عَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ «مَا بُعِثَ نَبِيٌّ إِلَّا أَنْذَرَ أُمَّتَهُ الأعْوَرَ الكَذَّابَ، أَلا إِنَّهُ أَعْوَرُ، وَإِنَّ رَبَّكُمْ لَيْسَ بِأَعْوَرَ، وَإِنَّ بَيْنَ عَيْنَيْهِ مَكْتُوبٌ "كَافِرٌ" 

Kutoka kwa Anas Mwenyezi Mungu awe eradhi naye amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie:

“Hakutumwa Nabii ila aliwaonya watu wake kutokana na mwongo wenye jicho moja.Fahamu kuwa ni mwenye jicho mojaNa Mola wako Mlezi si mwenye jicho moja.Na baina ya macho yake imeandikwa neno “kafiri”

  1. Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, alitoa kipaumbele zaidi katika kueleza fitna ya Mpinga Kristo, kama walivyofanya Mitume wengine, Kwa sababu ni mtihani mbaya zaidi kupata kutokea Duniani. Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: “Hakuna mtihani mkubwa tokea kuumbwa kwa Adam mpaka kufika kiyama kuliko mtihani wa Mpinga Kristo” [1]. Ndio maana, hakuna nabii aliyekuja isipokuwa aliwaonya watu wake na kuwabainishia uhalisia wa majaribu yake, huyu Mpinga kristo –Masihi Dajjali- amekuwa ni mtihani mkubwa kwa sababu uwezo aliompatia Mwenyezi Mungu kutokana na miujiza mikubwa inayovutia na kushangaza akili. Aliitwa Masihi kwa sababu ana jicho moja, na ikasemekana kwamba anaifuta dunia, maana yake ataimaliza Dunia kwa muda wa siku arobaini. Na Aliitwa Dajjal kwa sababu ya vitendo vya ulaghai, uwongo, na hadaa anazodhihirisha, hivyo atadai kuwa yeuye ni Mungu, na Mwenyazi Mungu atawajaribu viumbe wake kupitia huyu Mpinga kristo –Masihi Dajjali- [2].Alibainisha  Mtume Rehma na Amani zimshukie katika hadithi nyingi kuhusu huyu Mpinga kristo –Masihi Dajjali-, asili yake, na atakavyo izunguka dunia - isipokuwa Makka na Madina, kwa sababu ni haramu kwake kuikanyaga - na akaelezea wasifu wake wa kimaumbile, na nini Muislamu anatakiwa kufanya akikutana naye, mpaka Mtume Rehma na Amani zimshukie akabainisha  kuteremka kwa Isa bin Maryam, amani iwe juu yake, na kwamba Isa bin Maryam tasali nyuma ya imamu wa Waislamu, kisha atatoka nao kwenda kukutana na Mpinga Kristo na kupigana naye mpaka kumuua katika mlango wa Lodi pale Bait Al-Maqdis. Habari za Mpinga Kristo –Masihi Dajjali- zimetajwa kwa wingi sana kutoka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie kupitia zaidi ya maswahaba arobaini, hayo yamethibiti kwa dalili za Sunnah, na hakuna Akili Salama yenye kukanusha hilo [3].

2.   Kisha akaelezea Mtume Amani zimshukie kuhusu sifa zake muhimu za kimaumbile; Ni kwamba jicho lake moja ni chongo, na jingine limetokeza usoni mwake, na lina michirizi minene inayotoka pembezoni mwa jicho, hivyo kila jicho lina kasoro, jicho moja ni chongo na lingine linakasoro kubwa. [4].Miongoni mwa sifa zake katika Hadith nyingine, Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) ametaja kuwa nywele zake simejisokota na kujikunja, fupi, na ni mnene, kana kwamba macho yake ni zabibu inayoelea [5].

3.    Kisha Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, akamtakasa Mola wetu Mlezi kutokana na sifa hizi; Kwa vile Mpinga Kristo anadai uungu, kasoro hiyo ya chongo ni sifa mojawapo ya upungufu ambayo haitamaniki katika haki ya Mwenyezi Mungu. Pia sifa nyingine zote za mpinga-Kristo. Ni sifa za upungufu endapo mtu akiwa na sifa moja tu katika hizo, watu watamtukana, atakuwa na hali gani mtu ambaye atajikuta anazo sifa hizi zote kwa pamoja?! Utukufu wa juu kabisa ni wa Mwenyezi, na sifa zake zote ni nzuri.

