Alimtuma Mtume (s.a.w) Mua’dh kwenda yemen hali akilingania na akisimamia hukumu, karibia kabisa na mwaka wa tisa hijiriya(9h):

  1. Na akamweleza kwamba atawaendea watu katika mayahudi au manaswaara miongoni mwa waliokua na kitabu cha taurati au injili, ili ajiandae kwakuwa wao walikuwa ni watu wenye elimu kiujumla, [1].

  2. Kisha akamuusia aanze kuwalingania juu kukiri upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuukubali utume wa nabii wake (s.a.w), kwa sababu kuyakubali hayo mawili ndio msingi wa dini ambao hakitakubalika chochote katika matawi yake ila baada ya kuukubali misingi hiyo miwili, basi wao wanahitajika kwanza kuvikusanya, [2] kwani mayahudi na manaswara hawakutekeleza yale ambayo ingekuwa ni sababu ya kuwaokoa, kama kushuhudia kwa kukubali kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuukubali utume wa nabii Muhammad(s.a.w), basi wao walimshirikisha Mwenyezi Mungu pamoja na issa ibn maryam, na wakakanusha da’wah  ya Mtume (s.a.w) [3] 

  3. Kisha akamweleza Mtume (s.a.w) kwamba wakifuata utakayo waamrisha kwa kutamka shahada mbili, na wakakubali kumpwekesha Mwenyezi Mungu na wakakubali utume wa Nabii Muhammad (s.a.w), basi wajulishe kwamba hakika Mwenyezi Mungu amewafaradhishia kusali sala tano mchana na usiku, na uwafundishe namna ya kusali.

Na hakika yamejulisha maneno ya Mtume (s.a.w): “Ikiwa watakukubalia hilo” juu ya kufuata na kiutendaji sio alimradi kukubali uwajibu na ulazima, basi ni lazima wakubali na watekeleze sala katika nyakati zake [4].

4.   Kisha akaenda hatua kwa hatua baada ya kukubali uwajibu wa sala na kuitekeleza kwake, akahamia kwenye zaka, basi akamuamrisha awafundishe kwamba Mwenyezi Mungu amewalazimisha matajiri kutoa zaka, nacho ni kiwango kidogo kinachojulikana kinakusanywa kutoka katika mali zao, na kinagawiwa kwa masikini wao.

5.   Kisha akamuamrisha Mtume (s.a.w) Mua’dh (r.a) ikiwa watu watamkubalia hilo na wakatoa zaka ya mali zao, basi achukue kiasi cha zaka kujiepusha na kutoa mali nzuri ambazo wanazipenda wenye mali hizo na nafsi zao zimefungamana na mali hizo kwa kuzipenda; kama mfano, mtu akiwa na mbuzi anaempenda zaidi  na anampatia kipaumbele zaidi ima kwa wingi wa maziwa yake, au kwa sababu nyingine, basi mfano wa mbuzi huyo hatakiwi kuchukuliwa katika zaka, kwa kuwafanyia upole wenye mali, na Mwenyezi Mungu hakujaalia kuwaliwaza masikini katika kuwapitasha madhara matajiri, na ikiwa nafsi ya tajiri ikiridhika kwa kutoa kitu bora zaidi, basi itafaa kuchukua kwa ridhaa yake. Na amesema omar ibn al-khatwab (r.a) kumwambia mtu aliye mtuma kukusanya zaka: “Na usichukue katika zaka mnyama bora alienenepeshwa ili achinjwe, wala ruba- ambaye huwa anabakishwa nyumbani wala haachwi kujitafutia chakula kutokana na uzuri na ubora wake kwa anaemmiliki, wala mwenye mimba- ambaye anakaribia kuzaa, wala dume tegemezi katika wanyama” [5]

6.   Kisha akamtahadharisha Mtume (s.a.w) mwisho mbaya wa kudhulumu, katika kukusanya zaka au katika mambo mengine ya kiutawala na kihukumu, na makusudio ya kujiweka mbali na dua ya mwenye kudhulumiwa: ni kujiepusha na sababu zake; kwa sababu dhulma-kudhulumu- ndio inapelekea kupatikana maombi mabaya dhidi ya mwenye kudhulumu.

Na duwa ya mwenye kudhulumiwa huwa inasikika zadi na kujibiwa na wala hairudi patupu, hufunguliwa kwayo milango saba ya mbingu, na hakuna pazia kati yake na kujibiwa kwake, [6]  na katika hadithi: “ Watu watatu duwa zao hazirudi patupu-bila majibu-: mwenye kufunga saumu mpaka afungue, na kiongozi mwadilifu, na maombi ya mwenye kudhulumiwa, anayanyanyua Mwenyezi Mungu maombi hayo mawinguni na anayafungulia milango ya mbingu na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “ Naapa kwa nguvu zangu nitakunusuru kukusaidia japo baada ya muda” [7] 

Mafunzo

  1. Nabii Muhammad (s.a.w) alimtuma Mua’dh ibn jabal kwenda yemen hali yaku akiwa kwenye miaka ya ishirini katika umri wake, basi akabeba majukumu ya ugeni na kuwa mbali na watu wake na katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutii amri ya Mtume (s.a.w), ni mara ngapi sisi tunavumilia matatizo na majukumu kwa ajili ya njia hiyo?

  2. Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake, akiwabebesha maswahaba zake majukumu mazito makubwa, hali wakiwa katika ujana wao, na wao hawakuwa wakiyakimbia majukumu hayo, basi ni juu ya baba, mzazi, mwalimu, mlezi na wengineo kuwaandaa kuwazoesha walioko chini yao kuwapa majukumu, na wasiwadogeshe, na ni juu ya hao pia kuyapokea vyema majukumu hayo na kuyafanyia kazi.

  3. Chukuwa yaliyo sihi miongoni mwa maneno ya Mtume Muhammad (s.a.w), japo akiwa mpokezi au msimulizi wake ni mmoja, kwani alimtuma Mtume (s.a.w) Mua’dh akiwapeke yake kwa mambo makubwa miongoni mwa itikadi na ufahamu, na kutoka katika mamlaka hata katika mali za watu, na yote hayo yanajulisha juu ya kuzingatia maneno ya mtu mmoja.

  4. Jifunze kujuwa tabia za unao waendea, hakika alimueleza Mtume (s.a.w) Mua’dh (r.a) ya kwamba atawaendea watu waliopewa kitabu, ili kuchunga yanayo paswa kuwalingania [8] , katika vipaumbele vya dalili na njia za kulingania na mambo mengine, na kwa sababu wao ni watu wa elimu na mijadala, basi pupia kukusanya taaluma ya kutosha na yenye athari, kabla ya kazi yeyopte unayotaka kuifanya.

  5. Mtume (s.a.w) alitilia umuhimu zaidi kuwaelekeza wafanyakazi wake na watoa mawaidha, kwakuwa yeye hakumtuma Mua’dh mpaka alipombainishia hali halisi, na pia akampangia kazi, na akamuamrisha kuwa mwadilifu, na akamtahadharisha kutokana na kudhulumu, pamoja na ukamilifu wa Mua’dh kwenye dini yake na elimu yake, basi usiache kumuusia uliye naye, na nijuu ya anaye pewa wosia kuto kupuuza wosia huo.

  6. Mtume (s.a.w) alitilia umuhimu zaidi vipaumbele vya  kwanza kisha akaenda hatua kwa hatua, basi hakumuamrisha Mua’dh kuanza na madhambi ambayo watu hawaepukani nayo katika maisha yao na tabia zao, pamoja na kuwepo umuhimu wa kuyakemea hayo, lakini alianza na misingi ya dini, na funguo za imani nao ni shahada mbili, kisha sala, kisha zaka, na hivi ndio tunatakiwa kuwa katika malezi yetu na ulinganiaji wetu na kusomesha kwetu, bali tunapaswa kufanya hivyo katika kazi zetu zote, tuanze na lililo muhimu zaidi kisha linalo fuatia kwa umuhimu, amesema A’ishat (r.a) “Si vinginevyo hakika uliteremka wa kwanza ulioteremka katika ufunuo ni sura zilizo pambanuliwa, katika hizo pametajwa pepo na moto, mpaka watu walipoufuta uislamu ikateremka katika ufunuo yaliyo halali na haramu, kama ingeteremka mwanzoni tu “ msinywe pombe”  basi watu wangesema hatutaacha pombe milele, na kama ingeteremka mwanzoni “msizini” basi wangesema hatuwezi acha zinaa milele” [9]

  7. Imani, sala na zaka, ndio misingi ya imani kubwa ambayo imekaririwa kwa kukutanishwa katika qur’ani tukufu na maneno ya Mtume (s.a.w) kwa wingi sana, na ndani yake kuna malipo makubwa (thawabu) na kuathirika kiimani, kwa kiasi ambacho hakuna akijuaye isipokuwa ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi hata ukiwa wewe na wenzako mnatekeleza misingi hiyo basi pupieni kuifanya kikamilifu.

  8. Alimtahadharisha Mtume Muhammad (s.a.w) Mua’dh kuchukua zaka ambayo nafsi zimefungama nazo kutokana na ubora na uzuri wa sadaka hiyo, bali alimuamuru kuwa mwadilifu, na kufanya hivyo ni katika uadilifu na kuchunga hisia za watu na uelewa wa watu ambao ni juu ya kila mlinganiaji na baba na mlezi mwenye kusimamia mambo afanye kama hivyo, basi azingatie hayo katika kuamrisha kwake na kukataza kwake.

  9. pupia kulala hali yakuwa hakuna aliye dhulumiwa ambaye kakosa kulala kutokana na huzuni kwa yale uliyoyasema au kumtendea,sawasawa awe ni mume au motto, au mwanafunzi au mfanya kazi, au muuzaji au dereva, na wala usiirahisishe dhulma kwa yule unaye muona yuko chini yako, japo akiwa katika waasi, na hakika alimuhofisha nabii muhammad (s.a.w) Mua’dh kutokana na dhulma upeo wa kuhofisha,hata katika kutaamali na makafiri niongoni mwa watu wa kitabu, na baadhi yao wanaweza kuamini na wengine wasiamini.

  10. Amesema mshairi:Usifanye dhulma katu hata ukiwa na uwezo wa kufanya hivyo = kwani hakika dhulma mwisho wake inakuletea majutoMacho yako yAnasinzia hali aliyedhulumiwa halali yuko macho = akikuombea duwa mbaya na jicho la Mwenyezi Mungu halilali.

Marejeo

  1. Fath al-Bari cha Ibn Hajar (3/358).
  2. “Kashfu Litham ufafanuzi wa Umdat al-Ahkam” cha al-Saffarini (3/400).
  3. Kumkamilisha Mwalimu kwa Faida za Muislamu cha Qaadh Iyadh (1/239).
  4. Tazama: “katika ufafanuzi wa al-‘Umdah cha Ibn al-Attar” (2/798).
  5. Malik (2/372), na al-Tabarani katika Kamusi Kuu (6395). Na ameisahihisha Al-Nawawi katika “A l-Majmuu’” (5/427), na Ibn Katheer kaboresha upokezi wake katika “Irshad Al-Faqih” (1/248).
  6. Fath Al-Mun’im ufafanuzi wa Sahih Muslim cha Musa Shaheen Lashin (1/70).
  7. Al-Tirmidhiy (3598), na Ibn Majah (1752), kutoka kwa Abu Hurayrah, na meisahihisha Ibn al-Mulqin katika “Al-Badr al-Munir” (5/152).
  8. Fath al-Bari cha Ibn Hajar (3/358).
  9. Sahihi Al-Bukhari (4993).


  1. Alikuwa Mua’dh amepanda nyuma ya Mtume (s.a.w) juu ya punda.

  2. Akataka Mtume rehma na amani ziwe juu yake kubainisha mafunzo yake, akamuuliza: Je ni yapi anayostahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, juu ya waja wake miongoni mwa yaliyo wajibu kwao? na nizipi haki za waja ambazo ameziwajibisha juu ya nafsi yake?

  3. Mua’dh (r.a) akajibu kwa kusema “Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi zaidi juu ya hilo”, yaani: mimi sijui. na mfano wa maneno haya husemwa katika mambo ya kisheria, lakini akiulizwa mtu kunako mambo ya kidunia, au mambo yaliyofichikana na mengineyo miongoni mwa asiyo yajuwa Mtume (s.a.w) basi aseme “Mwenyezi Mungu ndio mjuzi zaidi”.

  4. Basi Mtume (s.a.w) akabainisha jawabu; akasema kuwa haki ya Mwenyezi Mungu –mtukufu - kwa waja wake waelekee kwake kwa kumuabudu, na ibada, Maana yake ni:  jina lililokusa kila anachokipenda Mwenyezi Mungu  mtukufu na anakiridhia, katika maneno na vitendo vya wazi na vya siri  [1], nayo ni hali ya kujidhalilisha na kutii na kuelekea moyo kwa anaestahiki kuabudiwa, na nilazima pamoja na kumuabudu Mwenyezi Mungu [2] wasimshirikishe na yeyote katika ibada yake- hata akiwa nabii ( alipewa ufunuo) au malaika au mja mwema- wala kwa aina yeyote ya ushikina- hata ikiwa ndogo kiasi gani, japo hata kwa kutamka tu, basi hii ndio haki ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake:

    “Na amekwisha toa hukumu mola wako kwamba msiMuabudu  yeyote isipokuwa yeye peke yake”

    [al-israai:23]

    na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    “Na sikuwaumba majini  na watu isipokuwa waniabudu mimi peke yangu (56)mimi sihitaji kutoka kwao riziki wala chakula (57) hakika Mwenyezi Mungu ndio mtoaji wa riziki zote tena mwenye nguvu Madhubuti ”

    [adh-dhariyat:56-58].

  5. Na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni haki ameiwajibisha Allah mtukufu juu ya nafsi yake kwa ukarimu tu kutoka kwake, na haikuwa wajibu kwake [3] kwamba wao ikiwa watamuabudu na wasimshirikishe na chochote, asiwaingize motoni basi “ mwenye kukutana na mola mtukufu ilihali hamshirikishi na chochote katika ibada ataingia peponi, na atakaekutana na Mwenyezi Mungu haliyakua ni mshirikina ataingia motoni” [4]

    “ Hakika mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu ameiharamisha pepo kwake, na mafikio yake itakua ni motoni na watu waovu hawana atakae wanusuru na kuwaokoa ”

    [al-maidat:72].

     Na maana ya hayo ni kwamba muislamu mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu, hatoishi motoni milele, na ikiwa mema yake yatakuwa zaidi kuliko maasi ataingia peponi na ataharamishiwa moto, na ikiwa ni katika waasi na maasi yakawa mengi zaidi basi hukumu yake inabaki kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akitaka atamuadhibu atakavyo kisha amuweke peponi, na akitaka anamsamehe na anamuingiza peponi. Ama aliyekufa katika ushirikina, hahika hatoingia peponi, bali ataishi motoni milele na milele pasina kikomo cha adhabu.

    “Hakika Mwenyezi Mungu hamsamehe mwenye kumshirikisha bali anasamehe tofauti na shirki kwa amtakae, na yeyote mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu basi anakuwa amezusha madhambi makubwa”

    [an-nisaa:48][5] .


  6. Aliposikia Mua’dh hiyo bishara njema kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w) alipenda awabashirie watu, lakini akaomba ushauri kwa Mtume (s.a.w), na Mtume akamshauri kuwa asifanye hivyo, kwa sababu baadhi yao, huwenda watakapo yajua hayo watabweteka kwenye kumpwekeshaMwenyezi Mungu Mtukufu, na watakuwa wavivu wa kufanya ibada na utiifu na wataacha kabisa. Na zimekuja hadithi zingine zikiashiria kwamba Mua’dh (r.a) alifahamu kuwa katazo la Mtume lilimaanisha wosia kwa maslahi ya kuto kubweteka na kwamba jambo hilo sio kosa kulizungumza kwa masilahi ya taaluma na mengineyo, na kwa ajili hiyo Mua’dhi Alisimulia watu karibu na kifo kwa kuhofia kupata madhambi ya kuficha elimu.

Mafunzo

  1. Usifanye jeuri kwa kutopanda kipandwa ambaco sio cha kifakhari, na ichunguze nafsi yako wakati inapo kataa kuchanganyika na tabaka tofauti za watu, au kula nao, ni katika mambo yanayoashiria kiburi cha wazi kabisa au jeuri iliyo jificha, na hakika Mtume (s.a.w) alipanda punda, na akapanda Mua’dh nyuma yake, naye Mtume rehma na amani ndio kiigizo chetu katika unyenyekevu, na kuchangamana na watu.

  2. Usijizuie kunufaika kwa vitu alivyo vidhalilisha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika wanyama, na utumie vitu hivyo kistaarabu, kwa hakika alipanda Mtume Muhammad (s.a.w) yeye na Mua’dh juu ya mnyama mmoja.

  3. Alitumia Mtume (s.a.w) njia ya kuuliza katika kumfundisha Mua’dh (r.a); ili kumuhimiza kuitumikisha akili, na ili lipate kuthibiti jawabu katika moyo wake baada ya kuwa ameshindwa kujibu, basi inapendeza kwa mlinganiaji achague njia ambazo zitaamsha hamasa, na zitachangamsha akili, na zitavuta usikivu na ufahamu wa karibu.

  4. sio aibu kwa mwanadamu kuto juwa kitu chochote katika mambo ya kidunia au kidini, hakukosea Mua’dh (r.a)- na yeye ni mjuzi wa watu kwa yaliyo halali na haramu- kwa kusema juu ya jambo asilolijuwa: “Mwenyezi Mungu ndio mjuzi zaidi” basi jiepuashe kutoa fat,wa (jawabu) katika dini, jiepushe kujibu maswali ya dini pasina elimu kwa kiburi au haya-aibu-:

    “ Wala msifuate njia za shetani hakika yeye kwenu ni adui wa wazi (168) si vinginevyo shetani anakuamrisheni mabaya na machafu na kumsemea Mwenyezi Mungu yale msiyopyajuwa”

    [al-baqarat:168-169].

    “Msiseme kwa ndimi zenu uongo kwamba hili ni halali na hili ni haramu, kwa ajili ya kumzushia Mwenyezi Mungu uongo, hakika ya wenye kumsemea Mwenyezi Mungu uongo hawatafaulu (116) ni starehe ndogo sana ya hapa duniani, na wanayo wao adhabu kali"

    [al-nahli:116,117].

  5. Kila haki unayoitafuta kwa watu au wayoitafuta kwako: Basi fahamu kuwa kunahaki kubwa zaidi ya hiyo, nayo ni haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yako, pia ni haki kubwa zaidi kuliko idadi ya kila neema zake kwako, basi likumbuke hilo, na yawe maisha yako yamefungamana nayo:

    “ Sema ewe Muhammad, hakika sala yangu, na kuchinja kwangu, na uzima wangu, na kifo changu, ni kwa ajili ya Mola wa viumbe wote (162) hana mshirika na nimeamrishwa kufanya hayo na mimi ni wa mwanzo kunyenyekea "

    [al-an’am:162,163]

  6. Mwenyezi Mungu anahitaji kutoka kwako usimshirikishe na chochote, yaani: kituchochote kama unavyo jiepusha kufanya ushirikina mkubwa, kama kuabudu masanamu, kuomba msaada kwa nyota na kutafuta ukati kwa maneno yasiyofaa, hivyo hivyo ndio ujiepushe na kufanya ushirikina mdogo, kama kuapa kwa viumbe, hata akiwa kiumbe huyo ni Mtume (s.a.w), na kuweka azima-hirizi- ambazo zinaondosha kijicho kwa madai yao, au kumshirikisha Mwenyezi Mungu kwa kusali vizuri kwa kutaka watu wakuone, na mfano wa hayo . Na yamepokelewa maneno katika hadithi al-qudsiy: “Mimi ninajitosheleza na washirika katika kunishirikisha, mwenye kutenda wema wowote akamshirikisha pamoja namimi mwingine asiyekuwa mimi, nitamwacha na ushirikina wake” [6] .

  7. Ulinde moyo wako, na upambane na kila shirki utayo pambana nayo moyo wako, na chukuwa bishara njema ya kheri, imekuja katika hadithi: “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu, atamtoa mtu katika ummati wangu, kwenye mkusanyiko wa watu wote siku ya malipo, kisha atamfunulia vitabu tisini na tisa [ yaani vya madhambi], na kila kitabu ni mfano wa kikomo cha macho, kisha atasema Mwenyezi Mungu: Je, unakanusha chochote katika hiki kitabu? Je, wamekudhulumu waandishi na wadhibiti wangu? Basi atasema: Hapana ewe Mola wangu! Atasema Mwenyezi Mungu: Je unao udhuru wowote? atajibu kwa kusema: Hapana ewe Mola wangu, atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ni kweli kabisa, hakika wewe unao wema kwetu, na kwa hakika leo hakuna kudhulumiwa, basi kitakuja kitambulisho kimeandikwa: Ninakiri kwa moyo na ninatamka kwa ulimi ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake, na ninakiri ya kwamba Nabii Muhammad ni mja wake nani Mtume wake, atasema Allah kumwambia mtu huyo: pima uzito wako, atasema Yule mtu: Ewe mola wangu wapi na wapi kitambulisho hiki na hivi vitabu! akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika wewe hutadhulumiwa leo, akasema: vitawekwa vitabu- vya madhambi- katika sahani ya mzani na kitambulisho kitawekwa katika sahani nyingine, vikawa vyepesi vitabu vya madhambi na kitambulisho kikawa kizito, hakiwezi kuwa kizito pamoja na jina la Mwenyezi Mungu kitu chochote” [7] .

  8. Hadithi za kutoa ruhusa juu ya kitu Fulani huwa hazienezwi kwa watu wote, ili ufahamu wao usije kukosa makusudio, na hakika Mua’dh aliisikia hiyo ruhusa lakini, ikawa sababu ya kumwongezea bidii katika ibada na woga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini mtu ambaye hajafikia daraja lake kiibada, haiaminiki kwa kupunguza ibada kwa uvivu na kubweteka juu ya anayoyafahamu katika habari.[8] Na haya yanakaribiana kabisa na maneno ya ibn masoud (r.a): “ Wewe huwasimulii watu maneno ambayo upeo wao haujayafikia isipokuwa itakuwa ni mtihani kwa baadhi yao[9] .

Marejeo

  1. Kitabu, Majmuu’ al-Fatawa (10/149, 150).
  2. Kitabu, Fath al-Bari cha Ibn Hajar (11/339).
  3. “Al-Kawthar Al-Jari katika Riyadh Ahadith Al-Bukhari” cha Al-Kurani (5/438).
  4. Sahihi Muslim (93), kutoka kwa Jabir bin Abdullah, Mungu amuwiye radhi.
  5. Almufhim katika mukhtasari wa Muslim wa al-Qurtubi (1/290)
  6. Sahihi Muslim (2985) kutoka kwa Abu Hurairah, Mungu amuwiye radhi.
  7. Sunani Al-Tirmidhiy (2639) na Ibn Majah (4300).
  8. Fath al-Bari cha Ibn Hajar (340/11).
  9. Tazama: Sahihi Muslim baada ya Hadithi Na. (5).

  1. Mtume (Rehma na Amani zimfikie) Ameeleza kuwa watu wake wote wataingia Peponi isipokuwa wale watakaokataa, na Makusudio ya kutumia neno Ummah hapa ni Ummah wa kulinganiwa ambao wito wa uislamu umewafikia katika wanadamu na majini, hivyo basi kila mwenye kusikia ulinganizi wa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) na akafikiwa na hoja na sheria za Mwenyezi Mungu, basi huyo yumo ndani ya ummah aliotumwa kwao Nabii Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake).

  2. Maswahaba walishangaa kwa hili yaani Vipi mtu mwenye akili timamu atakataa kuingia katika pepo, ambayo kuna neema ambazo jicho halijapata kuziona, wala sikio halijapata kusikia, na moyo wa mwanadamu haujawahi kufikiria? ndio maana waliuliza kwa mshangao kana kwamba wanakanusha mtu kufanya hivyo.

