عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِ‍يَّ ﷺ: أَيُّ الْعَمَلِ أَحَبُّ إِلى اللَّهِ؟ قَالَ: «الصَّلاةُ عَلى وقْتِهَا»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «ثُمَّ بِرُّ الْوَالِدَيْنِ»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «الجِهَادُ في سَبيل اللهِ» قَالَ: حَدَّثَنِ‍ي بِهِنَّ، ولَوِ اسْتَزَدْتُهُ لَزَادَنِ‍ي. 

Kutoka kwa Abdullah bin Masoud, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, ambaye amesema:

1. Nilimuuliza Mtume rehma na amani zimshukie: Ni amali gani anayoipenda zaidi Mwenyezi Mungu? Alisema: “kusali kwa wakati.” 2. Akasema: Kisha ipi? Akasema Mtume: “Basi waheshimuni wazazi.” 3. Akasema: Kisha ipi? Akasema Mtume Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu”. 4. Akasema: Alinieleza hayo tu, na lau ningeomba zaidi, angeniongeza.


1. Ibn Masoud, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alimuuliza Mtume rehma na Amani zimshukie kuhusu amali anazozipenda mno Mwenyezi Mungu Mtukufu ili azidi kufanya amali zake na kuzitanguliza juu ya amali nyingine na kujikurubisha kwake, basi Mtume, Amani imshukie, akamwambia kwamba lililo bora katika hilo ni kuswali kwa wakati wake. Na Swala ndio nguzo ya Uislamu, na ndio msingi wa uhusiano baina ya mja na Mola wake, na ndio nguzo ya pili ya dini, na ndio maana kuitekeleza katika wakati ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu aliupanga ndio ikawa amali bora zaidi inayopendeza kwa Mwenyezi Mungu mtukufu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu waja wake Waumini kwa kusimamisha swala na kuitekeleza inavyopaswa. Akasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika:

Hakika wamefanikiwa Waumini

“ (1) Ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao (2) Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi (3) Na ambao wanatoa Zaka (4) Na ambao wanazilinda tupu zao (5) Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa (6) Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka (7) Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao (8) Na ambao Sala zao wanazihifadhi (9) Hao ndio warithi (10) Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo”

[Al-Mu’minoon: 1-11]

Aliwasifia kuwa wanyenyekevu katika sala, na kuzidumisha. Na Mwenyezi Mungu utukufu ni wake, Amewaonya wanaopoteza sala kwa kuzichelewesha zaidi ya wakati wake, kwa kusema:

“Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Sala, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta malipo ya ubaya”,

[Maryam: 59]

Wafasiri walisema: Wamepoteza wakati, na kama ingekuwa ni kuacha, itakuwa ni kufuru [1]

 2. Kisha Ibn Masoud, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, akauliza juu ya matendo mema baada ya kuswali kwa wakati wake, na akamuelekeza katika kuwaheshimu wazazi. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewatilia umuhimu wazazi wawili, basi akahusisha kuwafanyia wema na kumuabudu Yeye na kumuunganishia sehemu zaidi ya moja, kama alivyosema Mola Mtukufu:

“Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili”

[An-Nisa: 36]

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

“Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema”

[Al-An’am: 151].

Kuwatukuza wazazi wawili ni kuwafanyia wema, kuwasindikiza kwa wema, na kuwausia, kuwahudumia, na kutowaasi, Amesema Mwenyezi Mungu.

“Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima (23) Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni”

[Al-Israai: 23, 24].

Nae Mtume Rehma na amani iwe juu yake ameeleza kuwa kuwaasi wazazi ni miongoni mwa madhambi makubwa; Akasema, rehma na amani iwe juu yake: “Je, nisikuambie dhambi kubwa katika madhambi makubwa? Mara tatu, Maswahaba wakasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tuambie” akasema: “Kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwadharau wazazi wawili” – Naye akaketi vizuri, na alikuwa kaegemea kisha akasema: “Na kusema uongo ni dhambi kubwa” Akasema: Akaendelea kuirudia mpaka tukasema: Laiti angenyamaza [2]

3. Kisha Ibn Masoud, Mwenyezi Mungu, awe radhi naye akauliza kuhusu amali zinazopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu baada ya kuswali kwa wakati wake na kisha kuwaheshimu wazazi. Kwa hiyo, Mtume rehma na amani iwe juu yake, akamwongoza kwenye jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na jihadi: ni kupigana na makafiri ili kusimamisha neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuonyesha ibada za Uislamu kwa kujitolea nafsi na fedha. Nayo ndio urefu wa nundu ya Uislamu. Kwa hayo huinuliwa bendera ya Dini, na neno la haki huinuka mpaka kiyama kitakapo simama, na kwayo Mwenyezi Mungu huwatukuza Waumini na huwadhalilisha maadui zake. Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu Mujahidina katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kusema:

“Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa”

[At-Tawbah: 111]

Na Mtume, amani iwe juu yake, alieleza kwamba hakuna kazi inayolingana na malipo ya jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; Alikuja mtu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie akasema: Nielekeze kwenye kitendo ambacho ni sawa na jihadi. Alisema: “Siwezi kuipata.” Akasema Mtume: “Je, Mujahid akienda vitani, je unaweza kuingia msikitini kwako na kusimama na usilegee, na ufunge na usifungue?” Akasema: Na ni nani awezaye kufanya hivyo? [3]

4. Kisha Abdullah bin Masoud akaeleza kuwa ametosheka na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie kwa vitendo hivyo, na ikiwa angeendelea kumuomba zaidi na kumuomba bila shaka Mtume, angemzidishia, Bali aliacha kwa kumuonea huruma Mtume, rehema na amani ziwe juu yake.

Mafunzo

1. (1) Maswahabah, Mungu awawie radhi, walikuwa wanapenda sana kutumia muda wao katika ibada, na kumuuliza Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam kuhusu ibada za karibu na kupendeza kwa Mwenyezi Mungu na yenye malipo makubwa. Kila Muislamu anapaswa kufuata mfano wao.

2. (1) Zaidi ya masahaba mmoja alimuuliza Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam kuhusu amali anazozipenda sana Mwenyezi Mungu, na kila mara alitaja jambo tofauti kutokana na hali tofauti za waulizaji. Anamjibu kila mmoja kwa kile anachohitaji zaidi na kinachofaa zaidi. walinganiaji, wanachuoni na waelimishaji lazima wazingatie hali na tabia za watu katika fatwa na mahubiri. 

3. (1) Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipenda sana kuswali katika nyakati zake, kiasi kwamba washirikina walipomzingira Siku ya Handaki, alisema: “Mwenyezi Mungu azijaze nyumba zao na makaburi yao kwa moto, wametushughulisha na swala ya kati mpaka jua likazama.” [4]  Pamoja na kwamba alikuwa na udhuru wa kisheria, Vipi mtu aliyekosa swala bila ya udhuru wa halali?! 

4. (1) Ibn Masoud, radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, alimuuliza Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, maswali kadhaa katika kikao kimoja, na Mtume hakumbana au kuchoshwa naye. walinganiaji na wanachuoni wajipambe kwa subira na ustahimilivu mbele ya watu.

5. (2) Kuwaheshimu wazazi wako ni miongoni mwa matendo makubwa zaidi ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Basi mwenye kuwa na wazazi wake mmoja au wote wawili walio hai, basi atumie fursa hiyo, na ajikurubishe kwa Mwenyezi Mungu kupitia kuwatendea wema. 

6. (2) kuwatendea wema wazazi kunafuta dhambi. Kutoka kwa Ibn Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi nimefanya dhambi kubwa, je, naweza kutubu na nikasamehewa? Akasema Mtume: “Unaye mama?” Akasema: Hapana. Akasema tena Mtume: “Je, una shangazi?” Akasema: Ndiyo, akasema: “Basi mtendee wema” [5]. 

7. (3) Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni amali kubwa kabisa na ukaribu, na hakuna amali yoyote inayolingana nayo, aliulizwa Mtume: Ni watu gani bora? Akasema: “Muumini anayepigania njia ya Mwenyezi Mungu kwa maisha yake na mali yake” 8. (3) Miongoni mwa jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kutumia juhudi na fedha katika kueneza dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kufikisha wito kwa watu, kuamrisha mema na kukataza maovu. [6]

9. (4) Kila mtu anatakiwa kuwa mpole kwa Mafaqihi na wasomi, kwa hivyo asiwaulize sana, na wala asiwatwishe maswali. Bali, ayafupishe na kuzingatia nyakati za uchovu wao na kutojali, na kadhalika.


Marejeo

1. Tafsir Ibn Katheer (5/243)

2. Imepokewa na Al-Bukhari (2654) na Muslim (87).

3. Imepokewa na Al-Bukhari (2785) na Muslim (1878).

4. Imepokewa na Al-Bukhari (2931) na Muslim (627).

5. Imepokewa na Al-Tirmidhiy (1904). 

6. Imepokewa na Al-Bukhari (2786) na Muslim (1888).


Miradi ya Hadithi