Mtume (Rehma na Amani zimfikie) alibainisha wazi kuwa ummah wake wote utaingia peponi kwa Fadhila na Rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu isipokuwa wale waliokataa kuingia humo na wakagoma kuingia, nao ni waliopinga Utume wake na kukiuka Sunnah (mwenendo) wake

Hadithi hii imebeba maana halisi ya dini, ambayo Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) ameeleza daraja muhimu za dini ambazo ni Uislamu, Imani na Ihsani (wema), pia alitaja baadhi ya alama za Siku ya Kiyama

Mtume (Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) anathibitisha kwamba dini ni kushauriana na kunasihiana, kwa mtu kufanya anayoyaweza katika kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu, na kitabu chake, na Mtume wake, viongozi wa Waislamu na watu wote.

Mtume (Rehma na Amani zimshukie) amesema kwamba Imani ina matunda matamu sana ambayo hawezi kuyaonja isipokuwa mwenye moyo uliojaa Imani. Kwa kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndio mola wake mlezi, na akafanya Uislamu kuwa ndio Dini aliyoiridhia na kuiamini, na akanyenyekea kwa Mtume wake Muhammad (Radhi Za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake), na kukiri Utume wake na wajibu wa kumuamini.

Ni: Abu Hafs, Umar bin Al-Khattab bin Nufail, Al-Qurashi, Al-Adawi, ambaye anakutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu, swala na salamu zimshukie, huko kwa Ka'b bin Luay, Al-Farouq, ni wa pili katika Makhalifah walioongoka, na wa kwanza kuitwa Amirul-Muuminina, na ni waziri wa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, alifariki mwaka wa (23 Hijiriya)[1] referencesNi: Abu Hafs, Umar bin Al-Khattab bin Nufail, Al-Qurashi, Al-Adawi, ambaye anakutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu, swala na salamu zimshukie, huko kwa Ka'b bin Luay, Al-Farouq, ni wa pili katika Makhalifah walioongoka, na wa kwanza kuitwa Amirul-Muuminina, na ni waziri wa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, alifariki mwaka wa (23 Hijiriya)

NI: Abu Huraira, Abd al-Rahman ibn Sakhr al-Dawsi, al-Azdi, alisilimu mwaka wa saba. amesema Ibn Abi Dawood: “Watu wa Hadith wamekubaliana kuwa Abu Hurairah ni katika maswahaba waliopokea hadithi nyingi.” Aliwahi kuwa kiongozi katika baadhi ya tawala, alifariki katika mji wa Madina mwaka wa (58 AH

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anaeleza kuhusu baadhi ya mambo ya siri yanayobainisha sifa na matendo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ameeleza kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa wa milele kabla ya kila kitu, na arshi yake ilikuwa juu ya maji kabla ya kuumba mbingu na ardhi. Kisha akasema kuwa Mwenyezi Mungu aliandika katika Kitabu kilichohifadhiwa, makadirio ya waja na matukio yote, baada ya hapo akaumba Mbingu na Ardhi.

Mola wetu Mtukufu anatuelezea kuhusu yeye mwenyewe, kwamba amejiharamishia dhuluma na amewazuia watu wasidhulumiane. Kisha akajipendekeza kwa waja wake, kwamba yeye ndie anaye ongoza, anaye toa riziki, anaye samehe, mwenye huruma. Na akabainisha kwamba hakuna yeyote mwenye uwezo wa kumdhuru au kumnufaisha. Pia akaelezea ukubwa wa hazina yake, kwamba haifirisiki, na yote ayapatayo mja, ni matokeo ya matendo yake mwenyewe, basi kila mmoja ajitahidi kutenda mema kwa ajili akhera yake.

Mtume (rehema na amani ziwe juu yake) anaeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ana Majina Mazuri tisini na tisa, yeyote atakayeyadhibiti kwa kufanya yanayoyahitajika; kama kujifunza maana yake, na akayafanyia kazi, ataingia Peponi.

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) aliwaeleza maswahaba zake baadhi ya sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, miongoni mwa sifa hizo ni kutolala usingizi, na kwamba usingizi ni jambo lisilofaa kwa Mola Mtukufu, kwa sababu usingizi ni sifa ya upungufu, na Mwenyezi Mungu ametakasika na sifa yoyote ya upungufu. Anayakubali matendo mema na kuyanyanyua kwake na kuyakataa maovu na kuwarejeshea, na Malaika hupandisha kwake matendo ya usiku kabla ya kuanza kuandika matendo ya mchana, na hupandisha kwake matendo ya mchana kabla ya kuanza kuandika matendo ya usiku. Na kwamba pazia lake limetokana na Nuru - au Moto - ikiwa pazia hilo lingeondolewa, basi nuru hiyo tukufu itachoma viumbe vyote.

