakika kila Mfalme ana ngome na ulinzi, na hakika ngome ya Mwenyezi Mungu ni mambo yaliyo haramu. 6. Hakika ndani ya mwili kuna mnofu wa nyama, ukiwa mzuri mnofu huo, basi mwili wote ni mzuri, na ukiharibika mnofu huo mwili wote umeharibika, sasa mnofu huo ndio moyo”

Kutoka kwa Abdullah bin Umar, Allah amuwiye radhi, ambaye amesema:1- Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinishika bega na kusema: “Kuwa katika dunia hii kama kwamba wewe ni mgeni. 2- Au mpita njia, 3- Ibn Umar alikuwa akisema: “Ikifika jioni, usisubiri asubuhi, na ukiamka asubuhi, usisubiri jioni. 4- Chukua kutoka kwenye afya yako yatakayo kunufaisha utakapo ugua, 5- Na Chukua kutoka kwenye uhai wako yatakayo kufaa wakati wa kufa kwako”

Kutoka kwa muawiyah (r.a) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake:1. “Mwenyezi Mungu anapomtakia kheri mja humpa ufahamu katika dini 2. Na hakika si vinginevyo, mimi ni mgawaji, na Mwenyezi Mungu ndio anaetoa 3. Na hautoacha kuendelea huu ummati Muhammad (s.a.w) ukisimama juu ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu, hawawadhuru watakao kwenda kinyume nao, mpaka itakuja amri ya Mwenyezi Mungu” .

Kutoka kwa Abuu Dar-Dai (r.a) amesema: nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake akisema:1. “Mwenye kupita njia akitafuta elimu katika njia hiyo, Mwenyezi Mungu humfanyia wepesi zaidi njia ya kwenda peponi. 2. Na hakika malaika naapa kwa Allah wanaweka mbawa zao kumridhia mtafuta elimu,  3. Na hakika mwenye kutafuta elimu wanamuombea msamaha viumbe wa mbinguni na ardhini, hata pia samaki katika maji. 4. Na hakika ubora wa mwanazuoni kwa waja wa Mwenyezi Mungu ni kama ubora wa mwezi juu ya nyota zote. 5. Na hakika wanazuoni ndio warithi wa mitume wa Mwenyezi Mungu mtukufu, na hakika mitume wa Allah hawakurithiwa dinari wala dir-ham; bali si vinginevyo walirithiwa elimu, basi atakeichukuwa atakua amechukua fungu kubwa sana. 

Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash-Ariyy (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema,1. Mfano wa aliyonituma kwayo Allah (s.w) miongoni mwa uongofu na elimu, ni kama mfano wa mvua nyingi iliyonyesha katika Ardhi Fulani, 2. Ikawa Ardhi hiyo ni safi ikapokea maji na kuotesha mazao na mimea. 3. Na ikawa sehemu nyingine ni kavu ikapokea maji, na Mwenyezi Mungu akawanufaisha watu kwa mvua hiyo wakanywa na wakanywesheleza mifugo na wakalima mazao. 4. Na ikanyesha sehemu nyingine ya ardhi, hakika sehemuhiyo ni jangwa halihifadhi maji na wala halioteshi mimea  5. Basi huo ni mfano  wa mtu aliopewa utambuzi katika dini na mwenyezimungu akamnufaisha na yale aliyonitumanayo kwayo, akayatambua na akawaelimisha watu wengine,na mfano wa Yule ambaye  hakuyapa kipaumbele wala hakukubali mwongozo wa mwenyezimungu ambao nimetumwa kwao.(Imepokelewa na Imam Bukhari na Muslimu).

Kutoka kwa Abdullah bin Amr, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kwamba Mtume, rehma na amani zimshukie, amesema:1- “Fikisha kwa niaba yangu hata ikiwa ni Aya. 2- Na simulieni kwa niaba ya Wana wa Israili, wala hakuna ubaya ndani yake. 3- Na mwenye kunisingizia uwongo kwa makusudi basi na ajiandalie makao yake Motoni.” 

Kutoka kwa Zaid ibn Thabit radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani ziwe juu yake akisema: 1. Mwenyezi Mungu amnawirishe mtu yeyote atakaesikia maneno kutoka kwetu, na akayahifadhi kwa ajili ya kuwafikishia watu wengine; 2. Basi huwenda msikilizaji (aliehifadhi vizuri) akawa sio mjuzi zaidi lakini kwa kuhifadhi kwake akawafikishia wengine ambao ni wajuzi zaidi katika kutohoa hukumu za kisheria kuliko yeye. . Na huwenda msikilizaji akawa sio msomi zaidi 

kutoka kwa Amru Ibun Al-a’swi (r.a), hakika yeye alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake akisema:1. “Atakapo hukumu hakimu na akajitahidi, kisha akapatia, basi anamalipo mara mbili. 2. Na atakapo hukumu na akajitahidi, kisha akakosea, basi anamalipo mara moja”

Kutoka kwa Al-Irbaadh bin Sariya, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:1- Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie alisimama kati yetu siku moja na kutuhutubia hotuba fasaha iliyozifanya nyoyo zitetemeke na macho kutoa machozi. 2- Ikasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mawaidha yako ni mawaidha ya kuaga, basi tuusie . 3- Akasema: “Juu yenu kumcha Allah. 4- Kusikia na kutii, hata kama mtumwa wa Kihabeshi. 5- Na mtaona ikhitilafu kali baada yangu. Ni lazima kushikamana na Sunnah zangu, na Sunnah za Makhalifa walioongoka, mzing’ang’anie kwa magego . 6- Jihadharini na mambo mapya yaliyozushwa. Kwani kila uzushi ni upotofu.” 

