عن ابن عبَّاس رضي الله عنه قال: (بُعِثَ رسولُ الله لأربعين سنةً، فمكثَ بمكةَ ثلاثَ عشْرةَ سنةً يُوحَى إليه، ثم أُمِر بالهجرةِ فهاجر عشْرَ سنين، ومات وهو ابنُ ثلاثٍ وستينَ سنةً)

kutoka kwa Ibn Abbas (r.a) amesema:“Alipewa utume Nabii Muhammad (s.a.w) Akiwa na umri wa miaka arobaini.Basi alikaa mjini makkat miaka kumi na tatu (13) akipewa ufunuo.Kisha akaamrishwa kuhama basi akahamia Madina miaka kumi.Na alikufa akiwa na umri wa miaka sitini na tatu(63)”


Uislamu umesimama juu ya kukiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi kuwa hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye (Allah) peke yake, na hakika Muhammad ni mjumbe na Mtume wake, na kutambua kuwa Mtume (s.a.w) ni msaidizi katika kuifikia imani nzuri, kwa nini isiwe hivyo wakati yeye mkamilifu wa watu na mwingi wao kwa fadhila na ubora juu yetu. Na katika hadithi hii Anasimulia ibn abbasi (r.a) hatua muhimu sana alizo zipitia Nabii Muhammad (s.a.w) katika uhai wake, basi anaeleza:

  1. Hakika Mtume rehma na amani aliteremkiwa na jibril (a.s) kwa wahyi (ufunuo) na akamuamuru kufikisha baada ya kufikisha (s.a.w miakla arobaini (40), yaani yeye alizaliwa mwaka wa hamsini na tatu 53 kabla ya kuhama kwake kwenda madina, na ulikuwa ukiitwa mwaka wa tembo, na akapewa utume mwaka wa kumi na tatu kabla ya kuhama kwake. Na hakika Mwenyezi Mungu alimchagulia mji wa makka ndio yawe mazazi ya Mtume wake (s.a.w) na sehemu ya kukulia kwake, katika mji huo ndio alizaliwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake kwenye nasaba tukufu, kwani baba yake ni Abdallah ibn abdu al-mutwalib, al-hashimiyyu, al- qurashiyyu, na mama yake ni A’mina bint wa abdi manafi ibn zuhrat al-qurashiyyat [1], alikuwa Mtume ni katika waarabu wenye nasaba tukufu. Amesema Mtume (s.a.w): “Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua kinanat katika watoto wa ismail, na akawachagua maquraysh katika kinanat, na akachagua kutoka kwa maquraysh banii hashim, na akanichagua mimi katika banii hashimu” [2]. Alikufa baba yake Mtume hali yakuwa yeye ni mimba katika tumbo la mama yake, basi akazaliwa Mtume (s.a.w) akiwa yatima, na akakulia katika uangalizi wa mama yake, kisha mama yake Alikufa hali Mtume akiwa na miaka sita, basi akaendelea kuwa chini ya uangalizi na malezi ya babu yake, kisha babu yake alikufa hali Mtume akiwa na umri wa miaka minane, basi hapo akamlea ami yake abuu twalib. [3] Aliendelea Mtume kuishi Makkat kwa kipindi cha hii miaka arobaini, Mwenyezi Mungu Mtukufu akimlea na akimuandaa maandalizi yanayoendana na kazi yake ambayo Mwenyezi Mungu aliyo mchagulia, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

” Hivi hakukukuta ukiwa yatima akakuhifadhi na kukuliwaza (6) na akakukuta ukiwa hujui chochote katika dini na akakupa mwongozo wa kutenda mema (7) na akakukuta ukiwa maskini kisha akakutajirisha kwa kutosheka”. (8)

[adh-dhuha:6-8],

Akaishi pamoja na watu wake maisha mazuri tena kwa tabia nzuri, akishirikiana nao kila jambo lenye manufaa, na mwenye kujitenga mbali na kila baya na chafu.Na hakika alimuoa Mtume (s.a.w) Khadija bint khuwaylid na Mwenyezi Mungu akampa riziki ya watoto wote kutokana na khadija, nao ni :Q asim, Abdallah, Zainab,Rruqayyat, Ummu kulthum na Fatuma- isipokuwa Ibrahim ambaye alimpata mjini madina kupitia Mariyat al-qibtiyah- [4] kisha jibril akamteremkia Mtume (s.a.w) akiwa katika jabal hiraai –pangoni-  na akamteremshia:

“ Soma - ewe Muhammad- kwa jina la mola wako aliye umba(1)ambaye aliye muumba mwanadamu kwa pande la damu (2) soma na mola wako ni mwingi wa ukarimu (3) ambaye aliyewafundisha wiumbe vyake kuandika kwa kalamu (4) alimfundisha mwanadamu vitu alivyokuwa hvijuwi ” (5)

[al-alaq],

basi akayafanyia kazi majukumu ya utume.

