Ibada katika wakati wa majaribu ina malipo makubwa, sawa na malipo ya wale wanaohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Kila jambo la Muislamu ni kheri kwake, akisamehewa anashukuru, basi atalipwa kheri yake, na akipatwa na hata mwiba katika kidole chake, Mungu humfutia dhambi kwa hilo.
Kila mwanadamu anafanya madhambi na uasi, kwa hivyo hakuna asiyefanya makosa baada ya Mitume. Bali mbora wa watu ni yule anaye anzisha toba baada ya kukosea.
Ni lazima mtu arudishe mali za dhulma kwa wanaostahiki, na awaombe msamaha waliowadhulumu, kabla ya kuadhibiwa kwa matendo mema na mabaya.
Amr, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, aliogopa kwamba ataadhibiwa kwa yale aliyoyafanya kabla ya kusilimu kwake, hivyo alitaka kuweka masharti kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amsamehe kwa hilo kabla hajasilimu.
Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam aliulizwa kuhusu hatima ya matendo mema kabla ya Uislamu, na akaeleza kuwa mja akiingia katika Uislamu atalipwa kwa mema aliyoyafanya kabla ya kusilimu.
Mtume (Rehema Na Amani Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) ametaja huruma za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambazo zimevizunguka viumbe vyake vyote, kuwa aliteremsha kwenye ardhi sehemu moja katika sehemu mia moja, ambayo kwayo watu wanahurumiana na kupendana, na kwa huruma hiyo wanyama pori huishi pamoja.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anawahimiza waja wake watubu, na Yeye, Mola aliye tukuka, Anasamehe dhambi zote, hata zikiwa kubwa kiasi gani.