Kutoka kwa Imran bin Huswaein, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie.““Umma Bora ni karne yangu.Kisha wale wanaowafuataKisha wale wanaowafuataImran akasema: Sijui alitaja karne mbili au tatu baada ya kizazi chake? -Kisha kutakuwa na watu baada yenu ambao watashuhudia lakini hawatauawa kishahidi.Wanafanya khiyana na hawaaminiki.Wanaweka nadhiri lakini hawazitimizi.Unene na vitambi vitadhihiri kwao

Kutoka kwa Anas bin Malik Mwenyezi Mungu awe radhi naye kwamba Mtume Rehma na Amani zimshukie amesema:“Anapowekwa mja kaburini mwake na wakageuka na kuondoka Ndugu zake, na akasikia mchakato wa viatu vyao vikigonga.Watamuijia Malaika wawili, watamkalisha, na watamuuliza: Unasemaje kuhusu mtu huyu, yaani Muhammad Rehma na Amani zimshukie?Atasema Muumini: Nashuhudia kwamba yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hapo ataambiwa: Tazama makazi yako ya motoni, Mwenyezi Mungu amekubadilishia kwa kukupa makazi mazuri peponi, akasema Mtume Rehma na Amani zimshukie: ataonyeshwa makazi yote mawili.Lakini kafiri - au mnafiki - atasema: Mimi sijui, nilikuwa nikisema yale waliyoyasema watu.Ataambiwa: Hukujua wala hukusoma.Kisha atapigwa nyundo ya chuma baina ya masikio yake, na atapiga ukelele utakaosikika kwa wanaomfuatia isipokuwa watu na majini.”

Kutoka kwa Abu Hurayrah Mwenyezi Mungu amuwiye radhi amesema: Amesema Mtume Rehma na Amani zimshukie:“Hakitakuja kiyama mpaka Elimu iondolewe.Na matetemeko ya ardhi yaongezeke.Na wakati uwe mfinyo.Na ugomvi –fitna- zitadhihiri.Kuongezeka Machafuko - ambayo ni mauaji, kuuwana -Na kuongezeka mali na zitakuwa nyingi”

Kutoka kwa Abu Hurayrah Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesimulia kutoka kwa Mtume Rehma na Amani zimshukie amesema:“Harakisheni kutenda matendo mema kabla ya kudhihiri mambo sita: Kuonekana Masihi DajjalKudhihiri Moshi,Kutokea Mnyama katika dunia,Jua Kuchomoza kutoka magharibi.Amri ya watu wote,Kifo cha mmoja wenu

Kutoka kwa Anas Mwenyezi Mungu awe eradhi naye amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie:“Hakutumwa Nabii ila aliwaonya watu wake kutokana na mwongo wenye jicho moja.Fahamu kuwa ni mwenye jicho mojaNa Mola wako Mlezi si mwenye jicho moja.Na baina ya macho yake imeandikwa neno “kafiri”

Kutoka kwa Abu Hurayrah-Mwenyezi Mungu amuwiye radhi - kwamba Mtume Rehma na Amani ziwe juu yake amesema:Kiyama hakitasimama mpaka jua lichomoze kutoka magharibi.Litakapo chomoza kutoka magharibi watu wote wataamini kwa pamoja.Siku hiyo: “kuamini hakutomfaa mtu chochote, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake”. [Al-An’am: 158]

Kutoka Kwa Adiy Ibn Hatim Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani ziwe juu yake amesema:"Hakuna yeyote kati yenu isipokuwa atazungumza na Mola wake, bila ya kuwepo mkalimani kati yao.Mwanadamu ataangalia upande wake wa kulia, hataona chochote isipokuwa matendo yake, na ataangalia upande wake wa kushoto, hataona chochote isipokuwa matendo yake, na atatizama mbele yake na hataona kitu isipokuwa moto.Jihadharini na moto, hata kwa kukitoa sadaka kipande cha tende.Basi asiyeipata atoe sadaka hata kwa neno jema”

Kutoka kwa Abu Hurayrah radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie kwamba Mtume Rehma na Amani zimshukie amesema: “Huu moto wenu anao uwasha mwana wa Adam ni sehemu moja katika sehemu sabini za joto la Jahannamu. Wakasema: ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Wallahi, huu moto wa Duniani ulikuwa unatosha kabisa kwa kuadhibu  kutokana na ukali wake,  Akasema: “Hakika moto wa Jahannamu ukali wake umeongezwa juu yake sehemu sitini na tisa, na kila sehemu moja ni sawa na joto la moto wa dunia nzima.”

Kutoka kwa Abu Hurayrah, radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie amesema: Mwenyezi Mungu amesema: “Nimewaandalia Waja wangu wema yale ambayo jicho halijaona, Hakuna sikio lililosikia, Haijatokea kwenye moyo wa mwanadamu. Someni maneno ya Mwenyezi Mungu: “Basi hakuna nafsi yoyote inayojua waliyo tunziwa na kufichiwa katika faraja na tulizo la macho yao” [Al-Sajdah: 17].

