Kutoka kwa Uqba Bin A`Amir (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: amesema Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) Je haujajua ayah zilizotelemshwa usiku huu, (hakika) sijaona chochote mfano wake, Surat Al Falaq Na Surat Al Nnaasi.

kutoka kwa A`amir bin Waathilah amesimulia kuwa: 1- Naafi`I bin Abdil Warith akikutana na Umar (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) katika sehemu inaitwa U`sfaana, na Umaru alikuwa amemfanya kuwa kiongozi katika mji wa makah, Umaru akamuuliza: ni nani umemuacha katika nafasi yako ya uongozi katika watu wa hilo bonde? 2- Akasema: (nimemuacha) kijana wa Abzaah, Umar akasema: ni nani huyo kijana wa Abzaah? Akasema: ni mjakazi katika wajakazi wetu, 3- Umaru akasema: unawaachia kiongozi mjakazi? 4- Akasema: Hakika yeye ni msomaji mzuri wa kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni msomi wa elimu ya mirath. 5- Umaru akasema: kweli hakika Nabii wenu (rehma na amani ziwe juu yake) alisema: hakika Mwenyezi Mungu hunyanyua kwa hiki kitabu watu, na kwa kitabu hiki huwashusha wengine.

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Amesema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: "Mwenyezi Mungu amesema: 1- Yeyote aliye na uadui na rafiki yangu, nimekwisha fanya vita juu yake. 2- Mja wangu hanikurubii na kitu kinachopendwa zaidi Kwangu kuliko nilicho mwajibishia. 3- Na mja Wangu huendelea kujikurubisha kwangu kwa ibada za sunnah mpaka nampenda. 4- Nikimpenda, ninakuwa sikio lake analosikia nalo, macho yake anayotumia kuona, na mkono wake anaopiga nao, na mguu wake anaoutembelea. 5- Akiniomba ninampa, na akiniomba ulinzi namlinda. 6- Na mimi sikusita juu ya jambo lolote ninalofanya huku nikisitasita kama ninavyo sitasita juu ya nafsi ya Muumini, anachukia kifo na mimi nachukia kumkwaza”

Kutoka kwa Abdullah bin Masoud, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, ambaye amesema: 1. Nilimuuliza Mtume rehma na amani zimshukie: Ni amali gani anayoipenda zaidi Mwenyezi Mungu? Alisema: “kusali kwa wakati.” 2. Akasema: Kisha ipi? Akasema Mtume: “Basi waheshimuni wazazi.” 3. Akasema: Kisha ipi? Akasema Mtume Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu”. 4. Akasema: Alinieleza hayo tu, na lau ningeomba zaidi, angeniongeza.

Kutoka kwa Abu Hurayrah, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie amesema: 1. “Mwenye kumuondolea Muumini dhiki za kidunia, Mwenyezi Mungu atamwondolea moja ya dhiki za Siku ya Kiyama. 2. Na mwenye kumfanyia wepesi aliyesongwa na mambo, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi duniani na akhera. 3. Na mwenye kumsitiri Muislamu, Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera. 4. Na Mungu humsaidia mja maadamu mja anamsaidia ndugu yake. 5. Na anaye pita njia kwa ajili ya kutafuta ilimu, Mwenyezi Mungu atamsahilishia njia ya kwenda Peponi. 6. Kila watu wanapokusanyika katika moja ya nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu. na wakisomeshana wao kwa wao, amani huwashukia. Na rehema huwafunika, Malaika huwazunguka, na Mwenyezi Mungu huwataja miongoni mwa walio pamoja Naye. 7. Na mwenye kucheleweshwa na vitendo vyake, nasaba yake haitamharakisha.”]

Kutoka kwa Abu Malik Al-Ash’ariy Mwenyezi Mungu awe radhi naye ambaye amesema: Mtume rehma na Amani zimshukie amesema: 1- “Usafi ni nusu ya imani, 2- Na kusema: Alhamdulilaah (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) inajaza mizani. 3- Na kusema: Subhaanallah) Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, hujaza au huyajaza yaliyo baina ya mbingu na ardhi. 4- Sala ni Nuru. 5- Na sadaka ni Ushahidi( juu ya Imani). 6- Subira ni mwangaza. 7- Na Qur’ani ni hoja kwako au dhidi yako. 8- Watu wote huondoka asubuhi, kwa hivyo yupo anayeiuza nafsi yake na akaiacha huru na mwengine akaiangamiza.”

