عن ابن عمرَ وأبي هُريرةَ رضي الله عنهم، أنهما سَمعا رسولَ الله يقولُ على أعوادِ مِنْبَرِه: «لَيَنْتَهِيَنَّ أقْوامٌ عن وَدْعِهمُ الجُمُعاتِ، أو لَيَخْتِمَنَّ اللهُ على قُلوبِهم، ثم لَيَكونُنَّ منَ الغافِلينَ»

Kutoka kwa Ibn Umar na Abu Hurayrah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kwamba walimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie akisema akiwa juu ya mimbari yake:

“Watu wakome kuacha Swalah ya Ijumaa. Au Mwenyezi Mungu atawapiga muhuri katika nyoyo zao, kisha wawe miongoni mwa walioghafilika”

Katika hadithi hii, kuna ubainifu wa uwajibu wa Swala ya Ijumaa kwa Waislamu wote, na onyo dhidi ya kuipuuza, na ubainifu wa adhabu kali anayostahiki mtu hapa duniani kwa kupuuza Swala ya Ijumaa.

Maana ya Hadithi ni kuwa moja kati ya mambo mawili yatatokea bila ya shaka watu kuacha kuswali swala ya ijumaa ama sivyo Mwenyezi Mungu anazipiga muhuri nyoyo zao na kuzifunika, kwa hivyo haziongoki kwenye haki na hazitambui mema na wala hazitakemea maovu. Mpaka zinakuwa pamoja na walioghafilika, na Mwenyezi Mungu anasema:

“Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa”

[Al-Baqarah: 7].

Maana ya Hadithi hiyo inathibitishwa na kauli ya Mtume rehma na amani zimshukie: “Mwenye kuacha Swala tatu za Ijumaa kwa kupuuza, Mwenyezi Mungu atapiga muhuri juu ya moyo wake”[1]

Swala ya Ijumaa ni faradhi ya mtu binafsi kwa kila Muislamu wa kiume aliye huru. Mwenyezi Mungu anasema:

“Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo Ni bora kwenu, lau kama mnajua”

[Al-Jumaa: 9].

Na Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Kila m wenye kubaleghe lazima aende kwenye sala ya Ijumaa, na kila anayekwenda Ijumaa lazima aoge "[2]

MAFUNDISHO:

  1. Muislamu ambaye anamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu uongofu na kufanya vizuri hajiingizi katika chuki na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na anaifanya kustahiki kuandikwa kwenye moyo na kughafilika katika kumtii Mwenyezi Mungu.

  2. Mambo makubwa yanahitaji amri ya jumla na katazo kuwekwa hadharani. Kwa ajili hiyo, makatazo ya kuacha jamaa na Ijumaa yanafaa kuwa kwenye mimbari pamoja na mkusanyiko wa watu, na kuongeza umuhimu wake.ni juu ya mlinganiaji, Mwalimu, Mwanasharia na mwenye kuelimisha aweke kila jambo mahali pake, kwani kinachofaa katika masomo kinapingana na kinachostahiki kuwa katika khutba ya Ijumaa, na kadhalika.

  3. Ukali wa mbinu za mlinganiaji, mwalimu na mlezi hutofautiana kulingana na hali. Baadhi ya mbinu zinastahili kuonyeshwa kwa upole, zingine zinastahili ushauri, zingine zinastahili lawama na mawaidha ya upole, na zingine zinastahiki hasira na ukali.

  4. Katika mawaidha, haijuzu kutaja majina ya watu wanao onywa hadharani, hivyo watafedheheka, na kukataza maovu kutaleta ubaya mkubwa kuliko huo, kwani Mtume Rehema na Amani zimshukie, amesema: “Watu wakome” na hakumtaja mtu hata mmoja.

  5. Sala ya Ijumaa ni wajibu kwa kauli moja ya wanavyuoni. Mwenyezi Mungu Mtukufu amemwahidi mwenye kuiacha aina za adhabu na mateso. Jihadharini na kustahiki ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu!

  6. Ijumaa ni siku bora Zaidi iliyochomozewa jua. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie: “Siku bora kabisa ya kuchomoza jua ni Ijumaa, siku hiyo aliumbwa Adam na ndani yake akaingia peponi, na siku hiyo ndio alitolewa peponi”[3]  Kwa hivyo, usiiruhusu siku hiyo iwe shahidi baya kwako, bali iwe shahidi mzuri kwako .

  7. Muislamu anatakiwa kuwa makini na mapema kuswali swalah ya Ijumaa, kuoga na kuvaa nguo bora kabisa. Malipo ya hayo ni makubwa.” Akasema Mtume rehma na amani zimshukie: “Anayeoga siku ya Ijumaa akaoga kwa uchafu, kisha akaenda zake msikitini saa ya kwanza, Ni kama ametoa kafara ya ngamia, Na mwenye kwenda katika saa ya pili ni kama amechinja ng'ombe, Na ye yote atakayekwenda saa ya tatu, ni kama amechinja kondoo dume, Na anayeenda saa nne ni kama ametoa kafara kuku, Na anayeenda saa tano ni kama ametoa yai, Basi imamu anapotokea, Malaika huhudhuria wakisikiliza ukumbusho” Mutafaqun Alayhi[4].

  8. Mshairi amesema:

    Ee siku ambayo, wema Wake umeumbwa kwake = Na nuru za uwongofu zimekusanyika siku hiyo.

Ni siku ambayo Mwenyezi Mungu ameiwekea = mpango thabiti wa kufuatwa.

Mwenyezi Mungu ameuthibitisha umoja wetu = katika mkutano wa ajabu kabisa

Kila wiki ina khutba = imamu ameongoka vipi anayeisikia

Kwa hakika ni Siku iliyo njema = Na ni siku ya taifa lililokusanyika.

Hakuna siku bora katika masiku = siku bora ni Ijumaa

Umoja wa kiislamu ni nembo inayojulisha = kuwa ummah uko kwenye kilele cha juu kabisa.

Marejeo

  1. Imesimuliwa na Abu Dawood (1052), al-Tirmidhi (500), an-Nasa’i katika al-Sunan al-Kubra (1668), na Ibn Majah (1125).
  2. Imepokewa na Abu Daawuud (342) na An-Nasa’i (1371).
  3. Imepokewa na Muslim (854).
  4. Imepokewa na Al-Bukhari (881) na Muslim (850).


Miradi ya Hadithi