148 - KUHIFADHI TOBA KWA KUFANYA MATENDO MEMA

عَنْ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ رضي الله عنه، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَرَأَيْتَ أَشْيَاءَ كُنْتُ أَتَحَنَّثُ بِهَا فِي الجَاهِلِيَّةِ مِنْ صَدَقَةٍ أَوْ عَتَاقَةٍ، وَصِلَةِ رَحِمٍ، فَهَلْ فِيهَا مِنْ أَجْرٍ؟  فَقَالَ النَّبِيُّ : «أَسْلَمْتَ عَلَى مَا سَلَفَ مِنْ خَيْرٍ»

Kutoka kwa Hakim bin Hizam, Allah amuwiye radhi, amesema:

1- Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, unaonaje mambo niliyokuwa nikiyaahidi kabla ya Uislamu, kama vile kutoa sadaka au kuwaacha huru watumwa, kuunga udugu, je nitapata dhawabu? 

2- Akasema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Umeyasilimisha yote yaliyotangulia katika kheri” ).

Ni: Hakim bin Hizam

Ni: Hakim bin Hizam bin Khuwaylid al-Qurashi al-Asadi Mwenyezi Mungu awe radhi naye, Abu Khalid, sahaba mkubwa, alizaliwa  katika Al-Kaaba miaka kumi na tatu kabla ya mwaka wa tembo, na alikuwa mmoja wa watukufu na bora zaidi macho - ni mwa  Maquraishi. Alisilimu siku ya kufungua mji wa makka, na kisha Uislamu wake ukawa mzuri, aliwakomboa watumwa mia moja katika zama za kabla ya Uislamu, na mia moja wengine katika Uislamu, hakufanya jambo lolote jema katika Ja - hiliyyah bali alifanya katika Uislamu kama hilohilo, Aliishi miaka mia na ishirini, nusu ya miaka hiyo katika Jahiliyyah, na nusu yake katika Uislamu, macho yake yalitoweka kabla ya kufa kwake, na alikufa Madina mwaka (54 Hijiria), na ikasemwa:  mwaka (58 AH)

Miradi ya Hadithi