2.   Baada ya ufunuo kuteremka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake, aliendelea kuishi makkat miaka kumi na tatu akipewa ufunuo, na akiwalingania watu kwa ufunuo huo, na alikutana na maudhi katika kazi hiyo, kupingwa vikali kiasi ambacho hakuna anaye weza kuvumilia kwayo, na hata aliyekuwa akimuamini pia alifanyiwa maudhi, na maudhi yalipozidi aliwaamuru waislamu kuhamia habashat mwaka wa tano wa utume, basi walihama zaidi ya maramoja, [5] . Na aliendelea Mtume kulingania katika mji wa makkat, na Mwenyezi Mungu alimtilia nguvu kupitia ami yake abuu twalib na mkewe khadija, mama wa waumini wakawa wanamtetea, mpaka ulipofika mwaka wa kumi wa utume, basi walikufa wote wawili, na akawa akitafuta mtu atakaekua akinusuru dini yake katika mji wa twaif hasa katika misimu ya hijja, na nyakati zinginezo, akawa akifanyiwa maudhi. [6]

3.   Baada ya Mtume (s.a.w) kukamilisha miaka kumi na tatu (13) katika mji wa makkat, Mwenyezi Mungu alimchagulia mji wa madina kuwa ndio makazi yake ya kuhamia, basi akahama Mtume (s.a.w) kwenda madina akisuhubiana na abuu bakari (r.a), baada ya kuwa maswahaba wengine  wamekwisha hamia huko, na walifuatia wengine katika walioweza kuhama baadae, aliendelea Mtume (s.a.w) katika mji wa madina akifanya kazi ya da’wah – kulingania- na jihadi na maslahi ya watu kwa kipindi cha miaka kumi, mpaka Mwenyezi Mungu akaitimiza neema yake ya dini na wakaingia watu katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi.

4.   Kisha akasimuliaAbdallah ibn abbas (r.a) kwamba hakika Mtume (s.a.w) alikufa hali akiwa na umri wa miaka sitini na tatu, (63) baada ya kulingania watu kwa miaka ishirini na tatu, miaka kumi na tatu katika mji wa makkat na miaka kumi katika mji wa madina, na kifo chake kilitokea chumbani kwa A’isha (r.a), siku ya jumatatu tarehe kumi na mbili mwezi wa tatu mwaka wa kumi na moja tokea kuhama Mtume (s.a.w).     

Mafunzo

  1. Amini uumbaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na rehma zake, na utafute msaada wake, kwa hakika alizaliwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akiwa yatima wa baba, kisha akafa mama yake  na babu yake hali akiwa bado ni mototo, basi akalelewa na ammi yake pamoja na ufaqiri aliokuwa nao, na wingi wa watoto zake, na desturi katika mazingira haya ni lazima yatima huyu kuishi katika hali ya dhiki na uangalizi mdogo,  lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye mikononi mwake ndio kuna makadirio ya mambo yote, basi akamfanya yatima huyu baada ya miaka na miaka kupita kuwa ndio bosi na bwana wa walimwengu, basi asikate tamaa mwanadamu katika rehma za Mwenyezi Mungu, vyovyote mambo yatakavyo kuwa yamembana, na awe na imani kuwa yupo mola anaye simamia na kuyaendesha mambo,  bali akilitaka jambo husema “ kuwa: basi linakuwa kama alivyo taka liwe”