Kwa kutoka kwa Abu Hurairah Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema: 1- “Watu aina saba Mwenyezi Mungu atawatia kwenye kivuli chake siku ambayo hakuna kivuli ila chake. 2- Imamu Muadilifu 3- Kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu. 4- Mtu ambaye moyo wake umefungamana na misikiti. 5- Watu wawili waliopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. wakakusanyika kwa ajili yake na kutawanyika kwa ajili yake. 6- Mwanaume aliyekaribishwa na mwanamke mwenye cheo na mrembo, akasema: Mimi namuogopa Mwenyezi Mungu. 7- Mtu aliyetoa sadaka na akaificha mpaka mkono wake wa kushoto usijue mkono wake wa kulia unatoa nini. 8- Na mtu aliye mtaja Mwenyezi Mungu kwa siri, mpaka akalia”.

Kutoka Kwa Abu Dharr, Mwenyezi Mungu awe radhi naye 1- Kwamba maswahaba walimwambia Mtume rehma na Amani zimshukie: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Watu wenye mali wamekwenda na ujira wao mkubwa, wanaswali tunaposwali, wanafunga sisi tunapofunga, na wanatoa sadaka kutokana na fedha zao za ziada. 2- Akasema Mtume: Je! Mwenyezi Mungu hakukufanyieni sadaka mnazotoa? 3- Kumtakasa Mwenyezi Mungu ni sadaka, kila kumtukuza ni sadaka, kila neno la kumsifu ni sadaka, na kila tahlili ni sadaka. 4- Kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka. 5- Na katika ndoa ya mmoja wenu kuna sadaka. 6- Wakasema maswahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, vipi mmoja wetu akidhi matamanio yake kisha apate ujira ?  Akasema Mtume: “Je, mnaonaje kama akiyaweka matamanio hayo kwenye haramu atapata dhambi ?” Basi akifanya katika halaali anapata thawabu"

Kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, ambaye amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimfikie: 1- “Hakuna siku ambazo matendo mema hupendwa zaidi na Mwenyezi Mungu kuliko siku hizi,” yaani siku kumi. 2- Wakasema Maswahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? 3- Akasema Mtume: “Hata jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa mtu atoke na nafsi yake na mali yake, wala kisirudi chochote

Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: “Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam alipendelea upandelea upande wa kulia katika kuvaa viatu vyake, kuchana kwake nywele, kujitoharisha kwake, na katika mambo yake yote”

Kutoka kwa Jabir bin Abdullah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, amesema:  1- Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie alikuwa akitufundisha istikharah katika mambo yote, kama alivyokuwa akitufundisha Sura kutoka katika Qur’ani.  2- Anasema: “Ikiwa mmoja wenu anakusudia kufanya jambo, basi na aswali rakaa mbili zisizokuwa za faradhi. 3- Kisha aseme: Ewe Mwenyezi Mungu, nakuomba uweza kwa ujuzi wako na uwezo wako kupitia uwezo wako, na nakuomba fadhila zako kubwa. Wewe unaweza, na mimi siwezi, na Wewe unajua, na mimi sijui, na Wewe ni Mjuzi wa mambo yaliyo fichikana. 4- Ewe Mwenyezi Mungu, ikiwa unajua kwamba jambo hili ni bora kwangu katika dini yangu na maisha yangu, na mwisho wa jambo langu - au akasema: Duniani na Akhera, basi nikadirie, unifanyie wepesi, kisha ubariki kwa hilo.  5- Na ikiwa mnajua kwamba jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu, na maisha yangu, na mwisho wa jambo langu, au akasema: Duniani na Akhera liondoshe kwangu mimi na uniepushe nalo.  6- Na kisha nikadirie kheri popote ilipo, kisha uniridhie.  7- Akasema: Na mtu ataje haja yake”

Kutoka kwa Al-Nawwas bin Samaan, Allah amuwiye radhi, amesema: 1- Nilimuuliza Mtume rehma na amani zimshukie kuhusu wema na dhambi. 2- Akasema: “Wema ni kuwa na tabia njema. 3- Na dhambi ni ile inayokutia wasiwasi kifuani mwako, na unachukia watu kuijua”

Kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam kuhusu yale aliyoyahadithia kutoka kwa Mola wake Mlezi, aliyebarikiwa na aliyetukuka amesema: 1- “Hakika Mwenyezi Mungu aliandika mema na mabaya, kisha akayabainisha. 2- Mwenye kukusudia kufanya jambo jema na asilifanye, Mwenyezi Mungu ataliandika kuwa ni wema kamili. 3- Na akikusudia kulifanya na akalitenda, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu humwandikia wema kumi, na humwongezea hadi kufikia mara mia saba, na zaidi ya hayo. 4- Ikiwa alikusudia jambo baya na akawa hakulitenda, basi Mwenyezi Mungu humwandikia jema kamili. 5- Na akikusudia kulifanya na akalitenda, Mwenyezi Mungu huliandika kuwa ni tendo moja baya.”

