Kutoka kwa Abuu Hurairah, hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake) amesema: “Jitahidini kufanya matendo mema, kwa sabubu kuna fitina kama kiza cha usiku totoro, Mtu anaamka akiwa ni muumini, jioni anakuwa kafiri, au jioni anakuwa ni muumini, asubuhi kafiri, Anaiuza dini yake kwa mapambo ya Dunia.
Kutoka kwa Mahmood bin Labiid amesema: amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake): 1. “Hakika ninalo ogopea kwenu zaidi ni shirki ndogo” 2. Wakasema: shirki ndogo ni nini eh Mtume wa Mwenyezi Mungu? 3. Akasema: ni riya yaani kufanya kwa kujionesha 4. Mwenyezi Mungu Mtukufu atawambia siku ya kiyama baada ya watu kulipwa kwa matendo yao: 5. “Nendeni kwa mlio kuwa mnajionesha kwao, muone je watakulipeni?!”
Kutoka kwa Abdullah bun Amri, kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), amesema: 1. “Mambo manne anaye kuwa nayo anakuwa ni mnafiki halisi, na anaye kuwa na moja wapo, anakuwa na sifa ya kinafiki mpaka ayaache; 2.Anapo aminiwa, anafanya hiyana 3.Anapo ongea hudanganya 4.Anapo ahidi, husaliti 5.Anapo kosana na mtu, anavuka mipaka.
Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie: “Mwenye kuzua katika jambo letu hili lisilokuwa ndani yake, litakataliwa.”
Kutoka kwa Abu Hurayrah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, amesema:1- “Dini ni rahisi, 2- Hakuna atakayeifanya dini kuwa ngumu ila itamshinda. 3- Basi semeni kweli na muwaite watu karibu. 4- Na toeni bishara njema. 5- Na tafuteni msaada asubuhi na mchana na nyakati za usiku.” .
Kutoka kwa Talha bin Ubaydillah Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yakeamesema: 1- Alikuja mtu mmoja katika watu wa Najd kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake), Sauti yake inasikika, lakini haeleweki anachosema, mpaka akakaribia, kumbe anauliza kuhusu Uislamu 2- Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake): "Swala tano kwa mchana na usiku", akasema: Je, ni lazima nifanye jambo lingine? Akasema: “Hapana, isipokuwa ukijitolea”. 3- Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake): "Na Saumu ya Ramadhani", akasema: Je, ni lazima nifanye jambo lingine? akasema: “Hapana, isipokuwa ukijitolea”. 4- (Talha bin Ubaydillah ) Akasema: Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake), akamtajia Zaka, akasema: Je, ni lazima nifanye jambo lingine? akasema: Hapana, isipokuwa ukijitolea. 5- (Talha bin Ubaydillah ) Akasema: Basi yule mtu akageuka na kusema: Wallahi siwezi kuongeza wala kupunguza katika haya. 6- Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake): "Atafaulu ikiwa ni mkweli." Na katika riwaya nyingine: “Ataingia Peponi ikiwa anasema kweli.
Kutoka kwa Aisha, (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake) amesema: 1- “Mambo kumi ni ya kimaumbile” 2- Kukata masharubu, 3- kuacha ndevu zikue, 4- Kupiga mswaki, 5- Kupandisha maji puani, 6- Kukata kucha, 7- Kuosha nafasi za vidole. 8- kunyofoa nywele za kwapa, 9- Kunyoa sehemu za siri 10- Kustanji”. 11- Musab akasema: Nimesahau la kumi ila nahisi ni kusukutua kinywa .
