Mtume Rehma na Amani zimshukie ameeleza swali la Malaika wawili waliomo kaburini; Mja ataulizwa kuhusu Mtume wake, kama alikuwa ni Muumini, ataonyeshwa makazi yake peponi na kaburi lake litakuwa pana zaidi, na akiwa kafiri ataonyeshwa makazi yake Motoni, na atateswa kaburini mwake mpaka kusimama qiyama
Mtume Rehma na Amani zimshukie anaeleza kuhusu baadhi ya dalili ndogo za Kiyama, nazo ni: Kuchukuliwa elimu, na kuongezeka matetemeko ya ardhi, kukaribiana kwa wakati, kuongezeka kwa mitihani na fitina, idadi kubwa ya mauaji. na kuongezeka pesa na kuzitumia kiholela.
Mtume Rehma na Amani zimshukie ametaja baadhi ya alama za Kiyama zitakazokuja kwa ghafla, na Mtume Rehma na Amani zimshukie anawaamrisha watu wake kuharakisha kutenda matendo ya kheri kabla ya kuonekana dalili hizo.
Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, anaeleza kuhusu baadhi ya sifa za Mpinga Kristo, majaribu makubwa zaidi duniani, na hakuna nabii asiyewaonya watu wake juu ya majaribu yake. Ana jicho moja, lililoandikwa kati ya macho yake ni "kafiri", ambalo kila Muislamu atalisoma.
Mtume (rehma na amani ziwe juu yake)ametaja kuwa moja ya dalili kuu za Kiyama ni kuchomoza jua kutoka magharibi, na likidhihiri kutoka Magharibi basi mlango wa toba hufungwa, na haikubaliwi toba ya mtu baada ya kutokea hali hiyo.
Ametaja Mtume Rehema na Amani zimshukie kuwa Siku ya Kiyama mwanaadamu atasimama kwa ajili ya hisabu mbele ya Mola wake Mlezi, Mola wake Mlezi atazungumza naye bila ya mfasiri wala mpatanishi, wakati huo mtu hatapata faida yeyote zaidi ya matendo yake.
Mtume Rehma na Amani ziwe juu yake anaeleza kuwa joto la moto wa Jahannam ni kubwa mara sabini kuliko joto la moto wa dunia hii.
Mola wetu mlezi, Mwenye utukufu, anafahamisha kwamba amewaandalia waja wake wema aina mbalimbali za neema ambazo hakuna kiumbe aliyewahi kuziona wala kuzisikia, na hakuna akili inayoweza kufikiria au kupita moyoni.
Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) ameeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomaliza kuumba, aliandika katika Ubao uliohifadhiwa katika Arshi Yake kuwa: Rehema yangu imeishinda hasira yangu.
Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) ametaja katika hadithi hii baadhi ya hatua za ukuwaji wa kijusi katika tumbo la mama, kupuliziwa roho na kuandikiwa mambo yake yote. Kisha akabainisha kwamba kinacho zingatiwa katika matendo yake ni mwisho, mwenye kuhitimisha uhai wake kwa matendo ya watu wa Peponi, basi atakuwa miongoni mwao, na mwenye kuhitimisha uhai wake kwa matendo ya watu wa Motoni, basi atakuwa miongoni mwao.
Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anamnasihi Mtoto wa ami yake Abdullah bin Abbaas kwa usia ulio kusanya tauhiid ya uluuhiyyah (kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu mmoja tu) kwamba asiombwe yeyote katika maombi ila yeye pekee, na wala asitake msaada kwa yeyote ila yeye pekee. Anauandaa moyo wake kwa kumwambia kwamba mambo yote yako katika mipango ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa hakika hayupo yeyote anaye weza kumnufaisha au kumdhuru ila kwa jambo ambalo amelipanga.
Mwenye nguvu katika Imani yake na kufanya kheri ni mbora kuliko dhaifu. Pupia mambo yenye kukunufaisha, na umuombe Mwenyezi Mungu msaada. Usichoke wala kudhoofika, ukiwafikishwa katika kheri, ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa tofauti na hivyo, usiseme (lau) kwa kutamani lililo kupita lirudi, bali sema: “Nipango ni ya Mwenyezi Mungu, anafanya atakalo”
Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anasahihisha itikadi ya Umma wake kwa sabubu ya yaliyo kuwa yamewaathiri kabla hawajawa waislam. Akasema kwamba, maradhi kama maradhi hayaambukizi, bali hilo linatokea kwa kutaka Mwenyezi Mungu Mtukufu. na akazuia kuitakidi mikosi kwa sababu ya muda au sehemu au watu fulani, na akasema kwamba inapendeza mtu kuwa na zana nzuri kwa kusema maneno mazuri.
Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) ana amrisha maswahaba zake watizame walio chini yao kineema na mambo ya kiDunia, walio mafakiri na madhaifu zaidi yao, na wala wasitizame alio wafadhilisha kwa riziki, afya na neema za kiDunia, kufanya hivyo ni bora na inapelekea kutodharau neema za Mwenyezi Mungu.
Mtume (Rehma na Amani zimshukie) ameeleza kuwa Mwenyezi Mungu kuna mambo ambayo ameyaficha na hakuna yeyote anayeyajua, na ni funguo za ghaibu, yaani: ni mambo yatakayotokea siku za usoni, yatakayotokea matumboni kutokana na watoto wachanga au kuharibika kwa mimba na kadhalika, na kujua lini itakuja mvua, wakati na mahali pa kufa kwa kila nafsi, na tarehe ya kiyama.
Mtume (Rehma na Amani zimshukie) amefahamisha kwamba mwenye kwenda kwa kuhani au mwongo na mfano wa hayo, kwa mtu anayedai kuwa anajua ghaibu na kadhalika, na akaamini anayodai; Basi atakuwa amekufuru, na hilo linaweza kumtoa katika Uislamu au kumsogeza karibu na hilo.
Ubora wa mtu sio uzuri wa umbo na kiwiliwili, bali lililo muhimu kwa mtu ni hali inayopatikana moyoni mwake katika imani au ukafiri.
Ameelezea Mtume Muhammad (s.a.w) kunako sifa tatu akizipata mwana Adamu katika nafsi yake hakika atakua ameonja ladha ya imani nazo ni: Awe Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake ndio wanapendeza kwake kuliko kila kitu, na apende kwa ajili ya Mwenyezi Mungu sio kwa ajili ya cheo au maslahi fulani, na iwe kitu anacho kichukia zaidi ni kurudi kwenye ukafiri, kama anavyo chukia kuingia motoni, hivyohivyo ndio auchukie ukafiri na kila kinacho pelekea ukafiri.
Mtume (Rehma na Amani zimshukie) anafahamisha kuwa umma wake utaiga mataifa yaliyopita ya Mayahudi na Wakristo katika uzushi katika dini na kufanya madhambi kwa kuiga kabisa na kuridhia upofu.
Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anawaelekeza maswahaba wajitahidi kutenda mema kabla fitina ambayo inampoteza mtu na kushusha Imani haijaenea. Ndani ya muda mfupi mtu anakuwa kafiri na Imani ilikuwa imekita katika moyo wake