Mtume Rehma na Amani zimshukie anaeleza kuwa mwanadamu anawajibika kujibu mambo manne; Kuhusu umri wake, elimu, pesa na mwili wake, ni lazima ajitayarishe kwa maswali hayo, na kutumia vitu hivyo kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kumpendeza.
Mtume Rehma na Amani zimshukie anafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amebainisha yale yanayoruhusiwa na yaliyoharamishwa kwa watu, lakini baadhi ya mambo yanaweza kuwatia shaka watu wengi bila ya kujua. Atakayejiepusha na mambo haya ataihifadhi dini yake, na mwenye kutumbukia katika hayo basi ataingia kwenye haramu.Kisha akamwambia Mtume Rehma na Amani zimshukie kwamba uzuri wa mwili na uharibifu wake unategemea moyo
Katika Hadith kuna amri ya kujiepusha na dunia, na mtu kuwa ndani yake ni kama mgeni anayechukua tu kutoka humo kile kinacho mtosha katika safari zake. Ibn Umar, Mungu amuwiye radhi, alikuwa akiwausia watu wa namna hii, na kwamba mtu asirefushe matumaini yake katika dunia hii na kudanganywa nayo, na angependekeza mtu afanye kazi katika wakati wa afya yake kabla ya ugonjwa, na katika maisha yake kabla ya kifo.
Anawaita watu na kuwavuta Mtume (s.a.w) katika jambo la kutafuta elimu ya kisheria na kupata ufahamu katika dini ya Mwenyezi Mungu, basi akataja kuwa Mwenyezi Mungu anapoitaka kheri kwa mja wake humfundisha dini na kumpa ufahamu ndani yake, kisha akataja Mtume wa Mwenyazi Mungu rehma na amani ziwe juu yake, ya kwamba hakika yeye anagawa aliyopewa na Mwenyezi Mungu kulingana na vile anavyotaka Mwenyezi Mungu, ili tu ummati wake wasije kumpandisha na kumpa thamani ya juu zaidi ya anavyostahiki, kisha akaubashiria ummati wake kuwa hii dini itaendelea kuwepo kwa muda wote ambao utaendelea kuwepo usiku na mchana.
Mwenyezi Mungu Mtukufu huifanya njia ya Pepo kuwa nyepesi kwa wale wanaotafuta elimu, na Malaika wa mbinguni wanamkirimu na kumtukuza, na waliomo mbinguni, ardhini na baharini wanamuombea msamaha. Wao ni kama mwezi na wengine ni kama nyota, na wao ni warithi wa Mitume waliochukua kutoka kwao urithi mkubwa zaidi, ambao ni ujuzi wao.
Amefananisha Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake hali za watu katika kupokea mwongozo ambao ameuteremsha Mwenyezi Mungu (s.w) juu ya Mtume wake Muhammad (s.a.w). Katika watu yupo miongoni mwao aliouhifadhi na kuuheshimu, na akafahamu yaliyomo katika mwongozo huo, na akaufanyia kazi, basi akainufaisha nafsi yake na akawa sababu ya kumnufaisha mwengine. Na katika watu kuna mtu anahifadhi elimu kwa ajili ya mtu mwingine zaidi kuliko ufahamu wake mwenyewe, na katika watu kuna watu wameipuuza elimu, wakawa hawakunufaika wenyewe wala hawakuwanufaisha wengine wasiokua wao.
Mtume rehma na Amani zimshukie anauhimiza umma wake kuwasilisha Sunnah zake, na anawaruhusu kuwaambia watu habari za Wana wa Israili, na anakataza kumsingizia uwongo, Mtume Amani iwe juu yake. Atakayemsingizia uwongo kwa makusudi, basi Moto ndio utakaompata.
Anahimiza Mtume muhammad (s.a.w) juu ya kuhifadhi hadithi na kuwafikishia watu, na anamwombea dua ya kheri mtu atakaefanya hivyo, kwa hakika ummati muhammad (s.a.w) unahitajia maarifa na utambuzi wa sheria za Mwenyezi Mungu aliye takasika na kutukuka na, na huwenda ambaye amesikia maneno ya Mtume muhammad (s.a.w) akawa hakuyafahamu vizuri kisha anamfikishia mtu ambaye atayafahamu maneno ya Mtume s(s.a.w) na akajua makusudio yake naye kuwafundisha watu wengine.