  3. Mtume (Rehma na Amani zimfikie) akawaeleza uhalisia wa jambo hilo, kwamba mwenye kumfuata, na akatekeleza amri zake na akaepuka makatazo yake, huyo atafaulu kuingia peponi na kuwekwa mbali na Moto. Ama mwenye kumuasi na kukiuka amri zake na akatakaa kufuata mwenendo wake, atakuwa amekataa kuingia Peponi mwenyewe kutokana na matendo yake mabaya na imani yake batili.

Na huyu mwenye kukataa mwenyewe kuingia Peponi anaweza kuwa katika walio kufuru, yaani wasiokuwa waislamu kabisa, basi huyu wa aina hii hataingia Peponi milele, kwani Mwenyezi Mungu amesema:

“Na anaye tafuta dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwake, na Akhera atakuwa miongoni mwa waliopata khasara.”

[Imran: 85].

Mwenyezi Mungu amesema pia:

“Hakika wale wanao zikanusha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi hawatafunguliwa milango ya mbingu, wala hawataingia Peponi mpaka apite ngamia katika tundu ya sindano. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wakosefu”

[Al-A'raf: 40].

Halikadhalika mwenye kukataa kuingia peponi anaweza kuwa miongoni mwa Waislamu waliofuata matamanio na wakaacha maamrisho, na wakafuata njia za waovu, au wakazua katika dini ambayo Mwenyezi Mungu hakuyaridhia, hawa hawataishi Motoni milele; Kwa vile ni Muislamu hatakaa motoni milele, kwani hapa kinachokusudiwa ni kwamba hawataingia Peponi pamoja na waliotangulia (waja wema), bali wataingia peponi baada ya kuhojiwa au kulaumiwa na kuadhibiwa.

Mafunzo

  1. Abu Huraira (Radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesimulia Hadith nyingi kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani zimfikie) hadithi ambazo hakuna mtu mwingine yeyote aliyezisimulia. Kwa sababu ya umakini wake juu ya maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimfikie)   na kujitolea muda wake mwingi kwa ajili ya hilo, kiasi kwamba alikuwa akilala msikitini pamoja na watu waliokuwa wakiishi msikitini, na alikuwa anakula chakula chao na kunywa vinywaji vyao, hashughulishwi na chochote cha kumtoa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, yote hayo ni kutokana na pupa na bidii ya juu zaidi aliyokuwa nayo katika kujifunza dini, kwa hivyo yeyote anayetaka kutafuta elimu au kufika mbali katika jambo fulani basi aige kitendo cha Abu Huraira, subira yake na kushikamana kwake na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimfikie).

  2. Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), katika hadith hii alitoa maneno mafupi yanayohitaji ufafanuzi wa kina zaidi, ili nafsi ziwe tayari kumsikiliza na kukariri atakayoyasema, ndio maana Maswahaba wakawahi kuuliza juu ya ufafanuzi wa jambo hilo. Tunajifunza katika hilo kuwa, Mwalimu, Mlezi, au Mlinganiaji anapaswa kuwa mbunifu katika kutumia mbinu ambazo zitasaidia kuzingatia maneno yake na kuyakariri.

  3. Kuingia Peponi ni ushindi mkubwa unaohitaji kufanyia kazi jambo moja jepesi ambalo ni kumfuata na kumtii Mtume (Rehema na Amani zimshukie).  Atakayeipuuza tunu hiyo hakika atapata hasara, na kupoteza fursa kubwa.

  4. Hakika njia ya kuingia peponi iko wazi na ni nyepesi, haihitaji kuvuka mipaka katika kufanya ibada zisizokuwa na msingi, na uwepesi wake ni kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu Pamoja na Mtume wake, Abdullah bin Masoud anasema: “hakika Sisi tunaiga (mwenendo wa Mtume) na hatuanzishi mapya na tunafuata (maamrisho yake) wala hatuzushi, na hakika hatutapotea maadamu tunashikamana na mafundisho ya Mtume (Rehema na Amani zimshukie)” [1].

  5. Mshairi amesema:Ikiwa wewe si mfuasi wa Muhammad,,,,,,,, basi hujaongoka."Hakika Dunia yako haitakuwa na faida kama hujamfuta yeye ,,,,,,, kwani wewe huwezi kuishi milele?Shida na raha za dunia hii zitaisha,,,,,,,,, = hivyo Basi ipe nyongo achana na starehe za dunia.Kuwa mvumilivu juu katika changamoto zake ,,,,,,, kisha tenda Mema Leo ili kesho ufurahi.

Marejeo

  1. “'Iielam Almuqiein `an Rabi Al a`lamina" Liabn Alqiam” Na Ibn Al-Qayyim (4/115).


Hadithi hii ni miongoni mwa misingi mikubwa iliyobainisha na kuikusanya daraja za dini, na kwa ajili hiyo Al-Qadi Iyad akasema: “Hii ni Hadithi kubwa inayojumuisha kazi zote za matendo yanayoonekana na ya yasiyoonekana, na Elimu yote ya kisheria inapatikana katika hadithi hii

Omar- Radhi za mwenyezi mungu zimshukie- anasema kwamba wao:

  1. Walipokuwa wamekaa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu akatokea mtu mmoja mwenye sura ya ajabu. Ni kijana mwenye nywele nyeusi sana, na si miongoni mwa maswahaba mashuhuri wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, Haionekani kuwa yeye ni msafiri, kwani dalili za safari hazionekani kwake, kama vile kichwa kuchafuka na vumbi la uso na nguo.

  2. Kisha mtu huyu akaingia kwenye duara la watu mpaka akakaa mbele ya Mtume akashikanisha magoti yake kwenye magoti ya Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) na kuweka viganja vyake juu ya mapaja yake. Tayari kwa kutafuta Elimu kwa unyenyekevu kwa Mtume, amani iwe juu yake, katika kikao hicho.

  3. Kisha akasema: Ewe Muhammad, niambie kuhusu Uislamu. na alisema: Ewe Muhammad! Kuwajulisha kuwa yeye ni Bedui; kwani wao ndio waliokuwa wakimuita Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kwa jina lake tu. Kwa vile hawakuwa na elimu na adabu kama za Maswahaba katika Muhajiri na Ansari ambao walisikia amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu na wakazitekeleza pale Mwenyezi Mungu aliposema: “Msiichukulie dua ya Mtume baina yenu kuwa ni dua ya nyinyi kwa nyinyi.” (An- Nur: 63). yaani: Msimuite kama mnavyoitana, yaani Usiseme: Ewe Muhammad, bali sema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.[1]

  4.  Mtume Rehma na Amani zimshukie akamjibu kuhusu Uislamu, ya kwamba Uislamu umeegemezwa juu ya nguzo tano mashuhuri, ambazo ya kwanza ni: kushuhudia kwamba hapana Mwenyezi Mungu Anaeabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja; Neno hilo ni tamko la kumpwekesha Mwenyezi Mungu ambalo Mwenyezi Mungu aliwatuma nalo manabii na mitume wote, ambalo ni lazima kutamka kwa ulimi, na kukiri moyoni, na kutenda kwa viungo vyake matendo yanayoendana na imani hiyo; na asiabudiwe yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala asimuogope yeyote isipokuwa Yeye tu, wala asiombe mwengine, na hampendi yeyote kama anavyompenda  Mwenyezi Mungu, na haweki nadhiri matumaini kwa yeyote sipokuwa yeye, na ibada nyenginezo anazifanya kwa ajili yake tu, na kuwa na yakini kwamba Yeye ndiye mwenye kudhuru na mwenye kunufaisha, kwamba hakuna yeyote mwenye manufaa au madhara kwa mja isipokuwa kwa idhini yake, yeye ndiye anaeabudiwa kwa haki, na kinyume na yeye ni uongo.

  5. Katika sharti la neno la tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ni kumuamini Mtume wake (Rehma na amani ziwe juu yake), kwa yale aliyokuja nayo, na kuamini kwamba ametumwa na Mola wake Mlezi, na kusadikisha aliyoyaleta kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na hilo lahitaji kuamini aliyoyafanya kuwa sheria, na kufuata aliyoyaamrisha, na kuepuka aliyoyakataza, na kumtukuza, na kumuunga mkono, na kumtetea, na kupigania dini pamoja naye.

  6. Nguzo ya pili ya Uislamu: kusimamisha swala ambayo ni kuisimamisha kwa namna inayostahiki, baada ya kutimiza masharti na kutekeleza nguzo, pia kuwa mnyenyekevu katika swala na kuhisi utukufu wa Mwenyezi Mungu. Mwenye nguvu ndani yake, na ndio maana hakusema: “Na tekelezeni Swala.”

  7. Nguzo ya tatu: kutoa zaka, ambayo ni wajibu kwa mtu mwenye mali ambayo Mwenyezi Mungu amempatia, kwa mujibu wa maelezo ya halali ambayo Sheria tukufu imebainisha. Hivyo basi mtu anatoa zaka yake kutokana na wema wake, akiamini kuwa ni wajibu kwake, na akitarjia ujira kwa Mwenyezi Mungu, wala hachagui mali iliyombaya na kuitoa kwa ajili ya zaka, bali anatanguliza radhi na malipo ya Mwenyezi Mungu katika mali yake. 

  8. Nguzo ya nne ya Uislamu ni kufunga mwezi wa ramadhani kwa kujiepusha na mambo yanayofunguza saumu kama vile chakula, vinywaji na kujamiiana katika mchana wa mwezi wa Ramadhani, kuanzia alfajiri hadi kuchwa kwa jua, kama ilivyo katika vitabu vya sheria, muumini hufunga, na hutaraji thawabu, wala hafungi kwa kulazimishwa. 

  9. Kisha nguzo ya tano: kuhiji kwenye Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu iliyoko Makka, na ibada nyenginezo, zenye hukumu maalumu, na ibada hiyo ni wajibu mara moja katika maisha, kwa sharti kwamba mtu awe ana uwezo wa kimwili na kifedha.

Ni vyema kutambua kwamba aliunganisha katika ufafanuzi wa Uislamu miongoni mwa nguzo zake tano ulizojengwa juu yake, kama ilivyo katika hadithi ya Abdullah bin Omar, Mwenyezi Mungu awawie radhi, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu Alisema: “Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano, kushuhudia kuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu na Mwingi wa Rehema.” kuswali, kutoa zaka, kuhiji Nyumba na kufunga Ramadhani”

Hii haimaanishi kuwa Uislamu umewekewa mipaka kwenye ibada hizo tu, bali ni nguzo zake ambazo uislamu hauwezi kuimarika pasipo nguzo hizo, na ibada nyingine zote ni nyongeza za jengo hilo, ambalo hasara yake inaathiri jengo hilo na uhai wake, tofauti na nguzo ambazo, ikiwa zimepotea, jengo huanguka mahali pa kwanza.

10.  Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) alipomaliza jibu lake, yule mtu akamwambia: “Umesema kweli.” Maswahaba walishangaa ni vipi atamuuliza juu ya jambo fulani kisha kulithibitisha jibu lenyewe; bila shaka muulizaji anayo Elimu ya kutosha juu ya hilo analouliza na sio kuwa hajui kabisa. 

11.  Kisha akamuuliza kuhusu Imani ambayo ni daraja ya pili ya Dini baada ya Uislamu, na akasema: Imani ni kumuamini Mwenyezi Mungu, yaani: Unamuamini Yeye kuwa ni Mola, Muumba, Mwenye kutoa riziki, Mmiliki, na Mdhibiti wa kila kitu, na unamuamini kuwa ni Mwenyezi Mungu anayeabudiwa na kutiiwa, na unaamini kwamba Yeye ana Majina Mazuri Zaidi na sifa za juu kabisa.

12.  Kuamini Malaika, ni kuamini uwepo wao, na kwamba wameumbwa kutokana na nuru, wala hawamuasi Mwenyezi Mungu juu ya Amri zake, na wanafanya wanayoamrishwa, na kuamini malaika aliowataja Mwenyezi Mungu kwa majina yao. na kazi zao; kama Jibril ni mwenye dhamana ya kufikisha wahyi (ufunuo) na ndiye Malaika mkuu, na Mikaeli amekabidhiwa mvua na mimea, na Israfil amekabidhiwa kupuliza baragumu, na mlinzi wa moto, na kadhalika.

13.  Kuamini vitabu ni: Kuamini kwamba ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba ni lazima kuamini yaliyomo ndani yake na kufanyia kazi hukumu zilizothibiti, pia Qur`aan imekuja kufuta sheria zote zilizokuwa kabla yake, kwa kuwa Torati na Injili ni vitabu ambavyo vimepotoshwa na kubadilishwa.

14.  Kuamini Mitume ni: kuamini waliyoyaleta, na kwamba Mwenyezi Mungu amewateremshia amri yake, na kwamba wao ni bora katika viumbe wa Mwenyezi Mungu, tunawaamini wote, waliotajwa katika Qur-aan na Sunnah na sisi tunaijua hadithi yake, na ambaye hatujui chochote juu yake, na wala hatutofautishi baina ya yeyote kati yao. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Hakika wale wanao mkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, kwa kusema: Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa. Na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya (50) Hao ndio makafiri kweli kweli. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha (51) Na walio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, wala wasimfarikishe yeyote kati yao, hao atawapa ujira wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mwenye kurehemu”.

[An-Nisa: 150-152].

15.  Kuamini Siku ya Mwisho ni: Kuamini kufufuliwa na kuhesabiwa, na kuamini uwepo wa Pepo na moto, na Njia na Mizani, na Uombezi wa Mtume na Mto wa Al-Kawthar, na mambo mengine yote ambayo habari zake Zimethibitishwa Katika qur`ani na Sunnah.

16.  Kuamini makadirio ni: kuamini kwamba Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na utukufu, anayajua matendo ya waja na yatakayowapata, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliandika yote katika Ubao Uliohifadhiwa kabla ya kuumbwa viumbe, na kwamba matendo ya waja hufanyika kwa mujibu wa yale yalioandikwa katika elimu na maandishi ya Mwenyezi Mungu, na kwamba matendo ya waja wote yameumbwa na Mwenyezi Mungu. Kama vile kukanusha na kuamini, kutii na kuasi.[2]

17.  Kisha akamuuliza kuhusu Ihsani ambayo ni daraja la tatu la dini, akamwambia kuwa Ihsani ni mtu kuMuabudu  Mola wake kwa ukamilifu kabisa kana kwamba anamuona mbele yake. Ikiwa mtu hakufikia kiwango hicho cha kuhisi kumuona Mwenyezi Mungu na kuogopa, basi ahisi kuwa Mwenyezi Mungu, anamuona. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na mtegemee Aliyetukuka Mwenye nguvu, Mwingi wa Rehema (217) ambaye anakuona unapoinuka (218) na kugeuka kwako kwa kusujudu (219) kwa hakika yeye ni mjuzi na msikivu Zaidi. (219).

[Al-SShuaraa: 217 - 220]

Daraja za dini zote zimefungamana kwani; Uislamu ni wa neno la jumla zaidi kuliko imani na ihsan, na vyote viwili vimejumuishwa humo, imani imejumuisha zaidi kuliko Ihsani, kwa hivyo anayetoka katika daraja la imani bado ni Mwislamu, na anayetoka katika daraja la ihsani bado yuko kwenye cheo cha imani. Amesema Mwenyezi Mungu:

“Mabedui walisema: “Tumeamini.” Sema: “Hamjaamini.” Lakini semeni: “Tumesilimu.” Na Imani bado haijaingia katika nyoyo zenu”.

[Al- hujraat: 14]

18.  Kisha muulizaji akamuuliza kuhusu kiyama, Kitasimama lini? Yeye, (Rehma na amani ziwe juu yake), alisema: “Mwenye kuulizwa sio mjuzi zaidi kuliko muulizaji.” Yaani elimu yangu juu yake si zaidi ya yako. Hakuna ajuaye wakati wake isipokuwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu amesema

“Mwenyezi Mungu ana ujuzi wa kiyama”

[Luqman: 34].

19.  Basi akabadilisha swali hili kwa kumuuliza juu ya ishara zake, basi Mtume akamjibu kwamba moja ya ishara zake ni kwamba kijakazi atakapomzaa bosi wake, ambayo ina maana ya kwamba watumwa kuwa wengi mpaka kufikia kijakazi kumzaa binti wa bosi, hivyo huyo binti atakuwa ni mtu huru, hali ya kuwa mama ni kijakazi. Au kwa maana nyingine ni wajakazi kuzaa wafalme, Au: Wasiokuwa Waarabu kuzaa Waarabu, na Waarabu ni mabwana na watukufu wa watu.[3]

20.  Alama zake nyengine ni kuwa masikini waliokuwa wakitembea peku na bila viatu, nakuwa uchi na hawapati kitu cha kusitiri katika mavazi, wachungaji na mabedui, wanakuwa matajiri na wenye mali, na kuanza kushindana katika kujinga majumba ya kifahari. Na Pengine hii inarejea kwenye Hadith inayosema: “Iwapo jambo atapewa asiyestahili, basi ingoje kiyama”[4], kama mambo wanapewa wale wasiostahiki, mpaka wakawa mabedui na wajinga ndio viongozi wa watu, wakawa kati ya wanaomiliki mali na ufahari.[5]

21.  Kisha yule mtu akaondoka, na Umar akakaa kwa muda mfupi, kisha Mtume, amani iwe juu yake, akamwambia: Je, umemjua mtu huyu ni nani? Umar akasema: “Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanajua zaidi.” Akasema (Rehma na amani ziwe juu yake): Huyu ni Jibril, amekuja kukufundisha dini yenu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa Malaika uwezo wa kuchukua sura ya wanadamu viumbe wengineo, na Jibril, amani iwe juu yake, alikuwa akimjia Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, mara kwa mara katika sura ya Dahiya al-kalbiyyu swahaba wa mtume amani iwe juu yake. 

Mafunzo

  1. Jibril, amani iwe juu yake, alipoingia kwa Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) alikaa mkao wa mwenye kutafuta elimu akiwa makini na tayari kukubali elimu anayopewa, bila ya kuwa na kiburi licha ya utukufu wake. naye ndiye mwenye dhamana ya kufikisha ufunuo na ni Roho Mtakatifu. Hapo tunajifunza kuwa na adabu na ni kwa kila anaemuuliza mwanachuoni azingatie adabu hiyo katika kukaa naye, na wala asimuulize kwa sura ya mtu mwenye kiburi, mwenye kujitosheleza, kama vile kukaa kwa kuegemea, au kutoa sauti isiyofaa.

  2. Nguzo za Uislamu ni miongoni mwa mambo ya mwanzo ambayo Muislamu anatakiwa kuyasimamia katika mipango yake ya kila siku na kila mwaka, kujilazimisha kuzifuata, na kukamilisha kila moja katika utendaji wake: basi atazame nguvu ya kukiri kwake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuukamilisha kwa kumtaja sana Mwenyezi Mungu, na kuboresha Swala yake. Na azidishe kusali sala za sunnah, kama vile ibada zisizo za wajibu, na Sunna za kawaida, na mawaidha ya swalah, na kutoa zaka kamili kwa wema, na kutoa sadaka mbalimbali, pia kufunga Ramadhani na asiiharibu kwa kufanya madhambi, aongeze utiifu kwa kujitolea. Na Kuhiji Nyumba ya Mwenyezi Mungu hata mara moja, na kuongeza anachoweza, kama Hajj na Umra.

  3. Jitahidi kutekeleza kila nguzo ya imani, na jiulize moyo wako ulifanya nini katika kila nguzo hizo, na vipi imani yako kwa Mwenyezi Mungu juu ya kustahili kuabudiwa kwake, na uungu wake, majina na sifa zake? ni ipi thamani ya Malaika na heshima yao kwako? Na Unafuraha kiasi gani juu ya vitabu vya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa viumbe vyake, na kuvitukuza, hasa hasa Qur’an? Je! Kiasi gani unawaheshimu Mitume wake, na mapenzi yako kwao je, ni mapenzi yanayokuiteni kuuliza undani wa maisha yao, ni ipi thamani yenu kwa Siku ya Mwisho na je, mnaikumbuka daima? Je! ni kiasi gani unaamini makadirio Ya Mwenyezi Mungu? Na kuridhika na yote yanakukuta?

  4. Kiwango cha juu kabisa cha Dini ni daraja ya Ihsani, je umejaribu kujilazimisha kumuabudu Mungu kana kwamba unamuona, au usipomuona basi kumbuka kuMuabudu  Mwenyezi Mungu, na jua kwamba Yeye anakuona vizuri kuliko ungewezeshwa kumuona. Mwenyezi mungu si rahisi kuonekana kwako.

  5. Ikiwa mtu ana hakika na anahisi uwepo wa Mwenyezi Mungu, kuonekana kwake mbele ya Mwenyezi Mungu na uchunguzi wake juu Yake, basi angeona aibu MwenyeziMungu kumuona mvivu katika kumtii, achilia mbali kumuona akifanya uasi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    “Na mtegemee Aliyetukuka Mwenye nguvu, Mwingi wa Rehema (217) ambaye anakuona unapoinuka (218) na kugeuka kwako kwa kusujudu (219) hakika yeye ni mjuzi na msikivu.

    [As-Shuaraa:217-220]

  6. Uislamu umeitukuza siku ya mwisho, japo haukubainisha wakati wake, lakini ikajulishwa dalili zake, nazo na nyenginezo zinatuhimiza kuikumbuka siku hiyo mara kwa mara, je ni lini tulikaa kuifikiria siku ambayo haiepukiki? 

Marejeo

  1. tazama “Sharh Riyadh as-Salihin” cha Ibn Uthaymiyn (1/347).
  2. “Jami’ al-Ulum wa al-Hakam” cha Ibn Rajab (1/103).
  3. Tazama: “Jami’ al-Ulum wa al-Hakam” cha Ibn Rajab (1/136-137).
  4. Imepokewa Na Al-Bukhari, Na.: (59), Kwa Kutoka Kwa Abu Hurairah
  5. Tazama: “Jami’ al-Ulum wa al-Hakam” cha Ibn Rajab (1/139).

  1. Amesema Mtume (Rehema na Amani zimshukie) kuwa Dini ni kupeana nasaha, na nasaha ni neno la ujumla linaloashiria kuwa mtu afanye bidii kuwafanyia wema wengine, Kwani kunasihi ni kama kuilinda Asali kutokana na uchafu.[1]Mtume (Rehma amani ziwe juu yake) akaifanya dini yote katika kupeana nasaha kwa sababu ya kuonesha utukufu wa jambo la kupeana nasaha, ingawa kuna mambo mengi katika dini lakini nasaha imepewa kipaumbele katika utukufu, kama Waarabu wanavyosema: Mali ni Ngamia.[2]

2.  Maswahaba wakauliza: Nasaha hii inatakiwa kwa ajili ya nani? Mtume (Rehma na amani ziwe Juu Yake) akawajibu kwa kuwabainishia kwa kusema:

3.  Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, maana ya “Nasaha” kwa Mwenyezi Mungu ni kumsafishia na kumtakasia Ibada yake kama inavyohitajika katika imani na matendo.

4.  Nasaha Kwa Kitabu Chake kitukufu, inayojumuisha utakaso wa kimatendo: ikiwemo kukiheshimu, kukifuata, na kukipenda.

5.  Nasaha kwa Mtume Wake, (Rehema na amani ziwe juu yake), inayojumuisha utakaso wa kimatendo: ikiwemo kumheshimu, kumfuata, na kumpenda.

Miongoni mwa nasaha kwa Mtume (Rehma na amani ziwe Juu Yake) ni kuyaeleza hayo katika familia na ndugu na jamaa. 

6.  Ama maimamu wa Waislamu ni Viongozi na Wanazuoni, nasaha kwao ni kujitahidi kufanya yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu kwa upande wao, ikiwa ni pamoja na kuwatii katika wema, na kuwasaidia kutenda mema, na kuswali nyuma yao, na kupigania dini pamoja nao, na kutowafanyia uadui na maasi, na Kutowafuata wanapoteleza na kukosea. na kuwatetea kwa misingi ya haki.[3]

7.  Ama nasaha kwa Waislamu wote ni kuwanasihi katika kufanya juhudi kwa kufanya yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu ili kuyafikia maslahi ya dini na dunia yao.Na hii ndio maana pana zaidi, na kwa ajili hiyo Mtume (Rehma na Amani zimshukie), akaweka kiapo cha utii kwa maswahaba zake juu ya kunasihi, na hiyo ni katika hadith Kutoka kwa Jarir bin Abdullah Al-Bajali amesema: “Niliweka kiapo cha utii kwa Mtume (Rehma amani ziwe juu yake), juu ya kusikiliza na kutii, na hayo Mtume alinitamkisha kiasi nilichoweza, ikiwemo kumnasihi muislam.[4]”Uhalisia wa nasaha uko kwa mtu mwenyewe, Kwani hulipwa kwa kufanya hivyyo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu hana haja ya kuomba Ushauri kwa yeyote[5]. 