Kutoka kwa Abu Hurayrah, Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: 1.mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani ziwe juu yake) akasema: “ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi husafari safari za baharini, na katika safari zetu hubeba maji machache, ikiwa tutayatumia kupata udhu basi tutapata kiu – kwa kukosa maji ya kunywa- je inafaa tupate udhu kwa maji ya bahari? 2. akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: “maji yake ni twahara”. 3. na kilichofia baharini ni halali"
Kutoka kwa Humran, mawlaa wa Uthman,1- Amesimlia kwamba Othman bin Affan, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, aliomba maji ya kutawadha, na akatawadha, akaosha vitanga vyake viwili vya mikono mara tatu, kisha akaweka maji mdomoni mwake na kupandisha maji katika pua yake, kisha akaosha uso wake mara tatu, Kisha akaosha mkono wake wa kulia hadi kwenye kiwiko mara tatu, kisha akaosha mkono wake wa kushoto vivyo hivyo, kisha akapangusa kichwa chake, Kisha akaosha mguu wake wa kulia hadi vifundoni mara tatu, kisha akauosha wa kushoto vivyo hivyo.2- Kisha akasema: Nilimuona Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anatawadha kama mimi.3- Kisha akasema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Mwenye kutawadha kama udhuu wangu huu, kisha akasimama na kusali rakaa mbili ambazo haongei nafsini mwake, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”4- Na Muslim akaongeza katika riwaya: “Na itakuwa swala yake na kutembea kwake kuelekea msikitini ni ibada” .
Kutoka kwa Ammar bin Yasir, Mungu amuwiye radhi, amesema:1- Mtume wa Mwenyezi Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) alinituma katika jukumu fulani, nikapatwa na janaba, lakini sikupata maji, nikajibiringisha katika mchanga kama mnyama, kisha nikaenda kwa Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) nikamsimulia tukio hilo. 2- Akasema: “hakika ilikuwa inatosha kufanya kwa mikono yako hivi” kisha akapiga ardhi kwa mikono yake mpigo mmoja, kisha akapangusa mkono wa kulia kwa mkono wa kushoto, na mkono wa kushoto kwa mkono wa kulia, na nje ya viganja vyake, na uso wake.
kutoka kwa Jabir bin Abdillah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, amesema: “Nimemsikia Mtume Rehema na Amani zimshukie akisema: “Baina ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha Swalah” .
Kutoka kwa Abu Sulaiman Malik bin Al-Huwairith, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, amesema: 1. Tulikuja kwa Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) tukiwa vijana tukikaribiana, tukakaa kwake siku ishirini, akadhani tumetamani familia zetu, akatuuliza kuhusu tuliowaacha katika familia zetu, tukamwambia. 2. na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) Alikuwa ni mpole mwenye huruma, akasema: “Rudini kwa ahali zenu. 3. Wafundisheni na waelekezeni. 4. na swalini kama mlivyoniona nikiswali, 5. Na ukifika wakati wa Swala, mmoja wenu aadhini, kisha awaongoze mkubwa wenu”
Kutoka kwa Abu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesimulia kuwa: 1. siku moja Mtume aliingia Msikitini, akaingia mtu fulani akaswali, kisha akamsalimia Mtume Rehema na Amani zimshukie, akajibu salamu na kusema: “Rudi ukaswali kwani hukuswali.” 2. Akarudi akaswali vile alivyoswali mwanzoni, kisha akaja akamsalimia Mtume (saw), akasema: “Rudi ukaswali kwani hukuswali.” Mara tatu, akasema Mtu yule: “Naapa kwa yule aliyekutuma kwa haki, mimi sifahamu kufanya vizuri kuliko hivi, basi naomba unifundishe. 3. Akasema Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) : “ukisimama kwa ajili ya Swala, basi toa takbira. 4. kisha soma aya nyepesi kwako katika Qur’ani . 5. Kisha rukuu mpaka utulizane katika rukuu, kisha inuka mpaka usimame sawasawa, kisha sujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu, kisha inuka mpaka utulie katika kikao, na ufanye hivyo katika Swala yako yote
Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, kutoka kwa Mtume, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, amesema: 1. “Mwenye kuswali swala ambayo hakusoma ndani yake Mama wa Qur’an, basi swala hiyo haijatimia, kayasema maneno haya mara tatu. 2. Akaambiwa Abu Hurayrah: Hakika sisi tunakuwa nyuma ya imamu? Akasema: Isomee moyoni mwako. 3. Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Amesema Mwenyezi Mungu: Nimeigawanya Swala baina yangu na mja Wangu vipande viwili, na mja wangu atapata alichoomba. 4. Iwapo mja atasema: “Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote” [Al-Fatihah: 2], basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Mja wangu amenisifu, na ikiwa atasema: “Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu.” [Al-Fatihah: 3], Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Amenisifu.” Akisema mja wangu "Mmiliki wa Siku ya Kiyama} [Al-Fatihah: 4] Anasema Mwenyezi Mungu:Mja wangu amenitukuza. 5. Akisema: “Wewe tunakuabudu na Wewe tunakuomba msaada” [Al-Fatihah: 5], Anasema: Haya ni baina Yangu na mja Wangu, na mja Wangu atapata analoliomba. 6. Akisema: “Tuongoze kwenye njia iliyonyooka (6), njia ya wale uliowaneemesha, si ya wale ambao wamewaghadhibikiwa, wala waliopotea. Mwenyezi mungu husema: Hili ni la mja wangu na atapata mja wangu kile alicho kiomba”
Kutoka kwa Ibn Umar na Abu Hurayrah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kwamba walimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie akisema akiwa juu ya mimbari yake: “Watu wakome kuacha Swalah ya Ijumaa. Au Mwenyezi Mungu atawapiga muhuri katika nyoyo zao, kisha wawe miongoni mwa walioghafilika”
Kutoka kwa Anas amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie alikuja Madina na watu wa madina walikuwa na siku mbili za kucheza sikukuu, akasema Mtume: “Siku mbili hizi ni zipi?” Wakasema: Tulikuwa tukisherekea kabla ya Uislamu, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani ziwe juu yake akasema: “Mwenyezi Mungu amewabadilishia kwa kilicho bora kuliko hizo siku mbili; Siku ya al-Adh-haa na siku ya al-Fitwr.”
Kutoka kwa Ibn Umar, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, amesema: “Swala ya jamaa ni bora zaidi kuliko swala ya mtu pekee kwa daraja ishirini na saba.’’
Kutoka kwa Abu Hurayrah Mwenyezi Mungu awe radhi naye kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie amesema: “Nyumba zinazopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu ni misikiti yake. Maeneo yanayochukiwa zaidi na Mwenyezi Mungu ni Masoko ’’.
Kutoka kwa Abdullah bin Muawiyah Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema: Mtume, rehma na Amani zimshukie, amesema: “Mambo matatu atakaye yafanya ameonja ladha ya imani. Mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba hapana mungu mwingine ila yeye Mwenyezi Mungu. Akatoa zaka ya mali yake kwa niya njema kutoka moyoni mwake, haliyakuwa nafsi yake inamuamuru kufanya hivyo kila mwaka. Hatoi mnyama aliyezeeka, wala mwenye ugonjwa wa ngozi, wala mgonjwa, wala dhaifu; Lakini toeni za kati na kati katika mali zenu; Mwenyezi Mungu hakukuombeni vilivyo bora zaidi, wala hakukuamrisheni mtoe vibaya.”
Kutoka kwa Abu Hurayra Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie amesema: “Enyi watu, Mwenyezi Mungu ni mzuri na hapokei ila kizuri. Na Mwenyezi Mungu amewaamrisha Waumini yale aliyo waamrisha Mitume, akasema: “Enyi Mitume kuleni vyakula bora na mtende mema” [Al-Muuminun: 51], na akasema: “Enyi mlio amini kuleni vyakula bora tulivyo kupeni katika riziki” [Al-Baqara: 172] 3- Kisha Mtume akamtaja alie safari safari ndefu iliyechafuka na vumbi, akinyoosha mikono yake mbinguni: Ewe Mola Mlezi, Mola Mlezi, na chakula chake ni haramu, na kinywaji chake ni haramu, na nguo yake ni haramu, Alilishwa vitu vilivyoharamishwa, ni vipi atajibiwa?!”