عنْ عمرَ رضي الله عنه، عنْ النّبيِّ ﷺ قال: «لو أنَّكُمْ تَوَكَّلُونَ على اللهِ حقَّ توكُّلِه، لرُزِقْتُمْ كما تُرْزَقُ الطَّيْرُ، تَغْدو خِماصًا، وتَرُوحُ بِطانًا»

Kutoka Kwa Umar, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, amesema:

1.“Lau mngemtegemea Mwenyezi Mungu kwa haki ya kumtegemea, mngelipewa riziki zenu kwa urahisi kama vile ndege wanavyo pewa riziki zao.  2. Wanatoka asubuhi wakiwa na njaa, na wanarudi jioni wakiwa wameshiba” 


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: “Na kwa Mwenyezi Mungu ndio wategemee Waumini (11) Na tuna nini hata tusimtegemee Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ametuongoa kwenye Njia zetu. Na hapana shaka sisi tutayavumilia hayo maudhi mnayo tuudhi. Na kwa Mwenyezi Mungu wategemee wanao tegemea”

[Ibrahim: 11, 12].

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na humruzuku kwa namna asiyo tarajia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake”

[Talaq: 3]

. Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na ukisha azimia basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea”

[Al Imran: 159].

Miradi ya Hadithi