Mafunzo

  1. Tamim alikuwa si muislamu, akasilimu mwishoni mwa uhai wa Mtume (Rehma na Amani zimshukie) na akapigania dini pamoja naye, na akawa mfanya ibada mzuri sana, mwenye kusimama kuswali swala za usiku, na msomaji wa Qur’ani. Hapo tunajifunza kuwa Ikiwa iliwezekana kwa mtu ambaye alikuwa si muislamu, kufanya hayo yote basi wewe usikate tamaa au kumkatia tamaa ndugu yako, bali endelea kufanya bidii katika kujifunza na kufanyia kazi elimu yako. 

  2. Kuyabeba majukumu, na kuyatekeleza kwa bidii  na nia njema, ni katika nasaha, kwa kutimiza wajibu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Kitabu chake, na Mtume wake, na Viongozi wa Waislamu na watu wote.

  3. Je, umewahi kutoa jihudi zako za dhati kwa ajili ya Mwenyezi mungu? Jihesabu mwenyewe na kumbuka haki zake juu yako, ikiwa ni pamoja na kumuamini, kutomshirikisha na chochote, kumtii, kuitikia wito wa swala na mambo mengine, na kuwa na nia thabiti katika aliyoyaamrisha na kukataza, na kumpenda zaidi na kumnyenyekea. 

  4. Je, umewahi kutoa jihudi zako za dhati kwa ajili ya kitabu cha Mwenyezi Mungu? Jihesabu mwenyewe na kumbuka haki zake juu yako, ikiwemo: kukiamini, kukisoma mara kwa mara, kutafakari maana yake, kuwalingania watu ili kukiamini na kukisoma, na kukilinda dhidi ya wanao potosha maneno au maana zake, pia kukiheshimu kwa utakatifu wake, na kisishikwe ila na mtu msafi aliye toharika kutoka na uchafu mkubwa na mdogo na kwamba mtu asikiweke kitabu hicho sehemu isiyofaa[6].

  5. Je, umewahi kutoa jihudi zako za dhati kwa ajili ya Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu? Jihesabu mwenyewe na kumbuka haki zake juu yako, ikiwa ni pamoja na: kumuamini, kumtii katika yale aliyokuja nayo, kuacha kufanya ambayo hakuyafundisha, kuheshimu haki yake, kumuusia, kumuenzi, kumuunga mkono, kumnusuru, kuhuisha mwenendo wake katika kueneza ulinganizi wake, na kukanusha tuhuma katika kila analolisema na kulitamka [7] halikadhalika kuwaheshimu maswahaba zake, na kuwatukuza, na kuwapenda. Kwa sababu maswahaba wa mtu ndio wanaomsaidia na kumuhami.

  6. Je, hujudi ipi umeifanya kwa ajili ya Viongozi wa Waislamu, na Watawala na Wanachuoni, na hukumu yao kwako...? Ikiwa ni pamoja na: kuwatii kwa haki, kuwasaidia kwa masilahi ya dini na dunia, kuwakumbusha pale wanapoghafilika, na kuwaita kwa ajili ya nasaha, na kutowadanganya katika nasaha, au kuwasifia zaidi ya stahiki zao na kuwapongeza katika batili pale wanapo kuwepo[8]. 

  7. Je, umejitolea kwa ajili ya Waislamu wa kawaida? Ikiwa ni pamoja na: kuwaelekeza katika yale yenye maslahi kwao, na kuwasaidia katika mambo ya Dini yao na mambo yao ya kidunia kwa kauli na vitendo, na kuwazindua walioghafilika, na kuwaelimisha wajinga, na kutoa sadaka kwa masikini, na kusitiri madhambi yao, na kuwaondolea madhara, na kuleta manufaa. katika Dini na dunia, na kuwatakia kheri duniani na Akhera, na kuacha kuwaudhi, Na kuwatakia yale anayoitakia nafsi yake[9]. 

  8. Maana moja wapo ya nasaha ni kuwatahadharisha watu juu ya kosa wanalolifanya, ikiwa wanafanya baya watakemewa hatua kwa hatua kwa mujibu wa daraja za kuondoa makosa, na kwa kuzingatia maslahi, hata ikiwa ni kwa njia ya kushitaki kwa watawala, yote haya yamo katika kunasihiana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. na haya ni katika mafundisho ya Mtume (rehema na amani ziwe juu yake), na ni muongozo wa maswahaba zake, Mwenyezi Mungu awawie radhi.Na Katika nasaha ni mtu kunasihiwa kwa siri kwani mtu akinasihiwa mbele ya watu, huchukia. Kwa sababu hiyo, Al-Fudayl bin Iyad amesema: Muumini hustiri na kunasihi, na muovu hutukana na kudhalilisha[10].

  9. Kuwashauri wenye mamlaka na madaraka ni kwa kadiri ya uwezo, mtu akihisi kuwa hawezi kupata madhara yao ikiwa atajitokeza kuwashauri, basi awausie, na ikiwa atajihofia basi inatosha kuchukia tu moyoni mwake, na ikiwa anajua kuwa hawezi kuwashauri, basi asifanye mfano wa matendo yao, Kwani akifuata vitendo vyao atakuwa anawahadaa na kuwazidishia fitina, hata kufikia kukosa dini yake.

  10. Hekima ya mwenye kutoa nasaha kwa watu ni kutoa nasaha kwa njia ya fumbo, isipokuwa kwa wale wasioelewa mafumbo, na lisiwepo sharti la kukubaliwa nasaha hizo, bali mtu anapaswa kutekeleza wajibu wake katika kunasihi. Na endapo anaenasihiwa akifanyia kazi nasaha hizo alizopewa hilo ndio bora zaidi, na kama hatozifanyia kazi basi atapata malipo ya kumnasihi ndugu yake.

  11. Moja ya njia za nasaha: ni kubainisha Hadith sahihi na dhaifu, na kuwafafanulia wasimulizi wa hadith, na ni nani anayefaa kujifunza kwake na asiyefaa – na hiyo inafanyika kwa mwenye ujuzi na elimu hiyo-. Aliulizwa Ahmad bin Hanbal: Mtu anayefunga na kuswali na kujitenga ndio anapendeza kwako, au anaezungumza dhidi ya watu wanaozua katika dini? Akasema Imaam Ahmad: Akisimama na kuswali, na akafanya I’tikafu, matendo hayo ni kwa ajili yake mwenyewe, na ikiwa anazungumza na kubainisha watu wa uzushi, basi hii itakuwa ni kwa masilahi ya Waislamu.[11]  na hii ndiyo bora zaidi. hivyo basi Mlinganiaji na Mwanasheria- Mjuzi - wanapaswa kuzungumzia mambo haya kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, akihesabu hilo katika kunasihi kwa ajili Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

  12. Jarir bin Abdullah (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) alipokuwa akiuza bidhaa anamuonesha mnunuzi dosari za bidhaa hiyo, kisha akamhiyarisha kwa kusema: Ukitaka nunua, na ukipenda ondoka, siku moja akaambiwa: Ukifanya hivo si bidhaa zako hazitoisha? akasema: (Niliweka kiapo cha utii kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu juu ya kutoa nasaha kwa kila Muislamu[12] . Na Ushauri haukomei tu katika kutoa maoni na kuinusuru dini, lakini Ushauri unatakiwa katika mambo yote. Mfanyakazi ananasihiwa katika kazi yake ili kuifanya kwa ukamilifu, na mfanyabiashara ananasihiwa kuwafahamisha watu juu ya kasoro za bidhaa yake, na Daktari anashauriwa kukamilisha kazi yake na kutoa dawa kwa ufanisi hata kama bei iko chini, na mwanafunzi anashauriwa kutafuta Elimu na kuwasaidia ndugu zake katika elimu hiyo kwa manufaa yake na taifa lake na kadhalika.

  13.  Amesema Mshairi:Nipe nasaha kwa uhuru kabisa ninapokuwa peke yangu = wala usininasihi katika mkusanyiko wa watu.Kwaani kumnasihi mtu mbele ya watu ni aina ya lawama ambazo sipendi kuzisikiliza.Ikiwa mtakataa na kupinga maneno yangu = basi msifadhaike pale mtakapovunjiwa heshima.

Marejeo

  1. Tazama: “Alam Al-Hadith” cha Al-Khattabi (1/189), “"Almuealim Bifawayid Muslimin" ” Cha Al-Maziri (1/293).
  2. Tazama: “Kashf al-Mushakil kutoka kwa Hadith ya Sahih mbili” ya Ibn al-Jawzi (4/219), na “Riyad al-Afham fi Sharh Umdat al-Ahkam” cha al-Fakhani (1/346).
  3. Tazama: “Sharh Riyadh as-Salihin” cha Ibn Uthaymiyn (2/393).
  4. Imepokewa na Muslim No.: (56).
  5. Tazama: “Alam Al-Hadith” cha Al-Khattabi (1/191).
  6. Tazama: “Al-Mufhim” cha Al-Qurtubi (1/243), “Sharh Riyadh Al-Salihin” cha Ibn Uthaymiyn (2/388).
  7. “Alam Al-Hadith” (Ufafanuzi wa Sahih Al-Bukhari) cha Al-Khattabi (1/192).
  8. Tazama: “Alam al-Hadith” (Sharh Sahih al-Bukhari) cha al-Khattabi (1/193), ““Almafham Lima 'Ushakil Min Talkhis Kitab Muslimin"” cha al-Qurtubi (1/244).
  9. Tazama: “"'iikmal almuealim bifawayid muslimin"” cha Al-Qadi Iyad (1/307), “Al-Kawakib Al-Darari fi Sharh Sahih Al-Bukhari” cha Al-Karmani (1/218).
  10. Tazama jamie aleulum walhakmi" " cha Ibn Rajab al-Hanbali (1/225).
  11. Majmuu’ al-Fatawa” cha Ibn Taymiyyah (28/231).
  12. Tazama (Ufafanuzi wa Sahih Al-Bukhari cha Ibn Battal (1/131).


Al-Abbas, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, anasimulia kutoka Kwa Mtume (Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) akisema:

  1. Imani ina ladha na utamu, na Mtume (Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) alitumia neno “ameonja” ingawa si kimininika wala si chakula, katika kuwakilisha maana yake; kwani Iwapo mtu ataonja chakula na kinywaji na akahisi ladha, basi pia anahisi athari ya Imani katika nafsi mtu ambaye imaan imemuingia na kukita katika nasi yake.[1]Na Miongoni mwa maana ya ladha hii ni kufunguka kwa moyo, na utulivu wa akili, na kuwa na raha ukiwa mbele ya Mwenyezi Mungu, hivyo mtu anakuwa hapendelei madhambi bali anajiepusha nayo, na kufanya mambo ya faradhi kwake inakuwa vyepesi, hali hii inamfanya kuvumilia tabu zote, wala hakati tamaa na Rehema za Mola wake Mlezi bali huridhika na makadirio yake juu yake, na ladha hii nzuri na tamu haipatikani ila kwa masharti.

2.   Sharti la kwanza ni kuridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndio Mola Mlezi, na kuridhika maana yake ni: kukinaika na kitu na kutosheka nacho dhidi ya kitu kingine, na kutosheka na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kuamini habari zake, na kusalimu amri kwake, na kuwa na subira na kujipa moyo katika hukumu Zake za makakadiro yake.Na kuridhika hapa hakukusudii kukiri uwepo wa Mwenyezi Mungu tu, kwani kukiri uwepo wake ni sharti la msingi katika Uislamu, lakini kinachokusudiwa ni kuridhika maalumu, ambako ni kuridhika Mwenyezi Mungu kuwa ndio Mtawala katika Maisha yake, na Muumba, mwenye kumuwekea sheria, na ameridhika na hukumu zake na kuridhia sheria yake, hivyo anamuabudu, anampenda, anamkubali, anamtegemea na ni muaminifu kwake, na hakuna mwingine anayeogopa woga wa siri tofauti na yeye, na kuridhika katika hukumu yake na makadirio yake. Na mtu huyo hafanyi lolote la kumkasirisha Mola Mlezi.[2] 

3.   Sharti la pili: kuridhia Uislamu kuwa ndio dini ya kweli, na hii ina maana ya kukubaliwa kisheria; hivyo basi anafuata maamrisho na kuacha makatazo, na amechagua Uislamu juu ya dini zote, na akaufanya kuwa nguzo yake imara ambayo ndio kimbilio na tegemeo lake, ambalo anapenda na kuchukia kwa misingi ya dini hiyo, na yupo tayari kutoa sadaka na kila chenye thamani ya kwa ajili yake.

4.   Sharti ya tatu: kuridhia kwamba Muhammad (rehma na amani zimshukie) ni Nabii wa kweli aliyetumwa, na hii ni pamoja na kuamini kuwa yeye ni mjumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kuyakubali aliyoyaleta kutoka kwa Mwenyezi Mungu, katika maamrisho na makatazo, na kuikubali Sheria hiyo, na kuithibitisha, na kutenda na kusalimu amri. Na kuridhika kwa wapenzi wanaomfuata, na wanaoongozwa na muongozo wake, na wanaomuiga, wanaofuata utiifu wake, na wanaojitolea maisha yao na vitu vyao vya thamani kwa ajili ya kulinda mienendo yake, na wanashauku ya kukutana naye.Hii inaonyesha kwamba hakuna mtu anayekuja na dhana ya imani isipokuwa ana misingi mitatu ya dini. Kumuamini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake na dini yake.

Mafunzo

  1. Al-Abbas bin Abdul-Muttalib, alimuamini mtoto wa ndugu yake, japo kuwa alikuwa mkubwa kuliko yeye, na kwa sababu hiyo alivumilia maudhi na uadui wa watu wake na familia yake, na hili ni tabia inayomsukuma mtu mwenye akili timamu. kukubali ukweli kutoka kwa mtu yeyote, awe Mkubwa au mdogo, na awe mwenye nguvu au dhaifu, tajiri au maskini.

  2. Al-Abbas, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, alithibiti pamoja na Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) wakati masahaba zake wengi walipokimbia siku ya vita vya Hunayn. Hii inaashiria ukweli wa Uislamu wake na kuipata ladha ya Imani licha ya kuwa alikuwa mgeni katika uislamu (yaan hakuwa na siku nyingi ameingia katika uislamu). Sasa inakuwa vipi kwa mtu aliyezaliwa katika Uislamu au amekaa ndani yake kwa miaka mingi na bado anamuabudu Mungu kwa kutegea?! tujitahidi kuthibitisha Imani katika vifua vyetu., ili tuwe kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    “Miongoni mwa Waumini wapo watu wanaotimiza ahadi zao kwa Mwenyezi Mungu”

    [Al-Ahzab: 23].

  3. Imani ina ladha ambayo hawezi kuitambua mtu aliyeishi katika imani hiyo kwa muda kwa sababu hatambui uhalisia wake, au hakuhisi thamani yake na vitu vingine. Basi Kila unapojiona unapendelea starehe za dunia kuliko starehe za imani, ikumbushe nafsi yako na ihimize kutafuta ladha ya Imani.

  4. Tafuteni radhi Radhi za Mwenyezi Mungu kwa kukumbuka kuwa Yeye ni Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima, Mjuzi wa yote, na sifa zake nyinginezo ambazo ndani yake nafsi hutulia kwa kuamini habari zake, na kusalimu amri kwa kufuata maamrisho na kuacha makatazo Yake, na kutulizana juu ya makadirio yake, na kwa kukumbuka neema zake za wazi na zilizofichikana, na kwamba yale tuliyokuwa hatuyajui katika neema zake ni makubwa zaidi. Na yale tuliyokuwa hatuyajui kuhusu uumbaji wake na hekima yake katika kuyasimamia ni makubwa kuliko tunayoyajua.

  5. Ridhika na Uislamu kuwa ndio dini kwa kujua kuwa ni sheria ya Mwenyezi Mungu, ambayo hakuna mjuzi Zaidi yake, wala mwenye hekima kuliko yeye, wala hakuna mwenye huruma kuliko Mwenyezi Mungu, na kwamba mwenye Akili anajua ukamilifu wake wa wazi kiasi ambacho kinamtosha kuridhia yote asiyoyajua.

  6. Tosheka kuwa Nabii Muhammad ndio Mtume wako, kwa kukumbuka ukamilifu wake katika kila tabia za kibinadamu, ikiwa ni pamoja na utimilifu wa elimu na akili yake, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu juu yake na kuhifadhiwa kwake. kumbuka kujitoa muhanga kwa ajili ya ummah wake, na huruma yake kwao, na kwamba akilinganishwa Mtume na watu wengine, mapungufu ya viumbe vyote yatadhihirika mbele ya Mtume (Rehma na Amani zimshukie). 

  7. Dunia hii, licha ya dhiki, uchovu na dhuluma ziliyomo ndani yake, inakuwa ni pepo kwa Muumini kwa kule tu kuridhika, kunyenyekea na Kuamani, ndio maana ikasemwa: “Kuridhika ni Pepo ya Duniani, na starehe kwa wanaojua”. Hivyo basi tunaweza kuingia katika pepo na bustani yetu duniani kwa kuridhika! Muislamu akipatwa na msiba au akakosa mlango wa riziki na kheri, anasalimisha amri yake kwa Mola wake mlezi, na anaamini kuwa hakuna litakalotupata isipokuwa lile aliyotuandikia Mwenyezi Mungu litupate. Na hapo muumini anahisi utuilivu, na anasalimika kutokana na kukata tamaa kwa aliyoyakosa.

  8. Amiri wa waumini, Omar bin Abdul Aziz, alikuwa akiomba dua hii: “Ewe Mola wangu niridhishe kwa amri yako, na unibariki katika kudra yako, niepushe kupenda kuharakisha ulichochelewesha, wala kuchelewesha ulichoharakisha”[3].

  9. Aliulizwa Yahya bin Muadh: Ni lini mja anafikia Daraja la kuridhika? Akasema: Akisimama katika misingi minne katika yale anayomridhisha Mola wake, kwa kusema akimwambia Mola wake: ewe mola wangu Ukinipa napokea, na ukininyima naridhika, na Ukiniacha nazidhisha kukuabudu, na ukiniita nakuitikia[4]). Ni lazima tujichunguze wenyewe; Je, tuna sifa hizi? Kwa kadiri tulivyo na sifa, tumefikia daraja la kuridhika.

  10. Amesema Mshairi:Kuridhika kwako ni bora kuliko Dunia na vilivyomo,,,,, Ewe mwenye kuimiliki nafsi, idhibiti na uiweke karibu.Roho haiwezi kukamilisha matarajio yake,,,,, bila ridhaa yako hata kidogo.Kunitazama kwako ewe ninayekuomba na kukutarajia,,,,,, ni bora kwangu kuliko dunia na vilivyomo.

Marejeo

  1. Tazama: sharh almushkat llttiby alkashif ean haqayiq alsunan (2/446).
  2. Tazama: Almifham Limaa 'Ashkal Min Talkhis Kitab Muslim ) Cha Al-Qurtubi (1/210). Al-Fatwa Al-Kubra Cha Ibn Taymiyyah (2/393).
  3. Tazama: “"'Adab Almurtaeaa Fi Eilm Aldduea"” Cha Ibn Abd Al-Hadi (Uk. 164).
  4. Tazama:“Lawame’ al-Anwar al-Bahiya” cha al-Saffarini (1/359).


  1. Mmoja wa wanachuoni wa Kiyahudi - Ka'b al-Ahbar aliyesilimu baada ya hapo [1]- alikuja kwa Umar bin al-Khattab, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, akamwambia kuwa anawahusudu Waislamu kwa aya, iliyoteremshwa ndani ya Qur’ani Tukufu, na kwamba Mayahudi walitamani ingeteremshwa kwao hata mfano wake, kwa sababu wangeliitukuza siku ile iliyoteremshwa, na wakaifanya kuwa ni sikukuu yao.

  2. Omar, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alimuuliza kuhusu aya hiyo, na mtu huyo akamwambia kuwa ni kauli ya Mwenyezi Mungu:

    “Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini.”

    [Al-Ma’idah: 3].

Bali Mayahudi waliifurahia Aya hiyo kwa sababu ndani yake mna habari za kukamilika kwa dini, na hupatikana kwa mambo. Ikiwa ni pamoja na: kukamilika kwa sheria, mipaka na wajibu, kuwafukuza washirikina kutoka katika Msikiti Mtakatifu na kutoingia humo, utukufu wa Uislamu na kudhihiri kwake, kudhalilisha ushirikina na watu wake, kuondolewa kwa khofu ya adui, na kuondolewa kwa (Naskhi)kufutwa katika dini hakuna kufuta hukumu au dini nyinginezo, kwa kuwa Uislamu ndio dini ya mwisho, na ushindi wa Makka.[2] Pia kutokana na ukamilifu wake ni kwamba hakuna mgongano baina ya maandiko yake, wala baina yao na akili iliyo wazi na timamu, na kwamba uislamu ni dini ambayo ni halali kwa jamii mbili katika kila wakati na mahali, na kwamba sheria yake inazingatia haja za mwanadamu, hutimiza matakwa yake, na kumletea usalama na utulivu miongoni mwa wanachama wake. Na ndani yake kuna utimilifu wa neema kwa kudhihiri sheria, kupatikana kwa usalama, kueneza dini duniani kote, na tamko la kuridhishwa na Mwenyezi Mungu na dini ya Kiislamu, kwa hivyo hakuna kufutwa ndani yake baada ya leo, na hakuna sheria nyengine itakayoifuta sharia yenu, kwani ndiyo dini ya mwisho[3] 

3.   Kisha Umar Mwenyezi Mungu amridhie, akamwambia kuwa Waislamu wanajishughulisha zaidi na wahyi kuliko nyinyi, kwani sisi tunaujua wakati na mahali pa kuteremka Aya hiyo, na tunaiheshimu. Imeteremshwa kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam alipokuwa amesimama Arafah, na ilikuwa siku ya Ijumaa, kwa hivyo tuna sikukuu mbili, si sikukuu moja. Sikukuu ya kila wiki ni siku ya Ijumaa, na siku ya Arafa, ambayo ni sikukuu ya Waislamu pia, amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: “Siku ya Arafa, siku ya kuchinja, na siku za al-Tashreeq ni sikukuu zetu, watu wa Uislamu, na ni siku za kula na kunywa”[4].

Mafunzo

Maadui wa Uislamu wanausoma vizuri Uislamu katika kutafuta tuhuma wanazozitoa, hivyo basi kila mtafutaji elimu ni lazima ajiandae kuulinda Uislamu na kuondosha tuhuma za wenye shaka.

  1. Usidanganywe kwa kufanya amani na makafiri; Hao ndio wenye wivu zaidi wa Waislamu kwa yale waliyopewa.

  2. Wasiokuwa Waislamu wanatuhusudu kwa wahyi aliotupa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mmeghafilika kuusoma na kuelewa maana zake!

  3. Fahamu kwamba Uislamu ni Dini iliyokamilika isiyo na upungufu, na hakuna mgongano baina ya maandiko yake na baadhi yao, wala baina yao na akili iliyo wazi. Ukiona mgongano au udanganyifu wa kutokamilika, basi rejea kwa watu wa elimu, watakutatulia tatizo, watakufafanulia mambo usiyo yaelewa, na waondoe utata unaofikiriwa.

  4. Sikukuu haziwi kwa rai na ijtihad, bali ni kwa kuziwekea masharti. Usisherehekee kile ambacho Sharia haikukitolea tamko, katika sikukuu za mataifa yaliyotangulia.

  5. Muislamu anatakiwa ajifakhiri kwa dini yake, ajifunze elimu ya sheria, na ajifakhiri nafsi yake kwamba awaone makafiri ni watu wasiojua dini yao, au kwamba kafiri ni mjinga wa dini yake. 

