عنْ عمرَ رضي الله عنه، عنْ النّبيِّ ﷺ قال: «لو أنَّكُمْ تَوَكَّلُونَ على اللهِ حقَّ توكُّلِه، لرُزِقْتُمْ كما تُرْزَقُ الطَّيْرُ، تَغْدو خِماصًا، وتَرُوحُ بِطانًا»

Kutoka Kwa Umar, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, amesema:

1.“Lau mngemtegemea Mwenyezi Mungu kwa haki ya kumtegemea, mngelipewa riziki zenu kwa urahisi kama vile ndege wanavyo pewa riziki zao.  2. Wanatoka asubuhi wakiwa na njaa, na wanarudi jioni wakiwa wameshiba” 


1-   Kutegemea ni miongoni mwa ibada za moyoni kabisa, na hupatikana kwa kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumtegemea kwa kuzingatia sababu, Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ametuambia kuwa tukimtegemea Mwenyezi Mungu, kwa haki ya kumtegemea, angeturuzuku kama anavyowaruzuku ndege;

2-   Ndege hutoka wakati wa asubuhi wakiwa na njaa, matumbo matupu, na hurudi mwisho wa siku wakiwa wamejaa matumbo. Lau tungekuwa wakweli katika kumtegemea na kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, angetujaalia kama ndege asiye na msaada, lakini wengi wetu tunategemea udanganyifu, uwongo na ulaghai katika shughuli. Au anabweteka na kuto kufanya sababu, au anategemea sababu kabisa, kwa namna ambayo anaona sababu pekee ndio zinasaidia kupatikana riziki na si vinginevyo [1]. Na uhalisia wa kutegemea ni mtu kufanya sababu kwa kumtumaini Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba kila jambo liko mkononi Mwake, asiache kufanya sababu na kusubiri riziki yake huku amekaa, kwani aina hii ni kubweteka, na si kutegemea kuzuri. Mtume (Rehma na Amani zimshukie) alivaa Ngao katika vita vyake, akachimba handaki katika vita vya akhzab, akatoka siku ya Hijrah akiwa amejificha, na akatumia mtu wa kumwongoza kwa ajili ya kuhama kwake, na akajificha ndani ya pango, na kuandaa mipango yake kwa ajili ya vita. Yeye ndiye mbora wa wanaomtegemea Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ameamrisha kumteegemea kwa azma na kuchukua njia ya lazima, akasema Mwenyezi Mungu mtukufu:

“Na mnapo dhamiria basi mtegemeeni Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaomtegemea”.

[Al Imran: 159]

MAFUNDISHO

1-   Iwapo Muislamu litamtia huzuni suala la riziki, basi hatakiwi kufanya lolote tofauti na kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu, aridhike na Anayomgawia, na awe na yakini kabisa kuwa ana Mola anayesimamia mambo yake, kisha sasa afanye sababu baada ya hapo.

2-   Watu wengi husema: “Tumaini langu ni Mwenyezi Mungu” bila kuwa na imani ya kweli katika kutegemea; kwani Kutegemea si kusema tu kwa ulimi, bali ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kuridhika na hukumu yake, kwa kumwamini Yeye.

3-   Anayemtegemea Mwenyezi Mungu kiuhalisia, hufanikishiwa malengo yake, na hulindwa kutokana na matamanio ya Shetani na vishawishi vyake. Amesema Mwenyezi Mtukufu:

“Na unaposoma Qur-aan, basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa (98) kwani Shetani hana uwezo wowote wa kuwashawishi waumini, na kwa Mola wao mlezi wanategemea”

[Al-Nahl: 98]

. Yeyote anayetaka Mwenyezi Mungu amlinde na Shetani na kumweka mbali naye, basi amtegemee vyema.

4. Anayetaka Mwenyezi Mungu amhifadhi katika mambo yake yote, na amtosheleze na yale yanayomsibu katika mambo ya dunia na akhera, basi amkimbilie Mwenyezi Mungu na amkabidhi jambo hilo; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Hakika Mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu basi yeye humtosha”

[Al-Talaq: 3]

Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Mwenye kusema: anapotoka nyumbani kwake :-“Kwa jina la Mwenyezi Mungu ninamtegemea Mwenyezi Mungu, hakuna nguvu wala uwezo isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu; Ataambiwa: Umetoshelezwa na umelindwa, na Shetani anajitenga naye."[2] 

