عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ لِمُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ حِينَ بَعَثَهُ إِلَى اليَمَنِ: «إِنَّكَ سَتَأْتِي قَوْمًا أَهْلَ كِتَابٍ، فَإِذَا جِئْتَهُمْ، فَادْعُهُمْ إِلَى أَنْ يَشْهَدُوا أَنْ لا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَأَخْبِرْهُمْ أَنَّ اللَّهَ قَدْ فَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَوَاتٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَأَخْبِرْهُمْ أَنَّ اللَّهَ قَدْ فَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً تُؤْخَذُ مِنْ أَغْنِيَائِهِمْ فَتُرَدُّ عَلَى فُقَرَائِهِمْ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَإِيَّاكَ وَكَرَائِمَ أَمْوَالِهِمْ، وَاتَّقِ دَعْوَةَ المَظْلُومِ؛ فَإِنَّهُ لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَ اللَّهِ حِجَابٌ» متفق عليه


Kutoka Ibn Abbas (r.a) amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake, kumwambia Mua’dh ibn Jabal wakati alipomtuma kwenda yemen:

1. “Hakika wewe utawaendea watu wa kitabu 2. Utakapo waendea, walinganie kwenye shahada wakiri kwa moyo kuwa hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye peke yake, na hakika Nabii Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. 3. Ikiwa watakukubalia hilo, basi waeleze kwamba hakika Mwenyezi Mungu amewafaradhishia sala tano mchana na usiku. 4. Ikiwa watakukubalia hilo, basi waeleze kuwa Mwenyezi Mungu amewafaradhishia juu yao, zaka ya mali zao, inachukuliwa kutoka kwa matajiri wao na inapelekwa kwa maskini wao.  5. Ikiwa watakukubalia hilo, basi jiepushe na kuchukua malizao bora zaidi. 6. Na ogopa duwa ya aliye dhulumiwa, kwani hakika hakuna kati yake na Mwenyezi Mungu pazia” . Imepokelewa na Bukhari na Muslimu. 


Alimtuma Mtume (s.a.w) Mua’dh kwenda yemen hali akilingania na akisimamia hukumu, karibia kabisa na mwaka wa tisa hijiriya(9h):

  1. Na akamweleza kwamba atawaendea watu katika mayahudi au manaswaara miongoni mwa waliokua na kitabu cha taurati au injili, ili ajiandae kwakuwa wao walikuwa ni watu wenye elimu kiujumla, [1].

  2. Kisha akamuusia aanze kuwalingania juu kukiri upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuukubali utume wa nabii wake (s.a.w), kwa sababu kuyakubali hayo mawili ndio msingi wa dini ambao hakitakubalika chochote katika matawi yake ila baada ya kuukubali misingi hiyo miwili, basi wao wanahitajika kwanza kuvikusanya, [2] kwani mayahudi na manaswara hawakutekeleza yale ambayo ingekuwa ni sababu ya kuwaokoa, kama kushuhudia kwa kukubali kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuukubali utume wa nabii Muhammad(s.a.w), basi wao walimshirikisha Mwenyezi Mungu pamoja na issa ibn maryam, na wakakanusha da’wah  ya Mtume (s.a.w) [3] 

  3. Kisha akamweleza Mtume (s.a.w) kwamba wakifuata utakayo waamrisha kwa kutamka shahada mbili, na wakakubali kumpwekesha Mwenyezi Mungu na wakakubali utume wa Nabii Muhammad (s.a.w), basi wajulishe kwamba hakika Mwenyezi Mungu amewafaradhishia kusali sala tano mchana na usiku, na uwafundishe namna ya kusali.

Na hakika yamejulisha maneno ya Mtume (s.a.w): “Ikiwa watakukubalia hilo” juu ya kufuata na kiutendaji sio alimradi kukubali uwajibu na ulazima, basi ni lazima wakubali na watekeleze sala katika nyakati zake [4].

4.   Kisha akaenda hatua kwa hatua baada ya kukubali uwajibu wa sala na kuitekeleza kwake, akahamia kwenye zaka, basi akamuamrisha awafundishe kwamba Mwenyezi Mungu amewalazimisha matajiri kutoa zaka, nacho ni kiwango kidogo kinachojulikana kinakusanywa kutoka katika mali zao, na kinagawiwa kwa masikini wao.

