18 - KUTUTWA UTUME KWA UJIO KWA NABII MUHAMMAD (S.A.W)

عن أبي هريرة أن رَسُول اللهِ قال: «وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ، لا يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هذِهِ الأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلا نَصْرَانِيٌّ، ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ: إِلَّا كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ» رواه مسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehme na Amani zimfikie) amesema:

-:Naapa kwa Yule Ambaye nafsi ya Muhammad Iko Mikononi Mwake. Hakuna hata mmoja katika Umma Huu atakae sikia ulinganizi wangu.Awe Myahudi au Mnaswara (Mkristo)Kisha akafa bila ya kuyaamini niliyotumwa nay o, isipokuwa atakuwa miongoni mwa watu wa Motoni.”

Imepokewa na Muslim.

Muhtasari wa Maana

Mtume (rehme na Amani zimfikie) anaapa kwamba hakuna yeyote atakayeishi katika zama zake au baada yake, akawa amesikia habari za ulinganizi wake kisha akaacha kumuamini. hakika mafikio yake yatakuwa ni motoni, hata kama ni Myahudi au Mnaswara (Mkristo).

Miradi ya Hadithi