- Mtume, Rehema na Amani zimshukie, anaeleza baadhi ya sifa njema, na anataja namana ya kumheshimu jirani, kwani Muumini anatakiwa kumheshimu jirani yake na kuhifadhi haki zake. Basi anamwekea dhamana kwa uadilifu na wema, anaikagua hali yake, anazungumza naye kwa maneno ya upole, anamsaidia katika anachohitaji, na wala hamdhuru kwa kauli au vitendo.
Ndio maana Mwenyezi Mungu, aliyetakasika, ameamrisha kumfanyia wema jirani kwa kusema:
“Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri” .
Na Jibril alishuka mara kwa mara kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam akimuusia kumtendea mema jirani yake. Akasema,
Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
“Jibril alikuwa akiniusia nimtendee wema jirani mpaka nikafikiri kwamba atamrithi. [1]
Na Mtume Rehma na amani iwe juu yake iliapa kwa kukosa imani kwa mwenye kumuudhi jirani yake
akasema, amani iwe juu yake:
“Wallahi haamini, na Wallahi haamini, na Wallahi haamini.” Ikasemwa.: Ni nani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Alisema: "Yule ambaye jirani yake hayuko salama kutokana na uovu wake". [2]
2- Vile vile ametaja kumuenzi mgeni kuwa ni miongoni mwa alama za kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na Mtume, rehma na amani zimshukie, akasema kuwa zawadi ya mwenyeji kwa mgeni wake na kumuenzi vizuri ni kumtukuza na kumruzuku chakula bora na mahala pa kulala mchana na usiku wake, kisha baada ya hayo amlishe Anachokula pasina kujidhiki, na ugeni hukamilika kwa siku tatu. Ikiwa mwenyeji anapenda mgeni akae naye baada ya hayo, basi ni sadaka na fadhila kutoka kwake, na hakuna ubaya kwake asipofanya hivyo. Kwakuwa kishatekeleza yaliyo wajibu kwake kwa kumfanyia takrima kwa muda wa siku tatu.
Bali Mtume rehema na amani zimshukie amefanya takrima bora kwa mgeni ni siku ya kwanza na usiku kwa sababu ya uchovu na dhiki iliyompata katika safari yake, hivyo atafarijika kwa hilo, Na anakuwa karibu na mwenyeji wake, na mafungamano ya mapenzi na huruma baina ya Waislamu yanaimarika. Hilo likifanyika siku ya kwanza, mwenyeji asijikalifishe baada ya hapo, lakini amhudumie kutokana na kile anachopata.
4- Kisha, Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akataja sifa ya tatu, nayo ni kwamba Muumini aangalie maneno yake anayotaka kuyazungumza; Ikiwa anaona ni mazuri au njia ya wema, anasema. Na akiona sivyo basi atakaa kimya. Kunyamaza ni tunu ikiwa kusema ni dhambi au kupelekea madhambi, na mtu atawajibika kwa kila analolisema.
“Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari” .
Na “Hakika mja anaweza kusema neno la radhi ya Mwenyezi Mungu bila ya kulizingatia, na Mwenyezi Mungu humnyanyua daraja kwa hilo. Na mtu anaweza kusema neno la kumkasirisha Mwenyezi Mungu, pasina kulizingatia, na akaingia motoni kwa neno hilo" [3]
Hadithi hii imekusanya milango ya wema, kwa hiyo wanavyuoni wametaja kwamba adabu za Kiislamu zinapatikana katika hadith nne. Hadithi hii, na Hadithi isemayo: “Sehemu ya wema wa Uislamu wa mtu ni kuacha kwake yasiyomhusu,” na kauli yake Mtume, rehma na amani ziwe juu yake, kwa yule aliyefupisha amri kwa ajili yake: “Usikasirike
na kusema kwake, rehma na amani zimshukie:
“Hataamini mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake kile anachoipendelea nafsi yake” [4]
1- Moja ya dalili za uthabiti na ongezeko la imani katika moyo wa Muumini ni kumheshimu na kumkirimu jirani yake na wala asimdhuru. Kwa hivyo tafuta alama hizo mwenyewe.
2-Jihadhari na kumdhuru jirani yako, kwani utazuiliwa kuingia Peponi.
Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie:
“Yule ambaye jirani yake hajasalimika na uovu wake hataingia Peponi” [5]
3-Kadiri jirani anavyokaribia mlango ndivyo anavyokuwa na haki zaidi, na ndivyo anavyostahili heshima zaidi. Jirani anapaswa kuhifadhi haki za jirani yake, hivyo asiangalie makosa yake, bali amzoeshe zawadi na wito, na amfanyie wema kwa kauli na vitendo.
