عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّـهِ ﷺ: «لَـمَّا قَضَى اللهُ الخَلْقَ كَتَبَ فِي كِتَابِهِ، فَهُوَ عِنْدَهُ فَوْقَ العَرْشِ: إِنَّ رَحْمَتِي غَلَبَتْ غَضَبِي
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّـهِ ﷺ: «لَـمَّا قَضَى اللهُ الخَلْقَ كَتَبَ فِي كِتَابِهِ، فَهُوَ عِنْدَهُ فَوْقَ العَرْشِ: إِنَّ رَحْمَتِي غَلَبَتْ غَضَبِي
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake):
1- “Mwenyezi Mungu alipomaliza kuumba, aliandika katika Kitabu chake. 2- Kilichopo katika kiti chake cha enzi. 3- Huruma yangu imeishinda hasira yangu”
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipo kadiria uumbaji wa viumbe, yaani kabla ya Mwenyezi Mungu kuumba viumbe kama ilivyoelezwa na mapokezi mengine[1]: Aliandika katika Ubao Uliohifadhiwa makadiriwa ya viumbe[2], au aliandika katika kitabu kingine kikubwa alicho nacho.
Kitabu hiki kimehifadhiwa na kipo kwa Mwenyezi Mungu juu Arshi, na Arshi ya Mwenyezi Mungu ni kiumbe kikubwa, ipo juu ya mbingu saba, imebebwa na Malaika watukufu, na maana ya neno Arshi ni Kiti chake cha Ufalme.Hii inaonesha ishara za utukufu wa Mwenyezi Mungu, na kwamba Yeye yuko Mbinguni juu ya Arshi yake. Amesema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika:
“Arrahmani, Mwingi wa Rehema, ametawala juu ya Kiti cha Enzi”
[Twaha: 5].
3. Mwenyezi Mungu Mtukufu aliandika katika kitabu hicho kuwa: “Rehema yangu imeshinda hasira yangu.” Hii ina maana kuwa Kiwango cha rehema zake kwa waja wake ni kikubwa zaidi kuliko kiwango cha hasira zake. Huruma yake inawafikia waja wake mara kwa mara katika sehemu mbalimbali, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“ikiwa Mwenyezi Mungu angeliwaadhibu watu kutokana na matendo yao, basi asingebakisha kiumbe yoyote katika dunia”
[Fatir: 45]
Na kama si kwa huruma yake, hakuna hata mmoja katika viumbe angelistahiki kuingia peponi” amesema Mtume rehma na Amani iwe juu yake: “Hataingia Peponi yeyote kwa matendo yake.” Maswahaba wakasema: Hata wewe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: hata mimi, isipokuwa Mwenyezi Mungu akinifunika kwa Fadhila na rehema zake[3]”Maana ya rehema ya Mwenyezi Mungu kutangulia hasira yake, ni ile hali ya kutowaadhibu wakosefu pale tu wanapotenda makosa, bali anawapa muda wa kuomba msamaha, na ikiwa wataomba msamaha basi watasamehewa.
Tulizana kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani kama alivyoandika makadirio ya viumbe katika Ubao Uliohifadhiwa, basi rehema yake iliandikwa pia, usihuzunike kwa yale uliyoyakosa, na wala usijali kuhusu yatakayokuja, muhimu ni kumuamini Mwenyezi Mungu.
Kitabu - chenye makadirio, kinachobainisha rehema ya Mwenyezi Mungu – kimehifadhiwa juu ya Arshi yake, kwa sababu ya utukufu wake, hivyo basi mwenye akili timamu anapaswa kuheshimu kitabu hicho heshima inayostaili, na atumie muda mwingi kuwazia jambo hilo, na kumuomba Mwenyezi Mungu mwisho mwema.
Rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ilitangulia ghadhabu yake, ndio maana anakubali toba ya wakosefu na waasi bila kujali wingi ya dhambi zao, hivyo basi tujitazame sisi wenyewe: Je! Macho yetu hayajatosheka kumuasi mwenyezi mungu? na masikio, maneno na mikono? hebu tusikilize wito wa Mwenyezi Mungu aliposema:
“Sema: Enyi waja wangu mliozidhulumu nafsi zenu, msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu husamehe dhambi yote, hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe, na Mwenye Huruma”
[Al-Zumar: 53].
Zikaribieni rehema za Mwenyezi Mungu, hata kwa inchi moja. Kwani alikuwako mtu katika Wana wa Israili aliyeuwa watu tisini na tisa, kisha alipotaka kutubia akamuuliza mtu mmoja kwa kusema, nimeuwa watu tisini na Tisa je ninaweza kutubu na mwenyezi mungu akakubali toba yangu? Akasema yule mtu: Hapana”, jamaa akakasirika na akamuua, akawa ametimiza watu mia moja. Kisha akamuuliza mtu mwingine, mtu huyi akamwambia, ndio inawezekana kutubia, ila nakushauri hama katika ardhi hii ambayo umefanya maovu mengi, nenda kwenye kijiji Fulani. Alipokuwa akielekea huko umauti ukamkuta, akafariki akielekea huko. Malaika wapeponi wakaja kuichukua roho yake wakidai kuwa huyu ni mtu mwema kwa sabau alishaamua kutubia na alikuwa anaenda katika ardhi nyingine ili kuhama ardhi aliofanya maovu mengi, na Malaika wa motoni nao wakaja wakidai kuwa jamaa huyo alikuwa muovu. mzozo ukawa mkubwa kati ya malaika wa rehma na yule wa adhabu, Mwenyezi Mungu akaamrisha hili liwe karibu na linguine liwe mbali, na kisha malaika akasema jaribuni kupima kwa umbali, walipopima umbali wakakuta kule alikokuwa akielekea ndio karibu zaidi kwa inchi moja tu, ikawa sababu ya kusamehewa.[4]
Mwenyezi Mungu Mtukufu ana ufalme na ujuzi wa kila kitu, na ana kiti cha enzi na kitabu ambacho ndani yake kumeandikwa kila kitu, pamoja na hayo, Mwenyezi Mungu ana huruma, lakini watu wengi wakiwa na mamlaka ya kiutawala au elimu (au mfano wa hayo, kama ubaba, nguvu za kimwili, cheo cha juu, mali, au vitu vinginevo.) hujikweza na kuwakandamiza walio chini yake, na kuwafanyia jeuri kwa sababu ya mamlaka yao, hivyo basi chukuwa tahadhari katika hilo.
Kila mtu anakosea na hii ni ishara ya upungufu wao, kwani kila mtu huwa ana huruma na hasira, na uhalisia wa kukamilika huruma ni kuwa huruma iwe mbele Zaidi kulikoa hasira, hivyo basi inapendeza kwa muislamu kujipamba na tabia hiyo ya huruma kuzidi hasira, pia mwanadamu anapaswa kumtegemea Mwenyezi Mungu ili kupata huruma kwa kuwa mwanadamu ni dhaifu zaidi.
Amesema Mshairi:
Ikiwa unatarajia rehema kutoka kwa mwenyezi mungu, basi Rafiki yangu kipenzi wahurumie walio dhaifu.
Na utafute radhi za Mwenyezi Mungu Muumba wetu = kwani kwa Utukufu wake aliumba viumbe
Na uombe malipo ya hayo kwa Mola wako Mlezi kwa rehema yake = Kwani Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa huruma atamrehemu.