عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو - رضي اللَّه عنهمَا - عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ، وَالْمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللَّهُ عَنْهُ»
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو - رضي اللَّه عنهمَا - عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ، وَالْمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللَّهُ عَنْهُ»
Kutoka kwa Abdullah bin Amr – Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili – kutoka kwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, amesema:
1. “Muislamu ni yule ambaye Waislamu wamesalimika kutokana na ulimi wake na mikono yake. 2. Muhajir ni yule anayeyaaacha aliyoharamisha Mwenyezi Mungu.”
1-Muislamu wa kweli ni yule anayezuia maovu yake kwa watu, basi Waislamu wakasalimika kutokana na madhara yake ya maneno na ya vitendo, na Mwenyezi Mungu amewaahidi adhabu kali wale wanaowadhuru Waumini kwa kusema:
“Hakika wanao muudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha (57) Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi za dhahiri
[Al-Ahzab: 57-58]
Maana ya Hadithi sio kutokuwepo Uislamu kwa wale wanaowadhuru Waislamu, bali kinachokusudiwa ni kukosekana ukamilifu wa Uislamu. Yeyote ambaye Waislamu hawatasalimika kutokana na ulimi na mkono wake, basi ukamilifu wa Uislamu unakosekana kwake, kwa sababu usalama wa Waislamu kutokana na ulimi na mkono wa mtu ni jambo la wajibu, kwani kumdhuru Muislamu ni haramu kwa ulimi na mkono. Hivyo maudhi ya mkono ni kitendo, na maudhi ya ulimi ni kwa maneno. [1]
Maudhi hayako kwenye mkono na ulimi tu, bali hupatikana hata katika viungo vingine, lakini zaidi hupatikana sana kutokana na matendo ya ulimi na mkono. Ulimi unasengenya, unatukana, unashuhudia uwongo, na kashfa. Ama mkono unadhulumu, unaiba, unaua na maasi mengine.
Bali Mtume Amani zimshukie alianza kwa kutaja ulimi kwa sababu ni mbaya zaidi, na kuudhi ni rahisi zaidi na zaidi, na hurefusha maiti na aliye hai, na ndio maana Muadh radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie aliposema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hivi tutawajibishwa kwa yale tunayoyasema? Akasema: “Mama yako na akuondokee ewe Muadh! Hivi unadhani watu watatupwa motoni kifudifudi - au akasema: Juu ya pua zao -kwa kosa linguine isipokuwa ni kutokana na mavuno ya ndimi zao?! [2]
Na Uhamaji wa kweli sio tu kuhama kutoka nchi ya ushirikina na kwenda katika nchi ya imani, bali ni mja kuacha kila alichoharamishiwa na Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, kuuhama mji wa ukafiri huku ukiendelea kufanya dhambi si kuhama kuliko kamilika; Asili ya hijra ni kuyaacha maovu na kukaa mbali nayo kwa kutafuta kheri na kuipenda, kwani kufanya hivyo ni kuacha maasi na madhambi, na ni pamoja na kuuhama mji wa ushirikina na kwenda mji wa Uislamu [3].
1. Fanya haraka umiliki sifa kamili za Uislamu ili upate ujira wa Waislamu wa kweli, na jihadhari na kuwadhulumu watu kwa kauli au vitendo.
2. Jihadhari na kuwadhulumu watu kwa ulimi na mkono; Ni sababu ya kufilisika kweli na kupoteza thawabu kwa kiasi ambacho ulichoka kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu. Akasema Mtume Amani iwe juu yake: "Je, mnamjua ni nani aliyefilisika?" Wakasema Maswahaba: Aliyefilisika miongoni mwetu ni yule ambaye hana dirham wala mali.” Akasema Mtume: “Waliofilisika katika Ummah wangu watakuja Siku ya Kiyama wakiwa na malipo ya Sala, Swaumu na Zaka. Naye atakuja haliyakuwa alimtusi huyu, na kumtuhumu yule, na kula fedha za mtu huyu, na kumwaga damu ya mtu huyu, na kumpiga mtu huyu. Huyu atapewa katika mema yake na mwingine pia katika Mema yake, Ikiwa mema yake yatakwisha kabla ya deni lake kulipwa, itachukuliwa kutoka katika dhambi zao na kuongezewa juu yake, Kisha akatupwa motoni [4] Jihadhari na hasara hiyo.
3. Maadili ni mizani baina ya Waumini, na Dini yote ni maadili, basi anaye kushindeni kwa kuwa na tabia njema basi amekushindeni katika Dini [5].
1. Fath al-Bari cha Ibn Rajab (1/37, 38).
2. Imepokewa na Ahmad (22665), Ibn Majah (3973), na Al-Tirmidhiy (2616).
3. Fath al-Bari cha Ibn Rajab (1/39).
4. Imepokewa na Muslim (2581).
5. “Madarij al-Salikeen” cha Ibn al-Qayyim (2/307).