  6. Mshairi alisema: Qur-aan iliteremka, kujenga umma bora = mpaka kukamilishwa dini na neema Ya Sayyid al-Ahrar, Ya Ras al-Aba =  Ewe rehema kwa walimwengu natamani ungedumu milele. Umetekeleza agizo la Mwenyezi Mungu peke yako na kubeba = agizo ambalo bendera zilielemewa kubeba

8.   Wengine walisema: Manabii walikuja na miujiza, na ikaisha = na ukatujia na hekima isiyomalizika Aya zake, kadiri muda unavyo zidi kuwa mrefu, huwa mpya = unazipamba ukuu wa ukombozi na ukale. Neno la heshima kutoka kwake = ni kukuusia juu ya ukweli, uchamungu, na kuunga udugu.

Marejeo

  1. Tazama: “Fath Al-Bari” cha Ibn Hajar (8/270).
  2. Tazama: “Zad al-Masir fi ‘Ilm al-Tafsiir” cha Ibn al-Jawzi (1/ 513), “Al-Mufhim Lama Ashkal min Takhlis Kitab Muslim” cha al-Qurtubi (7/ 339), “Tafsir Ibn Rajab al-Hanbali” (1/ 384).
  3. Tazama: “Al-Mufhim Lama Ashkal min Takhees Kitab Muslim” cha Al-Qurtubi (7/ 339).
  4. Ilijumuishwa na Abu Dawood (2419), Al-Tirmidhi (773) na Al-Nasa’i (4186).


  1. Amesema Mtume (Rehema na Amani zimshukie) kuwa Imani ni kama mti wenye matawi ambayo mengine yako katika daraja ya juu kuliko mengine. Na Mtume, (Rehma na amani Ziwe Juu Yake) amesema kuwa imaan imegawanyika katika sehemu sabini na zaidi, na hiyo ziada ni kati ya tatu hadi tisa, hivyo ni kana kwamba alisema: Imani ni kati ya sabini na tatu hadi sabini na tisa.

Na kusema kwake: “au: sehemu sitini” ni shaka ya msimulizi, na utofauti huo katika kubainisha idadi haina shida, kwa sababu kinachokusudiwa ni kuonyesha wingi wa daraja za Imani. Baadhi ya wanazuoni wamejaribu kubainisha migawanyiko hiyo kwa kutaja matendo mema katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake, na hizo ni jitihada za makadirio tu.

2.   Kisha Mtume (Rehma na amani Ziwe Juu Yake), akabainisha kuwa daraja bora kati ya hizo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu, nayo ni kusema Hapana Mola anaeabudiwa kwa haki Isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja. Na kinachokusudiwa sio kutamka tu. bali ni kuiimarisha kauli hiyo na kuifungamanisha na elimu, Yakini, ukweli, nia thabiti, upendo, utiifu, na yanayofungamana nayo, halikadhalika kukanusha kila kinachoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na kujiepusha na ushirikina mkubwa na mdogo.

Mgawanyo huu ndio msingi wa Imani. Kwa kuwa hayatakubaliwa matendo ya mtu pasina misingi hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

“Na anaye tafuta dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwake, na siku ya mwisho atakuwa miongoni mwa walio khasirika.”

[Imran: 85].

3.   Tawi la chini kabisa kwa ubora ni kuondosha chochote kinachowadhuru watu katika njia zao; Kama vile miiba, mawe, uchafu, misumari, vitu viliyokwama, na mengineyo. ikiwa mtu ameamrishwa kuondosha madhara njiani, hata kama sio yeye aliyeweka, basi kuepuka kuweka maudhi ni jambo bora zaidi.

4.   katika daraja za Imani ni kuwa na staha (aibu), ambayo ni tabia inayohitaji kufanya Wema na kuepuka Maovu, sawa sawa Tabia hii ipo kwa mtu na akawa anadumu nayo, au hakuwa nayo hapo awali lakini akajitahidi kuwa nayo. Staha ni Tabia anayoifahamu mtu mwenyewe kwa baadhi ya nyakati, na Faida za staha ni kwamba Mwenyezi Mungu asikuone pale alipokuzuia, wala asikukose pale alipokutaka uwepo. Maelezo Yaliyotangulia yanaonyesha kwamba Imani ni kusema(kuitamka), kutenda, na kuitakidi. hivyo basi kusema “hapana Mola anaeabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja” ni kusema na kutamka kwa ulimi na kuitakidi moyoni, ikifuatiwa na kutenda kwa viungo, kwa hiyo kuondosha maudhi njiani ni katika matendo ya viungo, na staha ni katika matendo ya moyo, hata kama Athari yake inaonekana kwenye ulimi na viungo.

Mafunzo

  1. Abu Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa ni swahaba wa Mtume (Rehma na amani Ziwe Juu Yake), na mwanachuoni mkubwa, na alikuwa kiongozi katika baadhi ya Miji mikubwa, Pamoja na hayo alikuwa miongoni mwa watu wenye unyenyekevu, upole na Utiifu. Katika hili tunaweza kujiuliza “Ni kiasi gani cha unyenyekevu wetu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu ametupatia kama ujuzi, cheo, au mali”?

  2. Imani ni kitu kikubwa zaidi, na ndicho anachokitaka Mwenyezi Mungu kutoka kwa waja wake, na imaani ina matawi na daraja nyingi, hivyo basi kiasi gani tunajifunza daraja hizo? na ni kiasi gani tunafanya juhudi kukamilisha alichokusudia Mwenyezi Mungu katika hizo daraja? Au sisi tumelidhika na baadhi ya daraja hizo na kupuuza nyingine? 

  3. Kuna Baadhi ya watu wanaowashutumu wenzao kwa kupuuza kwao baadhi ya sehemu za Imani, na kusahau kuwa huenda wao wenyewe ni wazembe katika sehemu nyingine ya Imani, mfano kuna mtu anajitahidi katika kutekaleza ibada ya saumu na swala, na anakuwa mzembe katika kuwa na tabia njema zenye masilahi ya watu wengi. Au unakuta mtu mwingine anajitahidi katika upande wa kuwa na maadili mema na anasahau wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu, yote haya yanatupeleka kuwa wapole kwa watu, na huhesabu nafsi zetu wenyewe kwa mujibu wa mizani ya kisheria, sio kama tuliyozoea.

  4. Imani ina daraja za juu na za chini, na zote Mwenyezi Mungu Mtukufu anazipenda, hivyo basi mtu asijishughulishe na ya chini kabisa akaacha ya juu, kwani katikakati ya hizo kuna daraja zaidi ya sabini, kwa hivyo bidii zetu na kutafuta kwetu daraja za juu ni jambo kubwa na bora zaidi, na pia tutambuwe hitajio letu kwa wanachuoni, na tuzidishe kutafuta elimu ya kisheria Kwa mujibu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Sunnah za Mtume Wake, ili tupate Kujua vipaumbele vya Sheria.

  5. Imani bora kabisa ni kusema: “hapana Mola anaeabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja” hivyo Basi tunahaja ya kujifunza maana zake, na jinsi ya kukamilisha matakwa yake, na kutamta maneno haya huku tukizijaza nyoyo zetu kwa mapenzi, unyenyekevu, na kuyakubali yote yaliyofungamana na kauli hiyo, kama vile maneno, itikadi, na matendo.

  6. Katika Kuondoa maudhi njiani yanaingia matendo mbalimbali ya watu katika maisha yao ya kila siku, ikiwemo: kuondoa kila kinachowadhuru watembea kwa miguu na magari, kama mawe, misumari, mabaki ya matairi, na mtu anaweza kuondoa mwenyewe au kuwaeleza wanaohusika kuyaondosha.

  7. Iwapo kuondoa maudhi njiani ni katika imani, basi kujiepusha kuweka maudhi njiani ni katika matendo mema, kwani kuwadhuru Waislamu na watu kwa ujumla ni katika matendo mabaya saana, na imetumika neno Maudhi hapa kwa ujumla, likijumuisha maudhi ya kihisia (yaani yanayoonekana)  kama vile kutupa mabaki ya makopo, kuweka magogo njiani, au maganda ya matunda n.k. na maudhi ya kimaana (yaani yasioyoonekana), kama vile sauti za kuudhi, harufu mbaya, na kukera watu katika namna ya kuendesha gari au kusimamisha gari katikakati ya barabara kwa muda mrefu bila sababu ya msingi, na ikiwa imekatazwa kufanya maudhi barabarani, basi ni halali kufanya kinyume chake yaani kufanya matendo mazuri, kama vile kuwarahisishia watu kwa kuweka vituo vya kupumzikia, na wepesi barabarani, kama miavuli na sehemu za kupumzikia, na hii imeashiriwa katika maneno ya Mtume (Rehma amani ziwe juu yake): “Jihadharini na kukaa njiani.” Maswahaba Wakasema: (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika sisi) Tunalazimika kukaa maeneo hayo! tukizungumza. Mtume (Rehma amani ziwe juu yake) Akasema: “Basi mkichagua kukaa mahala hapo, basi ipeni njia haki zake” maswahaba Wakauliza ni ipi haki ya njia? Mtume (Rehma amani ziwe juu yake) Akasema: “Kuinamisha macho, kujiepusha na maudhi, kuitikia salamu, kuamrisha mema na kukataza maovu”[1].

  8. Kuna malipo makubwa katika kuondosha maudhi njiani, hata kama watu hawaishi katika hizo njia, hivyo basi ni vizuri zaidi kuondoa madhara kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu, na maeneo yao ya makazi, kama vile sehemu za kazi, na sehemu za kujifunzia, na vile vile majumbani; Na kusafisha nyumba ya familia kuna fadhila nyingi, kwa sababu ya kufanya hivyo ni kuunga udugu  na kutimiza haki zao, na kuondoa maudhi misikiti kuna fadhila nyingi zaidi, kwani ni nyumba za Mwenyezi Mungu ambazo Mwenyezi Mungu ameidhinisha ziboreshwe kwa kumtukuza yeye, hivyo basi tujitahid ibada hii iwe ndani ya maisha yetu ya kila siku.

  9. Iwapo kuondoa maudhi katika njia ni sehemu ya Imani, basi kuondosha maudhi katika nyoyo za watu ni bora zaidi, nayo ni kwa kuwaondolea ujinga, na kuwaondolea yanayowatatiza na kuzuia migongano, na kila chenye kuleta wasiwasi na huzuni kati yao.

  10. Aibu na haya ni daraja katika daraja za Imani ambalo limetajwa kwa sababu lina athari kubwa, na maana ya haya au aibu ni tabia inayokaa ndani ya nafsi na inakuwa sababu ya kupatikana tabia nyingi nzuri, na inazuia tabia mbaya, na mtu anaweza kuwa nayo bila yeye kujua, au ikapotea tabia bila kuhisi chochote, ma mara nyingi hupotea Taratibu kwa sababu ya matendo machafu, je, hili tumelizingatia? Ikiwa ndio, Je, tunaahidi kuliendeleza?

  11. Haya si tabia mbaya inayotia aibu kuifanya bali ni tabia nzuri inampelekea mtu kuacha mabaya na kufanya mema, mfano mwenye kumuonea haya Mwenyezi Mungu kwa elimu aliyompa na asisomeshe, au pesa na asizitoe katika njia yake, au hata sauti au uwezo wa kuongea na wala asiwalinganie watu kwa kutumia vitu hivyo, na aliyedhihirisha uchi anaona haya kufichua siri hiyo, au kuonekana katika dhambi, au kutenda matendo mabaya; Kama woga, ubahili na uvivu.

  12. Haya au aibu kuu zaidi ni kumuonea haya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ukitaka kujua vizuri jambo hilo katika maisha yako basi tafakari haya maneno ya swahaba huyu aliposema: "Nakushauri umuonee Mwenyezi Mungu Mtukufu haya kama unavyomwonea haya mtu mwema unayemuhesimu".[2]

Marejeo

  1. Imepokewa na Al-Bukhari (2465) na Muslim (2121), kwa kutoka kwa Abu Saeed Al-Khudri
  2. Imepokewa na Ahmad katika Al-Zuhd (46), na Al-Bayhaqi katika Shu’ab Al-Iman (6/145) kutoka katika Hadithi ya Said bin Yazid


  1. Imran bin Al-Husein Mwenyezi Mungu amuwie radhi aliingia kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) na akafunga ngamia wake ili asitoroke wala kukimbia.

  2. Alipokuwa amekaa na Mtume likaingia kundi la kabila la Tamim, akasema Mtume kuwaambia: “pokeeni bishara” na ilikuwa jambo zuri kwao ni kupokea bishara hiyo kwa kuwa inatoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake) hata kama itakuwa kiasi kidogo namna gani, hususani kuwabashiria kuwa atakayesilimu hatabaki motoni milele... [1].

  3. Familia ya Tamim waliposikia bishara hiyo walidhani ni katika mambo ya kidunia nyoyo zao zikaelekea huko, wakasema: “Umetubashiria, basi sasa tupe, wakasema mara mbili. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) aliwakasirikia kwa kusema hivyo, na kutokujali bishara hiyo, na wakawa na matamanio ya Dunia yenye kuondoka, na walijua bishara njema ni utoaji wa mali tu.

  4. Baada ya hayo wakaingia kwake watu wa Yemeni, ni maash’ariy Watu wa Abu Musa Al-Ash’ari, akawaambia Mtume: “Pokeeni bishara, kwani familia ya Tamim hawakukubali. Japo kuwa familia ya Tamim walisilimu, lakini kwa sababu ya ugeni katika Uislamu wakati huo, habari njema hawakuikubali kama inavyo takikana, kwa kuwa waliweka sharti la kuikubali bishara hiyo wapewe mali. [2]

  5. Watu wa Yemen walikuwa wajuzi zaidi kuliko familia ya Tamim, kwa hivyo walizikubali bishara hizo bila vikwazo wala matakwa, na ndio maana Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alisema: “Imani iko Yemen, na busara inapatikana ndani Yemen” [3].

  6. Kisha baada ya kukubali bishara, walimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake) kuhusu ulimwengu huu au viumbe wanavyoviona. Haikuonekana katika swali kile walichouliza, lakini ilijulikana kupitia jibu Lake Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake).

  7. Mtume Rehema na Amani zimshukie alijibu swali lao kuwa Mola Mtukufu ni wa tangu enzi na enzi na hakuna chochote kilichokuwepo pamoja naye katika dunia hii, si mbingu wala ardhi, na hii haimaanishi kutokuumbwa vitu kabla ya mbingu na ardhi. Kwani Arshi iliumbwa kabla ya hapo na ipo. kama hadithi inavyoonyesha, na Mwenyezi Mungu huumba apendavyo [4].

  8. Kisha akawaambia kwamba Arshi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ilikuwa juu ya maji kabla ya kuumba mbingu na ardhi, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema katika qur`an:

    “Ni Yeye ndiye aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji”

    [Hud: 7].

    Na alipomaliza kuumba mbingu na ardhi akatulizana katika Arshi juu ya mbingu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

    “Mola wenu Mlezi ndiye aliye umba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akatawala juu ya arshi”

    [Al-Aaraf: 54].

Kiti cha Enzi cha Mwingi wa Rehema ni cha juu zaidi, n ani kikubwa na kitukufu kuliko viumbe vyote, na Arshi makusudio yake ni kiti cha ufalme.

9.   Kisha Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) akabainisha kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliandika hukumu za waja na yanayotokea ulimwengu mzima katika kitabu –Ubao- kilicho hifadhiwa, imepokelewa kutoka kwa Abdullah bin Amr bin Al-Aas. Amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu Amani Iwe juu yake akisema: “Mwenyezi Mungu aliandika hukumu za viumbe kabla hajaumba mbingu na ardhi. Kwa Miaka hamsini elfu, alisema: Kiti chake cha enzi kiko juu ya maji[5].

10.   Kisha akamwambia Mtume Rehema na Amani zimshukie kuwa Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi baada ya kuumba maji na arshi na kuandika hukumu za viumbe katika Ubao Uliohifadhiwa. Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amelieleza jambo hilo akisema:

“Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote (9) Na akaweka humo milima juu yake, na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanao uliza (10) Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu (11) Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua”

[Fussilat: 9-12].

11.   Kisha mtu akamwambia Imran kuwa ngamia wake ametoroka kutoka kwenye kamba na kukimbia, basi Imran akatoka kwenda kumuona, na kukuta kishatoweka machoni mwake, na kukawepo uzio baina yake na Ngamia. Ni uzio ambao huonekana jangwani kwenye joto kali kana kwamba ni maji.

12.   Imran alisikitika kuondoka kwake kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, amani iwe juu yake; Ambapo aliinuka na hakusikia Hadithi iliyobaki kutoka kwa Mtume Amani iwe juu yake.

Mafunzo

  1. Imran bin Husein alimfunga ngamia wake kwenye mlango wa Msikiti wa Mtume Amani iwe juu yake, na hii inaonyesha namna ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, katika suala la kuchukua sababu na kumtegemea Mwenyezi Mungu. Hakusema: Nimwache Ngamia bila kumfunga na nimtegemee Mwenyezi Mungu.

  2. Mtume Rehema na Amani zimshukie, alipenda kuwabashiria maswahaba zake, basi pambeni mazungumzo yenu mnapozungumza na watu kwa kila aina ya bishara, kama vile bishara ya yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu kwa watu wa imani. na subira kutokana na Pepo iliyo karibu na ijayo, Na katika bishara njema ni kuwaondoshea watu majonzi na khofu, na ni juu ya Waalimu wasiishie kueleza hukumu za fiqhi, mafundisho na nyenginezo bila ya kuzungumza na Nafsi.

  3. Ushindi wa Akhera ni wakipekee, na ndio maana Mtume Rehema na Amani zimshukie, akawakasirikia Banu Tamim kwa kuwa hawakutosheka na bishara hiyo na wakaomba Mali ambayo inakomea duniani tu. Je, tunapoteza kiasi gani pale ambapo tunatanguliza malipo ya Dunia na kuisahau Akhera.

  4. Usione haya kuuliza katika mambo ya Dini, sawasawa kuuliza juu ya hukumu za Sharia na yaliyo halali na haramu, au kuhusu hali halisi ya Kiyama na khabari za mataifa yaliyotangulia.

  5. Mfikirie kwa uzuri Mola wako Mlezi; Ana uwezo wa kukupatia kile unachotamani; Je, hivi aliyeumba ulimwengu mkubwa namna hii na kuushika mkononi mwake, hana uwezo wa kuitikia wito wako?!

  6. Iwapo Mwenyezi Mungu Mtukufu alikwisha andika hukumu za uumbaji kabla ya kuumbwa mbingu na ardhi, basi haifai kwa mja kuomboleza kwa yale aliyoyakosa kwa yale aliyokuwa akiyatarajia katika kheri, na wala asiwe na wasiwasi juu yake. nini kilimtokea kwa yale aliyokuwa anaonya juu ya uovu, kwa sababu kama mtumishi alifanya hivyo, alikuwa amechukizwa kulingana na amri ya Mungu Njoo hapa.

  7. Imran bin Huswein radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie alijuta alipotoka nje akimwangalia ngamia wake na kuacha Hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu Amani iwe juu yake, Majuto Hayo yanaashiria ubora wa elimu ya Kiislamu, na kwamba kuipata na kifahamu kwake ni bora kuliko kujishughilisha na Dunia na vilivyomo. Haifai kwa mwenye akili timamu kupuuza Ubora huo.

Marejeo

  1. Tazama: Fath al-Bari cha Ibn Hajar (13/409).
  2. Tazama: Fath al-Bari cha Ibn Hajar (13/409).
  3. Al-Bukhari (3499) na Muslim (52).
  4. Majmuu’ al-Fatawa cha Ibn Taymiyyah na linganisha: Fath al-Bari cha Ibn Hajar (6/289).
  5. Muslim (2653).

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anasimulia kutoka kwa Mola wake Mtukufu Hadithu qudusiyyu. Hadithu qudusiyyu, ni maneno ya Mwenyezi Mungu, amabayo si Qur`ani, yaani matamshi ni ya Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) na maana ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. kinyume na Qur`ani amabayo ni ya Mwenyezi Mungu, maneno na maana.

  1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaita waja wake kwa huruma: enyi waja wangu. Na anawaeleza kwamba amejiharamishia dhulumu japo kuwa yeye ni Muweza wa kila kitu, amesema Mtukufu:

    ““Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata uzito wa chembe moja”

    (An-Nisa: 40)

    Mwenyezi mungu ndiye mwenye ufalme na ndiye Muumba na mwenye amri, pamoja na hayo yote amekataa kudhulumu. Huu ni utangulizi wa kubainisha kwamba amewaharamishia watu dhuluma na kuwazuia wasidhulmiane.

Na Dhuluma maana yake; ni kuacha haki kwa kuweka kitu mahala pasipo stahiki. Na Mwenyezi Mungu ameharamisha ushirikina na kuufanya kuwa dhuluma kubwa. Kila dhuluma baina ya waja, katika nafsi, mali na heshima ni haramu hata kama ni kidogo sana. Mwenyezi amemuonya mdhulimaji:

“Wala usidhani kuwa Mwenyezi Mungu hana khabari na wanayoyafanya madhalimu.”

[Ibrahim: 42]

na akaamrisha uadilifu hata kwa maadui:

““Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu, Fanyeni uadilifu kwani kufanya Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu”

[Al- Maaidah: 8].

2.   Kisha Mwenyezi Mungu akawaita tena waja, na kuwaeleza kwamba viumbe wote wako katika upotevu, ila ambaye atamuonyesha haki na kumjalia aifuate; kwasababu wamezaliwa wakiwa hawajui chochote. Na mwanadamu kwa uwezo wake mdogo hawezi kujua kwa mtizamo wake ukweli wa kila jambo. Watu wametofaitiana wakatengeneza makundi, mambo yasiyo kuwa wazi yakakithiri, matamanio ya nafsi yakaenea. Mambo hayaendi kiakili, kwani kuna wenye akili wengi wameteleza. Na muongofu ni aliye ongozwa na Mwenyezi Mungu na kuwa imara katika haki, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaamrisha waja wamuombe uongofu.[1]

Uongofu haukomei kwenye kujaliwa kuwa mwislam, bali unajumuisha kujua hukumu na sheria zake, eidha kunyenyekea kwa kutekeleza aliyo yafundisha Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), kwa sababu hii, Mwenyezi Mungu akawaamrisha waja wake waumini, wawe wanaomba katika Sala kwa kusema:

"Utuongoze kwenye njia iliyonyooka”

[Al-Fatihah: 6][2]. 


3.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akawaita waja wake na kuwaeleza kwamba, viumbe wote wana njaa ila aliye mpatia chakula. Inatakiwa wamuombe yeye chakula; kwa sababu akitaka, anaharibu vyakula vyote ardhini, au anawafanya watu kuwa mafukara, au anawanyima chakula kwa kupitia maradhi au kuwekwa kizuizini au vyovyote vile. Hivyo basi mwanadamu hali chochote ila kwa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

4.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akawaita waja wake, na kuwambia kwamba viumbe wote wako uchi, hawana nguo ila aliye mvisha. Hivyo basi wanatkiwa wamuombe mavizi, kwani akitaka anawanyima. Chakula na mavazi ni mfano tu katika kuzungumzia riziki, viumbe wanahitaji riziki kutoka kwake kama wanavyo hitaji uongofu.:

““Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.”

[Al-Dhariyat: 58].

5.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akawaita waja wake na kuwakumbusha mapungufu yao ya kila siku ya kukosea usiku na mchana, na kwamba yeye anasamehe madhambi yote, kwa vyovyote yakatavyo kuwa mengi au makubwa, hivyo wanatakiwa wamuombe msamaha:

“Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu”

[Al-Zumar: 53]

 Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) ameeleza kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyosha mkono usiku ili aliye kosea mchana atubie, na ananyoosha mkono mchana ili aliye kosea usiku atubie mpaka juwa linachomoza”[3].6.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akawaita waja wake na kuwaeleza kwamba wao si chochote mbele yake, hawamdhuru kwa ukafiri wala vita au chochote kile, kwani hawana uwezo huo na wao ni sehemu katika ufalme wake, na wala hawawezi kumnufaisha si kwa Imani wala msaada au chochote kile, kwa sababu yeye amejitosheleza. Kisha akataja mbele yake mifano ya kuonyesha jinsi alivyo jitosheleza.7.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akarudia kuwaita waja wake na akawambia kwamba, utiifu wa waja haumnufaishi, lau ingelikuwa imani ya watu na majini, ni kama Imani ya Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), hilo lisingelimzidishia lolote katika ufalme wake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na anaye fanya juhudi basi bila ya shaka anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu”

[Al-Ankabut: 6]. 

