Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anatahadharisha kuhusu riya na kufanya ibada bila Ikhlaas, anaeleza kwamba hatima ya riya ni Mwenyezi Mungu kutomkubalia mja ibada, na wala hatamlipa siku ya kiyama, kwasababu amefanya ushirikina.

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anataja sifa nne miongoni mwa sifa za wanafiki ambazo haifai kwa mwislam kusifika nazo. Atakae sifika nazo zote, atakuwa ni mnafiki kabisa, na atakae sifika na moja wapo atakuwa amesifika na sifa ya kinafiki, nazo ni; hiyana, uongo, usaliti, na kuvuka mipaka katika ugimvi.

Mtume rehma na Amani zimshukie anafahamisha kuwa kufuata ni sharti la kukubaliwa ibada, basi mwenye kuzua kitu katika dini ya Mwenyezi Mungu, kitakataliwa na kurudishwa kwa mwenye nacho, na wala hatalipwa, bali ni mwenye dhambi na mzushi.

Mtume Rehma na Amani zimshukie anabainisha kuwa Dini ya Uislamu ni rahisi kuichukua, kwa sababu ya wepesi wa hukumu zake na urahisi wa gharama zake, na kwamba mwenye kuifanya dini kuwa gumu, mtu huyo anataka dini hiyo imshinde kuiingia, na atakuwa hana uwezo na atakatiliwa mbali, hivyo Muislamu anatakiwa kuwa na bidii na na kuwa nayo karibu. Na alitubashiria mtume kwa malipo makubwa kwa kuifuata dini hiyo. Kisha akaeleza kuhusu nyakati bora za ibada na unyenyekevu, ambazo ni mwanzo wa mchana na mwisho wake na mwisho wa usiku.

Bedui mmoja alimuuliza Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), kuhusu Uislamu, alimwambia kuhusu nguzo zake zinazojulikana sana, atakayezitekeleza ipasavyo, bila ya kuongeza wala kupunguza, basi atafaulu na kuingia Peponi. 

Bedui mmoja alimuuliza Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), kuhusu Uislamu, alimwambia kuhusu nguzo zake zinazojulikana sana, atakayezitekeleza ipasavyo, bila ya kuongeza wala kupunguza, basi atafaulu na kuingia Peponi. 

Mtu mmoja alimuuliza Mtume (Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake) kuhusu kupata udhu kwa maji ya bahari, akamwambia kuwa maji hayo ni masafi, na kwamba mizoga yake inajuzu kuliwa.

Uthman, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alitawadha kama alivyofanya Mtume rehma na amani ziwe juu yake, kisha akawaambia kuwa Mtume rehma na Amani zimshukie amesema: Mwenye kutawadha kama hivi, na kuswali rakaa mbili kwa ikhlasi na kunyenyekea ndani yake, atasamehewa madhambi yake, na swala yake na kutembea kwake kwenda msikitini kutahesabiwa kuwa ni swala za sunnah.

Ammar bin Yasir, Mwenyezi Mungu amuwie radhi yeye na wazazi wake, alipatwa na janaba katika baadhi ya safari zake na hakuweza kupata maji, hivyo akajizungusha kwenye udongo mpaka ili aweze kuswali. Aliporejea kwa Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akamueleza Mtume akambainishia asili ya tayammam, na kwamba ni pigo moja katika udongo ambalo anapangusa nalo mikono na uso.

Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) anatufahamisha kuwa swala ni kitenganishi baina ya Uislamu na ukafiri, hivyo mwenye kuacha swala amekufuru.

aliingia mtu msikitini akaswali kisha akaja kwa Mtume Rehema na Amani zimshukie akamsalimia, Mtume Rehema na Amani zimshukie akamuitikia, kisha akamuamrisha arudie swala, basi yule mtu akafanya kisha akarudi, na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akamuamrisha kurudia, akafanya hivyo mara tatu, yule mtu akamwambia kuwa hana namna nyingine ya kusali zaidi ya hiyo, Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akamfundisha kuswali.

Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, anasimulia kuwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema kuwa mwenye kuswali swala ambayo hakusoma al-Fatiha, ina upungufu, upungufu unaoathiri usahihi wake. Akaulizwa Abu hurayra kuhusu kuisoma alfatiha nyuma ya imamu katika swala ya jamaa: akasema isomwe kwa utukufu wa hadithi ya Mtume kutoka kwa Mola wake kwamba ameigawa alfatiha baina yake na mja wake.

Mtume rehema na amani zimshukie alitoa khutba juu ya mimbari, akionya juu ya kupuuza Swalah ya Ijumaa, kwa mwenye kuiacha, Mwenyezi Mungu atapiga muhuri moyo wake na kumpoteza na kuwa miongoni mwa walioghafilika.

Zamani watu wa Madiynah walikuwa wakisherehekea siku mbili za zama za kabla ya Uislamu, Mtume Rehma na Amani ziwe juu yake alipohamia kwao na kuona sherehe zao, akawauliza kuhusu hilo, wakamwambia. kwa hivyo akawakataza kusherehekea, na akawaambia kwamba Mwenyezi Mungu amewafidia siku hizo mbili kwa iliyo bora zaidi. Eid al-Fitr na Eid al-Adh-haa.

Mtume Rehma na Amani zimshukie anafahamisha kuwa swala ya jamaa ni bora kuliko swala ya mtu peke yake kwa daraja ishirini na saba.

Mtume Rehma na Amani ziwe juu yake anaeleza kuwa sehemu anayoipenda zaidi Mwenyezi Mungu Mtukufu ni misikiti; Ndipo mahali pa kumtaja na kumuabudu, na sehemu anazozichukia zaidi ni masoko. Ambapo vimejaa viapo vya uwongo, na ulaghai, dhuluma na udanganyifu.

Mtume Rehma na Amani ziwe juu yake anafahamisha mambo yanayodhihirisha imani ya mja ambayo ni tawhidi, kutoa zaka kwa uhuru na raha, kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na kuchagua zaka katika mali yake, ili asitoe zaka katika wanyama wagonjwa, wazee, au wenye kasoro

Mtume amani iwe juu yake anatuambia kuwa Mwenyezi Mungu ni mwema na hakubali chochote isipokuwa kizuri, na ndio maana akawaamrisha watu wote kula katika vitu vizuri, na akasema kwamba kula katika haramu ni moja ya vikwazo vinavyozuia dua kujibiwa.

Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema kuwa Zakaatul-Fitri hutolewa kutoka kwa kila Mwislamu, mwanamume au mwanamke, huru au mtumwa, mdogo au mkubwa, kwa kila mtu pishi ya chakula, na hutolewa kabla ya kusali sala ya Iddi

Mtume Rehma Na Amani Zimshukie anaeleza baadhi ya fadhila za funga, ikiwa ni pamoja na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amemhifadhia ujira yeye mwenyewe bila ya yeyote kujua malipo yake, na kwamba funga inamzuia asiingie katika uasi na madhambi, na kwamba harufu ya kinywa cha mfungaji inapendeza kwa Mwenyezi Mungu, hata kama watu wanaichukia, na kwamba mfungaji atafurahi Siku ya Kiyama atapoona malipo ya funga yake, kama anavyofurahi duniani kwa Mwenyezi Mungu kumwafikisha kufunga.