عَنِ الْمِقْدَامِ بْنِ مَعْدِي كَرِبَ رضي الله عنه، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ  يَقُولُ: «مَا مَلَأَ آدَمِيٌّ وِعَاءً شَرًّا مِنْ بَطْنٍ. بِحَسْبِ ابْنِ آدَمَ أُكُلَاتٌ يُقِمْنَ صُلْبَهُ، فَإِنْ كَانَ لَا مَحَالَةَ، فَثُلُثٌ لِطَعَامِهِ، وَثُلُثٌ لِشَرَابِهِ، وَثُلُثٌ لِنَفَسِهِ»

Kutoka kwa Al-Miqdam bin Ma’di Karib, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani ziwe juu yake akisema: 1. “Hakuna mwanadamu aliyejaza chombo kibaya kuliko tumbo. 2. Inamtosha mwanadamu vijitonge kadhaa vya kusimamisha uti wake wa mgongo.  3. Ikiwa haitaepukika, basi theluthi kwa chakula chake, na theluthi kwa kinywaji chake, na theluthi kwa ajili ya pumzi yake”


Muhtasari wa Maana

Kujaza tumbo kwa chakula ni madhara makubwa, kwani Muislamu hutosheka kwa chakula kinachozuia njaa na kumpa uchangamfu katika kazi

Miradi ya Hadithi