8.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akarudia kuwaita waja wake na akawambia kwamba, maasi yao hayamdhuru, lau kufuru  na maasi yao ingelikuwa kama kufuru ya Ibilisi, hilo lisingelimpunguzia chochote katika ufalme wake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Wala wasikuhuzunishe wale wanao kimbilia ukafirini. Hakika hao hawamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Bali Mwenyezi Mungu anataka asiwawekee chochote cha kuwafaa katika Akhera, na watapata adhabu kubwa (176) Hakika wale walio nunua ukafiri kwa Imani hawatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu, na wataadhibiwa adhabu chungu”

[Al Imran: 176, 177]. 


9.   Kisha Mwenyezi Mungu anasifia fadhila na neema zake ambazo haziesabiki wala kudhibitiwa, kwamba viumbe wote toka kuumbwa mbingu na Ardhi mpaka siku ya Kiyama, wakisimama katika eneo moja, kila mmoja  akamuomba anacho kitaka katika riziki na neema, na Mwenyezi Mungu akampa anacho kiomba, hilo haliathiri ufalme wake hata kidogo. Akatoa mfano wa sindano inapo wekwa baharini, je inapunguza chochote katika maji ya bahari?. Hivyo ndivyo zilivyo fadhila za Mwenyezi Mungu, hazina mwisho.

10.   Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaeleza kwamba hatima ya mwanadamu inategemea matendo yake, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu anaandika matendo yetu yote, kisha atatulipa. Atakaye pata kheri, amshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumuongoza kuwa na Imani na kumjalia kutenda mema, na atakaye pata kinyume, basi ni mavuno ya matendo yake mwenyewe, yeye ndiye wa kulaumiwa, asimlaumu yeyote zaidi yeke mwenyewe.

Mafunzo

  1. Jihadhari na dhuluma, kwani ndiyo dhambi mbaya sana, zingatia maana yake ili usidumbukie ndani yake. Miongoni mwa dhuluma ni ushirikina, ambao ni kumuwekea Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenza katika mambo ambayo haifa kuelekezewa zaidi yake yeye, hata kama ni shirki ndogo kwa kujionyesha mbele ya viumbe katika sala au elimu au vinginevyo. Miongoni mwa dhuluma, ni kudhulumu haki za waja, hata kama ni kwa kuwakata mishahara bila haki, au pakingi ya gari, au maneno ya mzaha. miongoni mwa dhuluma mbaya ni mtu kujidhulumu mwenyewe kwani anajiingiza motoni kwa starehe inayo isha.

  2. Tafakari kila unachotaka kukifanya, na daima kumbuka kumuomba Mola wako uongofu na riziki; hivyo viko katika mkono wa Mwenyezi Mungu pekee, naye anapenda kusikia mja anamuomba.

  3. Usizembee kumuomba Mwenyezi Mungu haja zako za Akhera, sisi tunamuhitajia Mwenyezi Mungu kila wakati, tuko uchi, tuna njaa, tumepotea ila kwa fadhila zake.

  4. Mwenyezi Mungu ametuumba ili tumtii, na akatuwekea usiku na mchana ili tumuabudu, pamoja na hayo yote, ni mara ngapi tunateleza na kutenda madhambi mchana au katika sitara ya usiku?!. Tuzibe mapungufu hayo kwa kufanya ibada na kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu msamaha daima, hasa asubuhi na jioni.

  5. Unapo fanya jambo jema, usiligeuze kuwa ni masimango, na wala usidhani kwamba ni lazima kujibiwa dua au kunyanyuliwa kwa sababu ya hilo jema, Mwenyezi Munge amerizika na wewe ndio muhitaji.

  6. Usihuzunike wala kuvunjika moyo unapoona maasi au kufuru, hilo halimdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote, kama Mola wako akitaka hawaezi kuyafanya. Tekeleza unayo amrishwa, kama ibada na nasaha, na wala usihuzunike.

  7. Usijione kwamba umeisha omba sana dua, na wala usidhani kwamba Mwenyezi Mungu anaona kwamba ameelemewa kutoa, amesema Mwenyezi Mungu:

    ““Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo”

    [Al-Rahman: 29]

    . Na akasema Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake): “Mkono wa Mwenyezi Mungu umejaa, hauishiwi kwa kutoa, anatoa usiku na mchana; mnaona je alivyo vitoa toka kuumba mbingu na Ardhi? Kwa hakika havijaisha vilivyopo kuliani kwake”[4]

  8. Kutoa mifano ni katika njia zenye matunda mazuri katika kufundisha na kuathiri, tizama picha hii inavyo kita na kueleweka: (nikama kiasi cha sindano inapo ingizwa baharini.” jitahidi kubainisha na kusogeza kinacho lengwa kwa kutoa mifano ya karibu inayo onekana.[5]

  9. Amesema mshairi:Kwa hakika ninaapa, dhuluma ni mbaya***lakini mdhulumaji ndiye mbaya.Kesho siku ya malipo tunaenda kwa Mwenyezi Mungu***nambele yake watakutana walio kuwa na ugomvi

  10. Amesema Mshairi mwingine:Usimuombe mwanadamu akutatulie tatizo*** muombe ambae milango yake haifungwi.Mwenyezi Mungu anachukia usipo muomba***na mwanadamu akiombwa anachukia.

Marejeo

  1. Tazama: “Al-Mufhim lamaa 'ashkil min talkhis muslimin" cha Al-Qurtubi (6/552-553).
  2. Tazama: “Jami’ al-Ulum wa al-Hakam” cha Ibn Rajab al-Hanbali (2/40).
  3. Muslim (2759), kutoka kwa Abu Musa al-Ash’ari.
  4. Al-Bukhari (7419) na Muslim (993).
  5. Tazama: “Sharh Riyadh as-Salihin” cha Ibn Uthaymiyn (2/433).



Hadith hii ni katika Hadith za msingi katika Majina Mazuri ya Mwenyezi Mungu:

  1. Ametaja Mtume (Rehema na Amani zimshukie) kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ana majina tisini na tisa.Na wanazuoni wamekubaliana kuwa sio kwamba Hadith hii inamaana kuwa majina ya Mwenyezi Mungu ni tisini na tisa tu,bali makusudio yake ni kuhabarisha kuwa hayo (majina) tini na tisa atakaye yadhibiti ataingia peponi, sio kwamba idadi yake ni tisini na tisa tu[1]. Kwani Mwenyezi Mungu anamajina yasiohesabika kwa idadi na majina hayo yote ni mazuri na yamebeba sifa, matukufu, kama ilivyo katika dua ya mtume (rehma na amani ziwe juu yake) (ewe Mwenyezi Mungu ninakuomba kwa kila jina lako (zuri), ulilojiita mwenyewe, au uliloliteremsha kwenye kitabu chako, au ulilomfundisha yeyote katika waja wako, au ulilobaki nalo katika elimu ya siri[2])

2.  Haya majina yaliyoelezwa kwa kusema: “Mia moja isipokuwa moja,” hii inamaana ya uthibitisho kwamba idadi hiyo ndio imekusudiwa, asije msikilizaji au msomaji akachanganya hilo.

3.  Mwenyezi Mungu Mtukufu amewafadhilisha viumbe vyake kwa kufanya malipo ya kuyadhibiti majina hayo kuwa ni kuingia peponi, na hilo linatosha kuwa ni fadhila na malipo makubwa. 

Na kudhibiti ambako ni sababu ya kuingia peponi kuna maana nyingi, Qur`ani imeeleza hilo pia na maneno ya waarabu, katika maana zake ni: - kuhifadhi (kuyakariri kichwani), kuyahesabu ili kuweza kuyafanyia kazi vizuri, na kufahamu vizuri kuisoma Qur`ani yote, kwani Qur`ani imejaa majina matukufu ya Mwenyezi Mungu.[3]  

Kwa hiyo, kinachokusudiwa hapa ni: Mwenye kuyaamini, na kuyadhibiti kwa idadi, na kuyahifadhi na kuyafanyia kazi, ataingia Peponi[4], 

Na Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), hakubainisha majina hayo mazuri, ili aache akili zikiitafakari Qur`an na Sunnah, na ziiishi maisha ya kuyatafuta, ili ziweze kufikia malengo, na ziongeze juhudi ya kufahamu Kitabu cha Mwenyezi Mungu na maana yake, kama mtume alivyoficha saa ya kujibiwa dua katika siku ya Ijumaa, na usiku wa cheo.

4.  Kisha Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) akamwambia, kuhusu mojawapo ya majina makubwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambalo ni jina la Witr, na maana yake ni: Mmoja,(asiyegawanyika) kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu hana mshirika wala anayelingana naye, ndio maana matendo mengi ameyafanya kuwa witri, kama  swala tano, kupata udhu sunnah ni mara tatu katika viungo vingi, na kutufu( kuzunguka Al ka`aba) mara saba, na siku za Tashreeq (kuchinja, kula na kunywa katika mwezi wa dhul hajah) ni tatu, na mbingu na ardhi ni saba.[5]

Mafunzo

  1. Mwenyezi Mungu amewaneemesha waja wake na akaweka wazi majina anayopenda kuitwa nayo, akasema Mwenyezi Mungu:

    “Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwayo”

    [Al-A’araf: 180]

    , na ameweka wazi kuwa mwenye kumuomba Mwenyezi Mungu kwa majina hayo ataingia Peponi. Haifai kwa Muislamu mwenye akili timamu anayejua kuwa Mwenyezi Mungu anapenda kuitwa kwa majina hayo, na kwamba amewaandalia Pepo wale wanaomwita kwayo kisha akazembea na kupuuza!

  2. Mwenye furaha ni yule anayetumia akili yake vizuri na kukitafakari Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake, (rehma na amani ziwe juu yake), na akang`amua katika kitabu hicho majina yake mazuri, na akafahamu maana yake, na kuyafanyia kazi, kwa kuomba kupitia majina hayo matukufu, ili aweze kufaulu kuingia peponi.

  3. Katika kuyadhibiti majina ya Mwenyezi Mungu ni kuyatumia katika kuomba dua, azidishe kunyenyekea na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kwa kutumia jina la Allah na kuomba kwa majina yake Matukufu kulingana na hali yake, kisha anasema: Ewe Mwingi wa Rehema., nihurumie, Ewe Mwenye kusamehe, nisamehe, Ewe mwenye kuruzuku, niruzuku, na kadhalika.

  4. Katika kuyadhibiti majina ya Mwenyezi Mungu ni mja kuweza kutimiza haki za majina haya, na kuyafanyia kazi maana yake; mja atakapojua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, atakuwa na uhakika na Yakini kwamba Mwenyezi Mungu atamruzuku,

Na kudhibiti jina la Mwenyezi Mungu, ambalo ni Mwingi wa Rehema, kunampelekea mtu kuwa ni mwenye kutarajia rehema zake na kumsukuma kuwa ni mwenye kuwarehemu viumbe Wake ili Muumba wao apate kuwarehemu. 

Na kudhibiti jina la Mwenyezi Mungu, ambalo ni mwenye kuruzuku, kunampelekea mtu kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa fadhila zake nyingi, na kutotafuta riziki katika njia alizoziharamisha Mwenyezi Mungu, kwasababu riziki zinatoka kwake, naye ni Mkarimu mwingi wa kutoa. 

5.   Ukipatwa na jambo; iwe neema au msiba, au jambo linalohitaji kufikiria, basi hudhurisha majina ya Mwenyezi Mungu kichwani kwako, ukiwa unazingatia kila jina na maana yake, iwe inaendana na hali yako, kisha muombe Mwenyezi Mungu kwa majina hayo, hakika utapata utulivu wa yakini na faraja ya moyo.

6.  Tafakari majina ya Mwenyezi Mungu, kisha lolote utakaloweza kulifanyia kazi vizuri, - kama vile jina la Mwingi wa Rehema, Mkarimu, Mwenye kusamehe, Mwenye kusamehe na kustiri, na Mwenye kushukuru - basi lifanyie kazi. Na yale ambayo hayafai kuyafanyia kazi (ispokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu) – kama jina la Mwenye Kujikweza. - Basi mwachie anayestahiki na kuwa mnyenyekevu, na mpole.

7.  Kuwa na utaratibu wa kudumu wewe mwenyewe Pamoja na familia yako na marafiki zako, wa kuwa mnamtaja na kukumbushana jina miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu, kisha mkawamnaishi nalo katika matendo yenu ya kila siku, na mkajua maana yake, na athari za imani zilizofungamana na katika kujua maana yake, halikadhali tumieni vitabu vinavyoaminika katika kutambua maana ya majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, yanategemea yale aliyoyabainisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma naAmani iwe juu yake) na maimamu wa mwanzo, sio kutumia vitabu vinavyoashiria kwa dhana tu.

8- Mshairi anasema:

Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba kwa majina mazuri, basi niitikie = nimeyadhibiti ili nipate baraka zake.

Tisini na tisa yote yamechorwa moyoni mwangu, na lile la (Allah) roho yangu iko tayari kutoka kwa ajili yake.

Na kwa majina hayo siachi kuwa mwenye kufuatilia na kujifunza = Kama ndege anayetarajia mwenye kiu alie kutana na umande,

Je, kwa ukarimu wako unaweza kumkatalia mwenye kuomba, kwa majina yako? = aliekesha usiku mzima gizani, akiomba nakukutarajia kwa kusema Ee Mwenyezi Mungu?!.

Références

  1. Tazama:“Sharhal-NawawijuuyaMuslim”(5/5). 
  2. ameitohoaAhmad(4318)naIbnHibban(972)kwaidhiniyaIbnMasoud,naimethibitishwanaal-
    Haythamikatika“Majma’al-Zawa’id”(10/136). 
  3.  Tazama:“AlamAl-Hadith”(SharhSahihAl-Bukhari)chaAl-Khattabi(2/1342),“SharhAl-Bukhari”cha IbnBattal(10/420),“Al-MasalihfiSharhMuwattaMalik”naIbnAl-Arabi(3/493). 
  4. Tazama:“Al-TafwehLashrhAl-Jami’Al-Sahihah”chaIbnAl-Mulqin(33/230).
  5. Tazama:“KukamilikakwaMwalimukwaFaidazaMuislamu”naAl-QadiIyadh(8/177),“SharhAl-
    NawawiAliMuslim”(6/17).




Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alisimama mbele ya maswahaba zake, akataja sentensi tano kuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu, nazo ni:

  1. Ya kwanza: kwamba Mwenyezi Mungu Ametakasika Halali Usingizi, kwani usingizi ni upungufu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu hana mapungufu yeyote. Bali kila Kiumbe kinahitaji usingizi kwa sababu ya tabu na uchovu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu kajitosheleza na hayo, aliumba mbingu Na ardhi bila kupata tabu wala uchovu, Ndio maana Akasema:

    “Mwenyezi Mungu ambaye hapana Mwenyezi mungu anaeabudiwa kwa haki ila Yeye Aliye hai, anayesimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala”

    [Al-Baqarah: 255].

  2.  Ya pili: Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alisisitiza sifa hii, kwa kusema: na haiwezekani Mwenyezi Mungu kulala, hivyo sentensi ya kwanza ilimaanisha kutopatikana usingizi kwa Mwenyezi Mungu, na ya pili inamaanisha kuwa haiwezekani kwake kufanya hivyo kamwe [1].

 Bali haiwezekani kwake kulala, kwa sababu usingizi ni uzembe usioendana na ujuzi na usimamizi wa mwenyezi mungu kwa viumbe vyote na itakuwaje asinzie hali ya kuwa ameshikilia mbingu kwa mkono wake. Na ikiwa Mwenyezi Mungu angelala, basi Mbingu zingeanguka chini na mpangilio wa ulimwengu ungevurugika, na hilo haliwezekani kamwe.

3.   ya tatu: Sifa nyengine ni kwamba Mwenyezi Mungu Anasimamia mambo kwa uadilifu, Anaweza kuwapunguzia watu riziki na kuwazidishia wengine, na kuwadhalilisha baadhi ya watu na kuwatukuza wengine, kwa hekima na uadilifu hupima matendo yao kwa uadilifu, huchukua matendo mema na matendo mabaya huyakataa na kuyarudisha, Mola Mtukufu amesema:

“Kwake Yeye hupanda Maneno mazuri na amali njema huinyanyua na kuitukuza”

(Fatir: 10).

4.   Ya nne: Ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu, hupelekewa matendo ya waja kila siku, Malaika walio pewa dhamana ya kuandika matendo ya waja wakati wa mchana hupeleka matendo yao kabla ya kuingia usiku, Na wanapeleka matendo ya usiku kabla ya kuingia mchana, bila kuchelewa wala kuchoka.” Amesema Mtume rehma na amani iwe juu yake: “Wanapokezana kwenu Malaika wa usiku na Malaika wa mchana, na wanaakutana nyakati mbili: wakati wa swala ya alfaji na sala ya al-asri, kisha wanaondoka malaika waliokuwa wakiandika matendo yenu. na mola wenu mlezi anawauliza hali akijua kila kitu: vipi mmewaacha waja wangu? Nao wanajibu kwa kusema: tuliwakuta wakiwa wanaswali, na tumewaacha wakiwa wanasali” [2].

5.   Ya tano: kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu kafichikana kutokana na viumbe wake kwa kizuizi cha nuru, na katika riwaya: cha moto; Kwani Yeye Mwenyezi Mungu Anasema:

“Macho hayana uwezo wa kumuona Mwenyezi Mungu bali Yeye anaona viumbe wake, Naye ni Mpole, Mwenye khabari”

[Al-An’am: 103].

Hakuna mgongano kati ya riwaya hizi mbili za nuru na moto. Kwa sababu moto una sifa mbili: kung'aa na kuunguza. Inawezekana Mwenyezi Mungu Mtukufu ameiondosha sifa ya kuungua na akabakisha sifa ya kung'aa, tofauti na moto wa Jahannam. Kwani huo ni moto unaowaka na kuunguza wala hakuna mwanga ndani yake, na nuru hiyo ni tofauti na nuru nyingine zote za dunia kama vile jua na taa; kwani yenyewe imekusanya kung’aa na kuunguza”.[3]

6.   Lau Mwenyezi Mungu angeliondoa pazia hilo, uzuri wake, na fahari yake na mwangaza wake ungeteketeza kila kitu anachokiona na kila chenye kumuona Mwenyezi Mungu, na hatimaye kuungua viumbe vyote; Kwani katika kisa cha nabii Mussa alipomuomba amuone Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu alikataa ila ili kumridhisha mja wake akataka kujidhihirisha katika mlima, mlima huo haukuweza kustahimili hilo pamoja na kuwa nikitu kigumu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Alipo jionyesha Mola Mlezi wake katika mlima, aliufanya uvurugike na kuporomoka.”

[Al-A’raf. 143]

. Hivyo basi Kutakuwa na hali gani endapo atakapo jidhihirisha kwa mwanadamu?

Mafunzo

  1. Jambo kubwa zaidi walilofanya wanazuoni wabobezi katika elimu ya Tauhid (kumpwekesha Mwenyezi Mungu): Ni kuzungumza kuhusu habari za Mwenyezi Mungu, hivyo basi mazungumzo yako yawe mazuri kwa kumtaja Mwenyezi Mungu. Wakati mwingine kuyataja na kwa kueleza kuhusu Majina na Sifa Zake kwa usahihi, na mara nyingine kuhusu maamrisho na makatazo Yake, na mara nyingine kuhusu mawaidha Yake na simulizi za watu wa kale alizosimulia, na mwisho wao ulikuwa vipi na uchukue mazingatio.

  2. Sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu ni katika mambo ya siri, hivyo basi chukua katika maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake, (Rehma na Amani ziwe juu yake), na uyafanyie kazi yale yaliyothibiti, hata yakiwa machache katika mtazamo wako. na uyaamini bila ya kupotosha maana yake, na pasina kumfananisha sifa za Mwenyezi Mungu na sifa za viumbe wake, kwani yeye amesema:  

    “Hakuna anayefanana Naye na Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona

    [Al-Shura: 11].

  3. Unapotaka kulala elekeza mambo yako yote kwa Mwenyezi Mungu kisha ulale kwa amani kwani Mwenyezi Mungu halali wala hafai kwake kulala, na Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi bora, na ni mwingi wa huruma kuliko wenye huruma. Ndio maana tunasema katika Dua kabla ya kulala: “Ewe Mola wangu, nausalimisha uso wangu Kwako, na ninakukabidhi mambo yangu, na nimerejea kwako kwa upendo na khofu, hakuna kimbilio au uokovu isipokuwa kwako tu” [4].

  4. Siku zote kumbuka ukaribu wa Mwenyezi Mungu kwako na kuwa yeye anaona na kushuhudia kila unachofanya, kwani Mwenyezi Mungu halali wakati jicho la dhalimu linapolala, na wala halali wakati mlinzi anapolala ikawa sababu ya kutokea uharibifu kwa sababu ya kulala kwake, na Mwenyezi Mungu halali wakati anapoona ukisimama na kusujudu, ukimwomba akurehemu na aitikie maombi yako.

  5. Ridhika na hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika yale anayoyapanga, iwe kakupandisha daraja au kakushusha, kuongezeka riziki au kupungua, utukufu au unyonge, iwe katika masomo, pesa, sifa kutoka kwa watu au wadhifa. Kwani Yeye Mwenyezi Mungu humgawia kila mtu kiasi chake na sehemu yake kwa hekima na uadilifu, hivyo basi kuwa ni mwenye kufanya yanayompendeza Mwenyezi Mungu Mtukufu.

  6. Ni wajibu kwa mja afanye haraka kutubia, na kuomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya kabla matendo hayajachukuliwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu, “hupelekwa kwake matendo ya usiku kabla ya kuanza kuandika matendo ya mchana, na matendo ya mchana kabla ya kuanza kuandika matendo ya usiku.”

  7. Kimbilia kufanya matendo mema kila usiku na mchana. Dawud al-Twaa’iy – Mwenyezi Mungu amrehemu – amesema: “Usiku na mchana ni vituo ambavyo watu huteremka mmoja baada ya mwingine mpaka mwisho wa safari yao, ukiweza kuandaa akiba itakayokupitisha kila kituo basi fanya hivyo, safari ya Maisha iko ukingoni, na safari hiyo iko haraka Zaidi. jiandae vyema kwa safari yako, na kamilisha yale unayoweza kuyafanya katika kheri, kwani ni kifo kinakuchukua ghafla. [5]

  8. Nafsi zimeumbwa kupenda vizuri katika kila kitu, na hakuna zuri zaidi kuliko Mwenyezi Mungu, na pazia lake ni Nuru, hivyo shikamana na Nuru hiyo.

  9. Jisalimishe kwa Mwenyezi Mungu katika khabari na hukumu zake, kuna mambo ambayo hatujui sababu yake, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyahukumu yatokee kwa hekima na busara zake, kuna mtu anaweza kuuliza: Kwa nini hatumuoni Mwenyezi Mungu katika dunia hii? Na asijue kwamba hii ni kutokana na udhaifu wetu na kutokuwa na uwezo wa uoni wetu; Mwenyezi Mungu ana pazia lake la nuru, na ikiwa Mungu angeondoa pazia hilo, uzuri wa uso wake na mwangaza wake ungeteketeza kila kitu ambacho Mwenyezi Mungu anakiona au kumuona yeye.

  1. 10- Amesema Mshairi:

Utukufu ni wake Ambaye ameweka ishara zake kwa viumbe = ili yawe wazi yaliyofichika kupitia aliyoyadhihirisha

Utukufu ni wake yule anayehuisha nyoyo za waja wake = kwa maelekezo yanayotokana na nuru yake inayowaongoza.

Hakuna zaidi baada ya kumjua Mwenyezi Mungu = ila ni kufanya yenye kuimarisha radhi zake

Wallahi hapana pa kujikinga ila kwako tu, kwani amekosa mwongozo yule ambaye hutokuwa Kimbilio Lake.