5.   Kisha akamuamrisha Mtume (s.a.w) Mua’dh (r.a) ikiwa watu watamkubalia hilo na wakatoa zaka ya mali zao, basi achukue kiasi cha zaka kujiepusha na kutoa mali nzuri ambazo wanazipenda wenye mali hizo na nafsi zao zimefungamana na mali hizo kwa kuzipenda; kama mfano, mtu akiwa na mbuzi anaempenda zaidi  na anampatia kipaumbele zaidi ima kwa wingi wa maziwa yake, au kwa sababu nyingine, basi mfano wa mbuzi huyo hatakiwi kuchukuliwa katika zaka, kwa kuwafanyia upole wenye mali, na Mwenyezi Mungu hakujaalia kuwaliwaza masikini katika kuwapitasha madhara matajiri, na ikiwa nafsi ya tajiri ikiridhika kwa kutoa kitu bora zaidi, basi itafaa kuchukua kwa ridhaa yake. Na amesema omar ibn al-khatwab (r.a) kumwambia mtu aliye mtuma kukusanya zaka: “Na usichukue katika zaka mnyama bora alienenepeshwa ili achinjwe, wala ruba- ambaye huwa anabakishwa nyumbani wala haachwi kujitafutia chakula kutokana na uzuri na ubora wake kwa anaemmiliki, wala mwenye mimba- ambaye anakaribia kuzaa, wala dume tegemezi katika wanyama” [5]

6.   Kisha akamtahadharisha Mtume (s.a.w) mwisho mbaya wa kudhulumu, katika kukusanya zaka au katika mambo mengine ya kiutawala na kihukumu, na makusudio ya kujiweka mbali na dua ya mwenye kudhulumiwa: ni kujiepusha na sababu zake; kwa sababu dhulma-kudhulumu- ndio inapelekea kupatikana maombi mabaya dhidi ya mwenye kudhulumu.

Na duwa ya mwenye kudhulumiwa huwa inasikika zadi na kujibiwa na wala hairudi patupu, hufunguliwa kwayo milango saba ya mbingu, na hakuna pazia kati yake na kujibiwa kwake, [6]  na katika hadithi: “ Watu watatu duwa zao hazirudi patupu-bila majibu-: mwenye kufunga saumu mpaka afungue, na kiongozi mwadilifu, na maombi ya mwenye kudhulumiwa, anayanyanyua Mwenyezi Mungu maombi hayo mawinguni na anayafungulia milango ya mbingu na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “ Naapa kwa nguvu zangu nitakunusuru kukusaidia japo baada ya muda” [7] 

Mafunzo

  1. Nabii Muhammad (s.a.w) alimtuma Mua’dh ibn jabal kwenda yemen hali yaku akiwa kwenye miaka ya ishirini katika umri wake, basi akabeba majukumu ya ugeni na kuwa mbali na watu wake na katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutii amri ya Mtume (s.a.w), ni mara ngapi sisi tunavumilia matatizo na majukumu kwa ajili ya njia hiyo?

  2. Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake, akiwabebesha maswahaba zake majukumu mazito makubwa, hali wakiwa katika ujana wao, na wao hawakuwa wakiyakimbia majukumu hayo, basi ni juu ya baba, mzazi, mwalimu, mlezi na wengineo kuwaandaa kuwazoesha walioko chini yao kuwapa majukumu, na wasiwadogeshe, na ni juu ya hao pia kuyapokea vyema majukumu hayo na kuyafanyia kazi.

  3. Chukuwa yaliyo sihi miongoni mwa maneno ya Mtume Muhammad (s.a.w), japo akiwa mpokezi au msimulizi wake ni mmoja, kwani alimtuma Mtume (s.a.w) Mua’dh akiwapeke yake kwa mambo makubwa miongoni mwa itikadi na ufahamu, na kutoka katika mamlaka hata katika mali za watu, na yote hayo yanajulisha juu ya kuzingatia maneno ya mtu mmoja.

  4. Jifunze kujuwa tabia za unao waendea, hakika alimueleza Mtume (s.a.w) Mua’dh (r.a) ya kwamba atawaendea watu waliopewa kitabu, ili kuchunga yanayo paswa kuwalingania [8] , katika vipaumbele vya dalili na njia za kulingania na mambo mengine, na kwa sababu wao ni watu wa elimu na mijadala, basi pupia kukusanya taaluma ya kutosha na yenye athari, kabla ya kazi yeyopte unayotaka kuifanya.

  5. Mtume (s.a.w) alitilia umuhimu zaidi kuwaelekeza wafanyakazi wake na watoa mawaidha, kwakuwa yeye hakumtuma Mua’dh mpaka alipombainishia hali halisi, na pia akampangia kazi, na akamuamrisha kuwa mwadilifu, na akamtahadharisha kutokana na kudhulumu, pamoja na ukamilifu wa Mua’dh kwenye dini yake na elimu yake, basi usiache kumuusia uliye naye, na nijuu ya anaye pewa wosia kuto kupuuza wosia huo.

