عَنْ أَبِي شُرَيْحٍ الكَعْبيِّ، أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ قَالَ: «مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ جَارَهُ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ جَائِزَتَهُ» قَالَ: وَمَا جَائِزَتُهُ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: «يَوْمٌ وَلَيْلَةٌ، وَالضِّيَافَةُ ثَلاثَةُ أَيَّامٍ، فَمَا كَانَ وَرَاءَ ذَلِكَ فَهُوَ صَدَقَةٌ عَلَيْهِ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيَقُلْ خَيْرًا أَوْ لِيَصْمُتْ».

Kutoka kwa Abu Shuraih al-Kaabi, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume, rehma na amani zimshukie, amesema:

1- “Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi amkirimu jirani yake. 

2- Na anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi amkirimu mgeni wake stahiki zake.” Akasema swahaba wa Mtume: Na stahiki zake ni nini, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Mchana mmoja na usiku mmoja, na ugeni ni siku tatu, tofauti na hayo ni sadaka juu yake” 

3- Na anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi na aseme mema au anyamaze” .

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mtukufu:

 “Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri”.

[An-Nisa: 36]

Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 “Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari” .

[Qaaf: 18]

Na amesema Mtukufu: 

“Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa? (24)Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni (25) Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona (26) Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?”

[Al-Dhariyat: 24-27].

Miradi ya Hadithi