عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ - رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ - عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «لا عَدْوَى وَلا طِيَرَةَ، وَيُعْجِبُنِي الفَأْلُ» قَالُوا: وَمَا الفَأْلُ؟ قَالَ: «كَلِمَةٌ طَيِّبَةٌ» متفق عليه

Kutoka kwa anas bun maali (Radhi za Mwenyezi ziwe juu yake), Kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), amesema: 1. “Hakuna a’d-waa, yaani maambukizi 2. Wala twiyara, yaani kuitakidi mikosi 3. Na ninafurahishwa fa-lu” wakasema: fa-lu ni nini? Akasema: “ni neno zuri” imepokelewa na Bukhari Na Muslimu


baba Hamza, au baba Thumamah, Anas bun Malik

baba Hamza, au baba Thumamah, Anas bun Malik, ukoo wa Annadhwari, Answari(ni katika waislaam walio mpokea Mtume Madina) amezaliwa miaka kumi kabla ya Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) kuhamia Madina, alikuwa ni mtumishi wa Mtume mara tu alivyo ingia Madina, na Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alimuombea dua ya kujaliwa watoto wengi, mali, umri mrefu na kusamehewa dhambi. Akawa ana watoto wengi na mali, na alikuwa ni swahaba wa mwisho kufariki kwa walio kuwa katika mji wa Basra. Amefariki mwaka (93H) [1]

Marejeo

1.  Rejea  yake ufafanuzi wake katika: “Maarifaat al-Sahaba” na Abu Nu’aym (4/1846), “aliastieab fi maerifat al'ashabi"na Ibn Abd al-Bar (4/1770), “Asad al-Ghaba” na Ibn al-Atheer (3/357), “Al-Isbah fi Tamazu al-Sahaba” cha Ibn Hajari Asqalani (4/267) .


Miradi ya Hadithi