عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو - رضي اللَّه عنهمَا - عَنِ النَّبِيِّ قَالَ:  «الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ، وَالْمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللَّهُ عَنْهُ»


Kutoka kwa Abdullah bin Amr – Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili – kutoka kwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, amesema:

1. “Muislamu ni yule ambaye Waislamu wamesalimika kutokana na ulimi wake na mikono yake.  2.  Muhajir ni yule anayeyaaacha aliyoharamisha Mwenyezi Mungu.”


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: “Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri

[Al-Ahzab: 58]

Pia Mwenyezi Mungu akasema: “Mkiyaepuka makubwa mnayo katazwa, tutakufutieni makosa yenu madogo, na tutakuingizeni mahali patukufu

[An-Nisa: 31]. 

 Na akasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka: “Na wanao yaepuka madhambi makubwa na mambo machafu, na wanapo kasirika wao husamehe”

[Al-Shura: 37]


Miradi ya Hadithi