Marejeo

  1. "Kifayat al-Haja fi Sharh Sunan Ibn Majah" cha al-Sindi (1/85).
  2. Al-Bukhari (555) na Muslim (632).
  3. Majmuu’ al-Fatawa cha Ibn Taymiyyah (6/387).
  4. Al-Bukhari (247) na Muslim (2710).
  5. “Jami’ al-Ulum wa al-Hakam” cha Ibn Rajab (2/382).


  1. Mtume Rehma na Amani zimshukie ametaja kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaumba Malaika kutokana na Nuru.Malaika ni miongoni mwa viumbe vya Mwenyezi Mungu, wana miili yenye kung'aa, yenye uwezo wa kujigeuza na kujifananisha na kujipa sura nzuri sana, na wana nguvu kubwa na uwezo mkubwa wa kuhama na kwenda mbio zaidi, na Malaika ni viumbe vingi ambavyo idadi yao anaijua Mwenyezi Mungu pekee. Aliwachagua wamuabudu Yeye na kutekeleza amri yake, kwa hivyo hawamuasi Mwenyezi Mungu kama alivyowaamrisha na kufanya wanayoamrishwa [1].

  2. Kisha akaelezea Mtume Rehma na Amani zimshukie kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaumba majini – nao ni viumbe vya ghaibu – siri- ambavyo watu hawavioni – kutokana na miale ya Moto iliyochanganyika na weusi wa moto.

  3. Kisha akataja Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu alimuumba Adam, baba wa watu wote kutokana na yale tuliyoelezwa ndani ya Qur’an na kuyaeleza katika Sunnah. Haya ni kwa ufupi tu, na Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) amepewa kila aina ya maneno, na maelezo ya kuumbwa kwa Adam yametajwa mara kwa mara katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu amemuumba kutokana na vumbi; Akalitia maji likawa tope, maana yake ni kwamba likachanganywa baadhi yake kwa baadhi, kisha likaachwa mpaka jeusi na linanuka, na hiyo ndio maana ya tope lililozeeka, kisha likapikwa kwenye moto mpaka likakauka na kuwa kama Mfinyanzi. [2]Hakika Mtume alieleza kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alichukua sehemu tofauti toauti ya Udongo ili kumuumba Adam, ndio maana watu wako katika aina tofauti na maumbile yao, kwa hivyo Abu Musa al-Ash’ariy Mwenyezi Mungu amuwiye radhi: Akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu Amani imshukie: “Mwenyezi Mungu alimuumba A’dam kutokana na Udongo wa sehemu tofauti tofauti ya ardhi, hivyo Wana wa Adamu wakaja kwa sura ileile ya ardhi, miongoni mwao walitokea wekundu, weupe na weusi, na baina ya hao, na Rahisi, huzuni, mbaya na nzuri."[3] Uumbaji wa Adamu haufanani na uumbaji wa Hawa, na uumbaji wa Yesu ni tofauti na wao wawili, na uumbaji wa hawa watu watatu ni tofauti na uumbaji wa wanadamu wengine wote.

Mafunzo

  1. Kuwaamini Malaika na Majini ni jambo la ghaibu, na kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake, amani iwe juu yake, inawataka kuyaamini waliyoyaelezea, Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu Waumini kwa kusema:

    "Wale wanaoamini ghaibu"

    [Al-Baqarah: 3]

    na Muislamu hana haja ya kuthibisha uwepo wa Malaika au majini kwa kutumia vipimo vya maabara au masomo. Kwani Muislamu anapaswa kuamini habari za Mwenyezi Mungu, ambazo ni ushahidi mkubwa zaidi wa kumsadikisha na kuthibitisha ukweli wa Mtume wake Muhammad, amani iwe juu yake.

  2. Hadithi hii ni ushahidi tosha juu ya utukufu na ukubwa wa uwezo wa Mwenyezi Mungu, kwani ameumba viumbe vitatu kutokana na vitu vitatu vya jinsia tofauti, na kila kimoja kina sifa zake, na kutafakari juu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu hupelekea moyo kuwa na imani, uchamungu na khofu ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, katika aya zake nyingi, Mwenyezi Mungu aliamuru waja wake kutafakari juu ya uumbaji wake.

  3. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameonyesha kuwaheshimu Malaika kwa kuwaumba kutokana naNuru, na anawataka waja wake kuwaheshimu na kuwapenda, basi Muislamu anaepuka yale yanayokwenda kinyume na hayo, kama vile kufuga mbwa na masanamu ndani ya nyumba - kwa sababu vitu hivyo vinawazuia Malaika - au vinawafanya watu kuendelea kudumu katika kutenda dhambi huku wakijua kwamba malaika wanaandika kila kitu.

  4. Mwalimu na Mlinganiaji wanatakiwa kuwabainishia watu yale yaliyofichikana, na wasiishie tu kubainisha yale waliyojifunza na kuyajua na kushuhudia na kujadiliwa kwa kina, vinginevyo hotuba watakazo kuwa wakizitoa zitakuwa hazina athari na yatakuwa maneno yasiyo na faida. 

  5. Amesema Mshairi:

Mwenyezi Mungu anazo ishara kila pande, huwenda = ishara ndogo kabisa ni kuwa yeye kuongoza

Na pengine miongoni mwa ishara zake kwa yale yaliyomo katika nafsi= ni ajabu ya hali ya juu, laiti ungeweza kuona 

Na ulimwengu umejaa mambo mengi ya siri= Ukijaribu kuzielezea, utachoka na utakata tamaa.

Marejeo

  1. Tazama: “Ulimwengu wa Malaika” cha Al-Ashqar katika sehemu tofauti, “Fath Al-Bari” cha Ibn Hajar (6/450).
  2. Tazama: “Al-Tafsiir Al-Wasat” cha Al-Wahidi (3/44), “Tafsir Al-Nasfi” (3/411).
  3. Ahmad (19582), Abu Dawood (4693), na al-Tirmidhiy (2955).



  1. Aisha Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, anaripoti kuwa ufunuo na (wahyi) wa kwanza kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, ulikuwa katika sura ya ndoto za kweli, Alikuwa akiona kitu katika ndoto yake, basi kinatokea kikamilifu mubashara na wazi kabisa kama nuru ya alfajiri, na hazikuwa ndoto zake kama ndoto za watu wengine, bali zilikuwa kana kwamba zinamuandaa kwa jambo kubwa. na wahyi ulianza kwa bishara njema na miuzijiza mbalimbali kama vile: kuota njozi njema, kusikia sauti za kokoto (mchanga) zikimtukuza Mwenyezi Mungu, kabla ya kuanza kulingania, kipindi hicho akiwa katika mji wa makkah, na muujiza wa jiwe kumsalimia kwa unabii na mengine mengi, yaliyolenga kumuandaa na ili ahisi ukubwa wa kile kinachokusudiwa, na ajitayarishe kwa yale yanayomngoja, na ili Malaika wasimshtue kwa yale ambayo nguvu za wanadamu haziwezi kustahimili, bali watamjia na ambayo yatautuliza moyo wake. [1]

  2. Kisha iliingia katika nafsi yake kupenda kuwa peke yake, na kuto changanyikana na watu, na kufanya hivyo huwa kuna athari ya kuuondolea moyo wasiwasi wa kidunia, hivyo akili na tabia ya mtu vinanyooka.

  3. Mtume (Rehema na Amani zimshukie) alikuwa akijitenga katika pango lililopo katika mlima wa Hira huko Makka, alikaa huko masiku mengi akimuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu. Alikuwa akitoka kwenda mlimani akiwa ameandaa chakula cha kutosha, na kinapoisha basi anarejea nyumbani kwa Bi Khadija na kuandaliwa kingine.

  4. Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimfikie) alipokuwa akiabudu aliteremshiwa wahyi wazi wazi, Malaika Jibril (Amani iwe juu yake), mwenye dhamana ya Wahyi akamtokea. Na kumwambia: “Soma.” Akajibu, “Mimi sijui kusoma”. Yaani: Mtume (Rehma na Amani zimfikie) alikuwa hajui kusoma wala kuandika, kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

    “Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, asiyejua kusoma na kuandika.”

    (Al-A’raf: 158).

  5. Mtume (Rehma na Amani zimfikie) alipomwambia kuwa hajui kusoma, malaika Jibril akamshika na kumkandamiza mpaka akachoka, kisha akamwachilia na kumwambia: “Soma.” Mtume akamjibu majibu yale ya awali, basi akamshika na kumkandamiza tena mpaka mara tatu, kisha akasema Jibril:

    “Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba (1) Amemuumba binaadamu kwa tone la damu (2) Soma! Na Mola wako Mlezi ni Mkarimu kushinda wote (3) Ambaye amefundisha kwa kalamu. (4) Kamfundisha mwanadamu aliyo kuwa hayajui. (5)

    [Al-Alaq: 1-5].

    Na hizi ayah za Qur`an ndizo zilikuwa ufunuo wa kwanza kwa Mtume Muhammad (Rehma na Amani zimfikie).

  6. Baada ya hapo Mtume (Rehma na Amani zimshukie) akarejea kwa mkewe Bi Khadija Mapigo ya moyo yakienda mbio kwa sababu ya woga uliompata (kutokana na alichokiuona), akaingia ndani akamuomba Bi Khadija amfunike, kwa kawaida Mtu mwenye hofu huwa anahisi baridi kali katika viungo vyake, hivyo Bi Khadija akamfunika hadi hofu ikamtoka.

  7. Kisha akampa khabari Mkewe na akamweleza yaliyompata kule pangoni, akamwambia: niliogopa sana. Maana yake: Aliogopa kwamba moyo wake ungepasuka kutokana na woga wake mkubwa wa kile alichokiona ambacho ni kumuona malaika Jibril akiwa katika umbile lake halisi. [2]

  8. Bi Khadija (radhi za Allah ziwe juu yake) akamtuliza, na kusema: Wallahi, Mwenyezi Mungu hatakuchukiza, na hilo lililo kukuta si jambo baya litokanalo na shetani, Hakika ya Matendo mema ni sababu ya kumlinda mtu kutokana na maangamizi, kisha akaanza kutaja tabia zake tukufu zikiwemo: -

  9. Kuunga udugu, kwa kuwatembelea na kuwajulia hali.

  10. kuwasaidia wasiojiweza, ikiwemo watu dhaifi, yatima na wengineo.

  11. Kutoa msaada wa mali kwa muhitaji,

  12. Kuwakirimu wageni kwa kuwapa chakula na vinywaji.

  13. Kuwasaidia watu waliofikwa na matatizo kwa misingi ya haki, sio kuwasaidia walioadhibiwa kwa uasi wao dhidi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

  14. Bi Khadija (Radhi za Allah ziwe juu yake) akampeleka kwa binamu yake Warqah bin Naufal, ambaye alikuwa ameacha ibada ya masanamu na akakubali Ukristo (halisi), na alikuwa msomi mzuri wa Taurati na injili, vilevile alikuwa anajuwa kuandika vyema lugha ya kiebrania, ambayo ndio lugha ya Wayahudi, na Alikuwa mzuri sana katika uandishi mpaka kufikia kuandika chochote alichotaka kutoka katika injili kwa lugha ya Kiebrania, pia Warqah bin Naufal alikuwa mzee sana mpaka akawa haoni.

  15. Mtume (Rehma na Amani zimfikie) aliposimulia Waraqah bin Naufal aliyoyaona, Waraqah akamwambia kuwa yule aliyemuona ndiye Malaika mwenye siri ya Mwenyezi Mungu aliyemteremsha kwa Nabii Musa, jina lake ni Jibril (Amani iwe juu yake), alimwita hivyo kwa sababu ndio malaika pekee aliyepewa jukumu la kufikisha wahyi(ufunuo); maneno ya Waraqat bin Naufal yaliashiria kuwa Muhammad (Rehma na Amani zimfikie), atakuwa  Mtume aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwa watu wote, kama vile Nabii  Musa (amani iwe juu yake) alivyotumwa kwa Wana wa Israili.

  16. Kisha Waraqah akaeleza kuwa watu wa Mtume watamkataa na kumpiga vita mpaka watamtoa katika Mji wake, na Waraqah alitamani kuwa laiti angelikuwa kijana wakati huo tena kijana mwenye nguvu ambaye ataweza kumtetea Mtume na kupigana vita pamoja naye, au walau angelikuwa tu hai wakati huo.

  17. Mtume (Rehma na Amani zimfikie) alishangaa maneno ya Waraqah, na kusikitika kwa kitendo cha watu wake kumtoa katika mji wake wa Makka wakati atapokuwa akiwalingania kwenye uokovu na kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu, hali ya kuwa Maquraishi wanaujua ukweli na uaminifu wake hapo kabla. Waraqa akamwambia kwamba ndivyo ilivyokuwa kwa Mitume wote na ndio desturi yao, na hakuna Mtume yeyote aliyekuja isipokuwa alifanyiwa uadui na kupigwa vita.

  18. Kisha Waraqah akamwambia kuwa kama atakuwa hai wakati wa kudhihiri utume wake na kuenea dini yake, kipindi watu wake watakapomfukuza na kumkataa, basi atamsaidia msaada ulio wazi kwa kiasi atacho weza, na kwa hoja zilizo dhahiri juu ya ukweli wake na utume wake.

  19. Kisha haukupita muda mrefu Waraqah akafariki, na wahyi ukachelewa kuteremka kwa muda.

Mafunzo

  1. Mtume (Rehma na Amani zimfikie) alimuoa Bi Aisha haliyakuwa ni mdogo sana: wakati alipoteremshiwa maneno matukufu mwenyezi mungu akimwambia (“Ewe Nabii! Waambie wake zako:

    Ikiwa mnataka maisha ya dunia na mapambo yake, basi njooni, nitakupeni kitoka nyumba, na kukuacheni vizuri kwa wema (28) Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya Akhera (pepo), basi Mwenyezi Mungu amewaandalia wafanyao mema, miongoni mwenu, malipo makubwa (29)

    [Al-Ahzab: 28, 29]

    Mtume (Rehma na Amani zimfikie) Akamuamuru Aisha kuwauliza wazazi wake, lakini Aisha akakataa na akasema: Niwaulize wazazi wangu kwa lipi? Mimi Namtaka Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na nyumba ya Akhera”[3], wakati huo Aisha alikuwa katika umri wa ujana, hivyo akawa ni mfano wa kuigwa katika kumpa kipaumbele Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, (Rehma na Amani zimfikie).

  2. Aisha (Mwenyezi Mungu amuwiye radhi), anaisimulia Hadithi hii, ambayo inaeleza fadhila na ubora wa Bi Khadija, ambaye alisema Aisha kuhusiana na Bi Khadija: “Sikumuonea wivu mwanamke yeyote kwa ajili ya Mtume (Rehma na Amani zimfikie), kama nilivyo muonea wivu Bi Khadija.[4]” Pamoja na hayo Wivu wake haukumzuia kusimulia hii hadithi. Na hapo tunajifunza kuwa Haifai kwa mtu kuficha sifa ya mtu au kumnyima haki yake (kwa sababu) ya kushindana naye au kuwa ni mpinzani wake, iwe katika kazi yake au katika maisha ya kila siku.

  3. Jibril kumbana Mtume (Rehma na Amani zimfikie) na kurudia mara kwa mara neno “Soma” kunaonyesha uzuri kurudia rudia neno mpaka lieleweke kutoka kwa mhusika, na kumuandaa msikilizaji asishughulishwe na chochote kinachoweza kumsumbua na kumtoa katika malengo. Pia ili akili iwe kwa yale anayosikia, na hii ni faida kwa walinganiaji, walimu na waelimishaji; kuwaepusha watu kutokana na mambo yenye kuwatoa katika lengo la elimu yanayo athari za kusikia au kuona kwao.

  4. Mtume (Rehma na Amani zimfikie) aliporejea kwa Bi Khadija akiwa na woga kwa yaliyompata: Bi Khadija hakubabaika wala hakuweweseka, na wala hakushughulika kumuuliza juu ya kile kilichotokea, bali aliharakisha kumfunika mpaka Mtume (Rehma na Amani zimfikie) alipotulia, na kumueleza Bi khadija  hakumkanusha wala kumtuhumu akili yake, bali alimsadikisha, na akambashiria kwamba mtu mwenye sifa hizo Mwenywzi Mungu hatamfedhehesha kamwe, na alithibitisha maneno yake kwa uthibitisho huu (Hapana, wallahi, kamwe..), na akamhakikishia kwa kumtajia sifa zake nzuri, na Bi Khadija hakuridhika na hilo, bali akamchukua hadi kwa binamu yake ambaye alimfafanulia vizuri kilichotokea, na baada ya hapo Bi khadija alikuwa wa kwanza kumwamini Mtume (Rehma na Amani zimfikie), na alikuwa mfano wa mke mwema anayemsaidia mumewe na kumuondolea dhiki na taabu anapofikwa na mazito maishani.

  5. Bi Khadija alitambua mwenendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba huwasaidia wale wanaosaidia watu, hivyo hatamfedhehesha Mtume wake, hivyo basi usipoteze nguvu za kimwili, akili, pesa, na wakati, katika kufanya yasio na faida bali Wafanyieni wema watu kwa moyo mkunjufu wenye nguvu, na kutaraji malipo kwa Mwenyezi Mungu, na ukiwa katika wakati wa furaha toa na saidia watu hakika utasaidiwa katika wakati cha shida na matatizo. 

  6. zilienea kwa watu wote sifa alizojipamba nazo mbora wa viumbe, na si kwa jambo alilolifanya mara moja tu, bali ni tabia zake  njema za kudumu mpaka zikageuka kuwa sifa zake mwenyewe, kama vile kuwaunga ndugu na jamaa kwa kuwatembelea, kuwasiliana nao, kutoa misaada na kudumisha kila uhusiano mzuri, na kuwa muungwana katika kuyasimamia mambo ya watu wasio weza kujifanyia mambo yao wenyewe, kama vile wanyonge, na kuwasaidia kipato cha mali au sababu zake, ikiwemo kuwapa kazi kwa wasiokuwa nazo, na kumkirimu mgeni anayepita nyumbani au mahali pa kazi, na kumsaidia kila mwenye shida.

  7. Jambo la msingi katika kutenda wema ni kujiepusha kusifiwa na watu mbele yako, ili usijikweze na kubadilisha nia kuelekea katika mambo ya kidunia, lakini kitendo cha Bi Khadija Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kinaonyesha kuwa inajuzu kwa mtu kumsifu ndugu yake hata akiwepo kwa manufaa, kama kumkomaza na kumuimarisha katika wakati wa mitihani, au kumpa bishara njema za matokeo ya subira yake Na mengineyo, hasa ikiwa mwenye kusifu anaamini kuwa mwenye kusifiwa hatajisikia wala kuwa na majivuno kwa maneno yake[5]. 

  8. Kwa kauli ya Waraqah bin Nofal aliposema: “Hakuja mtu na mfano wa ulichokuja nacho, isipokuwa hufanyiwa uadui.” Ni Ushahidi kuwa watu hufanya uadui kwa watu wema na wanaolingania katika haki, na hili si jambo jipya. Bali ndio njia ya Mitume na wanaofanya kazi yao katika kulingania. Hivyo basi Mlinganiaji yeyote hapaswi kuacha kulingania eti kwa kuzongwa na watu waovu wakimtaka aache kulingania mema.

  9. Mtume (Rehema na Amani zimshukie), alipenda kujitenga na kuwa peke yake kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alijitenga na watu na matamanio na maneno ya dunia. Kwani kuwa peke yako wakati mwingine kuna faida, Kama hakuathiri masilahi ya watu wengine, kama mtu kuacha kazi ili kutimiza masilahi yake binafsi ya upweke, kama wanavyofanya watu wa dini potovu, au kuabudu peke yake na hiyo haitakuwa ibada sahihi

Marejeo

  1. Tazama: “Maelezo ya Al-Nawawi juu ya Muslim” (2/197, 198)
  2. “Iikmal Almuealim Bifawayid Muslimin” Na Qadi Iyad (1/484, 485)
  3. Imepokewa na Al-Bukhari (4785) na Muslim (1475)
  4. Imepokewa na Al-Bukhari (3816) na Muslim (2435)
  5. Ufafanuzi wa Al-Nawawi katika kitabu cha sahihi Muslim (2/202)


 Na Amesema pia Mwenyezi Mungu “Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu (10) Waandishi wenye hishima na utukufu (11) Wanayajua mnayo yatenda”

[Al Infitar: 10 - 12].

UFAHAMU

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alisimama mbele ya maswahaba zake, akataja sentensi tano kuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu, nazo ni:

1- Ya kwanza: kwamba Mwenyezi Mungu Ametakasika Halali Usingizi, kwani usingizi ni upungufu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu hana mapungufu yeyote. Bali kila Kiumbe kinahitaji usingizi kwa sababu ya tabu na uchovu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu kajitosheleza na hayo, aliumba mbingu Na ardhi bila kupata tabu wala uchovu, Ndio maana Akasema:

“Mwenyezi Mungu ambaye hapana Mwenyezi mungu anaeabudiwa kwa haki ila Yeye Aliye hai, anayesimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala”.

[Al-Baqarah: 255]

  • 2- Ya pili: Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alisisitiza sifa hii, kwa kusema: na haiwezekani Mwenyezi Mungu kulala, hivyo sentensi ya kwanza ilimaanisha kutopatikana usingizi kwa Mwenyezi Mungu, na ya pili inamaanisha kuwa haiwezekani kwake kufanya hivyo kamwe [1] .
  • 3-Bali haiwezekani kwake kulala, kwa sababu usingizi ni uzembe usioendana na ujuzi na usimamizi wa mwenyezi mungu kwa viumbe vyote na itakuwaje asinzie hali ya kuwa ameshikilia mbingu kwa mkono wake. Na ikiwa Mwenyezi Mungu angelala, basi Mbingu zingeanguka chini na mpangilio wa ulimwengu ungevurugika, na hilo haliwezekani kamwe.
  • 4- ya tatu: Sifa nyengine ni kwamba Mwenyezi Mungu Anasimamia mambo kwa uadilifu, Anaweza kuwapunguzia watu riziki na kuwazidishia wengine, na kuwadhalilisha baadhi ya watu na kuwatukuza wengine, kwa hekima na uadilifu hupima matendo yao kwa uadilifu, huchukua matendo mema na matendo mabaya huyakataa na kuyarudisha, Mola Mtukufu amesema: “Kwake Yeye hupanda Maneno mazuri na amali njema huinyanyua na kuitukuza” (Fatir: 10).
  • 5- Ya nne: Ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu, hupelekewa matendo ya waja kila siku, Malaika walio pewa dhamana ya kuandika matendo ya waja wakati wa mchana hupeleka matendo yao kabla ya kuingia usiku, Na wanapeleka matendo ya usiku kabla ya kuingia mchana, bila kuchelewa wala kuchoka.” Amesema Mtume rehma na amani iwe juu yake: “Wanapokezana kwenu Malaika wa usiku na Malaika wa mchana, na wanaakutana nyakati mbili: wakati wa swala ya alfaji na sala ya al-asri, kisha wanaondoka malaika waliokuwa wakiandika matendo yenu. na mola wenu mlezi anawauliza hali akijua kila kitu: vipi mmewaacha waja wangu? Nao wanajibu kwa kusema: tuliwakuta wakiwa wanaswali, na tumewaacha wakiwa wanasali” [2]).
  • 6- Ya tano: kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu kafichikana kutokana na viumbe wake kwa kizuizi cha nuru, na katika riwaya: cha moto; Kwani Yeye Mwenyezi Mungu Anasema:

    “Macho hayana uwezo wa kumuona Mwenyezi Mungu bali Yeye anaona viumbe wake, Naye ni Mpole, Mwenye khabari” .

