121 - FADHILA ZA SURAT AL FALAQ NA SURAT AL NNAASI

عَنْ عُقبةَ بنِ عَامرٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ : «أَلَمْ تَرَ آيَاتٍ أُنْزِلَتِ اللَّيْلَةَ لَمْ يُرَ مِثْلُهُنَّ قَطُّ: ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ﴾ [الفلق: 1]، و ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ﴾ [الناس: 1]»

Kutoka kwa Uqba Bin A`Amir (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: amesema Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) Je haujajua ayah zilizotelemshwa usiku huu, (hakika) sijaona chochote mfano wake, Surat Al Falaq Na Surat Al Nnaasi.

Abuu Hammaad, Uqba Bin A`Amir Al Juhaniy

Jina lake ni: Abuu Hammaad, Uqba Bin A`Amir Al Juhaniy (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) swahaba mtukufu, alikuwa msomaji mzuri wa qur`ani, na msomi wa elimu ya mirathi na sheria, mwenye fasaha ya kuzungumza, na mwandishi na mshairi mzuri, alishiriki vita ya ufunguzi wa Siria na Misri pamoja A`mru Bin Al A`Swii (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao) na alikuwa kiongozi huko Misri katika utawala Mua`wiyah Bin Abii Sufyaani (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake). Alifariki mwaka wa 58Ah.


Marejeo

1. Tazama tafsiri yake katika: “Maarifa al-Sahaba” cha Abu Na’im (4/2150), “Asad al-Ghaba” cha Ibn al-Atheer (4/51), “Al-Isbah” cha Ibn Hajar (5/ 187).

Miradi ya Hadithi