5. Haki ya kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kutosheka na yale anayofanya Mwenyezi Mungu, amwamini Yeye, na kumkabidhi mambo yake. Bishr Al-Hafi – Mwenyezi Mungu amrehemu – alisema: Mtu fulani anasema: Ninamtegemea Mwenyezi Mungu, hali yakuwa anamsingizia Mwenyezi Mungu uwongo; Iwapo atamtegemea Mwenyezi Mungu atatosheka na yale anayoyafanya Mwenyezi Mungu. Na Yahya bin Muadh – Mwenyezi Mungu amrehemu – aliulizwa: Ni wakati gani mtu anakuwa amemtegemea Mwenyezi Mungu? Akasema: Atapokuwa radhi na Mwenyezi Mungu kuwa ni tegemezi [3].

6. Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaka kumlisha Bibi Maryam, Mungu amuwie radhi, akiwa katika uchungu wake, alimuamuru kulitikisa shina la mtende, basi ni nguvu gani ya mwanamke ambaye yuko katika hali ya kuzaa mtoto wake aweze kutikisa mtende mpaka Tende zianguke! Bali hata Kama angekuwa ni mtu mwenye nguvu kisha atikise mtende, asingaliweza kudondosha chochote, lakini Mwenyezi Mungu, Utukufu ni Wake, anapenda mja achukue sababu na kumwachia Mwenyezi Mungu matokeo ya sababu hiyo.

7. Umar Ibn Al-Khattab Mwenyezi Mungu amuwiye radhi alikutana na kundi la watu wa Yemen waliokuwa wakitegemea bila kufanya sababu, akasema: Ni akina nani nyinyi? Wakasema: Sisi ndio wenye kumtegemea Mwenyezi Mungu Akasema: Bali nyinyi ndio wenye kubweteka. Hakika mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu ni yule anayepanda mbegu shambani na anaweka tumaini lake kwa Mwenyezi Mungu [4].

8. Mlinganiaji na mwenye elimu atumie picha nyingi za balagha na kutumia mifano ambayo itabainisha maana na kuimarisha uelewa.

9. Abdullah bin Salam na Salman radhi za Allah ziwe juu yao wakakutana, mmoja wao akamwambia mwenzake: Ukifa kabla yangu, basi naomba tukutane, ili uniambie uliyokutana nayo kutoka kwa Mola wako Mlezi, na nikifa kabla yako, nitakutana nawe, na nitakuambia. Mmoja akamwambia mwingine: hivi wafu wanaweza kukutana na walio hai? Akasema: Ndio, roho zao huenda Peponi popote zinapotaka. Akasema: Fulani alifariki, hivyo akakutana naye katika ndoto, na akasema: “Mtegemee Mola wako na uwe na bishara njema, kwani sijapata kuona malipo makubwa kama ya kutegemea, Mtegemee Mola wako na uwe na bishara njema, kwani sijapata kuona malipo makubwa kama ya kutegemea” [5]

10. Luqman – Mwenyezi Mungu amrehemu – alimwambia mwanawe: “Ewe mwanangu, dunia ni bahari ambayo watu wengi walizama ndani yake. Ukiweza tengeneza jahazi la kumwamini Mwenyezi Mungu, na ulijaze kwa kumtii Mwenyezi Mungu, na tanga lake liwe ni kumtegemea Mwenyezi Mungu; Labda utaokoka” [9].

11. Amesema Mshairi:

Nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Muumba wangu, katika riziki yangu = na nikawa na hakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anaye niruzuku.

Na chochote katika riziki yangu hakinipiti, hata ikiwa iko chini ya bahari ya giza.

Mungu Mwenyezi ataileta kwa neema yake = hata kama sikuwa na ulimi fasaha Ni kwa nini Nafsi zinahuzunika juu ya riziki = Na haliyakuwa Mwingi wa Rehema ameshagawanya riziki za viumbe.



Marejeo

1. (Tazama: "Dalil Alfalhin Lituruq Riyaadh Alswaalihina" cha Ibn Allan Al-Siddiqi (1/197-198

2. Imepokewa na Al-Tirmidhiy (3426).

3. “Madarij al-Salikeen” cha Ibn al-Qayyim (2/ 114).

4. Imepokewa na Al-Bukhari (1523).

5. Attawakul A`Laa Allah” cha Ibn Abi Al-Dunya (uk. 51).

6. “Attawakul A`Laa Allah” cha Ibn Abi Al-Dunya (uk. 49).



Miradi ya Hadithi