عَنْ عَامِرِ بْنِ وَاثِلَةَ، أَنَّ نَافِعَ بْنَ عَبْدِ الْحَارِثِ، لَقِيَ عُمَرَ[ رضي الله عنه ] بِعُسْفَانَ، وَكَانَ عُمَرُ يَسْتَعْمِلُهُ عَلَى مَكَّةَ، فَقَالَ: مَنِ اسْتَعْمَلْتَ عَلَى أَهْلِ الْوَادِي؟ فَقَالَ: ابْنَ أَبْزَى، فقال: وَمَنِ ابْنُ أَبْزَى؟ فقال: مَوْلًى مِنْ مَوَالِينَا. قَالَ: فَاسْتَخْلَفْتَ عَلَيْهِمْ مَوْلًى؟ قَالَ: إِنَّهُ قَارِئٌ لِكِتَابِ اللهِ عزَّ وجلَّ، وَإِنَّهُ عَالِمٌ بِالْفَرَائِضِ، قَالَ عُمَرُ: أَمَا إِنَّ نَبِيَّكُمْ ﷺ قَدْ قَالَ: «إِنَّ اللهَ يَرْفَعُ بِهَذَا الْكِتَابِ أَقْوَامًا، وَيَضَعُ بِهِ آخَرِينَ»

kutoka kwa A`amir bin Waathilah amesimulia kuwa:

1- Naafi`I bin Abdil Warith akikutana na Umar (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) katika sehemu inaitwa U`sfaana, na Umaru alikuwa amemfanya kuwa kiongozi katika mji wa makah, Umaru akamuuliza: ni nani umemuacha katika nafasi yako ya uongozi katika watu wa hilo bonde? 2- Akasema: (nimemuacha) kijana wa Abzaah, Umar akasema: ni nani huyo kijana wa Abzaah? Akasema: ni mjakazi katika wajakazi wetu, 3- Umaru akasema: unawaachia kiongozi mjakazi? 4- Akasema: Hakika yeye ni msomaji mzuri wa kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni msomi wa elimu ya mirath. 5- Umaru akasema: kweli hakika Nabii wenu (rehma na amani ziwe juu yake) alisema: hakika Mwenyezi Mungu hunyanyua kwa hiki kitabu watu, na kwa kitabu hiki huwashusha wengine.

1. Anaeleza Swahaba Mtukufu A`amir bin Waathilah (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kwamba Naafi`I bin Abdil Haarith (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) ambae Umaru alimfanya kuwa kiongozi katika mji wa makkah, siku moja alitoka katika mji huo ili kutekeleza maslahi ya raia, akakutana Umaru (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) katika maeneo ya U`sfaana, nao ni mji ulioko magharibi mwa makkah kwa takriban kilometa 80, alivyokutana na Umaru akamuuliza kuhusu aliemuachia majukumu ya uongozi katika mji wa makkah, kwa kuwaongoza mambo yao na kuwaswalisha, na mengineyo. 

2. Naafi`i akamueleza kuwa amemuachia majukumu ya uongozi kijana jina lake ni ibn abzaa [1] , Umaru akawa hakumfahamu, akauliza hali yake, naafi`I akamwambia kwamba kijana huyo au moja ya wazazi wake kuna aliewahi kuwa mjakazi au mtumwa wetu tukamuacha huru. 

3. Umaru akachukia mtumwa kufanywa kuwa kiongozi, hali ya kuwa kuna watu waliohuru na wenye heshima katika maswahaba wa Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) na waliokuja baada yake ambao wanafaa kusimamia jukumu hilo.

 4. Hii haina maana kuwa haifai wajakazi kuongoza, wala kawmba Umaru (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) eti anawadharu wajakazi na watumwa na kuwaona wako chini ya waungwana (yaani watu walio huru), lakini aliuliza hivyo kwa kuchunga maslahi ya watu na kuepuka fitna, kwa sababu uongozi katika malengo yake ni kudhibiti mambo ya watu na kutekeleza maslahi yao, na jambo hilo linahitaji mtu mwenye uelevu na msimamo na mwenye kuogopwa ambae watu hawawezi kumgomea, na hili linahitaji mtu aliehuru na mwenye kuheshimiwa katika nasaba na nafasi yake katika jamii, na kinyume na hapo watu watamdharau na kuacha kumsikiliza na kumtii. [2]

5. Naafi`i akamueleza kuwa sababu ya kumpa majukumu hayo ni kwamba kijana huyo amehifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni msomi wa sheria na hukumu za mirathi, na kwamba mjakazi huyu Mwenyezi Mungu amemnyanyua kwa watu kwa sababu ya jambo hilo, na watu wa mji wa makkah wanajua sifa yake hiyo, na wanamuheshimu na kumtukuza na kutekeleza maamrisho yake, jambo ambalo linapelekea mambo kunyooka, na hali kutulia. 

