18 - KUTUTWA UTUME KWA UJIO KWA NABII MUHAMMAD (S.A.W)

عن أبي هريرة أن رَسُول اللهِ قال: «وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ، لا يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هذِهِ الأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلا نَصْرَانِيٌّ، ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ: إِلَّا كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ» رواه مسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehme na Amani zimfikie) amesema:

-:Naapa kwa Yule Ambaye nafsi ya Muhammad Iko Mikononi Mwake. Hakuna hata mmoja katika Umma Huu atakae sikia ulinganizi wangu.Awe Myahudi au Mnaswara (Mkristo)Kisha akafa bila ya kuyaamini niliyotumwa nay o, isipokuwa atakuwa miongoni mwa watu wa Motoni.”

Imepokewa na Muslim.

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Amesema Mwenyezi Mungu:

“Hakika Dini ya Haki aliyo iridhia Mwenyezi Mungu ni Dini ya Tawhidi, ya Mungu Mmoja, na kumnyenyekea Yeye kwa usafi wa moyo. Na Hawakutofautiana Mayahudi na Wakristo juu ya Dini hii, wakazua na wakabadilisha, isipokuwa ni baada ya kufikiwa na elimu, kwani kukhalifu kwao hakukuwa kwa kudanganyikiwa, bali yalikuwa hayo kwa uhasidi na ushindani tu. Na mwenye kupinga Ishara (dalili) za Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu”

[Al Imran: 19].


Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na anaye tafuta dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwake, na Akhera atakuwa miongoni mwa walio pata hasara (85). Vipi Mwenyezi Mungu atawaongoza watu walio kufuru baada ya kuamini kwao, na wakashuhudia ya kwamba Mtume huyu ni wa kweli, na zikawajia hoja za wazi, na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu (86). Hao malipo yao ni kuwa ipo juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote (87). Humo watadumu. Hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewa nafasi ya kujitetea”.

[Al Imran: 85 - 88].


Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 “Na anaye mpinga Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamuingiza katika moto wa Jahannamu. Na hayo ni mafikio mabaya.

[An-Nisa: 115].


Miradi ya Hadithi