عن عُبَيْدِ اللهِ بْنِ مِحْصَنٍ الخَطْمِيِّ رضي الله عنه، عن النبيِّ ﷺ قال: «مَنْ أَصْبَحَ آمِنًا فِي سِرْبِهِ، مُعَافًى فِي جَسَدِهِ، عِنْدَهُ طَعَامُ يَوْمِهِ، فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا»

Kutoka kwa Ubayd Allah bin Muhsin al-Khatmi, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema:

“Mwenye kuamka asubuhi akiwa na Amani, mwenye afya njema katika mwili wake, ana chakula cha siku yake, hivyo ni kana kwamba amemilikishwa dunia.”


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mtukufu: 

“Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka”

[Al-An'am: 82]

Na akasema Allah mtukufu:

 “Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji ulio kuwa na amani na utulivu, riziki yake ikiufikia kwa nafasi kutoka kila mahali. Lakini ukazikufuru neema za Mwenyezi Mungu; kwa hivyo Mwenyezi Mungu akauvika vazi la njaa na khofu kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyafanya” .

[An-Nahl: 112]

Na akasema Allah mtukufu:

 “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu”.

[An-Nur: 55]

Na akasema Allah mtukufu:

 “Na nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu au anaye kanusha Haki inapo mjia? Je! Si katika Jahannamu ndio yatakuwa makaazi ya makafiri”.

[Al-Ankabut: 67]

Miradi ya Hadithi