عَنْ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «إِنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّةِ. وَإِنَّمَا لِامْرِئٍ مَا نَوَى. فَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ إِلَى اللهِ وَرَسُولِـهِ، فَهِجْرَتُهُ إِلَى اللهِ وَرَسُولِـهِ. وَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيَا يُصِيبُهَا، أَوِ امْرَأَةٍ يَتَزَوَّجُهَا، فَهِجْرَتُهُ إِلَى مَا هَاجَرَ إِلَيْهِ» متفق عليه.

Kutoka kwa Umar bin Al-Khattab, (r.a) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.).

1. Hakika matendo huhesabika kwa nia tu. 

2. Na hakika kila mtu atalipwa kwa alilokusudia. 

3. Basi atakaekuwa kuhama kwake ni kwa ajili Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi kuhama kwake ni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. 

4. Na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya dunia ili aipate, au mwanamke ili amuoe, basi kuhama kwake ni lile aliloliendea.” (Imepokelewa na Imam Bukhari na Muslimu).

Muhtasari wa Maana

Mtume (s.aw) amesema kuwa kanuni katika kuzingatia na kukubalika matendo ni nia, ambayo hutofautisha kati ya mazoea na ibada, na hupambanua kati ya matendo mema na maovu. Na watu wawili wanaweza kufanya kitendo cha halali au cha kisheria na yakatofautiana makusudio yao, mmoja anaweza kuwa amekusudia kumtii Allah na akalipwa kwa ajili yake, na mwingine hakukusudia chochote na akawa hakulipwa. Yeyote anayehama kutoka nchi yake kwenda nchi nyengine kwa ajili ya  Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya kufuata Sunnah za Mtume wake, (s.aw) basi atalipwa, na mwenye kuhama kwa ajili ya kitu kisichokuwa hicho, hatapata  Zaidi ya alichokusudia.

Miradi ya Hadithi