6. Umaru alipoelezewa sababu ya kufanywa hivyo, aliikubali na kumuunga mkono kwa kumpa hoja na dalili ya usahihi wake, kwamba Mtume ameeleza kuwa hiki kitabu kinawaheshimisha watu na kunyanyua daraja zao duniani na akhera, na kisingelikuwa kitabu hicho wangelidhalilika, kama kinavyowadhalilisha waliokikufuru na wakaacha kufanyia kazi yaliyomo, hata kama walikuwa ni watu waheshimiwa na utukufu. 

1) Ni wajibu kwa kila aliepewa majukumu awe makini katika hayo majukumu, mwenye kufuatilia kila sehemu, kwani umaru alikutana na mfanyakazi wake jambo la kwanza alimuuliza, ni nani umemuachia majukumu yako? Na yukoje? Na kwanini umefanya hivi na kuacha vile?

2) Ni wajibu kwa kila kiongozi atakapomuachia mtu majukumu basi awe na sababu za msingi zilizompelekea amuchie majukumu hayo, hivyo basi atakapotaka baba, au mkuu wa shirika Fulani,au mkadarasi au mfanyakazi, kumuagiza mmoja wa wafanyakazi wake ili kusimamia jukumu Fulani basi inampasa achunguze kwanza uaminifu wake na umahiri wake katika kufanya kazi vizuri, na mfano wa hayo, na kiongozi wa siasa au waziri atakapotaka kuwakilishwa na mfanyakazi wake, hapa ni sharti huyo mfanyakazi wake awe na utaalamu wa uongozi na awe na uwezo wa kuitikia maslahi ya raia. 

3) Hadithi hii inaashiria kwamba mjuzi wa hukumu za kisheria katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na muenendo wa Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake, atatangulizwa katika kuongoza mambo ya waislamu muda ambao atakuwa anafaa kuongoza, hata kama ni masikini kuliko raia wake, muhimu awe anaweza kuchunga maslahi ya waislamu, na kujiepusha na yanayoweza kuchochea na kueneza fitna, kwani Umaru siku moja aliwahi kuwasimamisha uongozi maswahaba wakubwa katika baadhi ya nyadhifa kwa ajili ya kuchunga maslahi ya watu wote, kama alivyofanya kwa Sa`adi Bin Abii Wa`Qqaas, na Khalid Bin Waliid na wengineo. 

4) Kila mtu aiulize nafsi yake: kitabu cha Mwenyezi Mungu unakichukuliaje katika nafsi yako? Je ni kweli umekiamini na kukisadikisha na kudumisha kukisoma hadi Mwenyezi Mungu akakunyanyua kupitia kitabu hicho? Au umekiacha na Mwenyezi Mungu akakudhalilisha? Hapo kuna mambo mawili na si zaidi, amesema Qatadah Mwenyezi Mungu amrehemu, “hakukaa na qur`an mtu yeyote ispokuwa atanyanyuka akiwa na ziada au mapungufu” [3]

5) Mwanadamu huthaminiwa kwa kile alichonacho, hivyo basi ni wajibu kwa kila mwenye kutafuta elimu aelekeze hamu yake katika kutafuta elimu yenye manufaa kwani elimu kwake ina thamani na utukufu dunia na akhera. 

6) Ikiwa qur`ani inamnyanya daraja mwenye kuihifadhi na kuifanyia kazi kwa kumfanya kuwa kuongozi wa watu na imamu wao, basi hakika cheo kikubwa zaida ya hapo ni kunyanyuliwa akhera, Kutoka kwa Abdullah bin Amru (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake): “Ataambiwa mwenye Qur’ani: Soma, na upende daraja, na usome vizuri kama ulivyokuwa ukisoma duniani; kwani hakika sehemu yako iko kwenye aya ya mwisho utakayoisoma.” [4]

7) Amesema mshairi. Hivyo ewe nafsi, kuwa kama nyuki = Usijaribiwe kulala au wala usishawishike Qur’an imekuacha katika bustani yenye kung’aa = Basi chukua upendavyo katika neema zake maua yake yawasilishe katika ulimwengu = na halalisha asali yake yenye kushuhudiwa. usitake mtu mwingine astarehe katika bustani hiyo; = kwani ni Kiasi gani Nimesamehe kila mwenye kuacha dhambi zake Uwongofu uko katika uwongofu wake, na ushindi uko katika njia yake, =na utukufu uko katika kuinuliwa kwake.

Marejeo

1. Yeye ni Abd al-Rahman ibn Abza al-Khuza’i, wakitofautiana katika uswahaba wake, na wanahistoria wengi wanadai kwamba alikuwa ni sahaba ambaye alikutana na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akaswali nyuma yake na akasimulia kutoka kwake. Tazama: “Tahdheeb Al-Kamal” cha Al-Mazi (16/501), “Sir A’alam Al-Nubla” cha Al-Dhahabi (3/201).

2. “Al-Bahr Al-Mohet Al-Thajaj” cha Muhammad bin Ali Al-Ethithi (458/458).

3. " Maadili ya wasomi wa Qur'an" cha Al-Ajri (uk. 73)

4. Abu Daawuud (1464) na al-Tirmidhiy (2914).




Miradi ya Hadithi