عن زيدِ بنِ ثابتٍ، قال: سمعتُ رسولَ الله ﷺ يقول: «نضَّر اللهُ امرأً سَمِعَ منَّا حديثًا، فحفِظَه حتى يُبلِّغَه؛ فرُبَّ حاملِ فِقهٍ إلى مَن هو أفقهُ منه،ورُبَّ حاملِ فِقهٍ ليس بفقيهٍ».
عن زيدِ بنِ ثابتٍ، قال: سمعتُ رسولَ الله ﷺ يقول: «نضَّر اللهُ امرأً سَمِعَ منَّا حديثًا، فحفِظَه حتى يُبلِّغَه؛ فرُبَّ حاملِ فِقهٍ إلى مَن هو أفقهُ منه،ورُبَّ حاملِ فِقهٍ ليس بفقيهٍ».
Kutoka kwa Zaid ibn Thabit radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani ziwe juu yake akisema:
1. Mwenyezi Mungu amnawirishe mtu yeyote atakaesikia maneno kutoka kwetu, na akayahifadhi kwa ajili ya kuwafikishia watu wengine;
2. Basi huwenda msikilizaji (aliehifadhi vizuri) akawa sio mjuzi zaidi lakini kwa kuhifadhi kwake akawafikishia wengine ambao ni wajuzi zaidi katika kutohoa hukumu za kisheria kuliko yeye.
. Na huwenda msikilizaji akawa sio msomi zaidi
Anahimiza Mtume muhammad (s.a.w) juu ya kuhifadhi hadithi na kuwafikishia watu, na anamwombea dua ya kheri mtu atakaefanya hivyo, kwa hakika ummati muhammad (s.a.w) unahitajia maarifa na utambuzi wa sheria za Mwenyezi Mungu aliye takasika na kutukuka na, na huwenda ambaye amesikia maneno ya Mtume muhammad (s.a.w) akawa hakuyafahamu vizuri kisha anamfikishia mtu ambaye atayafahamu maneno ya Mtume s(s.a.w) na akajua makusudio yake naye kuwafundisha watu wengine.