عَنْ عَامِرِ بْنِ وَاثِلَةَ، أَنَّ نَافِعَ بْنَ عَبْدِ الْحَارِثِ، لَقِيَ عُمَرَ[ رضي الله عنه ] بِعُسْفَانَ، وَكَانَ عُمَرُ يَسْتَعْمِلُهُ عَلَى مَكَّةَ، فَقَالَ: مَنِ اسْتَعْمَلْتَ عَلَى أَهْلِ الْوَادِي؟ فَقَالَ: ابْنَ أَبْزَى، فقال: وَمَنِ ابْنُ أَبْزَى؟ فقال: مَوْلًى مِنْ مَوَالِينَا. قَالَ: فَاسْتَخْلَفْتَ عَلَيْهِمْ مَوْلًى؟ قَالَ: إِنَّهُ قَارِئٌ لِكِتَابِ اللهِ عزَّ وجلَّ، وَإِنَّهُ عَالِمٌ بِالْفَرَائِضِ، قَالَ عُمَرُ: أَمَا إِنَّ نَبِيَّكُمْ ﷺ قَدْ قَالَ: «إِنَّ اللهَ يَرْفَعُ بِهَذَا الْكِتَابِ أَقْوَامًا، وَيَضَعُ بِهِ آخَرِينَ»

kutoka kwa A`amir bin Waathilah amesimulia kuwa:

1- Naafi`I bin Abdil Warith akikutana na Umar (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) katika sehemu inaitwa U`sfaana, na Umaru alikuwa amemfanya kuwa kiongozi katika mji wa makah, Umaru akamuuliza: ni nani umemuacha katika nafasi yako ya uongozi katika watu wa hilo bonde? 2- Akasema: (nimemuacha) kijana wa Abzaah, Umar akasema: ni nani huyo kijana wa Abzaah? Akasema: ni mjakazi katika wajakazi wetu, 3- Umaru akasema: unawaachia kiongozi mjakazi? 4- Akasema: Hakika yeye ni msomaji mzuri wa kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni msomi wa elimu ya mirath. 5- Umaru akasema: kweli hakika Nabii wenu (rehma na amani ziwe juu yake) alisema: hakika Mwenyezi Mungu hunyanyua kwa hiki kitabu watu, na kwa kitabu hiki huwashusha wengine.

Muhtasari wa Maana

Umaru alikutana na mmoja wa viongozi wake aliowapa majukumu ya utawala  katika  mji wa makkah mji ambao ulikuwa wa watu wenye heshima zao, alivyokutana nae nje ya mji wa makkah kiongozi huyo akamueleza Umaru kwamba majukumu yake amemuachia mtu ambae si katika watu watukufu na waheshimiwa katika mji huo, Umaru aliposikia hivyo akamkalipia katika jambo hilo, kwa kuogopea asije kusababisha madhara kwa raia, baada ya kufahamishwa kuwa kijana Yule ni katika vijana waliohifadhi qur`ani , nafsi yake ikaridhika na kutulia, na kumshukuru aliefanya hivyo, na zaidi ya hapo akampa ushahidi wa maneno ya Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) kwamba hiki kitabu huwa kinawapa heshima watu na kuwadhalilisha wengine.

Miradi ya Hadithi