    [Al-An’am: 103]

    7- Hakuna mgongano kati ya riwaya hizi mbili za nuru na moto. Kwa sababu moto una sifa mbili: kung'aa na kuunguza. Inawezekana Mwenyezi Mungu Mtukufu ameiondosha sifa ya kuungua na akabakisha sifa ya kung'aa, tofauti na moto wa Jahannam. Kwani huo ni moto unaowaka na kuunguza wala hakuna mwanga ndani yake, na nuru hiyo ni tofauti na nuru nyingine zote za dunia kama vile jua na taa; kwani yenyewe imekusanya kung’aa na kuunguza [3]”.
  • 8- Lau Mwenyezi Mungu angeliondoa pazia hilo, uzuri wake, na fahari yake na mwangaza wake ungeteketeza kila kitu anachokiona na kila chenye kumuona Mwenyezi Mungu, na hatimaye kuungua viumbe vyote; Kwani katika kisa cha nabii Mussa alipomuomba amuone Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu alikataa ila ili kumridhisha mja wake akataka kujidhihirisha katika mlima, mlima huo haukuweza kustahimili hilo pamoja na kuwa nikitu kigumu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    “Alipo jionyesha Mola Mlezi wake katika mlima, aliufanya uvurugike na kuporomoka.”

    [Al-A’raf. 143]

    Hivyo basi Kutakuwa na hali gani endapo atakapo jidhihirisha kwa mwanadamu?

Mafunzo

1- Jambo kubwa zaidi walilofanya wanazuoni wabobezi katika elimu ya Tauhid (kumpwekesha Mwenyezi Mungu): Ni kuzungumza kuhusu1- habari za Mwenyezi Mungu, hivyo basi mazungumzo yako yawe mazuri kwa kumtaja Mwenyezi Mungu. Wakati mwingine kuyataja na kwa kueleza kuhusu Majina na Sifa Zake kwa usahihi, na mara nyingine kuhusu maamrisho na makatazo Yake, na mara nyingine kuhusu mawaidha Yake na simulizi za watu wa kale alizosimulia, na mwisho wao ulikuwa vipi na uchukue mazingatio.

  • 2- Sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu ni katika mambo ya siri, hivyo basi chukua katika maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake, (Rehma na Amani ziwe juu yake), na uyafanyie kazi yale yaliyothibiti, hata yakiwa machache katika mtazamo wako. na uyaamini bila ya kupotosha maana yake, na pasina kumfananisha sifa za Mwenyezi Mungu na sifa za viumbe wake, kwani yeye 
  • amesema:

    “Hakuna anayefanana Naye na Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona

    [Al-Shura: 11]

    3- Unapotaka kulala elekeza mambo yako yote kwa Mwenyezi Mungu kisha ulale kwa amani kwani Mwenyezi Mungu halali wala hafai kwake kulala, na Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi bora, na ni mwingi wa huruma kuliko wenye huruma. Ndio maana tunasema katika Dua kabla ya kulala: “Ewe Mola wangu, nausalimisha uso wangu Kwako, na ninakukabidhi mambo yangu, na nimerejea kwako kwa upendo na khofu, hakuna kimbilio au uokovu isipokuwa kwako tu” ([4]).
  • 4- Siku zote kumbuka ukaribu wa Mwenyezi Mungu kwako na kuwa yeye anaona na kushuhudia kila unachofanya, kwani Mwenyezi Mungu halali wakati jicho la dhalimu linapolala, na wala halali wakati mlinzi anapolala ikawa sababu ya kutokea uharibifu kwa sababu ya kulala kwake, na Mwenyezi Mungu halali wakati anapoona ukisimama na kusujudu, ukimwomba akurehemu na aitikie maombi yako.
  • 5- Ridhika na hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika yale anayoyapanga, iwe kakupandisha daraja au kakushusha, kuongezeka riziki au kupungua, utukufu au unyonge, iwe katika masomo, pesa, sifa kutoka kwa watu au wadhifa. Kwani Yeye Mwenyezi Mungu humgawia kila mtu kiasi chake na sehemu yake kwa hekima na uadilifu, hivyo basi kuwa ni mwenye kufanya yanayompendeza Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • 6- Ni wajibu kwa mja afanye haraka kutubia, na kuomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya kabla matendo hayajachukuliwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu, “hupelekwa kwake matendo ya usiku kabla ya kuanza kuandika matendo ya mchana, na matendo ya mchana kabla ya kuanza kuandika matendo ya usiku.”
  • 7- Kimbilia kufanya matendo mema kila usiku na mchana. Dawud al-Twaa’iy – Mwenyezi Mungu amrehemu – amesema: “Usiku na mchana ni vituo ambavyo watu huteremka mmoja baada ya mwingine mpaka mwisho wa safari yao, ukiweza kuandaa akiba itakayokupitisha kila kituo basi fanya hivyo, safari ya Maisha iko ukingoni, na safari hiyo iko haraka Zaidi. jiandae vyema kwa safari yako, na kamilisha yale unayoweza kuyafanya katika kheri, kwani ni kifo kinakuchukua ghafla. ([5])
  • 8- Nafsi zimeumbwa kupenda vizuri katika kila kitu, na hakuna zuri zaidi kuliko Mwenyezi Mungu, na pazia lake ni Nuru, hivyo shikamana na Nuru hiyo.
  • 9- Jisalimishe kwa Mwenyezi Mungu katika khabari na hukumu zake, kuna mambo ambayo hatujui sababu yake, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyahukumu yatokee kwa hekima na busara zake, kuna mtu anaweza kuuliza: Kwa nini hatumuoni Mwenyezi Mungu katika dunia hii? Na asijue kwamba hii ni kutokana na udhaifu wetu na kutokuwa na uwezo wa uoni wetu; Mwenyezi Mungu ana pazia lake la nuru, na ikiwa Mungu angeondoa pazia hilo, uzuri wa uso wake na mwangaza wake ungeteketeza kila kitu ambacho Mwenyezi Mungu anakiona au kumuona yeye.
  • Amesema Mshairi:
  •  Utukufu ni wake Ambaye ameweka ishara zake kwa viumbe = ili yawe wazi yaliyofichika kupitia aliyoyadhihirisha

Utukufu ni wake yule anayehuisha nyoyo za waja wake = kwa maelekezo yanayotokana na nuru yake inayowaongoza.

Hakuna zaidi baada ya kumjua Mwenyezi Mungu = ila ni kufanya yenye kuimarisha radhi zake Wallahi hapana pa kujikinga ila kwako tu, kwani amekosa mwongozo yule ambaye hutokuwa Kimbilio Lake.


Marejeo

1. "Kifayat al-Haja fi Sharh Sunan Ibn Majah" cha al-Sindi (1/85).

2.Al-Bukhari (555) na Muslim (632).

3. Majmuu’ al-Fatawa cha Ibn Taymiyyah (6/387).

4. Al-Bukhari (247) na Muslim (2710).

5. “Jami’ al-Ulum wa al-Hakam” cha Ibn Rajab (2/382).



Uislamu umesimama juu ya kukiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi kuwa hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye (Allah) peke yake, na hakika Muhammad ni mjumbe na Mtume wake, na kutambua kuwa Mtume (s.a.w) ni msaidizi katika kuifikia imani nzuri, kwa nini isiwe hivyo wakati yeye mkamilifu wa watu na mwingi wao kwa fadhila na ubora juu yetu. Na katika hadithi hii Anasimulia ibn abbasi (r.a) hatua muhimu sana alizo zipitia Nabii Muhammad (s.a.w) katika uhai wake, basi anaeleza:

  1. Hakika Mtume rehma na amani aliteremkiwa na jibril (a.s) kwa wahyi (ufunuo) na akamuamuru kufikisha baada ya kufikisha (s.a.w miakla arobaini (40), yaani yeye alizaliwa mwaka wa hamsini na tatu 53 kabla ya kuhama kwake kwenda madina, na ulikuwa ukiitwa mwaka wa tembo, na akapewa utume mwaka wa kumi na tatu kabla ya kuhama kwake. Na hakika Mwenyezi Mungu alimchagulia mji wa makka ndio yawe mazazi ya Mtume wake (s.a.w) na sehemu ya kukulia kwake, katika mji huo ndio alizaliwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake kwenye nasaba tukufu, kwani baba yake ni Abdallah ibn abdu al-mutwalib, al-hashimiyyu, al- qurashiyyu, na mama yake ni A’mina bint wa abdi manafi ibn zuhrat al-qurashiyyat [1], alikuwa Mtume ni katika waarabu wenye nasaba tukufu. Amesema Mtume (s.a.w): “Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua kinanat katika watoto wa ismail, na akawachagua maquraysh katika kinanat, na akachagua kutoka kwa maquraysh banii hashim, na akanichagua mimi katika banii hashimu” [2]. Alikufa baba yake Mtume hali yakuwa yeye ni mimba katika tumbo la mama yake, basi akazaliwa Mtume (s.a.w) akiwa yatima, na akakulia katika uangalizi wa mama yake, kisha mama yake Alikufa hali Mtume akiwa na miaka sita, basi akaendelea kuwa chini ya uangalizi na malezi ya babu yake, kisha babu yake alikufa hali Mtume akiwa na umri wa miaka minane, basi hapo akamlea ami yake abuu twalib. [3] Aliendelea Mtume kuishi Makkat kwa kipindi cha hii miaka arobaini, Mwenyezi Mungu Mtukufu akimlea na akimuandaa maandalizi yanayoendana na kazi yake ambayo Mwenyezi Mungu aliyo mchagulia, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

” Hivi hakukukuta ukiwa yatima akakuhifadhi na kukuliwaza (6) na akakukuta ukiwa hujui chochote katika dini na akakupa mwongozo wa kutenda mema (7) na akakukuta ukiwa maskini kisha akakutajirisha kwa kutosheka”. (8)

[adh-dhuha:6-8],

Akaishi pamoja na watu wake maisha mazuri tena kwa tabia nzuri, akishirikiana nao kila jambo lenye manufaa, na mwenye kujitenga mbali na kila baya na chafu.Na hakika alimuoa Mtume (s.a.w) Khadija bint khuwaylid na Mwenyezi Mungu akampa riziki ya watoto wote kutokana na khadija, nao ni :Q asim, Abdallah, Zainab,Rruqayyat, Ummu kulthum na Fatuma- isipokuwa Ibrahim ambaye alimpata mjini madina kupitia Mariyat al-qibtiyah- [4] kisha jibril akamteremkia Mtume (s.a.w) akiwa katika jabal hiraai –pangoni-  na akamteremshia:

“ Soma - ewe Muhammad- kwa jina la mola wako aliye umba(1)ambaye aliye muumba mwanadamu kwa pande la damu (2) soma na mola wako ni mwingi wa ukarimu (3) ambaye aliyewafundisha wiumbe vyake kuandika kwa kalamu (4) alimfundisha mwanadamu vitu alivyokuwa hvijuwi ” (5)

[al-alaq],

basi akayafanyia kazi majukumu ya utume.

2.   Baada ya ufunuo kuteremka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake, aliendelea kuishi makkat miaka kumi na tatu akipewa ufunuo, na akiwalingania watu kwa ufunuo huo, na alikutana na maudhi katika kazi hiyo, kupingwa vikali kiasi ambacho hakuna anaye weza kuvumilia kwayo, na hata aliyekuwa akimuamini pia alifanyiwa maudhi, na maudhi yalipozidi aliwaamuru waislamu kuhamia habashat mwaka wa tano wa utume, basi walihama zaidi ya maramoja, [5] . Na aliendelea Mtume kulingania katika mji wa makkat, na Mwenyezi Mungu alimtilia nguvu kupitia ami yake abuu twalib na mkewe khadija, mama wa waumini wakawa wanamtetea, mpaka ulipofika mwaka wa kumi wa utume, basi walikufa wote wawili, na akawa akitafuta mtu atakaekua akinusuru dini yake katika mji wa twaif hasa katika misimu ya hijja, na nyakati zinginezo, akawa akifanyiwa maudhi. [6]

3.   Baada ya Mtume (s.a.w) kukamilisha miaka kumi na tatu (13) katika mji wa makkat, Mwenyezi Mungu alimchagulia mji wa madina kuwa ndio makazi yake ya kuhamia, basi akahama Mtume (s.a.w) kwenda madina akisuhubiana na abuu bakari (r.a), baada ya kuwa maswahaba wengine  wamekwisha hamia huko, na walifuatia wengine katika walioweza kuhama baadae, aliendelea Mtume (s.a.w) katika mji wa madina akifanya kazi ya da’wah – kulingania- na jihadi na maslahi ya watu kwa kipindi cha miaka kumi, mpaka Mwenyezi Mungu akaitimiza neema yake ya dini na wakaingia watu katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi.

4.   Kisha akasimuliaAbdallah ibn abbas (r.a) kwamba hakika Mtume (s.a.w) alikufa hali akiwa na umri wa miaka sitini na tatu, (63) baada ya kulingania watu kwa miaka ishirini na tatu, miaka kumi na tatu katika mji wa makkat na miaka kumi katika mji wa madina, na kifo chake kilitokea chumbani kwa A’isha (r.a), siku ya jumatatu tarehe kumi na mbili mwezi wa tatu mwaka wa kumi na moja tokea kuhama Mtume (s.a.w).     

Mafunzo

  1. Amini uumbaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na rehma zake, na utafute msaada wake, kwa hakika alizaliwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akiwa yatima wa baba, kisha akafa mama yake  na babu yake hali akiwa bado ni mototo, basi akalelewa na ammi yake pamoja na ufaqiri aliokuwa nao, na wingi wa watoto zake, na desturi katika mazingira haya ni lazima yatima huyu kuishi katika hali ya dhiki na uangalizi mdogo,  lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye mikononi mwake ndio kuna makadirio ya mambo yote, basi akamfanya yatima huyu baada ya miaka na miaka kupita kuwa ndio bosi na bwana wa walimwengu, basi asikate tamaa mwanadamu katika rehma za Mwenyezi Mungu, vyovyote mambo yatakavyo kuwa yamembana, na awe na imani kuwa yupo mola anaye simamia na kuyaendesha mambo,  bali akilitaka jambo husema “ kuwa: basi linakuwa kama alivyo taka liwe”

  2. Mtume (s.a.w) aliendelea kwa miaka kumi na tatu akiwalingania watu katika mji wa makkat, alikuwa akitoka kwenda masokoni na kwenye mikusanyiko ya watu akiwalingania katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu, hachoki wala hapati uvivu wala hakati tamaa kutokana na kuamini watu wake, na wala hapati uzito kwa kumpinga kwao na kumtuhumu kwao, alikuwa ni mpole katika maneno yake na ulimi wake, pia ni mwenye huruma kwa watu wake, akiwaombea mwongozo kwa Mwenyezi Mungu, na anasaidia katika mambo mema ya watu kama kutunza amana na mengineyo, wala hakufadhaika kwa kifo cha ami yake ambaye alikuwa akimlinda kutokana na maudhi ya watu wake, wala hakudhoofika kwa kifo cha mke wake kipenzi khadija ambaye alimnusuru na kumtia moyo katika kuifikisha dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa nafsi yake na kwa mali yake, hivi kwanini Mtume asiwe kiigizo chema kwa walinganiaji na wanaotafuta elimu ya kisheria? Na watoa mawaidha katika njia ya kuvumilia maudhi na kusubiri wakati wa kuwalingania watu, na kuyavumilia maudhi ya watu haliyakuwa wao hawayapati maudhi mfano wa aliyoyapata Mtume (s.a.w)?

  3. lilipokuja agizo la Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake (s.a.w) la kuhama, basi Mtume hakuhuzunika kwa kuiacha familia, mali, nyumba na mji mtukufu wa makkat, bali si vinginevyo alitekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na shida na matatizo aliyokuwa nayo katika nafsi yake, nahii ndio hali ya muumini wa kweli, anayafanya kuwa mepesi yale anayokutana nayo kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

  4. Jambo la kuhama ni pana sana, na si lazima kuhama iwe kutoka mji na kwenda mji mwingine, bali inaweza kuwa kuhama kutoka katika mazingira na matendo kwenda kwenye mazingira na matendo mazuri zaidi kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

  5. Yalipitia maisha ya Mtume (s.a.w) katika hatua za aina yake na matukio tofauti, ambayo yako kati ya wepesi na uzito, na shida na starehe, na vita na amani, na siri na dhahiri, na kudhoofika na kuimarika yakashamili maisha hayo ya kibinadamu kila aina ya hali yake na hatua zake, na yakapita yote hayo kuwa ni mfano uliokamilika katika kumuenzi na kumuiga, na kupokea qadari (makadirio) za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hali yoyote.

  6. Kifo ni lazima hata kwa mtu mtukufu, na hata kwa mkamilifu wao kwa nguvu na akili, na hata kwa mwenye kulinda afya yake kutokana na vitu vyenye kuidhuru nafsi hiyo, na hata kwa mwenye kulingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kumwomba msamaha na afya, na hata kwa mwenye kuwanufaisha watu, basi haipendezi kwa mwenye akili kukisahau kifo, au kujisahaulisha kutokana na hesabu zake, na haipendezi kufadhaika kwa kufiwa na mtu wa karibu au mpenzi au mwana chuoni au mja mwema.

  7. Amesema mshairi:

Alizaliwa yatima akawa mtukufu wa sifa kwa wanadamu = basi wajifakhari masikini na mayatima.  

Kama alfajiri inavyotoka katika kiza kikubwa = ni kama roho inavyoingiza uhai kwa maiti hali ameshaoza   

Ni uzuri ulioje katika dunia kwa kuwa kubwa furaha yake = utaendelea uislamu ukiifunika dunia kwa furaha.

8.   Amesema hassani ibn thabiti: [7]

Watu wangu ndio ambao walimhifadhi nabii wao = na wakamsadikisha hali yakuwa watu wamemkanusha

Isipokuwa sifa za watu ambao ni wema waliotangulia = 

kwani watu wema wapo pamoja na wasaidizi.

Wakifurahia kiapo cha Mwenyezi Mungu kwa kauli zao = Alipowajia mtu mkarimu, na aliechaguliwa

Karibu, kwa usalama na kwa wasaa = ubora ulioje kwa Mtume, na ndio ubora wa ahadi na jirani.

Basi wakamweka katika nyumba isiyo na woga wowote = mwenye kuwa jirani yao kwa nyumba ndio jirani bora.

Marejeo

  1. Tazama: " Alsiyrat Alnabawiya " cha Ibn Hisham (1/110).
  2. Sahihi Muslim (2276), kutoka kwa Wathila bin Al-Asqa, Mungu amuwiye radhi.
  3. Tazama: “Alsiyrat Alnabawiya” cha Ibn Hisham (1/168: 179).
  4. Tazama: “Alsiyrat Alnabawiya” cha Ibn Hisham (1/187).
  5. Tazama: "Alsiyrat Alnabawiya: Ardhwul Waqayie Watahlil 'Ahdaathi"(uk. 191).
  6. Tazama: "Alsiyrat Alnabawiya: Ardhwul Waqayie Watahlil 'Ahdaathi"" (uk. 207).
  7. Sirat Ibn Hisham (1/664).


  1. Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anauhadharisha umma wake dhidi ya kusema katika dini kwa rai yao, kwa kufuata matamanio yao, mpaka kutokea mtu miongoni mwao ambaye ni mjinga na asieipenda elimu na watu wake, Aliacha mikusanyiko ya elimu na akapendelea starehe na uvivu, hivyo atasema hali akiwa ameegemea kiti chake au mto wake: Inatubidi tutosheke na amri na makatazo yaliyomo katika Qur’an. Kwani halali ni yale ambayo Qur’ani imeruhusu, na haramu ni yale ambayo Qur’ani imekataza.Na hili llimeshatibitika katika umma wake Mtume  rehma na amani iwe juu yake, kwa hiyo wakatokea Makhawariji, Rawaafidh, Qur-aaniyyuun, makafiri na wengineo, ambao walikuwa wameshikamana na maana ya dhahiri ya Qur'ani, na wakajiepusha kukimbilia kwenye Sunnah za Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam na kukataa kuzifanyia kazi Hadithi sahihi, kwa ujinga na kiburi ambacho kilizipofusha nyoyo zao na utambuzi.[1]

2.   Mtume, rehma na amanni zimshukie, alikemea kitendo chao hicho, na akaeleza kuwa maamrisho na makatazo ya Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam ni katika ulazima wa kufuata na kutii, kama zilivyo amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, hasemi kwa kufuata matamanio yake, na Sunna yake ni sheria inayopasa kufuatwa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: 

“Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho.”

[Al-Hashr: 7].

3.   Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie kuwa: Mwenyezi Mungu Mtukufu amempa Qur-aan, ambacho ni kitabu kilichoteremshwa kwake kwa njia ya muaminiwa wa wahyi Jibril, amani ziwe juu yake, ambacho kukisoma ni ibada, kila sura ndani yake inatoa ushindani ,  ambacho kimepokelewa maneno yake kwa njia ya mtiririko wa mapokezi, na pia akampa Sunnah, ambayo ndio  tafsiri ya Qur-aan na ubainifu wa hukumu zake na mipaka yake, na kwa ajili ya hayo Mola Mtukufu amesema:

““Kwa Ishara wazi na Vitabu. Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri”

[An-Nahl: 44].

Basi Allah akaitaja Sunnah kuwa ni ukumbusho, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwambia Mtume kuwa amemteremshia Mtume wake rehma na amani zimshukie.Na Sunnah imepambanuka kwakuwa imekuja na hukumu zilizo za ziada ya yale yaliyomo ndani ya Qur’an. Kama vile kukataza dhahabu kwa wanaume, na uwepo wa hiyari mbalimbali kwa watu wenye kuuziana, na katazo la binti kuolewa Pamoja na shangazi yake wa baba, na kuwaoa Pamoja mtu na mama yake mdogo au mama yake mkubwa katika ndoa, kukataza nyama ya punda wa nyumbani, na Kurusu mizoga ya samaki na nzige, na kadhalika.Hakuna chochote kilicho kuja kutoka kwa Mtume rehma na Amani zimshukie kwamba kinatokana na matashi yake, bali ni wahyi aliouteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume Wake, amani iwe juu yake, na ikiwa tofauti kati ya Sunnah na Qur’ani ni kwamba Sunnah ni wahyi kwa maana. Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, anafahamisha juu ya maana hiyo kwa maneno yoyote ayatakayo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Wala hatamki kwa matamanio (3) Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa kwake”

[An-Najm: 3, 4].

Mafunzo

  1. Tahadhari na ujinga, kujiepusha na kutafuta ilimu, na kufanya kiburi kukaa mbele ya wanachuoni. kwani hiyo ndiyo sababu ya uzushi na wafuasi wake.

  2. Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam alitahadharisha dhidi ya kuacha Sunnah zake, basi jihadhari na kuwa miongoni mwa wanaokengeuka.

  3. Katika Hadithi hii kuna karipio na kemeo kwa mwenye kuikadhibisha Sunnah ili waiondoe kwa Qur-an, na wale wanao tanguliza rai zao juu ya hadithi za Mtume .Na wanapoisikia hadithi sahihi miongoni mwa hadithi za Mtume husema; Sina ulazima wa kuifuata maana mimi ninayo madhehebu yangu ninayo yafuata.[2]

  4. Jihadharini na kudharau yale aliyoharamisha au aliyoamrisha Mtume, rehma na amani zimshukie. Kwani adhabu yake ni sawa na yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu, pamoja na natija ya kupinga yale aliyoyaweka Mtume, rehema na amani ziwe juu yake.

  5. Mwenye kukataa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameikataa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na ameacha kujisalimisha kwa maamrisho na makatazo yake, basi tahadhari na hayo.

  6. Sunnah ni wahyi kama Qur-aan, kwa hivyo kila kilichotoka katika sunnah kipo katika njia sahihi ni lazima kifuatwe, kisadikishwe na kuaminiwa.

  7. Vipi inajuzu kwa Muumini kudai kuwa anamuamini Mtume, amani iwe juu yake, kisha akaacha kumfuata?!

  8. Sio sharti kwa Hadithi Sahihi kuafikiana na Qur’an ili ikubalike; hadithi Nyingi za Mtume zimekuja na ziada ya elimu juu ya yaliyomo ndani ya Qur’an, basi ikikujieni Hadithi ya kweli inayonasibishwa kwa Mtume, amani iwe juu yake, ifanyie kazi ipasavyo.

  9. Lau kama Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam asingetiiwa katika yale ambayo ni zaidi ya Qur’ani, basi kumtii kungekuwa hakuna maana, na utiifu kwake makhsusi kwake yasingetimia.” Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

    “Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao”

    [An-Nisa: 80].

