عَنْ عَامِرِ بْنِ وَاثِلَةَ، أَنَّ نَافِعَ بْنَ عَبْدِ الْحَارِثِ، لَقِيَ عُمَرَ[ رضي الله عنه ] بِعُسْفَانَ، وَكَانَ عُمَرُ يَسْتَعْمِلُهُ عَلَى مَكَّةَ، فَقَالَ: مَنِ اسْتَعْمَلْتَ عَلَى أَهْلِ الْوَادِي؟ فَقَالَ: ابْنَ أَبْزَى، فقال: وَمَنِ ابْنُ أَبْزَى؟ فقال: مَوْلًى مِنْ مَوَالِينَا. قَالَ: فَاسْتَخْلَفْتَ عَلَيْهِمْ مَوْلًى؟ قَالَ: إِنَّهُ قَارِئٌ لِكِتَابِ اللهِ عزَّ وجلَّ، وَإِنَّهُ عَالِمٌ بِالْفَرَائِضِ، قَالَ عُمَرُ: أَمَا إِنَّ نَبِيَّكُمْ ﷺ قَدْ قَالَ: «إِنَّ اللهَ يَرْفَعُ بِهَذَا الْكِتَابِ أَقْوَامًا، وَيَضَعُ بِهِ آخَرِينَ»

kutoka kwa A`amir bin Waathilah amesimulia kuwa:

1- Naafi`I bin Abdil Warith akikutana na Umar (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) katika sehemu inaitwa U`sfaana, na Umaru alikuwa amemfanya kuwa kiongozi katika mji wa makah, Umaru akamuuliza: ni nani umemuacha katika nafasi yako ya uongozi katika watu wa hilo bonde? 2- Akasema: (nimemuacha) kijana wa Abzaah, Umar akasema: ni nani huyo kijana wa Abzaah? Akasema: ni mjakazi katika wajakazi wetu, 3- Umaru akasema: unawaachia kiongozi mjakazi? 4- Akasema: Hakika yeye ni msomaji mzuri wa kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni msomi wa elimu ya mirath. 5- Umaru akasema: kweli hakika Nabii wenu (rehma na amani ziwe juu yake) alisema: hakika Mwenyezi Mungu hunyanyua kwa hiki kitabu watu, na kwa kitabu hiki huwashusha wengine.

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu:

Na inapo teremshwa Sura wapo miongoni mwao wasemao: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Ama wale walio amini inawazidishia Imani, nao wanafurahi. 124, Ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi inawazidishia uovu juu ya uovu wao; na wanakufa hali ni makafiri. 125. . 

[At-Tawbah: 124, 125]

Amesema Mwenyezi Mungu:

29. Hakika wale wanao soma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakashika Sala, na wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika tulivyo waruzuku, hao hutaraji biashara isiyo doda.  30. Ili Yeye awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na awazidishie kutokana na fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani.  31. Na hayo tuliyo kufunulia kutoka Kitabuni ni Kweli yenye kusadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Hakika Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni Mwenye khabari na Mwenye kuona.  32. Kisha tumewarithisha Kitabu hao ambao tuliwateuwa miongoni mwa waja wetu. Kati yao yupo aliye jidhulumu nafsi yake, na yupo wa katikati, na yupo aliye tangulia katika mambo ya kheri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo fadhila kuu.  . 

[Fatir: 29 - 32]

Amesema Mwenyezi Mungu:

Mwenyezi Mungu atawainua walio amini miongoni mwenu, na walio pewa ilimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. 11

[Almujadlati: 11]

Miradi ya Hadithi