عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ - رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ - عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «لا عَدْوَى وَلا طِيَرَةَ، وَيُعْجِبُنِي الفَأْلُ» قَالُوا: وَمَا الفَأْلُ؟ قَالَ: «كَلِمَةٌ طَيِّبَةٌ» متفق عليه

Kutoka kwa anas bun maali (Radhi za Mwenyezi ziwe juu yake), Kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), amesema: 1. “Hakuna a’d-waa, yaani maambukizi 2. Wala twiyara, yaani kuitakidi mikosi 3. Na ninafurahishwa fa-lu” wakasema: fa-lu ni nini? Akasema: “ni neno zuri” imepokelewa na Bukhari Na Muslimu


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

﴾wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. .﴿

[Al-Baqarah: 195]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

131.﴾ Likiwafika jema wakisema: Haya ni haki yetu. Na likiwafika ovu husema: Musa na walio pamoja naye ni wakorofi. Hakika ukorofi wao huo unao wafikia unatoka kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wao hawajui. .﴿

[Al-A'raf: 131]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

﴾ Sema: Halitusibu ila alilo tuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu! .﴿

[At-Tawbah: 51]

﴾Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. .﴿

[Al-Hadid: 22]

Miradi ya Hadithi