  10. Mshairi alisema:

Na uwe mfuasi wa Sunnah za mbora wa tabia njema = kwani ndio anwani ya kuokoka kwa mja

Yeye ndiye aliyejumuisha mbora wa viumbe = na ihsani kutoka kwake ikawaenea watu wote

Na tangu alipokuja, upofu wan yoyo uliona = njia za uwongofu, na masikio yakaijua haki.

Ee Bwana, umbariki kadiri mvua inavyonyesha = ndivyo majani na matawi yake yalivyomea

Na umpelekee amani tamu na yenye harufu nzuri = Na familia na maaswahaba wakati wote bila kikomo.

Marejeo

  1. “Hashiyat al-Sindi juu ya Sunan Ibn Majah” (1/4).
  2. “iielam almuqiein ean rabi alealamina"” Ibn al-Qayyim (2/220).


 

  1. Mtume (Rehme na Amani zimfikie), ameapa kwa Mwenyezi Mungu akithibitisha jambo kubwa, akasema: Wallahi naapa kwa yule ambaye uhai na nafsi yangu vipo mikononi mwake, Akitaka ananifisha na akitaka anaipa uhai.

  2. Maudhui ya kiapo hiki yanazungumzia wajibu wa kuamini kwa wale wote waliofikiwa na wito wa Mtume (rehme na Amani zimfikie); katika ummah aliyotumwa kuwafikishia watu na majini, Waarabu na wasiokuwa Waarabu, tangu zama zake mpaka siku ya Qiyaamah. Na kufika kwa wito huo kunakokusudiwa ni ufahamu wa mwenye kuwajibikiwa (yaani aliebalehe) kuwa yupo Mjumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Analingania kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kukataza ushirikina, na kuyabainisha hayo yote na mengine mengi, sawa sawa awe amekinai katika hoja au asiwe amekinai, ile kufahamu ufahamu sahihi kuwa yupo Mtume mwenye sifa maalumu aliyetumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu unamtosheleza kusimamishiwa hoja dhidi yake. Na ama yule ambaye hakufikishiwa ujumbe kwa usahihi, hatusemi kuwa mtu huyu atasimamishiwa hoja dhidi yake, Kwani Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    “Na hatukuwa ni wenye kuadhibu, mpaka tumtume Mjumbe”

    [Al-Isra: 15].

  3. Mtume (Rehme na Amani zimfikie), amewataja Mayahudi na Manasara kwa sababu wao ndio watu wanaomfahamu zaidi Mtume Muhammad (Rehme na Amani zimfikie) na habari njema za utume wake ziliwajia kabla ya ujio wake, Pia kuwataja wao kunaashiria kwamba imani yao ya kuamini dini zilizotoka mbininguni haitaafaa kwa chochote baada ya ujio wa Mtume wa mwisho ambae ni Muhammad (Rehme na Amani zimfikie). Halikadhalika wapagani (wasiokuwa na dini) na wasioamini Mwenyezi Mungu wote wanaingia katika hukumu hiyo. Na hii ni ushahidi kwamba sheria ya za Mtume (Rehme na Amani zimfikie) zilifuta sheria zote zilizokuwa kabla yake.). [1]

  4. Kila mtu mzima mwenye akili timamu aliyefikiwa na wito huo (wa uislamu), kisha akafa bila kuamini ujumbe wa Mtume wa mwisho wala hakufuata sheria aliyoileta, basi atakuwa miongoni mwa watu wa Motoni atakaa humo milele, hayatamfaa matendo, nasaba, heshima wala hadhi yake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    “Na anaye tafuta dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwake, na Akhera atakuwa miongoni mwa walio pata hasara”

    [Al Imran: 85].

Mafunzo

Tunajifunza katika hadithi yafuatayo: -

  1. Abu Huraira (Mwenyezi Mungu amuwie radhi) alivuka umbali mrefu kutoka katika Mji wake, na akaridhia kukabiliana na misukusuko ya kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kwani ilikuwa inatosha kwake kusilimu katika Mji wake, na akabaki huko huko, bali alihama na kusuhubiana na Mtume (Rehme na Amani zimfikie) hadi akawa ni mpokezi na msimulizi wa Hadith nyingi, licha ya kuwa kusilimu kwake kulikuwa si zaidi ya miaka takribani mitatu tu, basi kila mmoja wetu ajitazame mwenyewe na kujiuliza maswali haya,  je nimefanya nini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Na nina pupa (hamasa) kiasi gani katika kufuata mwenendo wa Mtume (Rehme na Amani zimfikie) ambao ndio urithi wetu.

  2. Tunajifunza katika hadithi hii kuyatukuza mambo ya Imani, na tunyenyekee kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehme na Amani zimfikie) katika kila jambo alilotuamrisha, sawa sawa liwe linaendana na Matamanio yetu au liko tofauti. Kwa kusisitiza hilo Mtume (Rehme na Amani zimfikie), ameapa kwa yule ambaye uhai na kifo chake vimo mikononi mwake, juu ya mambo ya imani.

Mwenye undugu au Uhusiano na Myahudi au Mkristo basi amfanyie wema kwa kumlingania kwenye Uislamu, kwani dini yake haimfai kwa chochote, na akisilimu ana malipo mara mbili, Amesema Mtume (Rehme na Amani zimfikie): “Watu wa aina tatu watapata malipo mara mbili: (katika moja ya watu hao mtume akataja) Mtu katika Ahlul-Kitab (yahudi au naswara) atakayemuamini Mtume wake na kumuamini Nabii Muhammad (Rehme na Amani zimfikie)”[2]

Muislamu anapaswa kujivunia na kujifaharisha na dini yake, Fahari inayozidi fahari ya mwenye kujivunia mali na maendeleo yake, kwani wafuasi wote wa dini nyingine wanapata hasara kubwa kama hawatofuata dini ya Kiislamu pindi unapawafikia ulinganizi wake. Hakika Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kuwa Waislamu, na akatuongoza kuifuata haki na kushikamana nayo.

  Huruma  kubwa zaidi ni mtu kuihurumia nafsi yake na nafsi za ndugu na jamaa zake kwa kujitahidi kuziokoa  katika adhabu ya milele, kwani mtu yeyote hataingia Peponi mpaka amuamini Mtume (Rehme na Amani zimfikie) na awe ameamini ujumbe wake na kumfuata, na wanaolingania katika njia ya Mwenyezi Mungu ndio watu wenye huruma zaidi, kwani Wanajitahidi kulingania kwa ndimi zao, fedha, na elimu alizowapatia Mwenyezi Mungu  ili kuwatoa watu katika adhabu ya Mwenyezi Mungu, hakika katika jukumu hilo kuna hadhi na cheo kikubwa ambacho kila Mwislamu anatakiwa kuwa nacho, kwa kuwa na tabia ya kulingania katika njia ya  Mwenyezi Mungu Mtukufu. 

Amesema mshairi:

Fuata mwenendo wa mbora wa viumbe, kwani ndio njia ya kuwaokoa wanadamu.

neema zake zimekienea kila kiumbe = na wema wake umetawala duniani na akhera 

Alipokuja Mtume watu waliiona haki = na wakayaandaa masikio yao kuisikiliza.

Ewe Mola, mpe baraka ya kila tone la mvua inyeshapo, na Baraka ya kila yakimea majani na matawi.

Na umpelekee amani yenye harufu nzuri = Na familia na Maswahaba muda wote.

Marejeo

  1. Tazama: “Tuhfat al-Abrar” cha al-Baidawi (1/43), “Al-Maftahat fi Sharh al-Masabih” cha al-Mazhari (1/72).
  2.  Imepokewa na Al-Bukhari (97) na Muslim (154), kwa kutoka kwa Abu Musa Al-Ash’ariy 





  1. Anas bin Malik (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) anasimulia kuwa wakati akitoka msikitini akiwa Pamoja na mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) walikutana na mtu mmoja mbele ya msikiti, mtu huyo akamuuliza Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) wakati wa kusimama qiyama. inasemekana kuwa mtu huyo ndiye yule Bedui aliyekojoa msikitini kabla ya hapo, jina lake anaitwa Dhul-Khuwaisrah Al-yemeni[1].

2.   Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) alimuondoa katika swali lake na kumuelekeza katika swali muhimu zaidi, ambalo ni: Je, umetayarisha nini kwa ajili ya Qiyaamah? Je, umeandaa ibada nyingi kwa ajili ya siku hiyo?

Makusudio ya Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) katika swali hili ni kumzindua mtu huyu ili atambue wajibu wake na ajue yanayompasa kufanya, nayo ni kujiandaa kwa ajili ya siku ya hesabu kwa kutenda matendo mema yatakayokuwa sababu ya kuingia Peponi, na sio lazima kujua wakati wa kusimama Kiyama, japo kuwa ukweli ni kwamba Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayejua wakati wake.

3.   Yule mtu aliposikia swali la Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) nyenyekea na kutulia, akatathimini matendo yake na akayaona ni machache saana, akakiri mapungufu yake, na kuomba msamaha kwa kuuliza swali hilo.

4.   Kisha akaeleza kwamba hakujitayarisha kwa kufanya ibada kubwa, japo kuwa ibada za Sunnah na utiifu zinazomuingiza mtu peponi na kumuepusha na moto ni nyingi saana, lakini mtu huyu inaonekana alitosheka kufanya matendo faradhi ambayo Muislamu lazima ayafanye[2].

Na inaweza kuwa alisema hivyo kwa sababu ya unyenyekevu wake na kuogopa kujitangaza, au Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) alimuona hafanyi ibada kwa wingi, au alimaanisha kwamba ibada zote ziko chini zikilinganishwa na upendo wake wa dhati kwa Mungu na Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake), jambo ambalo hakuna ibada kubwa inayolingana na kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

5.   Hata hivyo, kubwa kuliko yote aliyoyaona yule Mtu katika matendo ambayo yatamnufaisha Siku ya Kiyama: ni mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na maana yake ni kuwa na mapenzi ya dhati ambayo athari zake zinahitaji utiifu kwa mambo mengineyo.

6.   Ndio maana Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) alimwambia ikiwa atakuwa na nia thabiti katika mapenzi yake, kwa kutekeleza masharti yake, basi atakuwa sambamba na ampendaye, maaana yake atakuwa sambamba na Mtume na maswahaba zake katika Pepo ya juu kabisa. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wapo pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na (wakweli) wasadikishaji, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao”

[An-Nisa: 69].

Na ndio maana Anas (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) alisema: “Nampenda Mtume na Abu Bakar, na Umar, na ninatarajia kuwa pamoja nao kwa sababu ya mapenzi yangu kwao, hata kama sijafanya kama waliyofanya.

Mafunzo

  1. Wazazi wa Anas na yeye pia hawakujali katika kumtumikia Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) haliyakuwa si mtumwa, na kazi ya utumishi kwa wakati huo ilikuwa ni kazi ya watumwa, si kwa Watoto wa waheshimiwa, pamoja na hayo mama wa Anasi alimshika na kumpeleka kwa Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) ili amtumikie. Na hapo tunajifunza kuwa desturi na maneno yanayosemwa kwa watu yasimzuie Muislamu kufanya matendo ya kumuingiza peponi kama anasi alivyomuhudumia Mtume bila kujali maneno ya watu. 

  2. Anas (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) alipenda sana kushikamana na Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) na kumtumikia licha ya umri wake mdogo, ndo maana zimekuja Hadith zikieleza kwamba Anasi alikuwa anacheza na vijana wenzake [3] wakati huo, hivyo basi tunajifunza kuwa si lazima katika kumlea kijana mdogo katika tabia njema kwa kumzuia mambo ambayo yanaendana na umri wake.

  3. Yule mtu alieuliza kuhusu wakati wa Qiyama, Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) hakujibu, bali alielekeza swali lake katika swali jingine lenye maslahi ya muulizaji na wengineo, na swali hilo lilihusu kutenda matendo mema kwa ajili ya siku ya kiama, na hii mbinu aliyoitumia Mtume inajulikana kwa wataalamu wa fasihi kama mbinu ya wenye hekima, ambayo mtu hujibu swali kwa faida ya muulizaji, na hiyo inamuongezea muulizaji faida ambayo hakuwa anajua. Kama jibu la Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) kwa mtu aliyemuuliza kuhusu kutawadha maji ya bahari, Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alimjibu kuwa “Maji yake ni safi, na mzoga wake ni halali kuliwa[4]”; katika sentensi hii Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alitoa ufafanuzi juu ya usafi wa maji ya bahari kwa ujumla, kisha akawaongezea kwamba mizoga ya bahari inajuzu[5]. Hivyo basi ni wajibu kwa Mlinganiaji na mwalimu achunge mahitaji ya watu, na atumie hekima katika maneno na majibu yake, asijibu tu kulingana na maswali yao, bali azungumze na watu kuhusu mambo yatayo wasaidia kidini na kidunia, pasina kuleta fitina, kwa kujibu kulingana na matakwa yao, ikiwa atafanya hivyo itakuwa hakuna faida katika ujuzi wake.

  4. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) aliigeuza fikra ya muulizaji kutoka katika maswali Yasiyo na tija kwake, ambayo hayana faida kujibiwa: (Qiyama kitasimama lini) kwenda hatua ya kivitendo: (Umetayarisha nini kwa ajili yake), ndio maana Imam Malik hakupenda kuzungumza maneno bala matendo, na ndivyo walivyokuwa wanachuoni wa kabla yake[6], na watu wengi hivi sasa katika mradi mbalimbali huzozana na kutofautiana katika mambo yasiyo na tija, hivyo basi ukiuliza uliza swali lenye faida.

  5. Vizuri Muislamu ayafanye maneno haya: “Umetayarisha nini kwa ajili ya Qiyama?” Kuwa ndio mfumo wa maisha yake, afanye hima kuwajibika kila siku kwa kufanya matendo mema, ili kuona namna ya kukutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu siku hiyo? Je, atakutana naye akiwa amemridhia au amemkasirikia?

  6. Kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, (Rehma na Amani ziwe juu yake), sio tu kwa madai na kusema tu, bali ni hisia ya Moyo, Kisha inafuata kupata radhi za anaependwa na kumtii. kulingana na Upendo uliopo moyoni, kiasi kwamba Kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kutafikia hatua ya kuwa zaidi ya pesa, watoto, na watu wote. Hivyo basi Anayedai kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi ajipime mwenyewe je anapata ushahidi wa mapenzi yake? Amesema Hassan Al-Basri: Baadhi ya watu walidai kuwa wanampenda Mwenyezi Mungu, basi akawajaribu kwa aya hii[7]:

    “Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi. Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakusameheni madhambi yenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu”

    [Al Imran: 31].

  7. Haijalishi unadhambi kiasi gani moyoni mwako, au unafanya madhambi kiasi gani katika Maisha yako, Kwa hivyo usiache kumpenda na kumtukuza Mwenyezi Mungu pamoja na kumpenda Mtume, Rehema na Amani ziwe juu yake, kwani sisi sote hatufikii nafasi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu peponi; Kwa sababu ya Daraja zao kubwa, na Ukubwa wa Ibada zao, na ukweli wa Imani zao na Utiifu, licha ya mateso na misukosuko waliyopitia. Pamoja na hayo yote tunaweza kuwa pamoja nao huko peponi kwa kuwapenda vyema, na kuwaheshimu, na kufuata mienendo yao, na kutanguliza upendo wao kuliko upendo wa watu wote.  Na hii Ni bishara njema kwa wale walio makini. Ndio maana Anas (Mwenyezi Mungu amuwie Radhi) akasema: “Sikupata kuwaona Waislamu wakifurahi zaidi baada ya Uislamu kwa kitu kingine kama walivyofurahia kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake” .

8.    Jitahidini kumpenda zaidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, (Rehma na Amani ziwe juu yake), kwa kufanya sababu za kupata upendo huo, kama vile kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumswalia Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) na kuusafisha moyo kwa kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuzikumbuka neema zao, na kuwatii kama unavyoona mpenzi anatafuta Radhi za kipenzi chake, mapenzi yako kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, rehema na amani ziwe juu yake, Yawe makubwa Zaidi, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

“Na miongoni mwa watu wapo wanao abudu Waungu wasiokua Mwenyezi Mungu, wanawapenda kama wanavyompenda Mwenyezi Mungu, lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi.”

[Al-Baqarah: 165]

Marejeo

  1. Tazama: Fath al-Bari cha Ibn Hajar (10/555).
  2. Tazama: Al-Mufhim cha Al-Qurtubi (6/646).
  3. Imesimuliwa na Muslim (2604).
  4. Imepokewa na Al-Tirmidhiy No. (69).
  5. Tazama: Al-Kawakib Al-Dariri cha Al-Karmani (22/35).
  6. Tazama: “"Jamie Bayn Aleilm Wafadlihi"” ya Ibn Abd al-Barr (2/95).
  7. "Tafsir Ibn Kathir" (2/32), ambayo Aya imetajwa hapa.


  1. Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amekataza kuwatukana maswahaba zake waliokutana naye na kumwamini na wakafa juu ya Uislamu, kwani wao ni watu bora zaidi baada ya Mitume, amani iwe juu yao. Kwa vile wao ndio waliopata tabu ya kueneza Uislamu katika sehemu za ardhi, na wakamtetea Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, na wakawakabili watu wao katika njia yake, na wakawafanyia uadui wale wanaomfanyia uadui, awe mgeni na mtu wa karibu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwateuwa kwa uswahaba wa Mtume Wake, amani iwe juu yake, kama alivyomteuwa kwa unabii wake.” Ibn Masoud radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: “Mwenyezi Mungu alizitazama nyoyo za waja wake na akakuta moyo wa Muhammad, rehma na Amani zimshukie, ndio bora ya nyoyo za waja Wake. Basi akamchagua kwa ajili yake, hivyo akamtuma na ujumbe wake, kisha akatazama ndani ya nyoyo za waja baada ya moyo wa Muhammad. Alizikuta nyoyo za maswahaba wake kuwa ndio nyoyo bora zaidi katika waja wake, hivyo akawafanya kuwa Mawaziri wa Mtume wake, wakipigania dini yake”[1]Na Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwasifu maswahaba wa Mtume wake katika sehemu zaidi ya moja ndani ya Qur’an, na akawafadhilisha kuliko waja wake wengine na akabainisha ridhaa yake kwao na msamaha wake kwao. Ndio maana kuwatukana na kuwadharau ni haramu na ni dhambi kubwa, na ni dalili ya unafiki na uzushi. Anaye wachukia Maswahaba ni dhalimu ambaye unafiki wake uko wazi kabisa, au kafiri anayeficha ukafiri na kuudhihirisha Uislamu. Kwa hiyo, baadhi ya wataalamu wa elimu ya kisharia walipendekeza kuwaua wale waliowasingizia masahaba na kuwatukana.[2]

2.   Kisha Mtume, Rehema na Amani zimshukie, anaeleza sababu za uharamu wake wa kuwatukana kwa kutaja fadhila zao na hadhi yao kubwa, hivyo anaapa kwa Mwenyezi Mungu ambaye ana uhai wa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, ambaye akitaka ataichukua au kuiacha mkononi mwake, na ikiwa ataipa majaribu au kuiponya, kwamba ujira wa matendo ya Maswahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao haulingani na chochote katika matendo ya watu wengine. Lau mtu mmoja angetoa dhahabu kama Mlima Uhud, malipo yake hayawezi kuwa sawa na malipo ya Swahaba kama angetoa tende zilizojaa vitanga vyake viwili vya mikono, na wala haiwezi kufikia japo nusu kitanga kimoja.Bali haya yalitokana na kujitolea kwao licha ya dhiki ya hali yao na uzito wa mahitaji waliyo kuwa nayo, na kwa sababu wao walikuwa kizazi cha kwanza kilichoeneza Uislamu na kubeba majukumu ya kulingania kwenye haki mabegani mwao, na wakapigana na wakauawa, wakashuhudia kushuka wahyi, wakafuatana na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie katika safari zake. Kwa hili na mengine mengi, wanastahili malipo makubwa zaidi. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akawasifu na kuwasema vizuri kwa kusema:

“Wapewe mafakiri Wahajiri walio tolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake, na wanamnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio wa kweli (8) Na walio andaa maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa”

[Al-Hashr: 8, 9].

Mafunzo

  1. Jihadhari na kuwatukana na kuwakashifu Maswahaba wa Mtume, rehma na Amani ziwe juu yake; kwakuwa ni kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

  2. Vipi unawatukana wale ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwasifu na kuwataja kwa uzuri na kuwateua kwa ajili ya kundi la Mtume Wake, rehma na Amani zimshukie.

  3. Waislamu wasijihusishe na fitna iliyotokea baina ya Maswahabah, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao. Walikuwa ni wafasiri wasiokusudia ila wema, na aliyepatia na liyekosea katika wao ni mwenye kusamehewa na mwenye kuridhiwa.

  4. Kila Muislamu anapaswa kuelimisha familia yake na kuwafundisha juu ya kuwapenda na kuwaheshimu Maswahabah, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.

  5. Ikiwa Maswahaba ni watu bora zaidi baada ya Mitume, na wao ndio walioshuhudia kushuka kwa wahyi, na wanajua yale yanayoruhusiwa na yale yaliyoharamishwa. basi inafaa sisi kuwaiga wao na tufuate mienendo yao. Abdullah bin Omar, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: “Mwenye kutaka kuiga basi awaige wale waliofariki dunia. Hao ni Maswahaba wa Muhammad Swalla Allaahu alayhi wa sallam, Walikuwa ni watu bora wa Ummah huu, wenye nyoyo njema, wenye elimu zaidi. na aliye dhihaki kidogo. Wamechaguliwa na Mwenyezi Mungu kuwa maswahaba wa Mtume wake, rehma na amani zimshukie, na kwa ajili ya kuifikisha dini yake. Basi igeni maadili na njia zao, kwani wao ni maswahaba wa Muhammad, rehma na amani zimshukie, ambao walikuwa kwenye uwongofu.”[3]

  6. Kila Muislamu anatakiwa asome wasifu wa Maswahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na aone jinsi walivyokuwa na jinsi maadili yao yalivyokuwa, na kwa nini daraja zao zilipanda. Baadhi ya watu walimwambia Al-Hasan Al-Basri, Mwenyezi Mungu amrehemu: Tuambie khabari za masahaba wa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: Akalia Al-Hasan Al-Basri, na akasema: “Alama za wema zilionekana miongoni mwao katika suala la ubora, uaminifu, mwongozo, na ukweli. Nguo zao ni zakawaida kwa thamani ya chini, kutembea kwao kwa unyenyekevu, mishipi yao ya kazi, na chakula chao na vinywaji vyao ni katika riziki za halali. Na utiifu wao kwa Mola wao Mlezi aliyetukuka, na kutafuta kwao haki katika yale wanayoyapenda na kuyachukia, na kuwapa haki itokayo kwao, matamanio yao yakawa na kiu.[4]Na miili yao ikayeyuka, na walidharau hasira za viumbe kwa kutafuta radhi ya Muumba, hawakuzidisha hasira, hawakusema vibaya, na hawakuvunja hukumu ya Mwenyezi Mungu katika Qur'an, walizishughulisha ndimi zao kwa kumtaja Mwenyezi Mungu, walitoa damu zao alipowaomba msaada, na walitoa pesa zao alipowakopa, na khofu yao ya viumbe haikuwazuia, maadili yao yalikuwa mazuri. kidogo kiliwatosha kutoka katika dunia hii hadi akhera yao.” .

7.   Inajuzu kwa mtu kuapa juu ya kitu bila ya mtu yeyote kumtaka kiapo; ili kukazia kwa alichosema.

8.   Kinachoangaliwa si wingi, bali ni yakini na imani, na pengine dirham itatangulia dirham elfu moja. Usidanganywe na wingi wa kujitolea watu, au ambayo yatakukatisha tamaa ya kutumia kile ambacho umejitahidi, kutoka kwa kile ambacho umejiwekea kutoka kwa nguvu zako.

9.   Enyi watu, lau mngetoa khazina zote za ardhi hazitofikia ujira wa kazi ndogo waliyo ifanya Maswahaba, vipi uwatukane au uwaudhi?

Marejeo

  1. Imesimuliwa na Ahmed (3600).
  2. “sherh Al-Nawawi katika sahihi Muslim” (16/93).
  3. Imesimuliwa na Abu Naim katika Hilyat al-Awliya’ (1/305-306).
  4. Imesimuliwa na Abu Naim katika Hilyat al-Awliya’ (2/150).