Yanajulisha maneno ya Mtume (s.a.w) juu ya kwamba hakimu (kiongozi)- na anaingia ndani yake kiongozi mtoa hukumu, mufti wa kutoa fat’waa na wengineo, wanalipwa juu ya kutoa muda na jitihada katika kuifikia haki, basi akiipata haki analipwa kwa kuipata vilevile kwa kujitahidi, anakua anamalipo mara mbili, na kama hakuipata haki baada ya kujitahidi basi anapata malipo ya kujitahidi tu.
Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, aliwahutubia maswahaba zake khutba ya kuvutia, kisha akawausia kumcha Mwenyezi Mungu, kuwatii wazazi, kushikamana na Sunnah, na kutahadhari na uzushi.
Mtume (s.aw) amesema kuwa kanuni katika kuzingatia na kukubalika matendo ni nia, ambayo hutofautisha kati ya mazoea na ibada, na hupambanua kati ya matendo mema na maovu. Na watu wawili wanaweza kufanya kitendo cha halali au cha kisheria na yakatofautiana makusudio yao, mmoja anaweza kuwa amekusudia kumtii Allah na akalipwa kwa ajili yake, na mwingine hakukusudia chochote na akawa hakulipwa. Yeyote anayehama kutoka nchi yake kwenda nchi nyengine kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya kufuata Sunnah za Mtume wake, (s.aw) basi atalipwa, na mwenye kuhama kwa ajili ya kitu kisichokuwa hicho, hatapata Zaidi ya alichokusudia.
Kumkumbuka Mwenyezi Mungu huzipa uzima mioyo na roho. Mwenye kumkumbuka Mwenyezi Mungu yu hai na mwenye furaha moyoni, na nyumba ambayo Mwenyezi Mungu anatajwa ndani yake ni yenye furaha na malaika wanaifahamu. Nyumba na mioyo isiyo mkumbuka mola mlezi ni wafu walioachwa, hawana kheri.
Mtu mmoja alikuja kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam akimlalamikia kuwa uislamu umekuwa na sharia nyingi na ibada za kupita kiasi, na kumtaka amuelekeze kwenye jambo kubwa ataloshikamana nalo na aongeze malipo yake, Basi Mtume amani iwe juu yake, akamuongoza kwenye kumtaja Mwenyezi Mungu.
Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anauongoza Ummah wake kwenye kanuni ya kuomba msamaha ambayo inahakikisha kwamba kama atayasema hayo kisha akafa, ataingia peponi.
Amesema Mtume Rehma na amani ziwe juu yake kuwa watu bora zaidi ni wale wanaojifunza Qur’an kwa kuhifadhi, kusoma, kuitafsir na mambo mengine, kisha kuwafundisha watu.
Hadithi inaonyesha kuwa kuitikia wito wa Mtume Rehema na Amani zimshukie ni wajibu hata kama anayeitwa yuko katika swala, na akaeleza Mtume kuwa Al-Fatihah ni surah kubwa kabisa katika Qur’an.
Hadith inaashiria kwamba Ayat al-Kursi ni aya kubwa na tukufu zaidi katika Qur’ani.
Mtume (rehema na amani ziwe juu yake) amesema kuwa Sura “Sema: Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja” ni sawa na theluthi moja ya Qur’an, kwa sababu ya kile kikichomo ndani yake katika maneno ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu.
Ameeleza Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) kwamba Surat Al Falaq na Surat Al Nnaasi hakuna chochote mfano wake, iwe kwenye vitabu vya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambavyo ameviteremsha kwa Manabii wake, au katika yale watu wanayoyapupia kijikingia.
Umaru alikutana na mmoja wa viongozi wake aliowapa majukumu ya utawala katika mji wa makkah mji ambao ulikuwa wa watu wenye heshima zao, alivyokutana nae nje ya mji wa makkah kiongozi huyo akamueleza Umaru kwamba majukumu yake amemuachia mtu ambae si katika watu watukufu na waheshimiwa katika mji huo, Umaru aliposikia hivyo akamkalipia katika jambo hilo, kwa kuogopea asije kusababisha madhara kwa raia, baada ya kufahamishwa kuwa kijana Yule ni katika vijana waliohifadhi qur`ani , nafsi yake ikaridhika na kutulia, na kumshukuru aliefanya hivyo, na zaidi ya hapo akampa ushahidi wa maneno ya Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) kwamba hiki kitabu huwa kinawapa heshima watu na kuwadhalilisha wengine.