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ambaye amesema: 1- “Jiepusheni na madhambi saba yenye kuangamiza.” Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ni yapi? Akasema Mtume: 2- “Kumshirikisha Mwenyezi Mungu, 3- Na uchawi, 4- Kuiua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu, isipokuwa kwa uadilifu. 5- Kula riba 6- Kula pesa za yatima 7- Kuikimbia vita 8- Na kuwatuhumu na machafu wanawake walio safi, Waumini walioghafilika”

Kutoka kwa Warad, Mwandishi wa Al-Mughirah, amesema:Muawiya alimwandikia Al-Mughirah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili: 1- Niandikie uliyoyasikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie na akamwandikia: 2- Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam alikuwa akisema kila baada ya kila swala: “Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja, Peke Yake, hana mshirika, ufalme ni wake, sifa njema ni zake, na Yeye ni Muweza wa yote. 3- Ewe Mwenyezi Mungu hakuna kizuizi kwa ulichotoa wala mtoaji kwa ulicho kizuia. 4- Na hanufaishi mwenye utukufu, bali utukufu ni wako” 5- Na akamuandikia: “Alikuwa akiharamisha yaliyosemwa na kusengenya. 6- Kuuliza sana 7- Kupoteza pesa 8- Amekataza kuwaasi akina mama. 9- Mauaji ya watoto wachanga wa kike 10- Na kuzuia (kuwa na choyo) na kuchukua (kupenda kupewa)” .

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam ambaye amesema: “Mwenyezi Mungu ameusamehe umma wangu kwa yale waliyojisemea ndani ya Nafsi maadamu haukufanya wala kusema.” 

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, hakika Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema: 1- “Mwenye kulingania kwenye uwongofu atapata ujira kama ujira wa wale wanaomfuata bila ya kuwapunguzia ujira wao hata kidogo. 2- Na anayelingania upotevu atapata dhambi sawa na dhambi za wale wanaomfuata bila ya kuwazuilia dhambi zao hata kidogo”  

Kutoka kwa Al-Nu’man bin Bashir Mwenyezi Mungu awe radhi naye, Kutoka kwa Mtume, rehma na Amani zimshukie, amesema: “Mfano wa mwenye kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu na akashikamana nayo ni kama watu waliosongamana katika meli. Baadhi yao wakawa sehemu yake ya juu, na baadhi sehemu yake ya chini, ikawa waliokuwa chini, wanapochota maji, wanapita kwa wale walioko juu yao. Na wakasema: Afadhali tungelitoboa katika sehemu yetu, ili tusiwaudhi walioko juu, Wakiwaacha na kufanya wanavyotaka, wote wataangamia, na wakizuiliwa mikononi mwao wataokoka wote kwa ujumla” 

Kutoka kwa Tariq bin Shihaab amesema: Mtu wa kwanza aliyeanza khutba ya siku ya Idi kabla ya swala ni Marwan, na mtu mmoja akasimama karibu naye na kumwambia: “Swala ni kabla ya khutba.” Akasema, “Kilichopo kimeachwa. Amesema Abu Said Radhiya Allaahu anhu: Ama mtu huyu ametimiza wajibu wake. Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie akisema: “Yeyote miongoni mwenu anayeona kitendo kiovu, basi na akibadilishe kwa mkono wake. Ikiwa hawezi, basi kwa ulimi wake. Ikiwa hawezi, basi kwa moyo wake, na hiyo ndiyo imani dhaifu zaidi”

Kutoka kwa Al-Mughira bin Shu’bah Mwenyezi awe radhi naye kutoka kwa Mtume, amani iwe juu yake, ambaye amesema: “Kundi la umma wangu litaendelea kushinda mpaka iwafikie amri ya Mwenyezi Mungu na hali wao ni washindi” Na katika riwaya nyengine: “Kundi katika ummah wangu litaendelea kushika amri ya Mwenyezi Mungu, na wale wanaowaacha au kuwapinga hawatawadhuru mpaka ifike amri ya Mwenyezi Mungu”