Mtume Rehma na Amani zimshukie alitaja asili ya kuumbwa kwa baadhi ya viumbe, hivyo akasema kwamba Malaika wameumbwa kutokana na Nuru, na Majini wameumbwa kwa moto, na kwamba Adam, amani iwe juu yake, ameumbwa kutokana na Udongo, kwa namna ambayo Mwenyezi Mungu ameeleza kwa kina ndani ya Qur'an.

Mama wa Waumini Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, anaeleza kuhusu mwanzo wa kuteremshwa wahyi kwa Mtume Rehma na Amani zimshukie, kwamba zilianza njozi za ukweli zilizokuwa zikitokea baada ya kuota. Kisha Jibril, amani iwe juu yake, akamteremkia Mtume (Rehma na Amani zimfikie) akiwa katika pango la Hira, alipokuwa akimuabudu Mwenyezi Mungu ndani yake. Na kuteremsha wahyi kwake. Maneno aliyoambiwa na Bi Khadija Mwenyezi Mungu amuwiye Radhi yalimtuliza na kumliwaza, halikadhalika aliyoambiwa na Waraqah bin Naufal

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) aliwaeleza maswahaba zake baadhi ya sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, miongoni mwa sifa hizo ni kutolala usingizi, na kwamba usingizi ni jambo lisilofaa kwa Mola Mtukufu, kwa sababu usingizi ni sifa ya upungufu, na Mwenyezi Mungu ametakasika na sifa yoyote ya upungufu. Anayakubali matendo mema na kuyanyanyua kwake na kuyakataa maovu na kuwarejeshea, na Malaika hupandisha kwake matendo ya usiku kabla ya kuanza kuandika matendo ya mchana, na hupandisha kwake matendo ya mchana kabla ya kuanza kuandika matendo ya usiku. Na kwamba pazia lake limetokana na Nuru - au Moto - ikiwa pazia hilo lingeondolewa, basi nuru hiyo tukufu itachoma viumbe vyote.

Ni Abuu Al-Abbasi, Abdallah Ibn Abbasi Ibn Abdul Al-Muttalib, Al-Qurashiy, Al-Hashimiy, Al-Madaniy, alizaliwa kwenye shi’bi ya banii hashim kabla ya kuhama Mtume (s.a.w) kwenda madina kwa miaka mitatu, nayeye (r.a) ndio wino (yaani mwanazuoni mkubwa)  wa ummat Muhammad(s.a.w) na mkalimani wa qur’ani, na mtoto wa ammiyake Mtume (s.a.w), na alikuwa akiitwa bahari kwa wingi wa elimu aliyokuwa nayo, hakika Mtume alimwombea dua kwa kusema: “ Ewe Mwenyezi Mungu mpe ufahamu katika dini ” () na yeye ni katika maswahaba waliopokea hadithi kwa wingi sana, aliingia katika uislamu akiwa mdogo, na aliishi na Mtume (s.a.w), baada ya kuufungua mji wa makkat, na alipokea hadithi kwake, na yalikufa macho yake mwishoni mwa umri wake, alikufa katika mji wa twaif mwaka (68h)[1] referencesRejea tafsiri yake katika: “Maarifaat al-Sahaba” cha Abu Naim (3/1699), “Kunasibiana katika Kuwajua Maswahaba” cha Ibn Abd al-Barr (3/933), “Asad al-Ghaba” cha Ibn al- Atheer (3/291).

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amekataza baadhi ya watu kukanusha hojja na dalili ya Sunnah kwa madai kuwa yaliyomo ndani ya Qur’an yanatosha. Sunnah ni wahyi kama Qur-aan.

Mtume (rehme na Amani zimfikie) anaapa kwamba hakuna yeyote atakayeishi katika zama zake au baada yake, akawa amesikia habari za ulinganizi wake kisha akaacha kumuamini. hakika mafikio yake yatakuwa ni motoni, hata kama ni Myahudi au Mnaswara (Mkristo).

Swahaba mmoja alimuuliza Mtume (Rehma na Amani zimshukie) kuhusu lini kitasimama Kiyama, Mtume (Rehma na Amani zimshukie) akamuuliza kwanza yale ambayo ni muhimu zaidi kuliko kujua wakati wake nayo ni maandalizi yake. mtu yule akasema kuwa hakutayarisha matendo mengi, isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mtume (Rehma na Amani zimshukie) akamwambia kwamba hii ni sababu ya kuingia Peponi, na kuwa karibu nae huko, ikiwa atakuwa na nia thabiti katika mapenzi yao.

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amekataza umma wake kuwatukana maswahaba zake. Kwani wao - kwa ukubwa wa walichoupa Uislamu – ni watu wenye malipo makubwa.

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anafahamisha kuwa watu bora zaidi ni maswahaba wake wanaoishi zama zake, kisha wanaowafuata na wafuasi wao baada yao. Kisha Mtume, amani iwe juu yake, akaeleza kuhusu upotovu wa wale walio baada ya karne hizo bora, na akataja kwamba wanadharau ushahidi, wanasaliti amana, na hawatimizi yale wanayojiwajibishia, na watakua na athari ya kupenda dunia na starehe yake.