4.   Miongoni mwa dalili za mpinga Kristo pia ni kwamba imeandikwa baina ya macho yake “kafiri”, ambayo Mwislamu huisoma, sawa awe anajua kuandika au hajui kusoma na kuandika, kwa sababu ya maana ya jumla ya kauli yake, amani iwe juu yake. "Kila Muislamu atalisoma" [6]. Neno "kila mtu" linaashiria ujumla, na ni maandishi ya kweli, ambayo Mungu aliyafanya kuwa ndio ishara, na ndio alama miongoni mwa dalili za uhakika zinazojulisha kutokuamini kwake, uwongo na ubatili. Mwenyezi Mungu huifanya ionekane kwa kila Muislamu, na huificha kwa yeyote anayetaka uovu na mitihani yake, na hakuna kujizuia kufanya hivyo.”[7]

Mafunzo

  1. Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) hakuuacha umma wake ila aliwabainishia uhalisia wa mtihani wa Mpinga Kristo, na akawaongoza kwenye yale yatakayowalinda na fitina yake. Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, hakuacha kheri bila ya kuiashiria, na hakuacha shari bila ya kukemea. Hii inatulazimu kumpenda, kumtii, na kutanguliza Maneno yake juu ya kauli ya watu wengine wote.

  2. Kutokana na aliyofahamisha Mtume, Rehema na Amani zimshukie, miongoni mwa mambo yatakayomkinga na mtihani wa Mpinga Kristo, kuhifadhi aya kumi za mwanzo wa Surat Al-Kahf; Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie: ”Mwenye kuhifadhi aya kumi za mwanzo wa Surat Al-Kahf Atakingwa kutokana na mitihani ya Al Dajjal” [8], na katika Hadith ya  Al-Nawas bin Samaan Mwenyezi Mungu awe radhi naye kwamba Mtume Rehema na Amani zimshukie amesema: “Yeyote katika nyinyi atakae kutana na Dajjal basi amsomee Aya za mwanzo za Surat Al-Kahf” [9].

  3. Mtume Rehema na Amani zimshukie alikuwa akipenda sana kujikinga katika kila sala kutokana na mtihani wa Mpinga Kristo; Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani ziwe juu yake) alikuwa akiomba dua: “Ewe Mola wangu najikinga Kwako kutokana na adhabu ya kaburi. na najikinga Kwako kutokana na mtihani wa Mpinga Kristo, na najikinga Kwako kutokana na mitihani ya uhai na kifo. Ewe Mola wangu najikinga Kwako kutokana na kufanya dhambi na madeni.” [10]. Ikiwa hivi ndivyo hali ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, basi ni lazima tuzidishe kuomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu kutokana na majaribu ya Masihi Dajjal- Mpinga Kristo.

  4. Mwalimu na mhubiri afuate njia ya manabii na awaonye watu kutokana na majaribu na mitihani ya wazi na ya iliyofichikana.

5.   Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie kuwa Mwenyezi Mungu huwakinga Waumini na mtihani wa Mpinga Kristo, na kuwapa msukumo wa kusoma neno “kafiri” baina ya macho yake tofauti na mtu mwingine Jambo kuu linalomlinda muumini dhidi ya Mpinga Kristo ni kutenda yatakayo ongeza imani yake na kushikamana nayo.

Marejeo

  1. Ahmed (16373).
  2. Fayd al-Qadiir cha al-Manawiy (3/194).
  3. Tazama: Mwanzo na Mwisho wa Ibn Kathir 19/195 na kabla na baada, na tazama Hadith za Aldijali cha Al-Awni.
  4. Tazama: “Iikmal Almuealim Bifawayid Muslimin” cha Qadi Iyad (1/522).
  5. Al-Bukhari (3441).
  6. Muslim (2933).
  7. Sherh ya Al-Nawawi katika kitabu cha sahihi Muslim (18/60).
  8. Muslim (809).
  9. Muslim (2937).
  10. Al-Bukhari (832) na Muslim (589).


Miradi ya Hadithi