عن ابن عمرَ وأبي هُريرةَ رضي الله عنهم، أنهما سَمعا رسولَ الله يقولُ على أعوادِ مِنْبَرِه: «لَيَنْتَهِيَنَّ أقْوامٌ عن وَدْعِهمُ الجُمُعاتِ، أو لَيَخْتِمَنَّ اللهُ على قُلوبِهم، ثم لَيَكونُنَّ منَ الغافِلينَ»

Kutoka kwa Ibn Umar na Abu Hurayrah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kwamba walimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie akisema akiwa juu ya mimbari yake:

“Watu wakome kuacha Swalah ya Ijumaa. Au Mwenyezi Mungu atawapiga muhuri katika nyoyo zao, kisha wawe miongoni mwa walioghafilika”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:

“Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua (9) Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa (10) Na wanapo iona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki”

[Al-Jumaa: 9-11].

Miradi ya Hadithi