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake):  1- “Mwenyezi Mungu alipomaliza kuumba, aliandika katika Kitabu chake. 2- Kilichopo katika kiti chake cha enzi. 3- Huruma yangu imeishinda hasira yangu”

Kutoka kwa Abdullah bun Masood, amesema: alitwambia Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) – na yeye ndiye mkweli anae kubalika - 1.Hakika mmoja wenu hukaa katika tumbo la mama yake siku arobaini, kisha anakuwa pande la damu kwa siku nyinge kama hizo, kisha anakuwa pande la nyama kwa siku nyingine kama hizo 2.Kisha Mwenyezi Mungu anamtuma malaika kwa ajili ya mambo manne, aandike matendo yake, kifo chake, riziki yake na atakuwa mwema au muovu 3.Kisha anapuliziwa roho. 4.Kwa hakika mtu anaweza kufanya matendo ya watu wa Motoni mpaka inabaki baina yake na kuingia Motoni kiasi cha dhiraa urefu wa mkono kutoka kwenye kiganja mpaka kwenye kiwiko, mipango ya Mwenyezi Mungu inamtangulia, anatenda matendo ya watu wa Peponi, aningia Peponi. 5.Na hakika mtu anaweza kufanya matendo ya watu wa Peponi mpaka inabaki baina yake na kuingia Peponi kiasi cha dhiraa, mipango ya mwenyezi mungu inamtangulia, anatenda matendo ya watu wa Motoni, anaingia Motoni” imepokelewa na Bukhari Na Muslimu.

Kutoka kwa Ibn wa Abbaas (Radhi za Mwenyezi ziwe juu yake), amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema: 1. “Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno (haya): 2. Mhifadhi Mwenyezi Mungu 3. Ili naye akuhifadhi 4. Muhifadhi Mwenyezi Mungu utampata mbele yako (kwa kila jambo lako) 5. Pindi utakapo omba, muombe Mwenyezi Mungu 6. Na ukitaka msaada basi taka msaada  kwa Mwenyezi Mungu 7. Tambua kwamba jamii ikikubaliana kukusaidia kwa lolote, haiwezi kukusaidia ila jambo ambalo Mwenyezi Mungu amekuandikia, na lau ikikubaliana ikudhuru kwa lolote, haiwezi kukudhuru ila kwa jambo ambalo Mwenyezi Mungu amekuandikia. 8. Kalamu imesha nyanyuliwa na karatasi zimesha kauka.  

1.Kutoka wa Abuu Hurairah, amesema: amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake):  “Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, 2..Na wote wana kheri 3.Pupia jambo lenye kukunufaisha, 4.Na umuombe Mwenyezi Mungu msaada, 5.Jambo lolote likikusibu, usiseme: lau ningefanya hivi na hivi, 6.Badala yake sema: Ni mipango ni ya Mwenyezi Mungu, anafanya atakalo 7.Kwa sababu (lau) inafungua kazi ya shetani”

Kutoka kwa anas bun maali (Radhi za Mwenyezi ziwe juu yake), Kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), amesema: 1. “Hakuna a’d-waa, yaani maambukizi 2. Wala twiyara, yaani kuitakidi mikosi 3. Na ninafurahishwa fa-lu” wakasema: fa-lu ni nini? Akasema: “ni neno zuri” imepokelewa na Bukhari Na Muslimu

Kutoka kwa Abu Hurairah, amesema: amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake) Tizameni walio chini yenu, 1- Na wala msitizame walio juu yenu 2- Kufanya hivyo ni sababu bora ya kuwafanya msizidharau neema za Mwenyezi Mungu kwenu ”

Kutoka kwa Abdullah bin Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimshukie) amesema: 1-    “Funguo za ghaibu ni tano anazozijua Mwenyezi Mungu pekee. 2.Mungu pekee ndiye anayejua kitakachotokea kesho. 3.Hakuna ajuaye kubadilisha matumbo ya uzazi isipokuwa Mwenyezi Mungu. 4.Hakuna ajuaye ni lini mvua itakuja ila Mwenyezi Mungu. 5.Na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani. 6.Hakuna ajuaye Qiyama itakuja lini ila Mwenyezi Mungu. 

Kutoka kwa Abu Hurayrah Mwenyezi Mungu awe radhi naye kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani zimshukie) amesema: “Mwenye kwenda kwa mtabiri au kohani na akaamini anayoyasema, Amekufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammad, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani.”

Kutoka kwa Abu Hurayrah – Mwenyezi Mungu amuwiye radhi – ambaye amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam: 1. “Mwenyezi Mungu haangalii miili yenu wala sura zenu; 2.Lakini Yeye anazitazama nyoyo zenu. Na akaelekeza vidole vyake kwenye kifua chake

Kutoka kwa Anasi (r.a), kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema: 1. “Mambo matatu yakiwepo kwa mtu atapata ladha ya imani. 2.Ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake ndio wanapendeza kwake zaidi kuliko wasiokuwa hao 3.Na kumpenda mtu na asimpende isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. 4. Na achukie kurudi kwenye ukafiri kama anavyo chukia kutupwa motoni”.

Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kwamba Mtume Rehma na Amani zimshukie amesema: 1- “Mtafuata njia za waliotangulia kabla yenu. 2- hatua kwa hatua, dhiraa kwa dhiraa, 3- Hata kama wangeingia kwenye shimo la mburukenge, nanyi mngaliingia.” 4- Tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni Mayahudi na Wakristo? Akasema Mtume Rehma na Amani zimshukie: "basi ni nani kama sio hao?!