عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ «خُلِقَتِ الْمَلَائِكَةُ مِنْ نُورٍ، وَخُلِقَ الْجَانُّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ، وَخُلِقَ آدَمُ مِمَّا وُصِفَ لَكُمْ»

Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie“Malaika waliumbwa kutokana na Nuru,Majini wameumbwa kwa Moto.Adam aliumbwa kwa jinsi mlivyoelezwa”

Muhtasari wa Maana

Mtume Rehma na Amani zimshukie alitaja asili ya kuumbwa kwa baadhi ya viumbe, hivyo akasema kwamba Malaika wameumbwa kutokana na Nuru, na Majini wameumbwa kwa moto, na kwamba Adam, amani iwe juu yake, ameumbwa kutokana na Udongo, kwa namna ambayo Mwenyezi Mungu ameeleza kwa kina ndani ya Qur'an.

Miradi ya Hadithi