عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّـهِ «لَـمَّا قَضَى اللهُ الخَلْقَ كَتَبَ فِي كِتَابِهِ، فَهُوَ عِنْدَهُ فَوْقَ العَرْشِ: إِنَّ رَحْمَتِي غَلَبَتْ غَضَبِي

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake): 

1- “Mwenyezi Mungu alipomaliza kuumba, aliandika katika Kitabu chake. 2- Kilichopo katika kiti chake cha enzi. 3- Huruma yangu imeishinda hasira yangu”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: 

“Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba atakaye fanya uovu miongoni mwenu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye ni Mwenye kusamehe na Mwenye Huruma”

[Al-An'am: 54].


Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na rehema yangu imeenea kila kitu. Lakini nitawaandikia khasa wanao mchamngu, na wanao toa Zaka, na wale ambao wanaziamini Ishara zetu”

[Al-A'raf: 156].


Pia akasema:

“Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe walio tubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu”

[Ghafir: 7].

Miradi ya Hadithi