4-Ujirani mwema hauishii katika kumheshimu jirani tu, bali pia kustahimili maudhi yatokayo kwake bila kukusudia. Al-Hassan Al-Basri, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “Ujirani mwema sio kuacha madhara, bali ujirani mwema ni kuvumilia madhara” [6]
5- Kumheshimu mgeni ni dalili ya kumwamini Mwenyezi Mungu, na kufuata mfano wa Mitume wa Mwenyezi Mungu, rehma na amani ziwe juu yao. Qur’ani imeeleza ukarimu wa Rafiki wa Mwenyezi Mungu, ambaye ni Nabii Ibrahim, amani iwe juu yake, na Mtume wetu Muhammad rehma na Amani zimshukie, alikuwa mtoaji mkarimu, mkarimu zaidi kuliko upepo uliotumwa, na ndio maana Abdullah bin Amr, Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili, alisema: "Asiyepokea wageni na kuwakirimu si mfuasi wa Nabii Muhammad, wala Ibrahim rehma na Amani ziwashukie wote wawili” [7]
6- Muislamu awe na sifa ya kumjali mgeni, na asimkatae mgeni akiona ni mwema, na hilo lisiishie kwa wale anaowajua kuliko wale asiowajua; Abu Hurairah, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alikuwa mgeni kwa watu wasiomjua, lakini wakakataa kumkaribisha, kisha akaleta chakula, akawakaribisha wale pamoja, lakini wakakataa kula naye. akawaambia: Hamumkaribishi mgeni wala hamuitikii mwaliko! Ninyi hamna Uislamu wowote. Kisha mtu mmoja miongoni mwao akamtambua na akamwambia: “karibu, njoo nyumbani, Mwenyezi Mungu akusamehe.” Kisha akasema Abu Hurairah, Mwenyezi Mungu awe radhi naye: Hili ni baya na baya zaidi, je, hamumkaribishi mgeni ila kwa yule mnayemjua? [8]
7- Muislamu aweke rehani kwa maneno yake, asizungumze kwa uhuru juu ya yale yanayoruhusiwa na haramu. Amesema Omar Ibn Al-Khattab: “Mwenye kusema mengi ataanguka mara nyingi, na anayeanguka mara nyingi, dhambi zake zitakuwa nyingi; na ikiwa dhambi zake ni nyingi, Moto utamstahili zaidi.” [9]
8-Muhammad bin Ajlan, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “Maneno ni manne: Kumtaja Mwenyezi Mungu, kusoma Qur-aan, kuuliza juu ya elimu na kujulishwa juu yake, au kuzungumza juu ya yale yanayokuhusu wewe katika mambo yako ya kidunia” [10]
9- Mtu mmoja alimwambia Salman, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani: “Ninasihi.” Akasema: “Usiseme.” Akasema: Anayeishi miongoni mwa watu haliwezi hili, Akasema: Ukisema basi sema kwa haki au nyamaza” [11]
10- Abu Bakr Al-Siddiq, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alikuwa akiushika ulimi wake na kusema: “Huu Ulimi umeniweka mahala tofauti” [12]
11- Ibn Masoud, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema: “Wallahi naapa kwa yule ambaye hapana Mungu badala yake, hakuna chochote katika ardhi kinachostahiki adhabu ya kifungo kirefu kuliko ulimi” [13]
12- Linda ulimi wako na utaingia Peponi; Mtume Rehma na Amani iwe juu yake amesema: “Mwenye kunidhaminia kilicho baina ya midomo yake miwili na kilicho baina ya miguu yake miwili, basi nitamdhaminia Pepo” [14]
Marejeo
- Imepokewa na Al-Bukhari (6015) na Muslim (2625), kwa kutoka kwa Ibn Omar, Mungu awe radhi nao.
- Imepokewa na Al-Bukhari (6016).
- Imepokewa na Al-Bukhari (6478) na Muslim (2988).
- Tazama: Maelezo ya An-Nawawi katika sahihi ya Muslim (2/19).
- Imepokewa na Muslim (46).
- “Jami’ al-Ulum wa’l-Hikum” cha Ibn Rajab al-Hanbali (1/ 353).
- "Jami' al-'Ulum wa'l-Hukam" cha Ibn Rajab (1/ 356).
- "Jami' al-'Ulum wa'l-Hukam" cha Ibn Rajab (1/ 356).
- "Jami' al-'Ulum wa'l-Hukam" cha Ibn Rajab (1/ 339).
- “Jami’ al-‘Ulum wa’l-Hukam” cha Ibn Rajab (1/ 340).
- “Jami’ al-‘Ulum wa’l-Hukam” cha Ibn Rajab (1/ 340).
- “Jami’ al-‘Ulum wa’l-Hukam” cha Ibn Rajab (1/ 340).
- “Jami’ al-‘Ulum wa’l-Hukam” cha Ibn Rajab (1/ 340).
- Imepokewa na Al-Bukhari (6474).