عَنْ أَبِي شُرَيْحٍ الكَعْبيِّ، أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ قَالَ: «مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ جَارَهُ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ جَائِزَتَهُ» قَالَ: وَمَا جَائِزَتُهُ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: «يَوْمٌ وَلَيْلَةٌ، وَالضِّيَافَةُ ثَلاثَةُ أَيَّامٍ، فَمَا كَانَ وَرَاءَ ذَلِكَ فَهُوَ صَدَقَةٌ عَلَيْهِ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيَقُلْ خَيْرًا أَوْ لِيَصْمُتْ».

Kutoka kwa Abu Shuraih al-Kaabi, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume, rehma na amani zimshukie, amesema:

1- “Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi amkirimu jirani yake. 

2- Na anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi amkirimu mgeni wake stahiki zake.” Akasema swahaba wa Mtume: Na stahiki zake ni nini, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Mchana mmoja na usiku mmoja, na ugeni ni siku tatu, tofauti na hayo ni sadaka juu yake” 

3- Na anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi na aseme mema au anyamaze” .

Abu Shuraih Al-Kaabiyyu

Abu Shuraih Al-Kaabiyyu Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ni sahaba mkubwa, mashuhuri kwa lakabu yake, na kulikuwa na tofauti ya mitazamo kuhusu jina lake. Ikasemwa: Jina lake ni Ka`b bin Amr, na ikasemwa: Amr bin Khuwaylid, na kauli iliyo sahihi zaidi ni Khuwaylid bin Amr bin Sakhr bin Abd al-Uzza, alikuwa mmoja wa watu wenye hekima, alisilimu kabla ya kufunguliwa mji wa Makkahh, na alibeba moja ya bendera za Banu Ka’ab bin Khuza’a katika siku ya kufunguliwa mji wa Makkah, kisha akaenda Madina na akafa huko katika mwaka wa sitini na nane wa Hijrah [1]

Marejeo

  1. Rejea ufafanuzi wake katika: “Ma’rifat al-Sahaba” cha Abu Naim (2/960), “Al-Isti’ab fi Ma’rifat al-Ashab” cha Ibn Abd al-Barr (2/455), “Asad. al-Ghaba fi Ma'rifat al-Sahaba” cha Ibn al-Atheer (6/160), “Al-Isaba fi Tamyiiz swahaba” cha Ibn Hajar (7/173).


Miradi ya Hadithi