  6. Mtume (s.a.w) alitilia umuhimu zaidi vipaumbele vya  kwanza kisha akaenda hatua kwa hatua, basi hakumuamrisha Mua’dh kuanza na madhambi ambayo watu hawaepukani nayo katika maisha yao na tabia zao, pamoja na kuwepo umuhimu wa kuyakemea hayo, lakini alianza na misingi ya dini, na funguo za imani nao ni shahada mbili, kisha sala, kisha zaka, na hivi ndio tunatakiwa kuwa katika malezi yetu na ulinganiaji wetu na kusomesha kwetu, bali tunapaswa kufanya hivyo katika kazi zetu zote, tuanze na lililo muhimu zaidi kisha linalo fuatia kwa umuhimu, amesema A’ishat (r.a) “Si vinginevyo hakika uliteremka wa kwanza ulioteremka katika ufunuo ni sura zilizo pambanuliwa, katika hizo pametajwa pepo na moto, mpaka watu walipoufuta uislamu ikateremka katika ufunuo yaliyo halali na haramu, kama ingeteremka mwanzoni tu “ msinywe pombe”  basi watu wangesema hatutaacha pombe milele, na kama ingeteremka mwanzoni “msizini” basi wangesema hatuwezi acha zinaa milele” [9]

  7. Imani, sala na zaka, ndio misingi ya imani kubwa ambayo imekaririwa kwa kukutanishwa katika qur’ani tukufu na maneno ya Mtume (s.a.w) kwa wingi sana, na ndani yake kuna malipo makubwa (thawabu) na kuathirika kiimani, kwa kiasi ambacho hakuna akijuaye isipokuwa ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi hata ukiwa wewe na wenzako mnatekeleza misingi hiyo basi pupieni kuifanya kikamilifu.

  8. Alimtahadharisha Mtume Muhammad (s.a.w) Mua’dh kuchukua zaka ambayo nafsi zimefungama nazo kutokana na ubora na uzuri wa sadaka hiyo, bali alimuamuru kuwa mwadilifu, na kufanya hivyo ni katika uadilifu na kuchunga hisia za watu na uelewa wa watu ambao ni juu ya kila mlinganiaji na baba na mlezi mwenye kusimamia mambo afanye kama hivyo, basi azingatie hayo katika kuamrisha kwake na kukataza kwake.

  9. pupia kulala hali yakuwa hakuna aliye dhulumiwa ambaye kakosa kulala kutokana na huzuni kwa yale uliyoyasema au kumtendea,sawasawa awe ni mume au motto, au mwanafunzi au mfanya kazi, au muuzaji au dereva, na wala usiirahisishe dhulma kwa yule unaye muona yuko chini yako, japo akiwa katika waasi, na hakika alimuhofisha nabii muhammad (s.a.w) Mua’dh kutokana na dhulma upeo wa kuhofisha,hata katika kutaamali na makafiri niongoni mwa watu wa kitabu, na baadhi yao wanaweza kuamini na wengine wasiamini.

  10. Amesema mshairi:Usifanye dhulma katu hata ukiwa na uwezo wa kufanya hivyo = kwani hakika dhulma mwisho wake inakuletea majutoMacho yako yAnasinzia hali aliyedhulumiwa halali yuko macho = akikuombea duwa mbaya na jicho la Mwenyezi Mungu halilali.

Marejeo

  1. Fath al-Bari cha Ibn Hajar (3/358).
  2. “Kashfu Litham ufafanuzi wa Umdat al-Ahkam” cha al-Saffarini (3/400).
  3. Kumkamilisha Mwalimu kwa Faida za Muislamu cha Qaadh Iyadh (1/239).
  4. Tazama: “katika ufafanuzi wa al-‘Umdah cha Ibn al-Attar” (2/798).
  5. Malik (2/372), na al-Tabarani katika Kamusi Kuu (6395). Na ameisahihisha Al-Nawawi katika “A l-Majmuu’” (5/427), na Ibn Katheer kaboresha upokezi wake katika “Irshad Al-Faqih” (1/248).
  6. Fath Al-Mun’im ufafanuzi wa Sahih Muslim cha Musa Shaheen Lashin (1/70).
  7. Al-Tirmidhiy (3598), na Ibn Majah (1752), kutoka kwa Abu Hurayrah, na meisahihisha Ibn al-Mulqin katika “Al-Badr al-Munir” (5/152).
  8. Fath al-Bari cha Ibn Hajar (3/358).
  9. Sahihi Al-Bukhari (4993).


Miradi ya Hadithi