  2. Mtume (s.a.w) aliendelea kwa miaka kumi na tatu akiwalingania watu katika mji wa makkat, alikuwa akitoka kwenda masokoni na kwenye mikusanyiko ya watu akiwalingania katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu, hachoki wala hapati uvivu wala hakati tamaa kutokana na kuamini watu wake, na wala hapati uzito kwa kumpinga kwao na kumtuhumu kwao, alikuwa ni mpole katika maneno yake na ulimi wake, pia ni mwenye huruma kwa watu wake, akiwaombea mwongozo kwa Mwenyezi Mungu, na anasaidia katika mambo mema ya watu kama kutunza amana na mengineyo, wala hakufadhaika kwa kifo cha ami yake ambaye alikuwa akimlinda kutokana na maudhi ya watu wake, wala hakudhoofika kwa kifo cha mke wake kipenzi khadija ambaye alimnusuru na kumtia moyo katika kuifikisha dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa nafsi yake na kwa mali yake, hivi kwanini Mtume asiwe kiigizo chema kwa walinganiaji na wanaotafuta elimu ya kisheria? Na watoa mawaidha katika njia ya kuvumilia maudhi na kusubiri wakati wa kuwalingania watu, na kuyavumilia maudhi ya watu haliyakuwa wao hawayapati maudhi mfano wa aliyoyapata Mtume (s.a.w)?

  3. lilipokuja agizo la Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake (s.a.w) la kuhama, basi Mtume hakuhuzunika kwa kuiacha familia, mali, nyumba na mji mtukufu wa makkat, bali si vinginevyo alitekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na shida na matatizo aliyokuwa nayo katika nafsi yake, nahii ndio hali ya muumini wa kweli, anayafanya kuwa mepesi yale anayokutana nayo kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

  4. Jambo la kuhama ni pana sana, na si lazima kuhama iwe kutoka mji na kwenda mji mwingine, bali inaweza kuwa kuhama kutoka katika mazingira na matendo kwenda kwenye mazingira na matendo mazuri zaidi kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

  5. Yalipitia maisha ya Mtume (s.a.w) katika hatua za aina yake na matukio tofauti, ambayo yako kati ya wepesi na uzito, na shida na starehe, na vita na amani, na siri na dhahiri, na kudhoofika na kuimarika yakashamili maisha hayo ya kibinadamu kila aina ya hali yake na hatua zake, na yakapita yote hayo kuwa ni mfano uliokamilika katika kumuenzi na kumuiga, na kupokea qadari (makadirio) za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hali yoyote.

  6. Kifo ni lazima hata kwa mtu mtukufu, na hata kwa mkamilifu wao kwa nguvu na akili, na hata kwa mwenye kulinda afya yake kutokana na vitu vyenye kuidhuru nafsi hiyo, na hata kwa mwenye kulingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kumwomba msamaha na afya, na hata kwa mwenye kuwanufaisha watu, basi haipendezi kwa mwenye akili kukisahau kifo, au kujisahaulisha kutokana na hesabu zake, na haipendezi kufadhaika kwa kufiwa na mtu wa karibu au mpenzi au mwana chuoni au mja mwema.

  7. Amesema mshairi:

Alizaliwa yatima akawa mtukufu wa sifa kwa wanadamu = basi wajifakhari masikini na mayatima.  

Kama alfajiri inavyotoka katika kiza kikubwa = ni kama roho inavyoingiza uhai kwa maiti hali ameshaoza   

Ni uzuri ulioje katika dunia kwa kuwa kubwa furaha yake = utaendelea uislamu ukiifunika dunia kwa furaha.

8.   Amesema hassani ibn thabiti: [7]

Watu wangu ndio ambao walimhifadhi nabii wao = na wakamsadikisha hali yakuwa watu wamemkanusha

Isipokuwa sifa za watu ambao ni wema waliotangulia = 

kwani watu wema wapo pamoja na wasaidizi.

Wakifurahia kiapo cha Mwenyezi Mungu kwa kauli zao = Alipowajia mtu mkarimu, na aliechaguliwa

Karibu, kwa usalama na kwa wasaa = ubora ulioje kwa Mtume, na ndio ubora wa ahadi na jirani.

Basi wakamweka katika nyumba isiyo na woga wowote = mwenye kuwa jirani yao kwa nyumba ndio jirani bora.

Marejeo

  1. Tazama: " Alsiyrat Alnabawiya " cha Ibn Hisham (1/110).
  2. Sahihi Muslim (2276), kutoka kwa Wathila bin Al-Asqa, Mungu amuwiye radhi.
  3. Tazama: “Alsiyrat Alnabawiya” cha Ibn Hisham (1/168: 179).
  4. Tazama: “Alsiyrat Alnabawiya” cha Ibn Hisham (1/187).
  5. Tazama: "Alsiyrat Alnabawiya: Ardhwul Waqayie Watahlil 'Ahdaathi"(uk. 191).
  6. Tazama: "Alsiyrat Alnabawiya: Ardhwul Waqayie Watahlil 'Ahdaathi"" (uk. 207).
  7. Sirat Ibn Hisham (1/664).


Miradi ya Hadithi