عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِ‍يَّ ﷺ: أَيُّ الْعَمَلِ أَحَبُّ إِلى اللَّهِ؟ قَالَ: «الصَّلاةُ عَلى وقْتِهَا»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «ثُمَّ بِرُّ الْوَالِدَيْنِ»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «الجِهَادُ في سَبيل اللهِ» قَالَ: حَدَّثَنِ‍ي بِهِنَّ، ولَوِ اسْتَزَدْتُهُ لَزَادَنِ‍ي. 

Kutoka kwa Abdullah bin Masoud, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, ambaye amesema:

1. Nilimuuliza Mtume rehma na amani zimshukie: Ni amali gani anayoipenda zaidi Mwenyezi Mungu? Alisema: “kusali kwa wakati.” 2. Akasema: Kisha ipi? Akasema Mtume: “Basi waheshimuni wazazi.” 3. Akasema: Kisha ipi? Akasema Mtume Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu”. 4. Akasema: Alinieleza hayo tu, na lau ningeomba zaidi, angeniongeza.


Abdullah bin Masoud bin Ghafil bin Habib

Abdullah bin Masoud bin Ghafil bin Habib, Al-Hudhali, Abu Abd al-Rahman, sahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam aliyesilimu huko Makkah zamani, alihama marambili, na alishiriki viya vya Badr na matukio yote pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie na ndiye mbeba viatu vya Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, alikuwa akimvisha Mtume anaposimama, na kuvibeba mikononi mwake anapokaa mtume amani iwe juu yake, alikufa huko Madina katika mwaka wa (32 AH) au (33 AH) [1]

Marejeo

1.Rejea ufafanuzi wake: “Ma’rifat al-Sahaba” na Abu Na’im (4/ 1765), “Al-Istifa’ fi Ma’rifat al-Ashab” cha Ibn Abd al-Barr (3/987). “Al-Isaba fi Tamayez al-Sahaba” cha Ibn Hajar (4/198).

Miradi ya Hadithi