عن حُمْرَانَ، مَوْلَى عُثْمَانَ، أَنَّ عُثْمَانَ بْنَ عَفَّانَ رضي الله عنه دَعَا بِوَضُوءٍ فَتَوَضَّأ،َ فَغَسَلَ كَفَّيْهِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ مَضْمَضَ وَاسْتَنْثَرَ، ثُمَّ غَسَلَ وَجْهَهُ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ غَسَلَ يَدَهُ الْيُمْنَى إِلَى الْمِرْفَقِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ غَسَلَ يَدَهُ الْيُسْرَى مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ مَسَحَ رَأْسَهُ، ثُمَّ غَسَلَ رِجْلَهُ الْيُمْنَى إِلَى الْكَعْبَيْنِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ غَسَلَ الْيُسْرَى مِثْلَ ذَلِكَ،ثُمَّ قَالَ: رَأَيْتُ رَسُولَ اللهِ ﷺ تَوَضَّأَ نَحْوَ وُضُوئِي هَذَا،ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «مَنْ تَوَضَّأَ نَحْوَ وُضُوئِي هَذَا، ثُمَّ قَامَ فَرَكَعَ رَكْعَتَيْنِ لَا يُحَدِّثُ فِيهِمَا نَفْسَهُ، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ»، وزاد مسلم في رواية: «وَكَانَتْ صَلاَتُهُ وَمَشْيُهُ إِلَى الْمَسْجِدِ نَافِلَةً»

Kutoka kwa Humran, mawlaa wa Uthman,

1- Amesimlia kwamba Othman bin Affan, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, aliomba maji ya kutawadha, na akatawadha, akaosha vitanga vyake viwili vya mikono mara tatu, kisha akaweka maji mdomoni mwake na kupandisha maji katika pua yake, kisha akaosha uso wake mara tatu, Kisha akaosha mkono wake wa kulia hadi kwenye kiwiko mara tatu, kisha akaosha mkono wake wa kushoto vivyo hivyo, kisha akapangusa kichwa chake, Kisha akaosha mguu wake wa kulia hadi vifundoni mara tatu, kisha akauosha wa kushoto vivyo hivyo.
2- Kisha akasema: Nilimuona Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anatawadha kama mimi.
3- Kisha akasema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Mwenye kutawadha kama udhuu wangu huu, kisha akasimama na kusali rakaa mbili ambazo haongei nafsini mwake, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”
4- Na Muslim akaongeza katika riwaya: “Na itakuwa swala yake na kutembea kwake kuelekea msikitini ni ibada”  .

Muhtasari wa Maana

Uthman, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alitawadha kama alivyofanya Mtume rehma na amani ziwe juu yake, kisha akawaambia kuwa Mtume rehma na Amani zimshukie amesema: Mwenye kutawadha kama hivi, na kuswali rakaa mbili kwa ikhlasi na kunyenyekea ndani yake, atasamehewa madhambi yake, na swala yake na kutembea kwake kwenda msikitini kutahesabiwa kuwa ni swala za sunnah.

Miradi ya Hadithi