عَنْ عُقبةَ بنِ عَامرٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ : «أَلَمْ تَرَ آيَاتٍ أُنْزِلَتِ اللَّيْلَةَ لَمْ يُرَ مِثْلُهُنَّ قَطُّ: ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ﴾ [الفلق: 1]، و ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ﴾ [الناس: 1]»

Kutoka kwa Uqba Bin A`Amir (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: amesema Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) Je haujajua ayah zilizotelemshwa usiku huu, (hakika) sijaona chochote mfano wake, Surat Al Falaq Na Surat Al Nnaasi.
Amesema Mwenyezi Mungu:
1. Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko, 2. Na shari ya alivyo viumba, 3. Na shari ya giza la usiku liingiapo, 4. Na shari ya wanao pulizia mafundoni, 5. Na shari ya hasidi anapo husudu. .
[Al-Falaq: 1 - 5]
Amesema Mwenyezi Mungu:
1. Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu,2. Mfalme wa wanaadamu, 3. Mungu wa wanaadamu, 4. Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, 5. Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, 6. Kutokana na majini na wanaadamu.
[Annaas: 1-6]