عَنْ عَامِرِ بْنِ وَاثِلَةَ، أَنَّ نَافِعَ بْنَ عَبْدِ الْحَارِثِ، لَقِيَ عُمَرَ[ رضي الله عنه ] بِعُسْفَانَ، وَكَانَ عُمَرُ يَسْتَعْمِلُهُ عَلَى مَكَّةَ، فَقَالَ: مَنِ اسْتَعْمَلْتَ عَلَى أَهْلِ الْوَادِي؟ فَقَالَ: ابْنَ أَبْزَى، فقال: وَمَنِ ابْنُ أَبْزَى؟ فقال: مَوْلًى مِنْ مَوَالِينَا. قَالَ: فَاسْتَخْلَفْتَ عَلَيْهِمْ مَوْلًى؟ قَالَ: إِنَّهُ قَارِئٌ لِكِتَابِ اللهِ عزَّ وجلَّ، وَإِنَّهُ عَالِمٌ بِالْفَرَائِضِ، قَالَ عُمَرُ: أَمَا إِنَّ نَبِيَّكُمْ ﷺ قَدْ قَالَ: «إِنَّ اللهَ يَرْفَعُ بِهَذَا الْكِتَابِ أَقْوَامًا، وَيَضَعُ بِهِ آخَرِينَ»

kutoka kwa A`amir bin Waathilah amesimulia kuwa:

1- Naafi`I bin Abdil Warith akikutana na Umar (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) katika sehemu inaitwa U`sfaana, na Umaru alikuwa amemfanya kuwa kiongozi katika mji wa makah, Umaru akamuuliza: ni nani umemuacha katika nafasi yako ya uongozi katika watu wa hilo bonde? 2- Akasema: (nimemuacha) kijana wa Abzaah, Umar akasema: ni nani huyo kijana wa Abzaah? Akasema: ni mjakazi katika wajakazi wetu, 3- Umaru akasema: unawaachia kiongozi mjakazi? 4- Akasema: Hakika yeye ni msomaji mzuri wa kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni msomi wa elimu ya mirath. 5- Umaru akasema: kweli hakika Nabii wenu (rehma na amani ziwe juu yake) alisema: hakika Mwenyezi Mungu hunyanyua kwa hiki kitabu watu, na kwa kitabu hiki huwashusha wengine.

UqbaBin A`AmirAlJuhaniy

jina lake ni A`amir bin Wathila bin Abdillah Al Kinaniy, alizaliwa mwaka wa vita ya uhdi, na mtume alifariki yeye akiwa na miaka 8, na alikuwa katika maswahaba walifishwa mwishoni mwa mwaka wa 110 hijiria. Msimulizi wa hadithi: Ni: Abu Hafs, al-Faruq, Umar ibn al-Khattab al-Qurashi al-Adawi Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ni Khalifa wa pili katika makhalifa Waongofu, na ni mmoja kati ya kumi waliotabiriwa kuingia Peponi wakiwa hai, alikuwa balozi wa Quraish kabla ya Uislamu; Ikitokea vita baina yao, Wanamtuma Kutafuta amani na Hukumu, alisilimu mwaka wa sita baada ya Mtume kutumwa, na kusilimu kwake kulikuwa ni Ushindi kwa Uislamu na Waislamu, na alihudhuria Vita vyote pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu amani iwe juu yake, na alishika ukhalifa baada ya kifo cha Abu Bakar Al-Siddiq Mwenyezi Mungu awe radhi naye katika mwaka wa (13 Hijiria). Alikuwa maarufu kwa uadilifu pamoja na ukali na ujasiri katika ukweli, na wakati wa utawala wake nchi nyingi zilikombolewa kama vile Iraq, siria, Misri na nyinginezo. Aliuawa katika mwaka wa (23 AH), na akazikwa katika chumba cha Bi Aisha, Mungu amuwiye radhi, karibu na Mtume Rehma na Amani zimshukie na Abu Bakar as-Siddiq Mwenyezi Mungu awe radhi naye . [1]


Marejeo

1.  Rejea ufafanuzi wake katika: “Ma’rifat al-Sahaba cha Abu Na’im” (1/38), “Asad al-Ghaba cha Ibn al-Atheer” (4/137), “Al-Isbah cha Ibn Hajar” (4/484).

Miradi ya Hadithi