Kutoka kwa Umar bin Al-Khattab, (r.a) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.).1. Hakika matendo huhesabika kwa nia tu. 2. Na hakika kila mtu atalipwa kwa alilokusudia. 3. Basi atakaekuwa kuhama kwake ni kwa ajili Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi kuhama kwake ni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. 4. Na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya dunia ili aipate, au mwanamke ili amuoe, basi kuhama kwake ni lile aliloliendea.” (Imepokelewa na Imam Bukhari na Muslimu).

Kutoka kwa Abu Musa Al-Ash’ariy, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake amesema: 1- “Nyumba ambayo anatajwa Mwenyezi Mungu ndani yake, na nyumba asiyotajwa Mwenyezi Mungu ni kama walio hai na wafu. Na katika sahihi al-Bukhari: 2- “Mfano wa mwenye kumtaja Mola wake Mlezi na yule asiyemtaja Mola wake Mlezi ni kama aliye hai na maiti.” 

Kutoka kwa Abdullah bin Busr Mwenyezi Mungu awe radhi naye. 1- Kwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika sheria za Kiislamu zimekuwa nyingi, basi niambie jambo moja nishikamane nalo . 2- Akasema: “Ulimi wako uendelee kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu.

Kutoka kwa Shaddad bin Aws Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka Kwa Mtume rehma na amani zimshukie, amesema: 1- “Bwana wa kuomba msamaha ni kusema: Ewe Mola Mlezi, wewe ni Mola wangu, hapana mungu ila Wewe, umeniumba na mimi ni mja wako. 2- Na ninatimiza ahadi yako kwa kadri ya uwezo wangu. 3- Najikinga Kwako kutokana na shari ya niliyoyafanya. 4- Ninakiri neema yako juu yangu, na ninakiri dhambi yangu kwako. 5- Basi nisamehe; kwani hakuna anayesamehe dhambi ila wewe." 6- Akasema: “Na mwenye kusema hayo mchana akiwa na yakini nayo, basi akafariki mchana huo kabla ya kuingia jioni, bila shaka atakuwa ni katika watu wa Peponi” 

Kutoka kwa Abu Abd al-Rahman al-Sulamiy, kutoka kwa Uthman bin Affan, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake amesema: 1. “Mbora wenu ni yule mwenye kujifunza na kufundisha Qur’an”.2. Na Abu Abd al-Rahman alisoma zama za utawala wa Uthman, mpaka alipokuwa haji. 3. Akasema: Na Jambo hili la kusomesha ndio limenifanya nikae kitako hapa.  

Kutoka kwa Abu Said bin Al-Mu’alla, Mwenyezi Mungu amuwiye Radhi amesema: 1- Nilikuwa nikiswali msikitini, akaniita Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie lakini sikumjibu. 2- Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nilikuwa naswali. 3- Akasema Mtume: “Je, Mwenyezi Mungu hakusema: Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuiteni kwenye yale yanayokuhuisheni” [Al-Anfal: 24]. 4- Kisha akaniambia: “Nitakufundisha Sura, ambayo ni Sura kubwa kabisa katika Qur’ani, kabla hujatoka msikitini.” 5- Kisha akanishika mkono, na alipotaka kutoka, nilimwambia: “Je, hukusema: Nitakufundisha Sura, ambayo ni Sura kubwa kabisa katika Qur’ani” 6- Akasema: “Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote” [Al-Fatihah: 2], ambazo ni Aya saba zinazorudiwa, na Qur’ani kubwa Tukufu niliyopewa”. 

Kutoka kwa Ubay bin Ka’b radhi za mwenyzi mungu ziwe juu yake amesema: 1- Alisema Mtume (Rehme na Amani zimfikie) :“Ewe Baba  Mundhir, je, unajua ni Aya gani katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu iliyo kubwa kwako?” 2- Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi. 3- Akasema: “ewe Baba Mundhir, unajua ni aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu iliyo kubwa kwako?” 4- Nikasema: (Mwenyezi Mungu, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ispokuwa yeye, Aliye Hai, msimamizi wa kila jambo) (na hii ni aya ya 225 sura ya pili yaan ayutul kursiyu). 5-(Mtume) Alipiga kifua changu, 6- Na akasema: “Wallahi elimu itulizane kwako, ewe Baba Mundhir.” 

Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, aliwaambia maswahaba zake: 1- Je, mmoja wenu anashindwa kusoma theluthi ya Qur-aan katika usiku mmoja? 2- ikawa ngumu kwao, wakasema: Ni nani anaweza kufanya hivyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? 3- Akasema: “Qul Huwa Allah ahd, Allah Alssamad (yaani suratul ikhlaas yenye maana ya) Mwenyezi Mungu ni Mmoja, Mwenyezi Mungu ndio Mkusudiwa.) ni theluthi ya Qur’ani.