عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو - رضي اللَّه عنهمَا - عَنِ النَّبِيِّ قَالَ:  «الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ، وَالْمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللَّهُ عَنْهُ»


Kutoka kwa Abdullah bin Amr – Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili – kutoka kwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, amesema:

1. “Muislamu ni yule ambaye Waislamu wamesalimika kutokana na ulimi wake na mikono yake.  2.  Muhajir ni yule anayeyaaacha aliyoharamisha Mwenyezi Mungu.”


Muhtasari wa Maana

Mtume Rehma na Amani ziwe juu yake anaeleza kuwa Muislamu wa kweli ni yule anayewaokoa Waislamu na madhara yake, na aliyehama kiukweli ni yule anayeyaacha madhambi na uasi.

Miradi ya Hadithi