121 - FADHILA ZA SURAT AL FALAQ NA SURAT AL NNAASI

عَنْ عُقبةَ بنِ عَامرٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ : «أَلَمْ تَرَ آيَاتٍ أُنْزِلَتِ اللَّيْلَةَ لَمْ يُرَ مِثْلُهُنَّ قَطُّ: ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ﴾ [الفلق: 1]، و ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ﴾ [الناس: 1]»

Kutoka kwa Uqba Bin A`Amir (Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: amesema Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) Je haujajua ayah zilizotelemshwa usiku huu, (hakika) sijaona chochote mfano wake, Surat Al Falaq Na Surat Al Nnaasi.

1- Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) alimueleza Uqbah bin A`amir (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kwamba ametelemshiwa ufunuo (wahyi) wa surah mbili, haikuwahi kuteremka chochote mfano wake hasa zinazohusu kinga, kwa sababu ayah zote za surah hizo mbili ni kinga kwa mwenye kuzisoma., na kuna kuondoa husuda, na kukinga shari za mwenye kuhusudu ambayo hakuna katika surah nyingine . 

2- Hizo sura mbili ni: Suuratul falaqi na suuratu nnaasi. Amezielezea mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na aman ziwe juu yake kwa kutaja ya kwanza. Kwa umashuhuri wake katika kinga kama zilivomahushuhuri sura zote mbili kwa jina la kinga mbili, kwa sababu ya kuanza kwake na neno (sema najikinga). Na maana ya falaq ni : kila kinacho achan na Kitu na kupambanua na kua wazi kama alfajiri inavyo pambazuka na mbegu inavyotoka kwenye kokwa. Na kujikinga maana yake ni: kurejea kwa Mwenyezi Mungu na kushikamana nae kwa kutafuta ulinzi kutoka na shari za shetani na vimbi vyake na wasi wasi wak, kwa ajili ya kinga ya kila chenye shari Kinga hizi mbili zimethibiti katika kinga   na zinguo nayo ni katika hadith nyingi miongoni mwazo ni ile aliyo ipokea abuu said alkhudhry radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikua Mtume rehma na amani ziwe juu yake akijikinga kutokana na majini, na vijicho vya watu, mpaka ilipo telemka kinga mbili {Suuratulfalaqi na suuratunnaas}, hivyo basi zilipo teremka akaanza kuzitumia na akaacha tofauti na hizo ... Na Mtume kutumia sura hizo mbili na kuacha tofauti na hizo kwa sababu sura hizo mbili zimekusanya kinga zote na zinajitosheleza. 

Mafunzo

Tunajifunza katika hadithi hii yafuatayo; 

1- Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) alitumia namna miongoni mwa namna walizokuwa wakizitumia waarabu, nayo ni pale aliposema: “hujajua”, namna hii imekuja mara nyingi katika Qur`ani, na ni namna na njia ya kuvuta uelewa wa watu, na nafsi kumuelekea muulizaji, na kuwa na shauku ya jawabu na kupata elimu. Na hapo tunajifunza kuwa ni vizuri kwa wanazuoni na wasomi na walinganiaji na walezi, watumie namna hii mara kwa mara katika ufikishaji, hasa mwanzoni, ili kuiwekea mkazo katika mazungumzo na kuvuta usikivu na ufahamu wa wasikilizaji. 

2- Hadithi hii inaashiria kwamba kinga mbili (surat falaq na surat nnas) ni bora katika yale muislamu anayoyatumia katika kinga na zinguo (ruqya), hata kama hayazuiwi kuyatumia katika kinga kama dua na dhikri za kisheria, kama ilivyokuwa haizuiwi kutumia sababu halali za kidunia ambazo zinamkinga mtu katokana na shari mbalimbali, lakini hizi surah mbili ndiyo kubwa na msingi katika kufikia malengo.

3- Katika surat naasi kuna sifa ya shetani kwamba yeye ni khans na maana yake ni: anaerudi nyuma na kukimbia pale mja anapomtaja Mola wake Mlezi, hivyo basi mja anapolazimiana na kufanya adhkari na kusoma dua mbalimbali, anakuwa mbali na shetani, basi inatupasa kupupia kumtaja Mwenyezi Mungu kila muda, na tujikinge kwa Mwenyezi Mungu kila tunapatokewa na wasi wasi au kila tunaposhawishiwa kufanya dhambi. 

4- Zingatia kuadhimisha yale aliyoyaadhimisha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika surah za qur`ani, kwa kuzihifadhi na kujifunza na kuzitafakari ayah zake, na kuwafundisha wengine, iwe nyumbani au shuleni, au katika tafiti za wanazuoni, kwani hiyo ndio kipaumbele dhidi ya mengine. 

5- Hadith na ayah hizi zinaashiria haiwezekani kuondoa maudhi ya wenye husda na kubatilisha matendo ya wachawi waharibifu ispokuwa kwa kuomba msaada kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye pekee ndiyo Mola Mlezi wa watu, na Muumba wao, na Mwenye kumiliki mambo yao yote, halitokei jambo lolote katika ufalme wake bila ya idhini na ruhusa yake.

Miradi ya Hadithi